Je , wewe ni mpenzi wa MITINDO ? MITINDO ni
sehemu sahihi kwa MJASIRIAMALI yeyote kwa UWEKEZAJI. Hii ni
kutokana na kubadilika kwake na kuletwa kwa bidhaa mpya ambazo
huifanya kutokupitwa na wakati.Kama unapenda KUTAJIRIKA kwenye
SEKTA YA FASHENI NA MITINDO , basi baki na mimi Kwa Kujiunga
na " DARASA LA SEMINA " ( Google Classroom ).
MUHIMU : Ili
kuendelea Kujifunza Zaidi na Kugundua FURSA mbalimbali
zilizojificha katika
'SEKTA YA FASHENI NA MITINDO " , jiunge na "FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na " DARASA LA SEMINA " ( Google Classrom ) kwa kulipa ADA YA UANACHAMA
( Tshs 10,000 kwa Mwezi ) ili uweze Kuzigundua na kujifunza "
FURSA ZINAZOKUZUNGUKA " na Kuzifanyia Kazi na KUFANIKIWA na hatimaye kupata UYAJIRI.
Ndimi Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam ,Tanzania , Afrika Mashariki ,
Kama
hujajiunga na " FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na "DARASA LA
SEMINA " ( Google Classroom ) tuwasiliane Kwa Maelekezo Zaidi
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
ULIZA MASWALI , TOA MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO kwa Email hii:-
EMAIL : fursaafrikamashariki@gmail.com
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Thursday, July 18, 2019
Wednesday, July 17, 2019
UKOSEFU WA ELIMU YA MSINGI YA FEDHA HUTUPELEKEA KUWA MASKINI . JIFUNZE HAYA USIYOYAJUA KUHUSU ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.
( 1 ).FEDHA SIYO MAKARATASI.
Watu
wengi wamekuwa wanafikiria fedha ni yale makaratasi au sarafu ambazo
tunazishika. Na hapa ndipo wengi wanapokwama, kwa sababu wanakosa ule
msingi muhimu kuhusu fedha. Kwa kukosa msingi muhimu kuhusu fedha, watu
wanashindwa kuzipata kwa wingi na hata kuzitumia vizuri.
Fedha
ni wazo ambalo lina thamani. Fedha ni matokeo ya mtu kuwa na wazo
ambalo linaongeza thamani kwa wengine. Bila ya thamani hakuna fedha.
Hivyo kama unataka fedha zaidi, lazima ujue thamani gani unatoa kwa
wengine.
Kuwa
na chanzo kimoja cha kipato pekee ni utumwa. Huwezi kuondoka kwenye
umasikini kama unategemea kipato chako kitoke sehemu moja pekee. Kama
umeajiriwa pekee, hata kama unalipwa kiasi kikubwa cha fedha, bado
unabaki kwenye umasikini. Kama unafanya biashara na unategemea wateja
wachache nayo pia inakuweka kwenye umasikini.
Utaondoka
kwenye umasikini kwa kuwa na vyanzo vingi vya kipato. Bahari huwa
haikauki kwa sababu mito mingi inaishia kwenye bahari. Hiyo kama unataka
usikaukiwe na fedha, kuwa na vyanzo vingi vya kipato.
(3) MATUMIZI NI BOMU.
Watu
wengi wamekuwa wanaanza maisha na kipato kidogo, na yanaenda. Kipato
kinaongezeka na matumizi yanaongezeka, kila kipato kinapoongezeka na
matumizi pia yanaongezeka. Matumizi ni bomu kama hayatadhibitiwa.
Matumizi yana tabia ya kuongezeka pale tu kipato kinapoongezeka.
Huwezi
kuondoka kwenye umasikini kama huwezi kuyadhibiti matumizi yako.
Haijalishi unatengeneza kipato kikubwa kiasi gani, matumizi ni bomu,
usipolitegua litakulipua.
( 4 ).MADENI NI UTUMWA.
Umesikia
hapo, na najua huenda kimoyomoyo unakataa, unajiambia siyo kweli, kwa
sababu huenda umeshalishwa sumu kwamba bila madeni maisha hayawezi
kwenda. Unajua nini, wale wanaonufaika na madeni ndiyo wanasambaza
propaganda za aina hiyo. Madeni ni utumwa, na huwezi kuondoka kwenye
umasikini kama huwezi kuondokana na madeni.
Kuna
madeni mazuri na mabaya, na masikini wote huwa wapo kwenye madeni
mabaya. Madeni mabaya ndiyo yanawafanya watu kuwa watumwa, wanajikuta
wanafanya kazi sana kulipa madeni, halafu wanakopa tena. Kwa hiyo maisha
yao yote yanakuwa mzunguko wa kopa, lipa, kopa tena.
( 5 ).BIASHARA NI MKOMBOZI.
Zile
zama za nenda shule, soma kwa bidii, faulu na utapata kazi nzuri na
inayolipa zimeshapitwa na wakati. Kila mtu anaona wingi wa watu wenye
sifa za kuajiriwa, lakini hakuna nafasi za ajira. Na hata walioajiriwa,
mazingira ya kazi na hata kipato wanachoingiza hakiridhishi.
Kwa
zama tunazoishi sasa, mkombozi pekee, kitu pekee kitakachokuwezesha
kuwa na maisha mazuri ni kuwa na biashara yako. Hivyo ni muhimu sana uwe
na biashara kama unataka kutoka kwenye umasikini.
( 6 ). UWEKEZAJI NI KIJAKAZI WAKO.
Inapokuja
kwenye fedha, kuna mambo mawili, kuna kuifanyia kazi fedha, pale ambapo
inabidi ufanye kazi ndiyo fedha iingie. Halafu kuna fedha kukufanyia
kazi wewe, ambapo fedha inaingia hata kama hufanyi kazi moja kwa moja.
Ili
kuondoka kwenye umasikini na kufikia uhuru wa kifedha, ni lazima fedha
ziwe zinakufanyia kazi wewe. Na hapa ndipo unapohitaji kuwa na
uwekezaji, ambao unafanya kazi ya kuuzalishia fedha, hata kama wewe
umelala.
( 7 ). KODI NI UWEKEZAJI.
Kodi
ni gharama unayolipa kwa kuishi kwenye jamii iliyostaarabika. Ni kodi
tunazolipa ndiyo zinazoleta huduma mbalimbali tunazozitegemea kwenye
jamii. Huduma za afya, huduma za elimu, ulinzi na usalama, miundombinu
kama barabara na mengineyo ni matokeo ya kodi tunazolipa.
Hivyo
kodi ni uwekezaji ambao kila mmoja wetu anapaswa kuufanya ili tuwe na
jamii bora. Tunapaswa kuondokana na dhana potofu kwamba kodi ni kitu
kibaya. Kwa sababu hebu pata picha, umekazana kutafuta fedha na ukawa
tajiri, halafu unaishi sehemu isiyo salama, je utaweza kufurahia utajiri
wako?
( 8 ).BIMA NI MKOMBOZI.
Kuna
hatari mbalimbali ambazo zinatuzunguka kwenye maisha, na kadiri
unavyopiga hatua kifedha, ndivyo hatari zinakuwa kubwa zaidi. Hili
limekuwa linazua hofu kwa wengi na wakati mwingine kuwazuia hata
kufanikiwa.
Ili
kuondokana na hatari zinazokuzunguka na kukuzuia kuanguka pale
unapokutana na changamoto kubwa, unapaswa kuwa na bima. Kwa bima
unachangia kiasi kidogo cha fedha, lakini unapopata tatizo, unalipwa
kiasi kamili cha fedha au mali ulizopoteza.
( 9 ). WATOTO WAKO HAWAHITAJI FEDHA ZAKO.
Wazazi
wengi wamekuwa wanakazana kutafuta fedha na mali kwa wingi, ili
kuwaachia watoto wao urithi na wasiwe na maisha magumu. Lakini wote
tumekuwa tunaona nini kinatokea baada ya wazazi hao kufariki, utajiri na
mali zote zinapotea, kwa kutumiwa vibaya na watoto walioachwa.
Watoto
wako hawahitaji sana fedha wala mali zako, bali kikubwa wanachohitaji
ni msingi muhimu wa kufuata na kusimamia inapokuja kwenye swala la
fedha. Kuliko uwape watoto fedha bila ya misingi, ni bora uwape misingi
bila ya fedha. Kwa sababu misingi itawawezesha kupata fedha zaidi wakati
fedha pekee bila misingi zitapotea.
( 10 ). KUTOA NI UWEKEZAJI.
Mmoja
wa watu matajiri sana kuwahi kuwepo hapa duniani, John D. Rockefelar
amewahi kunukuliwa akisema unatumia nusu ya kwanza ya maisha yako
kukusanya fedha, halafu nusu ya pili unaitumia kuzigawa fedha hizo
kwenda kwa wengine.
Moja
ya vitu vinavyowafanya matajiri kuendelea kuwa matajiri ni utoaji.
Matajiri wengi wamekuwa watoaji wa misaada mbalimbali ya kijamii na hilo
limekuwa linawasukuma kufanikiwa zaidi kifedha. Hivyo kutoa ni
uwekezaji ambao unamlipa sana mtu baadaye.
Tuesday, July 16, 2019
FURSA 19 KATIKA SEKTA YA ELIMU ----------------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "
Mara kadhaa tumesikia watu wakisema "ELIMU NI UFUNGUO WA MAISHA ". Lakini
ni mara chache sana tumechukua MUDA kutafakari kwa kina
undani wa kauli hii. Pamoja na yote yanayosemwa, ukweli
utabaki kuwa kweli ndio nguzo pekee ya kumsimika mwanadamu
katika maisha.
ELIMU humpatia mtu msingi wa kifikra na maarifa stahiki ya kuweza kupambanua maisha , kufanya kazi vyema na kuwasiliana na watu. Tukiachlia hayo , elimu ina faida nyingi sana , elimu itakufanya uishi maisha yenye FURAHA, UHURU , KUJITEGEMEA , KUTAFSIRI NDOTO zako , ELIMU itakufanya ujiamini hasa pale unapoongea na watu, hukuunganisha na dunia , kuelewa tamaduni mbalimbali za watu duniani , pamoja na kukutayarisha kuwa na mafanikio. SEKTA YA ELIMU ni sekta ya mabilioni ya pesa duniani kote. Vile vile ni sekta pana na iliyojigawa sana kati ya sekta zote naweza kusema.Ukianzia shule za awali , shule za msingi , shule za kati , sekondari , vyuo vya ufundi kama vile VETA , vyuo vya ualimu na vyuo vikuu utagundua ukweli kuwa ukubwa wa sekta hii unabainisha wazi kabisa FURSA zilizopo kwenye SEKTA YA ELIMU . Kwa ufupi ebu tuangalie fursa zilizopo kwenye sekta ya elimu ambazo wewe MJASIRIAMALI unaweza kufanya leo na kupata UTAJIRI
MUHIMU : Ili kuendelea Kujifunza Zaidi na Kugundua FURSA mbalimbali zilizojificha katika
'SEKTA YA ELIMU " , jiunge na "FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na " DARASA LA SEMINA " ( Google Classrom ) kwa kulipa ADA YA UANACHAMA ( Tshs 10000 kwa Mwezi ) ili uweze Kuzigundua na kujifunza " FURSA ZINAZOKUZUNGUKA " na Kuzifanyia Kazi na KUFANIKIWA na hatimaye kupata UYAJIRI.
Ndimi Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam ,Tanzania , Afrika Mashariki ,
Kama hujajiunga na " FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na "DARASA LA SEMINA " ( Google Classroom ) tuwasiliane Kwa Maelekezo Zaidi
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
ULIZA MASWALI , TOA MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO kwa Email hii:- EMAIL : fursaafrikamashariki@gmail.com

Monday, July 15, 2019
NJIA PEKEE YA KUJIHAKIKISHA USALAMA KWENYE KAZI AU BIASHARA YAKO.
“In
today’s competitive economy, it’s not enough to simply do your job
well. Developing a reputation as an expert in your field attracts people
who want to hire you, do business with you and your company, and spread
your ideas. It’s the ultimate form of career insurance.” ― Dorie Clark
Wakati
mapinduzi ya viwanda yanaanza, watu waliambiwa ili kuwa na usalama wa
kazi basi soma kwa bidii, faulu sana na utapata kazi nzuri ambayo
utaifanya mpaka kustaafu kwako na hapo utalipwa mafao ya kukuwezesha
kuishi mpaka uzeeni.
Mapinduzi
ya viwanda yamefika tamati na sasa tupo kwenye mapinduzi ya taarifa.
Katika zama hizi uhakika pekee wa wewe kuwa na usalama kwenye kazi au
biashara siyo tu elimu au taaluma uliyonayo, bali kutengeneza ubobezi
kwenye kile unachofanya kiasi kwamba watu watapenda kufanya kazi na
wewe.
Unapaswa
kujijengea sifa ya ubobezi wa hali ya juu kwenye kile unachofanya kiasi
kwamba kila mwenye uhitaji unaohusu unachofanya anakufikiria wewe au
anaambiwa waje kwako.
Na
hilo linawezekana kama utaweka juhudi katika kujua vizuri kile
unachofanya, kukifanya vizuri na pia kutengeneza mtandao wa watu
wanaojua kuhusu unachofanya na hivyo kusambaza sifa zako kwa wengine
wengi.
JINSI YA KUPATA WAZO LA TOFAUTI NA WENGINE NA KUFANIKIWA
Katika kupata wazo bora, zingatia mambo yafuatayo;
Moja; anza na chochote unachojali sana.
Watu
wengi wamekuwa wanafikiria kwamba ili uweze kuleta mabadiliko makubwa
kwako na kwa wengine basi inabidi uwe na wazo kubwa na la kipekee sana.
Wazo ambalo wengine hawajawahi kuwa nalo. Huo siyo ukweli, unaweza
kuanza na wazo lolote na ukaweza kulijenga kwa utofauti na
ukajitofautisha sana.
Anza
na chochote unachojali, unachopenda, unachoamini, unachojua, ulichozoea
au ambacho umesomea. Chochote kile ambacho unaona kinaweza kuwa bora
zaidi ya kilivyo sasa, unaweza kukichukua kama wazo lako la kufanyia
kazi.
Mbili; uliza maswali ambayo hayaulizwi.
Watu
wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea kwa sababu wanafanya kile ambacho
kila mtu anafanya, na hawathubutu kujaribu vitu vya tofauti. Sasa kwa
wazo unalotaka kufanyia kazi kuliboresha zaidi, anza kwa kuuliza maswali
ambayo watu wengine hawaulizi.
Maswali
hayo yanaweza kuwa, vipi kama.... vipi kinyume cha... Hapa unajaribu
kupata picha ya tofauti na wengi walivyozoea, kwa kuona upande wa pili
wa vitu au kwa namna ya tofauti.
Tatu; angalia uzoefu wako binafsi.
Baada
ya kujiuliza maswali ya tofauti kwenye wazo unalotaka kufanyia kazi,
angalia uzoefu wako binafsi kwenye wazo hilo. Usijidharau kwa sababu
labda huna elimu kubwa au uzoefu mkubwa kwenye jambo hilo. Labda siku za
nyuma umewahi kujaribu kufanya tofauti na ukapata matokeo ya tofauti,
hiyo inatosha kukuonesha kwamba kuna uwezekano wa kupata matokeo tofauti
na ambayo watu wanapata sasa.
Nne; chagua eneo la ubobezi kwenye wazo lako.
Wazo
unalokuwa nalo linaweza kuwa pana, sasa unahitaji kuchagua eneo ambalo
utabobea kwenye wazo hilo ili kujitofautisha kabisa na wengine. Badala
ya kutaka kufanya kila kitu, unachagua eneo moja ambalo utaweka muda na
nguvu zako na kuweza kutengeneza ubobezi mkubwa. Ni kupitia ubobezi huu
ndiyo unaweza kupiga hatua kubwa kwenye wazo hilo.
Tano; fanya utafiti.
Watu
wengi wamekuwa wanapata mawazo mapya ya kuboresha zaidi, lakini
hawanufaiki nayo kwa sababu huwa hawaweki kazi inayopaswa kuwekwa ili
mtu kubobea kwenye kitu hicho. Moja ya kazi kubwa unayopaswa kuweka ni
kufanya utafiti. Siyo kusoma tafiti, badala yake kufanya utafiti mpya,
kwa kuangalia yale maeneo ambayo unataka yawe bora kisha kuja na njia
bora za kuyaboresha kutoka kwenye tafiti mbalimbali zinazogusa wazo
hilo.
Sita; unganisha mawazo.
Kuna
maeneo mengine ambayo yameweza kupiga hatua kubwa, ambayo ni tofauti na
wazo unalofanyia kazi wewe. hii haikuzuii wewe kujifunza kutoka maeneo
hayo. Jifunze kupitia maeneo mbalimbali kwa hatua ambazo watu wameweza
kupiga, kisha unganisha mawazo hayo na wazo unalofanyia kazi kuweza
kuona jinsi gani ya kuboresha wazo unalofanyia kazi. Kumbuka misingi ya
mafanikio kwenye kila eneo inafanana, hivyo kwa kuangalia jinsi ambavyo
mawazo mengine yamefanikiwa, utaweza kufanikisha wazo lako pia.
Saba; tengeneza nguzo ya kubeba wazo lako jipya.
Baada
ya kuchagua wazo unalotaka kuboresha, ukauliza maswali ya tofauti,
ukatumia uzoefu wako, ukafanya utafiti na hata kujifunza kutoka maeneo
mengine, unakuwa umejifunza mambo mengi sana kuhusiana na wazo lako
jipya. Hapa unakuwa na maarifa na taarifa nyingi ambazo mtu mwingine
siyo rahisi kuyaelewa. Hivyo ili wazo lako la kuboresha liweze kueleweka
na kutumiwa na wengine, unahitaji kutengeneza nguzo ya kubeba wazo
lako. Hapa unatengeneza mfumo unaobeba wazo lako jipya, kwa namna ambayo
watu wengine wanaelewa jinsi linavyofanya kazi na matokeo ya tofauti
yanavyopatikana.
Kwa
hatua hizo saba, unakuwa umekamilisha wazo lako la tofauti, ambalo
linaleta matokeo bora kuliko yale ambayo yamezoeleka. Baada ya hapo sasa
unakwenda kwenye hatua ya pili ambayo ni kujenga wafuasi kwenye wazo
lako.
FURAHA ZAO LA FEDHA-------------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "
Ile kauli kwamba matajiri hawana furaha au huwezi kuwa na fedha na
ukawa na furaha, ni mtego ambao watu wamekuwa wanajitengenezea wenyewe
bila ya kujua.
Ipo hivi rafiki, wengi tunapokuwa tunaanzia chini, huwa tunafikiri tutakapopata fedha basi ndiyo zitakuwa jawabu la kila kitu. Hivyo tunaahirisha maisha yetu yote mpaka pale tutakapopata fedha.
Na hata kwa upande wa furaha, tunaahirisha furaha yetu tukiamini tukishakuwa na fedha basi ndiyo tutakuwa na furaha. Tunaacha kufanya yale mambo madogo madogo ya kila siku ambayo yanatuletea furaha, tukiamini kwamba tukishakuwa na fedha nyingi, basi furaha itakuja yenyewe.
Lakini hilo ni kinyume kabisa na msingi wa furaha, fedha haileti furaha, bali furaha inaleta fedha. Kwa kifupi ni kwamba fedha ni zao la furaha, na siyo kama wengi wanavyofikiri kwamba furaha ni zao la fedha.
Hivyo basi, usiahirishe furaha yako sasa kwa sababu unatafuta kwanza fedha na unafikiri ukishakuwa nayo basi utapata furaha. Badala yake ishi maisha yako kamili sasa, fanya vile vitu vidogo vidogo vinavyoleta furaha kwenye maisha yako na hivi vitakuwezesha kupata fedha zaidi na kwa kutokutumia nguvu kubwa kama unavyofanya unapokuwa huna furaha.
Usipuuze kitu chochote muhimu kwenye maisha yako kwa sababu unakazana kupata fedha, weka kipaumbele chako kwenye furaha na fedha itakuwa matokeo.
Jipende wewe mwenyewe kwanza, fanya kile unachopenda na zungukwa na wale wanaokupenda, haya yatakuletea furaha na furaha yako itavutia fedha zaidi kwako.
Fuata hili na hutafikia kwenye hali ya wengi ambao wana fedha lakini hawana furaha, wewe tayari unayo kanuni ya kuwa na furaha na kuwa na utajiri kwa wakati mmoja. Ifanyie kazi.

Subscribe to:
Posts (Atom)