Tuesday, July 16, 2019

FURSA 19 KATIKA SEKTA YA ELIMU ----------------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

Mara  kadhaa  tumesikia  watu  wakisema  "ELIMU   NI  UFUNGUO  WA  MAISHA ". Lakini  ni  mara  chache  sana   tumechukua   MUDA  kutafakari  kwa  kina   undani    wa  kauli  hii. Pamoja   na  yote  yanayosemwa, ukweli  utabaki   kuwa  kweli  ndio   nguzo  pekee  ya   kumsimika  mwanadamu   katika maisha.
ELIMU  humpatia   mtu    msingi  wa  kifikra  na maarifa   stahiki  ya  kuweza  kupambanua  maisha , kufanya  kazi   vyema  na  kuwasiliana  na  watu. Tukiachlia  hayo , elimu  ina   faida  nyingi  sana , elimu  itakufanya  uishi  maisha  yenye  FURAHA, UHURU , KUJITEGEMEA , KUTAFSIRI  NDOTO  zako , ELIMU  itakufanya   ujiamini  hasa  pale  unapoongea  na  watu, hukuunganisha  na  dunia  , kuelewa  tamaduni  mbalimbali  za  watu duniani , pamoja  na kukutayarisha  kuwa  na  mafanikio. SEKTA   YA  ELIMU  ni  sekta  ya   mabilioni    ya  pesa  duniani  kote. Vile  vile  ni  sekta  pana  na  iliyojigawa    sana   kati  ya  sekta   zote   naweza  kusema.Ukianzia  shule  za  awali  , shule  za  msingi , shule  za  kati , sekondari , vyuo  vya  ufundi  kama  vile  VETA , vyuo  vya   ualimu  na  vyuo   vikuu  utagundua  ukweli  kuwa   ukubwa  wa  sekta  hii  unabainisha  wazi  kabisa  FURSA  zilizopo  kwenye  SEKTA   YA  ELIMU . Kwa  ufupi   ebu  tuangalie  fursa  zilizopo  kwenye  sekta  ya  elimu  ambazo  wewe  MJASIRIAMALI  unaweza  kufanya   leo  na  kupata   UTAJIRI


MUHIMU : Ili   kuendelea  Kujifunza  Zaidi na  Kugundua  FURSA  mbalimbali zilizojificha katika  
'SEKTA   YA ELIMU "jiunge   na   "FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG "  na    " DARASA  LA  SEMINA " ( Google  Classrom )  kwa  kulipa  ADA  YA  UANACHAMA ( Tshs 10000  kwa  Mwezi ) ili   uweze  Kuzigundua na  kujifunza " FURSA  ZINAZOKUZUNGUKA " na  Kuzifanyia  Kazi na  KUFANIKIWA  na   hatimaye  kupata  UYAJIRI.

Ndimi  Rafiki na  Kocha  Wako  Mwl    Japhet  Masatu , Dar  es  salaam ,Tanzania , Afrika   Mashariki , 

Kama   hujajiunga  na  "  FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG " na  "DARASA  LA  SEMINA " ( Google  Classroom )  tuwasiliane   Kwa  Maelekezo  Zaidi


WhatsApp /  Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539


ULIZA  MASWALI , TOA  MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO  kwa  Email  hii:-  EMAIL fursaafrikamashariki@gmail.com

Monday, July 15, 2019

NJIA PEKEE YA KUJIHAKIKISHA USALAMA KWENYE KAZI AU BIASHARA YAKO.

“In today’s competitive economy, it’s not enough to simply do your job well. Developing a reputation as an expert in your field attracts people who want to hire you, do business with you and your company, and spread your ideas. It’s the ultimate form of career insurance.” ― Dorie Clark
Wakati mapinduzi ya viwanda yanaanza, watu waliambiwa ili kuwa na usalama wa kazi basi soma kwa bidii, faulu sana na utapata kazi nzuri ambayo utaifanya mpaka kustaafu kwako na hapo utalipwa mafao ya kukuwezesha kuishi mpaka uzeeni.
Mapinduzi ya viwanda yamefika tamati na sasa tupo kwenye mapinduzi ya taarifa. Katika zama hizi uhakika pekee wa wewe kuwa na usalama kwenye kazi au biashara siyo tu elimu au taaluma uliyonayo, bali kutengeneza ubobezi kwenye kile unachofanya kiasi kwamba watu watapenda kufanya kazi na wewe.
Unapaswa kujijengea sifa ya ubobezi wa hali ya juu kwenye kile unachofanya kiasi kwamba kila mwenye uhitaji unaohusu unachofanya anakufikiria wewe au anaambiwa waje kwako.
Na hilo linawezekana kama utaweka juhudi katika kujua vizuri kile unachofanya, kukifanya vizuri na pia kutengeneza mtandao wa watu wanaojua kuhusu unachofanya na hivyo kusambaza sifa zako kwa wengine wengi.

JINSI YA KUPATA WAZO LA TOFAUTI NA WENGINE NA KUFANIKIWA

Katika kupata wazo bora, zingatia mambo yafuatayo;
Moja; anza na chochote unachojali sana.
Watu wengi wamekuwa wanafikiria kwamba ili uweze kuleta mabadiliko makubwa kwako na kwa wengine basi inabidi uwe na wazo kubwa na la kipekee sana. Wazo ambalo wengine hawajawahi kuwa nalo. Huo siyo ukweli, unaweza kuanza na wazo lolote na ukaweza kulijenga kwa utofauti na ukajitofautisha sana.
Anza na chochote unachojali, unachopenda, unachoamini, unachojua, ulichozoea au ambacho umesomea. Chochote kile ambacho unaona kinaweza kuwa bora zaidi ya kilivyo sasa, unaweza kukichukua kama wazo lako la kufanyia kazi.
Mbili; uliza maswali ambayo hayaulizwi.
Watu wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea kwa sababu wanafanya kile ambacho kila mtu anafanya, na hawathubutu kujaribu vitu vya tofauti. Sasa kwa wazo unalotaka kufanyia kazi kuliboresha zaidi, anza kwa kuuliza maswali ambayo watu wengine hawaulizi.
Maswali hayo yanaweza kuwa, vipi kama.... vipi kinyume cha... Hapa unajaribu kupata picha ya tofauti na wengi walivyozoea, kwa kuona upande wa pili wa vitu au kwa namna ya tofauti.
Tatu; angalia uzoefu wako binafsi.
Baada ya kujiuliza maswali ya tofauti kwenye wazo unalotaka kufanyia kazi, angalia uzoefu wako binafsi kwenye wazo hilo. Usijidharau kwa sababu labda huna elimu kubwa au uzoefu mkubwa kwenye jambo hilo. Labda siku za nyuma umewahi kujaribu kufanya tofauti na ukapata matokeo ya tofauti, hiyo inatosha kukuonesha kwamba kuna uwezekano wa kupata matokeo tofauti na ambayo watu wanapata sasa.
Nne; chagua eneo la ubobezi kwenye wazo lako.
Wazo unalokuwa nalo linaweza kuwa pana, sasa unahitaji kuchagua eneo ambalo utabobea kwenye wazo hilo ili kujitofautisha kabisa na wengine. Badala ya kutaka kufanya kila kitu, unachagua eneo moja ambalo utaweka muda na nguvu zako na kuweza kutengeneza ubobezi mkubwa. Ni kupitia ubobezi huu ndiyo unaweza kupiga hatua kubwa kwenye wazo hilo.
Tano; fanya utafiti.
Watu wengi wamekuwa wanapata mawazo mapya ya kuboresha zaidi, lakini hawanufaiki nayo kwa sababu huwa hawaweki kazi inayopaswa kuwekwa ili mtu kubobea kwenye kitu hicho. Moja ya kazi kubwa unayopaswa kuweka ni kufanya utafiti. Siyo kusoma tafiti, badala yake kufanya utafiti mpya, kwa kuangalia yale maeneo ambayo unataka yawe bora kisha kuja na njia bora za kuyaboresha kutoka kwenye tafiti mbalimbali zinazogusa wazo hilo.
Sita; unganisha mawazo.
Kuna maeneo mengine ambayo yameweza kupiga hatua kubwa, ambayo ni tofauti na wazo unalofanyia kazi wewe. hii haikuzuii wewe kujifunza kutoka maeneo hayo. Jifunze kupitia maeneo mbalimbali kwa hatua ambazo watu wameweza kupiga, kisha unganisha mawazo hayo na wazo unalofanyia kazi kuweza kuona jinsi gani ya kuboresha wazo unalofanyia kazi. Kumbuka misingi ya mafanikio kwenye kila eneo inafanana, hivyo kwa kuangalia jinsi ambavyo mawazo mengine yamefanikiwa, utaweza kufanikisha wazo lako pia.
Saba; tengeneza nguzo ya kubeba wazo lako jipya.
Baada ya kuchagua wazo unalotaka kuboresha, ukauliza maswali ya tofauti, ukatumia uzoefu wako, ukafanya utafiti na hata kujifunza kutoka maeneo mengine, unakuwa umejifunza mambo mengi sana kuhusiana na wazo lako jipya. Hapa unakuwa na maarifa na taarifa nyingi ambazo mtu mwingine siyo rahisi kuyaelewa. Hivyo ili wazo lako la kuboresha liweze kueleweka na kutumiwa na wengine, unahitaji kutengeneza nguzo ya kubeba wazo lako. Hapa unatengeneza mfumo unaobeba wazo lako jipya, kwa namna ambayo watu wengine wanaelewa jinsi linavyofanya kazi na matokeo ya tofauti yanavyopatikana.
Kwa hatua hizo saba, unakuwa umekamilisha wazo lako la tofauti, ambalo linaleta matokeo bora kuliko yale ambayo yamezoeleka. Baada ya hapo sasa unakwenda kwenye hatua ya pili ambayo ni kujenga wafuasi kwenye wazo lako.

FURAHA ZAO LA FEDHA-------------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

Ile kauli kwamba matajiri hawana furaha au huwezi kuwa na fedha na ukawa na furaha, ni mtego ambao watu wamekuwa wanajitengenezea wenyewe bila ya kujua.
Ipo hivi rafiki, wengi tunapokuwa tunaanzia chini, huwa tunafikiri tutakapopata fedha basi ndiyo zitakuwa jawabu la kila kitu. Hivyo tunaahirisha maisha yetu yote mpaka pale tutakapopata fedha.
Na hata kwa upande wa furaha, tunaahirisha furaha yetu tukiamini tukishakuwa na fedha basi ndiyo tutakuwa na furaha. Tunaacha kufanya yale mambo madogo madogo ya kila siku ambayo yanatuletea furaha, tukiamini kwamba tukishakuwa na fedha nyingi, basi furaha itakuja yenyewe.
Lakini hilo ni kinyume kabisa na msingi wa furaha, fedha haileti furaha, bali furaha inaleta fedha. Kwa kifupi ni kwamba fedha ni zao la furaha, na siyo kama wengi wanavyofikiri kwamba furaha ni zao la fedha.
Hivyo basi, usiahirishe furaha yako sasa kwa sababu unatafuta kwanza fedha na unafikiri ukishakuwa nayo basi utapata furaha. Badala yake ishi maisha yako kamili sasa, fanya vile vitu vidogo vidogo vinavyoleta furaha kwenye maisha yako na hivi vitakuwezesha kupata fedha zaidi na kwa kutokutumia nguvu kubwa kama unavyofanya unapokuwa huna furaha.
Usipuuze kitu chochote muhimu kwenye maisha yako kwa sababu unakazana kupata fedha, weka kipaumbele chako kwenye furaha na fedha itakuwa matokeo.
Jipende wewe mwenyewe kwanza, fanya kile unachopenda na zungukwa na wale wanaokupenda, haya yatakuletea furaha na furaha yako itavutia fedha zaidi kwako.
Fuata hili na hutafikia kwenye hali ya wengi ambao wana fedha lakini hawana furaha, wewe tayari unayo kanuni ya kuwa na furaha na kuwa na utajiri kwa wakati mmoja. Ifanyie kazi.

FEDHA KAMA WAZO ----------------------------" Fursa Afrika Mshariki Blog "

TENGENEZA GEREZA LA AKIBA --------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

MBINU YA KUONGEZA KIPATO 2019 ----------- " Fursa Afrikan Mashariki Blog.