Ili uweze kufanikiwa, unapaswa kuzitawala hisia na mawazo yako kila wakati. Hupaswi kuruhusu mawazo hasi kuingia kwenye akili yako. Hisia hasi kama za hasira, wivu, huzuni, hofu na hata kukata tamaa, hazipaswi kupata nafasi ndani yako.
Unapaswa kuwa bize na malengo na mipango yako ya kila siku kiasi kwamba mawazo na hisia hasi havipati nafasi kabisa kwenye akili yako. Na ukiweza kufanya hivi hutapata nafasi ya kuwa na huzuni au kupata sonona.
Zoezi la kufanya; kila wakati kagua mawazo na hisia ambazo unazo, je ni
hasi au chanya. Kama ni hasi badili mara moja kwenda chanya. Huwezi
kufanikiwa ukiwa na mawazo na hisia hasi. Lazimisha akili yako ifikiri
chana na mara zote jiweke kwenye hisia chanya. Hili litakuwezesha kuona
matumaini na kujituma zaidi.
No comments:
Post a Comment