Thursday, July 25, 2019

FURSA 11 ZA BIASHARA KATIKA MATANGAZO NA MASOKO ----------------- " Fursa Afrika Masahriki Blog "

Je, wewe  ni  mtu  wa  MASOKO na  MATANGAZO ? Unapenda   kufanya  kazi   kwenye  sekta  hii  hujui  fursa  sahihi   ya   KUWEKEZA ?   Kama   unayo  nia  ya  dhati  ya  kuwekeza   kwenye  sekta  hii , basi  endelea   kufutana  nami katika  DARASA   LA  SEMINA--ONLINE.


MUHIMU : Ili   kuendelea  Kusoma  na  Kujifunza  Zaidi na  Kugundua  FURSA  mbalimbali  zilizojificha  na  unazoweza  kufanya  katika   SEKTA  YA "MATANGAZO  NA MASOKO "

JIUNGE   na   "FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG "  kwa  pamoja  na    " DARASA  LA  SEMINA--FURSA  ZA   BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classrom )   kwa  kulipa  ADA  YA  UANACHAMA ( Tshs 10,000  kwa  Mwezi ) ili   uweze kusoma  MAKALA mbalimbali za  FURSA  na   Kuzigundua na  kujifunza " FURSA  ZINAZOKUZUNGUKA " na  Kuzifanyia  Kazi na  KUFANIKIWA  na   hatimaye  kupata  UTAJIRI.

Utaziona  MAKALA  lakini  hutaweza  kuzifungua  mpaka  uwe  umejiunga  na  kuwa  mwanachama . UTAJIFUNZA  MENGI  SANA kupitia  DARASA  LA  SEMINA.

Kujiunga  tuma   fedha  Tshs  10,000   kwa


  MPESA  NAMBA  0755400128   (  Majina  JAPHET  CHIBAJILO )
        TIGO   PESA   NAMBA   0716924136 ( Majina   Japhet   Masatu )
        AIRTEL  MONEY   0688 361 539  ( Majina  Japhet   Masatu )

(1).Ukishatuma  ADA  tuma kwa  meseji   E-MAIL  yako. Baada  ya  hapo  tutatumia  E--MAIL  yako  hiyo  kukuunganisha  na   Darasa. Utajifunza  mengi  usiyoyajua.

(2).Utapokea   MASOMO  kwa  njia  ya  E-MAIL ambapo  ni  njia  nzuri  zaidi  ya  kuyatunza  siku  zote  pasipo  kupotea  au  kuharibika.
 


Ndimi  Rafiki na  Kocha  Wako  Mwl    Japhet  Masatu , Dar  es  salaam ,Tanzania , Afrika   Mashariki , 

Kama  bado    hujajiunga  na  "  FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG " na  "DARASA  LA  SEMINA---FURSA  ZA  BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classroom )  tuwasiliane   Kwa  Maelekezo  Zaidi


WhatsApp /  Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539


Mwl   Japhet   Masatu  ni   Mwalimu  Kitaaluma , Kocha  wa Maisha  na   Mafanikio ,  Mshauri ,  Mjasiriamali.

Mwl   Japhet   Masatu  anaendesha  Mafunzo  Ya  Maisha  na  Mafanikio  kwa   Wale  Waliojitoa  hasa  Kufanikiwa  Kupitia  Programu  ya  "  MAISHA  NA  WEWE "  na  "  FURSA   ZA   BIASHARA   AFRIKA   MASHARIKI "

ULIZA  MASWALI , TOA  MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO  kwa  Email  hii:-  EMAIL fursaafrikamashariki@gmail.com

FURSA 22 ZA BIASHARA KATIKA SEKTA YA MAGARI NA UFUNDI MAGARI ( AUTOMOTIVE )

Kwenye  SEKTA  YA   MAGARI  kuna  FURSA   nyingi   sana  ambazo  watu   wengi wanazifanya  lakini   bado  zinafungua  milango  kwa  WAJASIRIAMALI  kuwekeza. Kwenye   SEKTA  hii  tutaongelea  MAGARI ,PIKIPIKI ,BAJAJI , BOTI , MELI ,  na  vyombo  vingine  vya   moto.


MUHIMU : Ili   kuendelea  Kusoma  na  Kujifunza  Zaidi na  Kugundua  FURSA  mbalimbali  zilizojificha  na  unazoweza  kufanya  katika   SEKTA  YA " MAGARI  NA  UFUNDI  MAGARI ( AUTOMATIVE ) "

JIUNGE   na   "FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG "  kwa  pamoja  na    " DARASA  LA  SEMINA--FURSA  ZA   BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classrom )   kwa  kulipa  ADA  YA  UANACHAMA ( Tshs 10,000  kwa  Mwezi ) ili   uweze kusoma  MAKALA mbalimbali za  FURSA  na   Kuzigundua na  kujifunza " FURSA  ZINAZOKUZUNGUKA " na  Kuzifanyia  Kazi na  KUFANIKIWA  na   hatimaye  kupata  UTAJIRI.

Utaziona  MAKALA  lakini  hutaweza  kuzifungua  mpaka  uwe  umejiunga  na  kuwa  mwanachama . UTAJIFUNZA  MENGI  SANA kupitia  DARASA  LA  SEMINA.

Kujiunga  tuma   fedha  Tshs  10,000   kwa


  MPESA  NAMBA  0755400128   (  Majina  JAPHET  CHIBAJILO )
        TIGO   PESA   NAMBA   0716924136 ( Majina   Japhet   Masatu )
        AIRTEL  MONEY   0688 361 539  ( Majina  Japhet   Masatu )

(1).Ukishatuma  ADA  tuma kwa  meseji   E-MAIL  yako. Baada  ya  hapo  tutatumia  E--MAIL  yako  hiyo  kukuunganisha  na   Darasa. Utajifunza  mengi  usiyoyajua.

(2).Utapokea   MASOMO  kwa  njia  ya  E-MAIL ambapo  ni  njia  nzuri  zaidi  ya  kuyatunza  siku  zote  pasipo  kupotea  au  kuharibika.
 


Ndimi  Rafiki na  Kocha  Wako  Mwl    Japhet  Masatu , Dar  es  salaam ,Tanzania , Afrika   Mashariki , 

Kama  bado    hujajiunga  na  "  FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG " na  "DARASA  LA  SEMINA---FURSA  ZA  BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classroom )  tuwasiliane   Kwa  Maelekezo  Zaidi


WhatsApp /  Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539


Mwl   Japhet   Masatu  ni   Mwalimu  Kitaaluma , Kocha  wa Maisha  na   Mafanikio ,  Mshauri ,  Mjasiriamali.

Mwl   Japhet   Masatu  anaendesha  Mafunzo  Ya  Maisha  na  Mafanikio  kwa   Wale  Waliojitoa  hasa  Kufanikiwa  Kupitia  Programu  ya  "  MAISHA  NA  WEWE "  na  "  FURSA   ZA   BIASHARA   AFRIKA   MASHARIKI "

ULIZA  MASWALI , TOA  MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO  kwa  Email  hii:-  EMAIL fursaafrikamashariki@gmail.com

Tuesday, July 23, 2019

TUMIA MTANDAO WA INTANETI VIZURI.

Mtandao wa intaneti una nguvu kubwa ya kuweza kuwafikia wateja wengi zaidi. Watu wengi wamekuwa wanachukulia mtandao wa intaneti kama sehemu ya kutoa maarifa na taarifa pekee, lakini pia unaweza kutumika kupata wateja zaidi wa biashara yako.
Katika kutumia mtandao wa intaneti kupata wateja zaidi unapaswa kuwa na vitu viwili;
Moja unapaswa kuwa na tovuti ya biashara yako, hii inaeleza kila kitu kuhusu biashara yako. Hapa ndipo nyumbani kwa biashara yako mtandaoni. Watu wanaweza kuingia na kupata taarifa muda wowote ule, masaa 24 kila siku. Unaweza pia kuuza bidhaa zako moja kwa moja kwenye tovuti ya biashara yako.
Mbili unapaswa kuwa na blogu ya biashara yako. Blogu hii unaitumia kutoa taarifa na maarifa yanayohusiana na biashara yako. Unaweza kuitumia blogu kutoa elimu kwa wateja wako kuhusu biashara yako, hivyo watu wanapokuwa na shida na kutafuta suluhisho, wanaletwa kwenye blogu ya biashara yako. Kwa kupata ushauri wako mzuri, wanakuamini na kuwa tayari kununua kile unachouza.
Tumia vitu hivyo viwili ili biashara yako iweze kunufaika na mtandao wa intaneti.

TUMIA SIMU KUUZA.

Simu yako ni nguvu kubwa sana ya kukuwezesha kuwafikia wateja wengi na kuwauzia pia. Itumie simu yako kama kifaa cha masoko na mauzo kwa kuwasiliana na wateja wako kabla na baada ya kununua.
Kila mteja anayefika kwenye biashara yako au anayejibu kutokana na matangazo yanayotolewa na biashara, taarifa zake zinapaswa kuhifadhiwa. Hifadhi namba zao za simu na tengeneza mpango wa kuwa unawapigia simu wateja wako.
Kwa wale ambao hawajanunua wapigie kuwaeleza manufaa ya kile unachouza na kuwashawishi kuja kununua. Kwa ambao wameshanunua wapigie kujua wanaendeleaje na kile walichonunua kimewafaaje.
Kwa kutumia simu yako vizuri utaweza kuwafikia wateja wengi na kuuza zaidi.
Njia bora ya kuandaa mpango huu wa simu ni kurusha matangazo ambayo yanawataka wateja wako kupiga simu, kutuma ujumbe au kuja kwenye biashara yako. Na mteja akishakutafuta, basi tunza mawasiliano yake, hasa simu na hapo utaendelea kuyatumia kwa masoko na mauzo zaidi.

PIMA KILA KITU.

Kila hatua unayochukua kwenye biashara yako, unapaswa kuipima, la sivyo hutaweza kujua kama inaleta matokeo sahihi au la. Usiendeshe biashara yako kwa kubahatisha, badala yake iendeshe kwa kupima kila unachofanya na kisha kufanya maamuzi sahihi kutokana na matokeo unayoyapata baada ya kupima.
Kwenye biashara, mara nyingi unachotaka wewe siyo ambacho soko linataka, unachopenda wewe siyo ambacho soko linapenda. Hivyo acha kujifikiria wewe na angalia soko linapenda nini kisha lipe.
Kama unaendesha matangazo, pima matangazo hayo kwa kutumia njia mbalimbali kama kutumia vichwa vya habari tofauti, kutumia vyombo vya habari tofauti, kutoa ofa tofauti, kutumia bei tofauti na hata kutoa ofa tofauti. Kisha pima matokeo unayopata kwa kila njia unayotumia na ile inayoleta matokeo mazuri ndiyo inakuwa njia kuu.
Kila unachofanya kwenye biashara yako, unapaswa kukipima na kujua matokeo yake. Na hata baada ya kupata matokeo bora kabisa na kuchagua njia kuu, bado unapaswa kuendelea kupima kadiri unavyokwenda ili uweze kujua matokeo unayopata na kama kuna njia bora zaidi basi itumike hiyo.
Unapokuwa unapima, unapaswa kuanza kwa hatua ndogo na ukishapata matokeo basi unakwenda kwenye hatua kubwa. Kwa mfano kama unajaribu tangazo, anza kwa kuwafikia watu wachache kisha ukishaona njia bora ndiyo unapeleka tangazo hilo kwa watu wengi zaidi.

HATUA MBILI ZA KUONGEZA KIPATO CHAKO -----------"Elimu Ya Msingi Ya Fedha "

Rafiki yangu mpendwa, moja ya vitu ambavyo nimekuwa nakusisitizia sana wewe rafiki yangu ni kuwa na vyanzo mbadala vya kukuingizia kipato. Hii ndiyo njia pekee kwako kuweza kupata uhuru kamili wa maisha yako.
Kama kipato chako kinategemea mtu mmoja au wachache basi haupo huru, utalazimika kufanya kile ambacho anayedhibiti kipato chako anakutaka ufanye, hata kama hutaki kukifanya au unaona siyo sahihi kufanya.
Mfano unapokuwa umeajiriwa na chanzo pekee cha kipato chako ni mshahara unaopata kwenye ajira hiyo, unajikuta unakuwa chini ya mwajiri wako, kufanya chochote anachotaka hata kama kwa upande wako siyo kitu sahihi au muhimu kufanya.
Hivyo ili kupata uhuru kamili, ili kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unapaswa kuwa na vyanzo tofauti, kipato chako kusitegemee mtu mmoja au watu wachache.
Zipo njia nyingi sana za kuongeza njia za kuingiza kipato na hatimaye kuongeza kipato chako. Lakini njia zote hizi tunaweza kuzigawa kwenye hatua mbili, ambayo inarahisisha sana uchukuaji hatua wa mtu katika kuongeza kipato.
Hatua ya kwanza; ongeza thamani zaidi pale ulipo sasa.
Hatua ya kwanza ya kuongeza kipato chako ni kuongeza thamani zaidi pale ulipo sasa. Hapa huhitaji kuanza kufanya kitu kipya, bali unaendelea kufanya kile unachofanya sasa, lakini kwa viwango vya juu zaidi ambavyo vinakuwezesha kutengeneza kipato zaidi.
Kama una biashara hapa unakazana kuwahudumia vizuri zaidi wateja ambao tayari unao, kuongeza wateja wapya na kuwapa vitu vipya ambavyo wateja wanahitaji lakini kwako havipatikani.
Kama upo kwenye ajira ni kuongeza thamani unayotoa kwenye ajira hiyo, kwa kuchukua majukumu mengi na makubwa, kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi na kufanya kazi yako kwa viwango vya juu zaidi. Japokuwa kwenye ajira kuna ukomo, bado ni sehemu ya kuanzia ili kuondoka kwenye utumwa huo.
Hatua hii ni muhimu sana kwa kila mtu kuitumia kwa sababu haihitaji uwe na rasilimali za ziada. Mfano watu wengi wamekuwa wanasema wangekuwa na fedha wangeanzisha au kukuza zaidi biashara walizonazo. Kwa kuwa hawapati fedha wanazotaka, basi wanabaki vile walivyo. Kama kila mtu angefanyia kazi hatua hii ya kwanza na kufanya zaidi pale alipo sasa, wangeweza kutengeneza kipato zaidi na kwenda kufanya kile hasa wanachotaka kufanya.
Hatua ya pili; fanya kitu cha tofauti.
Hatua ya pili kwenye kuongeza kipato chako ni kufanya kitu cha tofauti na unachofanya sasa. Hapa ndipo unakwenda kuanza biashara mpya kama huna biashara au kuanza biashara ya tofauti na ile unayofanya sasa au kwenye eneo tofauti na unalofanyia biashara sasa.
Hii ni hatua muhimu na unayopaswa kuichukua kwa umakini, kwa sababu inahitaji maamuzi unayokwenda kuyasimamia kwa muda mrefu. Wengi wamekuwa wanachukua hatua hii bila ya kujitathmini vizuri na kujikuta wametengeneza gereza zaidi kwa kile kipya wanachokwenda kufanya.
Mfano mtu anakwenda kuanzisha biashara mpya wakati biashara anayofanya sasa bado hajaweza kuiendesha vizuri, kinachotokea ni biashara zote mbili kufa. Au mtu anatoka kwenye ajira moja na kwenda kwenye ajira nyingine, kitu ambacho hakibadilishi sana hali yake ya maisha.
Kama unataka kuongeza kipato chako, anzia hapo ulipo sasa na chagua kitu cha kufanya zaidi. Kama ni biashara fikiria wateja wapya unaoweza kuafikia, huduma na bidhaa mpya unazoweza kuwapatia na ubora wa huduma unazotoa. Kama ni kwenye ajira angalia majukumu makubwa zaidi unayoweza kufanyia kazi, muda zaidi unaoweza kuweka kwenye kazi zako na thamani kubwa zaidi unayoweza kuzalisha. Ukishaweka juhudi kubwa kwenye kile unachofanya sasa, ndipo sasa unaweza kufanya kitu cha tofauti.
Kila mtu ana fursa nyingi za kufanya zaidi kwenye kile anachofanya sasa, hebu anza kutumia fursa hizi ili kuongeza kipato chako zaidi.

PATA HASARA MWANZONI KUPATA FAIDA MBELENI.

Kikwazo kikubwa cha ukuaji wa biashara imekuwa kushindwa kumshawishi mteja kununua kwa mara ya kwanza. Hivyo hapa ndipo unapaswa kuweka nguvu zako kubwa.
Kwa sababu tayari una mkakati bora wa kutoa thamani kubwa kwa wateja wako, hawataweza kuona hilo mpaka pale watakaponunua kwako kwa mara ya kwanza.
Swali ni je utawezaje kumshawishi mteja kununua kwako kwa mara ya kwanza, mteja ambaye hajawahi kununua kabisa kwako?
Jibu ni kwa kuondoa vizingiti au vikwazo vyote ambavyo vinamzuia mteja kwa sasa. Kikwazo kikubwa kabisa kimekuwa ni hatari ambayo mteja anaona iko mbele yake, ya kupoteza fedha zake iwapo anachonunua hakitamfaa.
Hatua za kuchukua ni kuwa na mkakati wa kupata hasara mara ya kwanza mteja anaponunua kwako, lakini kwa kuwa utamhudumia vizuri na atarudi tena na tena, basi utaweza kutengeneza faida siku za mbeleni.
Hapa unaweza kutoa zawadi kwa mteja anaponunua kwa mara ya kwanza au kuwa na punguzo fulani. Vyote ni kumfanya achukue hatua ya kununua kwako kama kukujaribu, na akishanunua kwako mara moja, ataendelea kununua.
Zawadi au punguzo unalompa mwanzo linaondoa kabisa ile faida ambayo ungeweza kuipata, lakini anapokuja kununua tena, unatengeneza faida.
Chukua mfano unauza kitu ambacho bei yake ni elfu 10 na faida unayopata ni elfu 3. Mteja ananunua kitu hicho kila mwezi mara moja na unaweza kwenda naye kwa angalau miaka mitatu. Sasa unaweza kumpa mteja wako zawadi au punguzo la hiyo elfu tatu na hata zaidi anaponunua kwa mara ya kwanza. Lakini atakapoendelea kununua, utarudisha faida hiyo na zaidi.
Kabla ya kuchukua hatua hii unapaswa kukokotoa kiasi cha faida unachopata na muda ambao mteja atanunua ili uweze kupata matokeo mazuri.