Kwenye
moja ya tafiti ambazo Daniel ametumia kwenye kitabu chake, inaonesha
kwamba wale ambao wako kwenye umasikini mkubwa, ambao wanaishi chini ya
kiwango cha kawaida cha maisha, wanakuwa na wakati mwingi wa kukosa
furaha kuliko ambao hawapo kwenye ufukara.
Mfano
kitendo tu cha kuumwa na kichwa, kinawapelekea walio kwenye ufukara
kupatwa na wasiwasi zaidi kuliko ambao hawapo kwenye ufukara.
Katika
changamoto za kawaida za maisha, kama kuumwa, kufukuzwa kazi, biashara
kufa, kutengana na mwenza, zinawaumiza zaidi walio kwenye umasikini
kuliko wale ambao hawapo kwenye umasikini.
Na
kikubwa zaidi ambacho Daniel ametushirikisha kwenye hili ni kwamba kwa
walio masikini, maamuzi yoyote anayofanya ni ya kupoteza.
Iko
hivi, sisi binadamu huwa tunaepuka hali ya kupoteza na kupenda hali ya
kupata. Hivyo hatua yoyote ya kupoteza tunayochukua, huwa tunajisikia
vibaya na hilo linachangia kukosa furaha.
Kwa
kuwa masikini ana uhaba wa fedha, kila fedha aliyonayo haimtoshi, hivyo
akitumia fedha hiyo kupata kitu fulani, anakuwa amechagua kukosa kitu
kingine. Una elfu 5 mfukoni, unataka kwenda kujiburudisha mahali,
ungependa kununua chakula na kinywaji, lakini fedha hiyo haitoshi, hivyo
utaishia kupata chakula tu, au kinywaji tu.
Haijalishi
chakula utakachopata au kinywaji utakachokunywa kitakuwa kizuri kiasi
gani, akili yako haitaangalia kile ulichopata, bali itafikiria kile
ulichokosa. Hilo ndiyo linachangia hali ya kukosa furaha kwa walio
masikini.
Maumivu
ya kukosa ni makubwa kuliko raha ya kupata. Ukipoteza elfu 10, utaumia
kuliko raha utakayoipata kwa kuokota kiasi hicho hicho cha fedha.
No comments:
Post a Comment