Kwa kelele za dunia ni mihangaiko yetu
ya kila siku ni rahisi sana kusahau kusudi la maisha yako. Na
ukishasahau kusudi la maisha yako, huna tofauti na meli ambayo haina
uelekeo. Unaweza kwenda kasi sana, lakini haitakusaidia, kwa sababu
unakuwa tayari umeshapotea.
Unapofika mwisho wa mwaka jikumbushe
kusudi la maisha yako, jikumbushe kwa nini upo hapa duniani, jikumbushe
nini kinakusukuma kutoka kitandani kila asubuhi.
Kusudi la maisha yako ndiyo linapaswa
kukupa msukumo wa kufanya makubwa. Na unapolikumbuka mara zote,
linakuwezesha kuchukua hatua sahihi ili kuweza kulitimiza.
Jikumbushe kusudi la maisha yako na jiulize yale unayofanya yanachangiaje kwenye kufikia kusudi la maisha yako.
HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA !
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment