Tuesday, July 23, 2019

PATA HASARA MWANZONI KUPATA FAIDA MBELENI.

Kikwazo kikubwa cha ukuaji wa biashara imekuwa kushindwa kumshawishi mteja kununua kwa mara ya kwanza. Hivyo hapa ndipo unapaswa kuweka nguvu zako kubwa.
Kwa sababu tayari una mkakati bora wa kutoa thamani kubwa kwa wateja wako, hawataweza kuona hilo mpaka pale watakaponunua kwako kwa mara ya kwanza.
Swali ni je utawezaje kumshawishi mteja kununua kwako kwa mara ya kwanza, mteja ambaye hajawahi kununua kabisa kwako?
Jibu ni kwa kuondoa vizingiti au vikwazo vyote ambavyo vinamzuia mteja kwa sasa. Kikwazo kikubwa kabisa kimekuwa ni hatari ambayo mteja anaona iko mbele yake, ya kupoteza fedha zake iwapo anachonunua hakitamfaa.
Hatua za kuchukua ni kuwa na mkakati wa kupata hasara mara ya kwanza mteja anaponunua kwako, lakini kwa kuwa utamhudumia vizuri na atarudi tena na tena, basi utaweza kutengeneza faida siku za mbeleni.
Hapa unaweza kutoa zawadi kwa mteja anaponunua kwa mara ya kwanza au kuwa na punguzo fulani. Vyote ni kumfanya achukue hatua ya kununua kwako kama kukujaribu, na akishanunua kwako mara moja, ataendelea kununua.
Zawadi au punguzo unalompa mwanzo linaondoa kabisa ile faida ambayo ungeweza kuipata, lakini anapokuja kununua tena, unatengeneza faida.
Chukua mfano unauza kitu ambacho bei yake ni elfu 10 na faida unayopata ni elfu 3. Mteja ananunua kitu hicho kila mwezi mara moja na unaweza kwenda naye kwa angalau miaka mitatu. Sasa unaweza kumpa mteja wako zawadi au punguzo la hiyo elfu tatu na hata zaidi anaponunua kwa mara ya kwanza. Lakini atakapoendelea kununua, utarudisha faida hiyo na zaidi.
Kabla ya kuchukua hatua hii unapaswa kukokotoa kiasi cha faida unachopata na muda ambao mteja atanunua ili uweze kupata matokeo mazuri.

ONDOA KABISA HATARI KWA MTEJA.

Tumeona kikwazo cha wateja kununua kwa mara ya kwanza kwako ni hatari ya kupoteza fedha zao iwapo kitu walichonunua hakitawafaa kama walivyotaka. Tumejifunza njia moja ya kuwapa ofa au zawadi ambayo itawasukuma kununua.

Ipo njia nyingine yenye nguvu zaidi, ambayo ukiitumia lazima mteja anunue. Njia hiyo ni kuondoa kabisa hatari kwa mteja. Yaani hapa unaondoa nafasi yoyote ile ya mteja kupoteza fedha zake, na unakwenda mbele zaidi kwa kumlipa kwa muda au chochote alichopoteza.

Jay anaiita mbinu hii BETTER-THAN-RISK-FREE GUARANTEE (BTRF). Biashara nyingi huwa zinamrudishia mtu fedha aliyonunulia kitu kama hakijamfaa, au kumpa kitu kingine. Sasa wewe unahitaji kwenda zaidi ya hapo, unahitaji kumrejeshea mteja kile alicholipa, lakini pia kumlipa fidia kwa muda aliopoteza au usumbufu uliomsababishia.

Kwa kuwa tayari kumlipa fidia mteja wako pale ambapo hajaridhishwa na ulichomuuzia inaonesha unamjali sana na pia una uhakika sana na kile unachouza. Kadiri mteja anavyopata uhakika wa aina hii, ndivyo anavyokuwa tayari zaidi kununua kile unachouza.

Kama kweli unajali kuhusu wateja wako na kama kweli unaamini kwenye kile unachouza na umechagua kuwazia wateja sahihi, unaweza kutumia mbinu hii na hutapata hasara yoyote. Kwa sababu kwanza utawahudumia wateja sahihi na watakuwa tayari kwenda na wewe kwa muda mrefu.

KUWA NA KITU CHA KUKUTOFAUTISHA NA WENGINE.

Ili kufanikiwa kwenye biashara au chochote unachofanya, unapaswa kujitofautisha na wale wanaofanya kile unachofanya. Hivyo hapa unahitaji kutengeneza utofauti wako na kuwaeleza wateja nini wakija kwako wanapata ambacho hawawezi kupata sehemu nyingine yoyote ile.
Angalia jinsi washindani wako wanafanya mambo yao, kisha wewe kuwa na njia bora zaidi ya kufanya ambayo inawapa wateja thamani kubwa, kisha hakikisha wateja wanajua kuhusu utofauti wako. Njia zote za masoko unazotumia zinapaswa kueleza utofauti wako na wengine, ili wateja washawishike kuja kwako na siyo kwenda kwa wengine.
Baadhi ya maeneo ambayo unaweza kujitofautisha kwenye biashara ni bei, huduma, ubora, upekee, uharaka, uhakika na mengine.
Njia bora ya kujitofautisha ni kuchagua eneo dogo (niche) ambalo utalihudumia vizuri zaidi kuliko kuhangaika na eneo kubwa. Hapa unachagua aina fulani ya wateja, wenye sifa za kipekee ambao utaweza kuwahudumia vizuri na kuachana na wateja wengine wote. Kuachana na wateja wengine huwa ni kitu kigumu kwa wafanyabiashara wengi, lakini unapaswa kukumbuka kwamba huwezi kuwaridhisha watu wote.
Tengeneza ujumbe unaobeba utofauti wako kibiashara na kila unapokutana au kuwasiliana na wateja hakikisha unawapa ujumbe huo. Ujumbe huu unapaswa kurudiwa rudiwa mara nyingi mpaka watu wauelewe na kuihusisha biashara yako na ule utofauti unaotengeneza. Yaani pale mteja anapotaka kitu cha tofauti na kinachomfaa yeye, basi anajua atakipata kwako

JUA UNAKOKWENDA.

Kama hujui unakokwenda, huwezi kufika na hata ukifika hutajua kama umefika. Hatua ya kwanza kuchukua ili kupata unachotaka ni kujua wapi unapokwenda.
Unapaswa kujua kwamba kila mtu kwenye maisha kuna kitu anauza, iwe upo kwenye biashara au ajira, hivyo jua ni nini unachouza na uweze kukiuza vizuri zaidi.
Zipo njia tatu za kukuwezesha kuuza zaidi, kupata wateja wapya, kuuza zaidi kwa wateja ulionao na kuwafanya wateja ulionao waje kununua mara nyingi zaidi.
Kama umeajiriwa, unauza muda wako, utaalamu wako na uzoefu wako kwa mwajiri wako. Na kitu kimoja ambacho kila mwajiri anapenda sana ni mtu ambaye anaweza kutatua matatizo na siyo anayesababisha matatizo.
Chochote unachochagua kufanya, hakikisha unakifanya kwa utofauti mkubwa na wengine wanavyokifanya. Usikubali kufanya kwa mazoea au kuiga kile ambacho wengine wanafanya.
Wape wateja wako urahisi wa kusema ndiyo kwa kile unachouza, kwa kutoa thamani kubwa sana ambayo hawawezi kuipata sehemu nyingine yoyote ile. Yaani unapaswa kutoa thamani kubwa kiasi kwamba mteja atajiona ni mjinga kujaribu kutafuta sehemu nyingine ya kununua.

TATIZO HUJUI UNACHOTAKA.

Pata picha, unataka kuwa na safari, unaondoka nyumbani umebeba mizigo yako na kuelekea kituo cha mabasi. Unakaribishwa na kuulizwa unaenda wapi, unasema popote basi linapokwenda. Je unafikiri basi hilo litakupeleka wapi?
Unaweza kushangaa na kujiuliza inawezekanaje mtu mwenye akili timamu aende kituo cha basi kwa ajili ya safari halafu hajui anakokwenda!
Kabla hujaendelea kushangaa, hebu jiulize kwanza maswali haya muhimu; unakwenda wapi na maisha yako? unakwenda wapi na biashara unayofanya? Unakwenda wapi na kazi uliyonayo? Unakwenda wapi na mahusiano uliyonayo?
Kwa maneno mengine, miaka 5, 10, 20 na zaidi ijayo unajiona wapi? Kama huwezi kutoa jibu moja kwamba unajiona wapi katika vipindi hivyo, kwa hakika huna tofauti na anayeenda kwenye kituo cha mabasi huku akiwa hajui anakwenda wapi.
Na hivi ndivyo watu wengi wanavyoendesha maisha yao, wanakazana sana kufanya chochote wanachofanya, lakini hawajui wanakwenda wapi, hivyo wanafanya leo kama walivyofanya jana, huku kesho ikiwa haipo kwenye mawazo yao kabisa.
Kama mpaka sasa maisha yako huyaelewi, kama umeshajaribu kazi na biashara nyingi lakini bado huoni matokeo mazuri, tatizo lako ni moja, hujui nini hasa unachotaka, hujui wapi hata unakotaka kufika.
Na kama hutachukua hatua ya kwanza muhimu ya kujua kwanza nini unachotaka na wapi unapotaka kufika, hutaweza kuwa na maisha bora. Kila siku utaishia kuyumbishwa kama bendera inayopeperushwa na upepo. Watu watakuja kwako na kila aina ya fursa mpya na utahangaika nazo, na hakuna hata moja itakayokusaidia kufanikiwa.
Jua kwanza ni nini hasa unachotaka, jua ni wapi unakotaka kufika, kisha weka juhudi zako zote katika kufika kule unakotaka kufika. Kuwa kiziwi na kipofu kwa vitu vingine vyote visivyohusiana na kile unachotaka. Usiwe mtu wa kukimbizana na kila aina ya fursa mpya, badala yake weka nguvu kubwa kufika kule unakotaka kufika.
Kujua unachotaka na kuweza kukipata, anza kwa kujiuliza maswali haya muhimu sana;
  1. Mimi ni nani?
  2. Ni nini ninachotaka?
  3. Ni nini kinanipa furaha?
  4. Nini hakinipi furaha?
  5. Uimara wangu uko wapi?
  6. Udhaifu wangu uko wapi?
  7. Ni mchango gani mkubwa naweza kutoa kwa wengine kupitia maisha yangu, kazi yangu, biashara yangu na mahusiano yangu?
Ukijiuliza na kujipa majibu sahihi kwenye maswali hayo saba, na kufanyia kazi majibu hayo, utaweza kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.

Sunday, July 21, 2019

FURSA 31 ZA BIASHARA KATIKA SEKTA YA UJENZI NA MAJUMBA----------------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

 FURSA   katika  SEKTA  YA  UJENZI imenufaisha  wafanyabiashara  wakubwa  duniani. Mfano  mzuri  ni  Rais  wa  Marekani ,  DONALD  TRUMP  ambaye  amepata   UTAJIRI  wake  kwenye  kuwekeza  kwenye  SEKTA  YA  UJENZI  NA  MAJUMBA.Bila  shaka  kutokana  na  tambo  za  bilionea   huyu , Rafiki  yangu , mdau  wangu  utakuwa  umekwisha  sikia  jengo   lenye  jina   la  huyu  mtu  maarufu   la  "  TRUMP  TOWER "  yaani  " MNARA  WA  TRUMP ". Sio  lazima  uwe  na  MTAJI  WA  MAMILIONI  YA  PESA ndio  uwekeze  kwenye  MAJENGO. Unaweza  kuanza  kidogo  na  ukaendelea  kupanua  biashara  yako  kadri  siku  zinavyozidi  kusonga  mbele. Kama  una  LENGO   au   ungetamanai  kuwekeza  kwenye   MAJENGO  endelea  kusoma  na  kujifunza  fursa  zilizopo  kwenye  jukwaa  hili.



MUHIMU : Ili   kuendelea Kusoma na  Kujifunza  Zaidi na  Kugundua  FURSA  mbalimbali  zilizojificha  na  unazoweza  kufanya  katika  
'SEKTA  YA UJENZI   NA  MAJUMBA "jiunge   na   "FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG " ili  usome  MAKALA  mbalimbali   kwa  pamoja  na    " DARASA  LA  SEMINA--FURSA  ZA   BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classrom )---ONLINE   kwa  kulipa  ADA  YA  UANACHAMA ( Tshs 10,000  kwa  Mwezi ) ili   uweze kusoma  MAKALA mbalimbali za  FURSA  na   Kuzigundua na  kujifunza " FURSA  ZINAZOKUZUNGUKA " na  Kuzifanyia  Kazi na  KUFANIKIWA  na   hatimaye  kupata  UTAJIRI.

Utaziona  MAKALA  lakini  hutaweza  kuzifungua  mpaka  uwe  umejiunga  na  kuwa  mwanachama . UTAJIFUNZA  MENGI  SANA kupitia  DARASA  LA  SEMINA.

Kujiunga  tuma   fedha  Tshs  10,000   kwa


  MPESA  NAMBA  0755400128   (  Majina  JAPHET  CHIBAJILO )
        TIGO   PESA   NAMBA   0716924136 ( Majina   Japhet   Masatu )
        AIRTEL  MONEY   0688 361 539  ( Majina  Japhet   Masatu )

Ukishatuma  ADA  tuma  pia  EMAIL  yako  kwa  njia  ya  Meseji kuhusu  malipo tayari  kwa   kuunganishwa.


Ndimi  Rafiki na  Kocha  Wako  Mwl    Japhet  Masatu , Dar  es  salaam ,Tanzania , Afrika   Mashariki , 

Kama  bado    hujajiunga  na  "  FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG " na  "DARASA  LA  SEMINA---FURSA  ZA  BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classroom )  tuwasiliane   Kwa  Maelekezo  Zaidi


WhatsApp /  Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539


Mwl   Japhet   Masatu  ni   Mwalimu  Kitaaluma , Kocha  wa Maisha  na   Mafanikio ,  Mshauri ,  Mjasiriamali.

Mwl   Japhet   Masatu  anaendesha  Mafunzo  Ya  Maisha  na  Mafanikio  kwa   Wale  Waliojitoa  hasa  Kufanikiwa  Kupitia  Programu  ya  "  MAISHA  NA  WEWE "  na  "  FURSA   ZA   BIASHARA   AFRIKA   MASHARIKI "

ULIZA  MASWALI , TOA  MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO  kwa  Email  hii:-  EMAIL fursaafrikamashariki@gmail.com

FURSA 33 ZA BIASHARA KATIKA SEKTA YA KILIMO NA UFUGAJI --------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

 Je, una   Malengo  ya Kufanya  biashara  kwenye   SEKTA  YA  KILIMO ? Tazama  FURSA  zilizopo  kwenye   Sekta  hii  unazoweza  kufanya   bila   MTAJI  mkubwa. SEKTA YA  KILIMO  na  Chakula , ni  moja  ya  biashara  muhimu  sana  kwa  wanadamu  kote  duniani   na  mahitaji  yake   yanaongezeka  kila  kukicha.Hakuna  siku  biashara  hii  itakuja  dorora  na  kuishiwa  FURSA , hii  ni  kwa  sababu  ya  ongezeko  kubwa   la  watu  duniani  hali  inayopelekea  mahitaji  ya  chakula  kuwa  makubwa  kuliko  jana  na  juzi.Hii  ni  sehemu   bora  ya  kutengeneza   mtonyo   mnene. UWEKEZAJI  kwenye  SEKTA  YA  KILIMO  hujumuisha  Kilimo  cha  Mazao  mbalimbali , uzalishaji  na  uuzaji  wa   mazao  mbalimbali  na  KILIMO.



MUHIMU : Ili   kuendelea  Kujifunza  Zaidi na  Kugundua  FURSA  mbalimbali  zilizojificha  na  unazoweza  kufanya  katika  
'SEKTA  YA  KILIMO"jiunge   na   "FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG "  kwa  pamoja  na    " DARASA  LA  SEMINA--FURSA  ZA   BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classrom )   kwa  kulipa  ADA  YA  UANACHAMA ( Tshs 10,000  kwa  Mwezi ) ili   uweze kusoma  MAKALA mbalimbali za  FURSA  na   Kuzigundua na  kujifunza " FURSA  ZINAZOKUZUNGUKA " na  Kuzifanyia  Kazi na  KUFANIKIWA  na   hatimaye  kupata  UTAJIRI.

Utaziona  MAKALA  lakini  hutaweza  kuzifungua  mpaka  uwe  umejiunga  na  kuwa  mwanachama . UTAJIFUNZA  MENGI  SANA kupitia  DARASA  LA  SEMINA.

Kujiunga  tuma   fedha  Tshs  10,000   kwa


  MPESA  NAMBA  0755400128   (  Majina  JAPHET  CHIBAJILO )
        TIGO   PESA   NAMBA   0716924136 ( Majina   Japhet   Masatu )
        AIRTEL  MONEY   0688 361 539  ( Majina  Japhet   Masatu )

Ukishatuma  ADA  tuma  pia  EMAIL  yako  kwa  njia  ya  Meseji kuhusu  malipo tayari  kwa   kuunganishwa.


Ndimi  Rafiki na  Kocha  Wako  Mwl    Japhet  Masatu , Dar  es  salaam ,Tanzania , Afrika   Mashariki , 

Kama  bado    hujajiunga  na  "  FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG " na  "DARASA  LA  SEMINA---FURSA  ZA  BIASHARA  AFRIKA  MASHARIKI " ( Google  Classroom )  tuwasiliane   Kwa  Maelekezo  Zaidi


WhatsApp /  Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539


Mwl   Japhet   Masatu  ni   Mwalimu  Kitaaluma , Kocha  wa Maisha  na   Mafanikio ,  Mshauri ,  Mjasiriamali.

Mwl   Japhet   Masatu  anaendesha  Mafunzo  Ya  Maisha  na  Mafanikio  kwa   Wale  Waliojitoa  hasa  Kufanikiwa  Kupitia  Programu  ya  "  MAISHA  NA  WEWE "  na  "  FURSA   ZA   BIASHARA   AFRIKA   MASHARIKI "

ULIZA  MASWALI , TOA  MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO  kwa  Email  hii:-  EMAIL fursaafrikamashariki@gmail.com