Saturday, July 10, 2021

TUMIA MBINU HIZI SIKU ZOTE KUPAMBANA NA CHANGAMOTO YOYOTE MBELE YAKO.

HAKIKISHA! Siku Zote Unapopambana Na Changamoto Yoyote Ile Usisahau Kutumia Mbinu Hizi Muhimu Zenye Matokeo Ya Haraka…!

Rafiki yangu mpendwa,

Katika maisha lazima ujue kila wakati unaweza kukutana na changamoto.

Na watu wanasema kila ukitoka kwenye changamoto moja utaingia kwenye changamoto nyingine, duniani hapa kama hauko kwenye changamoto basi utakuwa umetoka kwenye changamoto au unaelekea kwenye changamoto nyingine.

Shida sio changamoto unazokutana nazo, tatizo kubwa ambalo watu linawakabili ni namna ya kushughulika na changamoto ambazo zile zinatokea katika maisha yao.

Na Leo lingependa nikwambie namna ambavyo unaweza kutoka kwenye changamoto yoyote inayokukabili, inawezekana leo upo kwenye changamoto kwenye taaluma yako inawezekana leo upo kwenye changamoto ya mahusiano yako au upo kwenye changamoto ya kiuchumi, au upo kwenye changamoto ya kazi, kazi unayofanya au eneo lako la kiofisi au kwenye biashara yako.

Bila kujali upo kwenye changamoto ipi kuna maeneo manne ukiweza kuyazingatia yatakusaidia sana kutoka kwenye changamoto yako tena kwa haraka.

Kumbuka tena washindi ni wale ambao wakipita kwenye changamoto wanaondoka kwenye changamoto zao kwa haraka sana bila kuchelewa.

Jambo La Kwanza; Ambalo unatakiwa kulifahamu katika maisha yako ni kwamba unapopitia changamoto USIKUBALI ile hali ya kujiambia changamoto yako ni SPESHO.

Changamoto SPESHO, maana yake ni kuna watu wanafikiri wanapopitia matatizo ni wao ndio wa kwanza kupitia katika matatizo hayo na hakuna mtu mwingine yeyote aliyepitia katika changamoto hiyo.

SI KWELI, ukiwa na fikra ya namna hiyo utashindwa kabisa kukabiliana na changamoto yako.

Changamoto yoyote leo unayokutana nayo, cha kwanza ambacho ningependa nikuambie. Kuna mtu ameshawahi kukutana na changamoto kama hiyo, na katika wale waliokutana na changamoto kama hizo hakika wako ambao wameshinda hizo changamoto.

Lakini kuna mtu leo anapitia changamoto kama ya kwako na hakika anaweza akashinda pia, wewe ukajua na kufikiri kwamba changamoto yako ni SPESHO na hakuna mtu ambaye anachangamoto kama ya kwako, hakika hautavuka, hautatoka katika hiyo changamoto.

Kuna watu ambao wakipitia matatizo wanaona changamoto yao hakuna mtu mwingine yeyote mwenye nayo. Wanaona kama lile tatizo ndio mara yao ya kwanza wanalipitia duniani yaani ni kama limevumbuliwa hakuna mtu mwingine ambaye amekutana nalo.

SI KWELI, usikubali hata siku moja kwamba changamoto yako ni SPESHO hakuna mtu mwenye changamoto kama hiyo, ukiwa na fikra kwamba changamoto yako ni spesho , hautapata uvumbuzi mapema na utaona hakuna msaada.

Cha kwanza kabisa kataa fikra inayokuambia changamoto yangu ni spesho hakuna mtu kama mimi, mtu aliyopo kama mimi, hakuna mtu aliyepata matatizo kama mimi.

SI KWELI, wako wengi na wameshinda na wewe unaweza kuishinda.

Jambo La Pili; Unalotakiwa kulifahamu ni kwamba changamoto yoyote unayopitia ni SAIZI YAKO, watu wengi ambao changamoto zinawazidi sio kwa sababu wanashindwa kuzitatua kwa sababu walikata tamaa.

Ningependa nikuambie changamoto yoyote ile unayokabiliana nayo leo ya KIFEDHA, ya KIMAHUSIANO, ya KITAALUMA, KAZINI KWAKO au kwenye BIASHARA, inawezekana kabisa umekosa usingizi kabisa kwa sababu ya changamoto inayokukabili.

Ninachotaka nikuhakikishie ni kwamba changamoto hiyo unayokutana nayo leo ni SAIZI YAKO.

Ukiwa na fikra ya namna hiyo tafsiri yake ni kwamba utafanya kila unachoweza, kuweza kukabiliana nayo, unapokubali kwamba changamoto hii ni SAIZI YAKO. Unaulazimisha ubongo wako kutafuta suluhisho unaposema changamoto hii imenizidi umri unauambia ubongo wako ila tu kwa sababu hakuna kitu ninaweza kufanya.

Ninachotaka kukuambia ni kwamba changamoto ni saizi yako, ya mambo unayopitia leo.

Jambo La tatu; Ambalo ni la msingi sana, kulijua katika kutoka kwenye changamoto unayokutana nayo ni kujua katika kila changamoto KUNA MLANGO WA KUTOKEA, kuna njia za wewe kutoka kwenye changamoto ukweli ni kwamba hukuuona huo mlango wakutokea.

Ukweli ni kwamba haujaona njia za kutoka kwenye changamoto zinazokukabili haimaanishi kwamba changamoto yako imekosa suluhisho, kuna suluhisho kwenye changamoto yako inawezekana haujaiona ndio maana tunasema kama leo unapitia changamoto usikubali tu kukaa nyumbani, usikubali tu kukaa ndani, usikubali kujifungia, tafuta watu uzungumze nao, nenda mahali toka nje fuatilia kitu fulani utapata suluhisho.

Hakuna changamoto ambayo haina suluhisho katika maisha hata ya kwako, iwe inawezekana umefika sehemu unasema kwamba nimejaribu kila nilichofanya kupata suluhisho.

SI KWELI, changamoto uliyonayo ina suluhisho kama hutokata tamaa utapata suluhisho ya changamoto yako.

Jambo La Mwisho; Ambalo litakusaidia kutoka kwenye changamoto ambayo inakukabili sasa hivi kwa haraka sana nikijua kwamba changamoto zinapokuja saa zingine zinatuepusha na mabaya makubwa ambayo hatuyaoni.

Kuna watu wengi sana wanapitia changamoto za mahusiano na kusema yule nilimpenda sana, nikajitolea na leo hayupo tena kwenye maisha yangu, kuja kugundua kwamba hapana kumbe ni sababu ya wao kupata watu sahihi zaidi, kuna watu walifukuzwa kazi, kuna watu waliondolewa ofisini kwa kudhalilishwa lakini leo wanamiliki makampuni yao au wengine wamepata kazi kubwa zaidi.

Kwa hiyo kila wakati unapokutana na changamoto uwe na jicho la ziada la kuangalia usiangalie kile tu ulichokosa lakini pia kuna kitu ambacho kiko leo.

Kwa nini inakuwa hivyo mara nyingine tukiambiwa tuache vya sasa hivi tulivyonavyo ili tupate bora, tulivyoandaliwa mbele yetu hatutakuwa tayari kufanya maamuzi magumu ya namna hiyo kwa sababu yanatuumiza, lakini changamoto zinakuja pia kutuepusha na mabaya ambayo kwa macho ya kawaida hatuyaoni, ndio maana changamoto unayopitia leo ni mbaya na inakuumiza sana.

Lakini kesho utamshukuru mungu na kusema afadhali nimepitia hii changamoto. Kwa sababu imenisaidia kuwa hivi nilivyo sasa.

 KAZI   KWAKO   MDAU  WANGU .

TUWASILIANE   KWA 

 ( WhatsApp  + 255 716924136 )  kwa  USHAURI NA  MAONI  YAKO   WEWE  UNASEMAJE ??

JINSI MITANDAO YA KIJAMII INAVYOHARIBU AKILI YAKO NA JINSI YA KUEPUKA HILO.

Rafiki yangu mpendwa, mdau  wangu 
Ugunduzi wa mtandao wa intaneti yalikuwa ni mapinduzi makubwa mno kwenye maendeleo ya binadamu.
Kwani mtandao huo ulileta uhuru wa kila mtu kuweza kuwasiliana na yeyote akiwa popote.

Watu waliamini mtandao wa intaneti utaleta demokrasia na uhuru wa kweli, ambapo kila mtu anaweza kujifunza chochote anachotaka, anaweza kuwasiliana na yeyote na anaweza kushirikisha maoni yake bila kuzuiwa na yeyote.

Lakini ndoto hizo zimekuja kuyeyuka baada ya kugunduliwa kwa mitandao ya kijamii na simu janja.
Mitandao hii ambayo ilianza kama vitu tu vya watoto na vijana, sasa imepenyeza kwenye maisha ya walio wengi na imekuwa na madhara makubwa.




Mitandao ya kijamii imeharibu akili za wengi kwa njia mbalimbali, leo tunakwenda kuangalia njia moja ambayo ina madhara makubwa kwako na kikwazo kwa mafanikio yako.
Njia hiyo ni kutaka raha ya haraka (instant gratification).

Iko hivi rafiki, ili uweze kufikia mafanikio makubwa, lazima uwe tayari kuchelewesha raha (delayed gratification). Uweze kuweka juhudi kubwa mwanzoni na kuwa na subira kabla hujaanza kupata raha.

Hilo linajengwa na ukomavu wa kiakili, ambapo unaweza kuweka umakini wako kwenye jambo moja kwa muda mrefu bila ya kuhama hama.
Hicho ndicho ambacho mitandao ya kijamii inakwenda kuvunja na kukufanya uwe na uteja kwenye mitandao hiyo, kwa sababu unaitegemea ili kupata raha ya muda mfupi.

Muuzaji mkubwa wa madawa ya kulevya ambaye aliachana na biashara hiyo baada ya kufungwa kwa muda mrefu aliulizwa ni jinsi gani walikuwa wanapata wateja wengi wa kuwauzia madawa ya kulevya.
Muuzaji huyo alijibu walikuwa wakienda kwenye mji, wanawakusanya watumiaji wengi wa madawa kisha wanawapa ofa ya bure.
Haichukui muda watu hao wanakuwa wateja wao wa kudumu, kwa sababu madawa yanajenga uraibu kwao.

Hivyo pia ndivyo mitandao ya kijamii inaharibu akili yako, kwa kujenga uraibu wa kulata raha ya haraka.
Kabla ya ujio wa mitandao ya kijamii, watu waliweza kuweka muda wa kutosha kwenye kusoma vitabu au kufanya mazungumzo na wengine.
Lakini sasa mtu hawezi kusoma hata kurasa kumi kabla hajagusa simu yake. Watu wanaweza kuwa hawajaonana miaka lakini wanapokutana baada ya salamu kila mtu anahangaika na simu yake.

Kukufanya utake raha ya muda mfupi na kuwa tegemezi kwa mitandao hiyo kupata raha hiyo ndiyo madhara makubwa sana ya mitandao ya kijamii kwenye akili yako.
Hili linavunja kabisa ustahimilivu wako, ambao unahitajika sana ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako.

Akili yako ikishaharibiwa na mitandao ya kijamii, uwezo wako wa kuweka vipaumbele sahihi kwenye maisha yako unaharibiwa kabisa.
Unakuwa huwezi tena kuweka umakini wako kwa muda mrefu kwa yale ambayo ni sahihi kwako.
Mitandao hiyo inakujengea hofu ya uongo, hofu ya kwamba kuna kitu unakosa kama hujaingia kwenye mitandao hiyo hata ndani ya muda mfupi tu.

Tatizo kubwa zaidi ni kwamba hakuna anayeliona na kulizungumzia tatizo hili wazi wazi. Wanasema kulijua tatizo ni nusu ya kulitatua. Wengi ambao akili zao zimeshaharibiwa na mitandao ya kijamii hawajui hata kama wana tatizo. Wao wanaona ni sehemu ya kawaida ya maisha yao, kumbe wameshageuzwa kuwa tegemezi kwenye mitandao hiyo.

Tatizo hilo halizungumziwi kwa sababu wengi hawana uelewa na wale wanaomiliki mitandao hiyo wanapima mafanikio kwa idadi ya walio tegemezi kwenye mitandao hiyo.
Hivyo hili linabaki kuwa wajibu wako mwenyewe kama hutaki liendelee kuwa na madhara kwako.

Mitandao ya kijamii imeajiri watu wenye elimu kubwa kwa lengo moja tu, kuteka umakini wako na kukufanya kuwa tegemezi.

Ni wakati wa kuwa huru sasa na kushika hatamu ya maisha yako ili uweze kufika kwenye mafanikio makubwa.

Chukua hatua sasa maana kadiri unavyochelewa, ndivyo mitandao hiyo inavyozidi kutawala na kuharibu akili yako. JIUNGE   SASA  NA  " DARASA  ONLINE "   uanze  kubadili maisha yako.

Rafiki yako mpendwa

KOCHA  MWL.  JAPHET  MASATU , DAR  ES  SALAAM, TANZANIA

 WASILIANA   NAMI  SASA

 

 ( WhatsApp + 255 716  924136  )  / + 255 755 400 128

 

AFYA NI MTAJI NAMBA MOJA UNAOPASWA KUUJENGA NA KUULINDA ILI KUFANIKIWA.

Rafiki yangu mpendwa, mdau wangu
Mtaji umekuwa sababu ambayo wengi wanaitumia kama kikwazo kwao kufanikiwa.
Na wengi wanapozungumzia mtaji, huwa wanaangalia mtaji wa aina moja tu, fedha.

Kuna mitaji mingine muhimu ambayo mtu anakuwa nayo na anaweza kuitumia kufanya makubwa kwenye maisha yake, lakini haitambui wala kuitumia.
Anang’ang’ana na mtaji mmoja tu, ambao hata akiupata bado changamoto kwake haziishi.

Leo nakwenda kukushirikisha aina nyingine ya mtaji ambao unapaswa kujijengea na kuulinda ili uweze kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Kabla sijakuambia mtaji huo ni upi, kwanza nikupe taarifa muhimu kuhusu mafanikio, ambazo wengi wamekuwa hawakupi.

MOJA; mafanikio yanataka uweze kufanya maamuzi bora na haraka kuliko wengine. Maamuzi yanawatofautisha sana wanaofanikiwa na wanaoshindwa.

MBILI; mafanikio yanataka uweze kufanya kazi kwa juhudi kubwa na kwa muda mrefu kuliko wengine. Haijalishi unafanya nini, juhudi zinahitajika sana.

TATU; mafanikio yanakutaka uwe na uvumilivu mkubwa licha ya kupitia magumu na kukatishwa tamaa. Wanaofanikiwa siyo kwamba njia yao inakuwa rahisi, ila wanakuwa wagumu kuliko magumu wanayokutana nayo.

Vitu hivyo vitatu ni muhimu kuliko kingine chochote kwako kufanikiwa. Kufanya maamuzi sahihi, kuweka juhudi kuwa na kuwa mvumilivu.
Vyote hivi vitatu ni zao la AFYA.
Na hiyo AFYA ndiyo mtaji muhimu mno kwako kuweza kufanikiwa.
Bila ya afya bora, hakuna makubwa unayoweza kufanya kwenye maisha yako.




Wengi hudhani afya ni kutokuwa na magonjwa, lakini hilo siyo kweli.
Shirika la afya duniani linaeleza afya kama kuwa vizuri kimwili, kiakili, kiroho, kijamii na kiuchumi.
Kwa maana hiyo ya afya, unaweza kuwa huna ugonjwa wowote, lakini bado afya yako ikawa siyo nzuri.

Unaweza kujionea hapa ni kwa nini afya ndiyo mtaji muhimu kwako kufikia mafanikio makubwa, kwa sababu imegusa kila eneo la maisha.

Ili uweze kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako, unapaswa kujenga afya yako kwenye maeneo haya matano.

( 1 ).  MWILI.
Mwili wako ndiyo hekalu la maisha yako, ndiyo gari la kukufikisha kwenye mafanikio yako makubwa.
Bila mwili imara, hutaweza kuweka juhudi za kutosha ili uweze kufanikiwa.
Maana mafanikio yanakutaka uweke juhudi kubwa na kwa muda mrefu.
Jenga afya yako ya mwili kwa kuwa na ulaji mzuri, kufanya mazoezi na kupata muda wa kupumzika.
Linda afya yako ya mwili kwa kuepuka magonjwa na tabia hatarishi.
Mwili unapokuwa imara, unaweza kuendesha mapambano ya mafanikio.

( 2 ). AKILI.
Akili yako ndiyo inayofanya maamuzi, mafanikio yanahitaji sana maamuzi sahihi kwenye maisha. Hivyo ni muhimu kuijenga afya ya akili ili uweze kufanya maamuzi bora kwenye maisha yako.
Jenga afya yako ya akili kwa kuilisha maarifa sahihi na kufanya mazoezi ya kufikiri kwa kina katika hali mbalimbali. Pia kuwa na muda wa kutafakari mambo yako.
Linda afya yako ya akili kwa kuepuka habari hasi, vilevi mbalimbali na mitandao ya kijamii. Vyote hivyo vinadhoofisha akili yako na kuifanya isiweze kufanya maamuzi bora.
Bila ya maamuzi bora, mafanikio yatakuwa magumu kwako.

( 3 ). ROHO.
Roho yako ndiyo kichocheo cha wewe kuendelea na safari ya mafanikio hata pale unapokutana na magumu yanayokatisha tamaa. Kama haupo imara kiroho, hutaiweza safari ya mafanikio kwa sababu ina magumu na inakatisha sana tamaa.
Jijengee afya ya kiroho kwa kusali, kufanya tahajudi na kuwa na imani imara.
Linda afya yako ya kiroho kwa kuepuka waliokata tamaa na wasiokuwa na imani, maana mambo hayo huambukizwa kwa urahisi.

( 4 ). UCHUMI.
Uchumi ni eneo muhimu kinalokupa utulivu wa kuyaendesha maisha yako. Kama hujui kesho utapata wapi fedha ya kula, akili yako haiwezi kutulia kwenye mafanikio makubwa unayotaka kufikia.
Hivyo unapaswa kujenga afya yako ya kiuchumi ili uwe na uhakika wa kuyaendesha maisha yako wakati unaendelea kupambana na mafanikio.
Kujenga afya yako ya kiuchumi hakikisha una akiba ya kuweza kuyaendesha maisha yako kwa angalau miezi sita hata kama utapoteza kipato unachoingiza sasa.
Kulinda afya yako ya kiuchumi epuka matumizi kuzidi mapato yako. Kwa kila kipato unachoingiza, tenga sehemu ya kipato hicho ambayo utaweka kama akiba.

( 5 ). JAMII.
Jamii ni wale wanaokuzunguka, ambao unawahitaji sana kwenye safari yako ya mafanikio. Huwezi kufanikiwa peke yako, chochote unachotaka kinatoka kwa watu wengine.
Jenga afya yako ya kijamii kwa kuboresha mahusiano yako na wengine, kuwajali na kuweka maslahi yao mbele. Jua utapata unachotaka kwa kuwapa wengine kile wanachotaka.
Linda afya yako ya kijamii kwa kuepuka kuwasema wengine vibaya, majungu na kuwadhulumu wengine. Hata kama unaona unaweza kufanya kwa siri, jua kuna siku mambo yote yatakuwa hadharani.

Jenga afya yako kwenye maeneo hayo matano na utakuwa moto wa kuotea mbali kwenye safari yako ya mafanikio. Kwani utakuwa na mwili wenye nguvu ya kupambana, akili yenye uwezo wa kufanya maamuzi bora, roho yenye hamasa ya mafanikio, uchumi unaokuweka huru na jamii inayokupa kile unachotaka.




KARIBU  UJIUNGE   " DARASA  ONLINE " na ujifunze jinsi ulivyo na nguvu kubwa ndani yako za kukuwezesha kufanya makubwa mno.


Unaweza kuwa unajichukulia poa na kuona huwezi kufika kwenye mafanikio makubwa, lakini kwa kujifunza   zaidi   kwa  undani  utaona wazi nguvu zako zilipo na jinsi ya kuzitumia kufanya makubwa  na  kufanikiwa. HAKUNA  UCHAWI.


Rafiki, umejifunza hapa jinsi AFYA ilivyo mtaji muhimu kwako kufanikiwa, chukua hatua sahihi sasa ili kujenga afya imara itakayokuwezesha kufika kwenye mafanikio makubwa.

Rafiki yako anayekupenda sana,
KOCHA   MWL.  JAPHET   MASATU, DAR ES  SALAAM , TANZANIA

Tuwasiliane  nami  sasa ili  nikuunge  katika   "DARASA   ONLINE "  kwa   kutumia  EMAIL   YAKO   YA  GMAIL "


( WhatsApp  + 255 716 92 4136  ) /   + 255 755 400128

Tuesday, June 29, 2021

JINSI UNAVYOWEZA KUWA BILIONEA , HATUA KWA HATUA.

Whatever the mind of man can conceive and believe, it can achieve.” - Napoleon Hill

Rafiki yangu mpendwa,

Napoleon Hill, baada ya kufanya utafiti kwa watu zaidi ya 500 waliofikia utajiri mkubwa kwenye maisha yao na kuwalinganisha na wengine ambao hawakuweza kufikia utajiri, alikuja na kanuni rahisi ya mafanikio na utajiri aliyoishirikisha kwenye kitabu chake alichokiita THINK AND GROW RICH.

Sentensi moja ambayo unaweza kuitoa kwenye kitabu chake na ikabadili kabisa maisha yako ni ile inayosema; chochote ambacho akili ya mwanadamu inaweza kuelewa na kuamini, inaweza kukifikia.

Soma tena taratibu na uielewe kauli hiyo, kwani ina nguvu ya kuifungua akili yako na ikakuwezesha kupata kila unachotaka, ikiwepo kufika kwenye ubilionea.

Najua unavyosoma hapa kuna kisauti ndani yako kinakuambia hilo haliwezekani, kinakupa ushahidi kwamba katika mazingira yako hakuna aliyefikia ubilionea, wewe utawezaje. Sauti hiyo inakukumbusha kipato kidogo ulichonacho au madeni makubwa uliyonayo na kukuhakikishia huwezi kufika kwenye ubilionea.

Leo nina habari njema kabisa kwako, kwamba sauti hiyo haina nguvu kwako kama akili yako itaelewa na kuamini kile kweli unachotaka.

Na kwa ushahidi tu, hapo ulipo sasa hujafika kama ajali, bali ni matokeo ya kile ambacho akili yako imeelewa na kuamini kwa muda mrefu. Kama ulikuwa unaamini wewe ni wa chini na huwezi kupiga hatua, hayo ndiyo umezalisha mpaka sasa. Na kama utaamini unaweza kufanya makubwa, hilo pia ndiyo litatokea.

Ujumbe wangu kwako leo rafiki yangu ni huu, unaweza kuwa bilionea. Na ushahidi ni mabilionea ambao tayari wapo duniani. Kama wengine wameweza kufikia ubilionea, kwa nini wewe ushindwe?

Na kama alivyowahi kusema Benjamin Franklin, wachache kuwa matajiri ni ushahidi kwa wengine kwamba inawezekana.



Je upo tayari kujifunza kutoka kwa wale ambao wameweza kufikia utajiri na mafanikio makubwa kwenye maisha yako?

Kama jibu ni NDIYO  basi KARIBU    UJIUNGE   DARASA   ONLINE  LA  " MAISHA  NA  MAFANIKIO "  UJIFUNZE  SIRI   ZA  MAFANIKIO   YAO.

 WASILIANA  NAMI  SASA  ILI  NIKUUNGE.

KOCHA  MWL;  JAPHET   MASATU , DARA ES  SALAAM--TANZANIA

( WhatsApp + 255 716 924136 ) ,  + 255 755 400128

 

IJUE SIRI KUELEKEA SAFARI YAKO YA MAISHA NA MAFANIKIO

Siri Ambayo Itaharakisha Safari Yako Ya Mafanikio.

Picha linaanzia hapa,

 Mstari unachorwa kati ya wale wanaofika mbali na wale ambao hawafiki mbali.

Kuna tofauti kubwa sana kati ya watu wanaofanikiwa na wasiofanikiwa.

Na kuna mambo mengi sana watu wanajaribu kuyatofautisha katika makundi haya mawili.

Lakini moja ya eneo muhimu sana ambalo linafanya watu wafanikiwe sana na wengine wasifanikiwe ni namna wanavyotumia akili zao kufikiria kufanya mambo na kupata mawazo, lakini kuna aina mbili kisayansi ambazo zinaweza kutofautisha makundi haya ya watu wawili.

Aina ya kwanza tunaita GROWTH MINDSET na aina ya pili tunaita FIXED MINDSET, hizi ni aina mbili za watu wanavyofikiri labda kitu cha kujiuliza MINDSET ni nini?.

 MINDSET ni mfumo wa kufikiri ambao umeshajengeka ndani yako na hauitaji kujadiliana nao ili kupata matokeo.

Kwa maneno mengine unapokuwa na FIXED MINDSET, kwenye jambo Fulani ni kwamba jambo lolote linapotokea ubongo wako unakuwa  umeshaamua utafanya nini au utachukua hatua gani.

Lakini kwenye GROWTH MINDSET, tunasema ni ile hali ambayo ubongo wako unakuwa umeshajiandaa kupokea taarifa tofauti na zile ambazo hazikuwepo hapo kabla.

Ukweli ni kwamba watu wanaofanikiwa ni wale wenye GROWTH MINDSET.

Watu wenye GROWTH MINDSET, ni kwamba wako tayari kuanza kujifunza , ulishawahi kukutana na mtu ambaye hataki kabisa kujifunza anaamini yeye anajua kila kitu huyo hawezi kufanikiwa.

Mtu ambaye  anayefanikiwa kwenye GROWTH MINDSET ni mtu ambaye anasema ni kweli ninajua lakini ninahitaji kujua zaidi, ni mtu ambaye pia yupo tayari kuona watu wengine wanaweza kuliko yeye, mtu anayefanikiwa ni Yule anayesema ni kweli mimi ni mtaalamu kwenye uhandisi lakini ninaamini yupo mtu mtaalamu kwenye jambo la biashara kwa maneno mengine anaamini watu wengine wanaujuzi ambao yeye hana, na anauhitaji kukamilisha kile kitu ambacho anataka kukifanya lakini unapokuwa mtu wa FIXED MINDSET hutofanikiwa.

Watu wa FIXED MINDSET, moja ya sifa yao kubwa ni kwamba kila wakati wanajiona wao ni watu wanaojua sana, wanajiona wao ni watu wenye utaalamu kuliko watu wengine lakini kama kweli unataka kufanikiwa kwenye eneo lako  wanasema hivii siku zote unapotaka kufanikiwa tambua kwamba chochote unachokijua sasa hivi ni kidogo sana kuliko kile ambacho unatakiwa kukijua kwa maana nyingine unakuwa tayari kujifunza na kusonga mbele katika kufahamu kile kitu ambacho unakitaka, lakini kuna jambo ambalo unaweza kulifanya kwa haraka sana, ili kutoka kwenye FIXED MINDSET na kuelekea kwenye GROWTH MINDSET.

Jambo la kwanza, Kila siku tenga muda angalau wa nusu saa wa kujifunza kitu kipya katika eneo lako la utaalamu ambalo unaliishi kwa maneno mengine tafuta vitabu vitakavyokusaidia kupiga hatua, au tafuta mtu ambaye utaweza kuzungumza naye lakini hakikisha kila siku kuna jambo jipya ambalo unajifunza katika kukuza ufahamu wako.

Jambo la pili, Jaribu kila siku kujiuliza hivi ninasonga mbele au ninarudi nyuma kwa maneno mengine jaribu kujikagua na kujifanyia review yakuona kama unapiga hatua au haupigi hatua kwenye maisha yako, ukifanya mambo haya mawili kila siku yatakusaidia kutoka kwenye FIXED MINDSET kwenda kwenye GROWTH MINDSET.

Lakini siku zote hasara ya kuwa na FIXED MINDSET, ni kwamba utafanya mambo yale yale kwa namna ile ile bila kupata matokeo tofauti, wataalamu walisema kwamba kama utafanya jambo lile lile kwa namna ile ile utapata matokeo yale yale.

Kwa hiyo GROWTH MINDSET, inasema sijui kama ninavyotakiwa kujua kwa maneno mengine nipo tayari kujifunza, unapomzungumzia WARREN BUFFET, mtaalamu mkubwa kwenye mambo ya uwekezaji, unapomzungumzia  BILLGATE hao wote wana operate kwenye GROWTH MINDSET.

Wanajifunza jambo jipya kila siku wanasoma kitu kipya cha kuwakuza .

Je, LEO uko tayari kusoma kitu kipya ili kukuza ubongo wako?

KARIBU   UJIUNGE  SASA  " DARASA  LA   MAISHA  NA  MAFANIKIO "  ONLINE     ILI  UJIFUNZE  SIRI   ZA  MAISHA   NA   MAFANIKIO  KWA   MAPANA  NA  MAREFU

WASILIANA  NAMI    SASA    KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU

 ( WhatsApp  + 255 716924136 ) /  + 255 755 400128 /  + 255 688 361 539 

EMAIL : japhetmasatu@gmail.com

 

Saturday, June 26, 2021

JINSI YA KUPATA UTULIVU WA AKILI , TEKNOLOJIA IMEVURUGA AKILI ZA WATU WENGI.

Je, Ungependa Kupata Utulivu Wa Akili?

Wahenga waliwahi kusema“ Usipoziba Ufa Utajenga Ukuta”.

Hakuna anayeweza kubisha kwamba kumekuwa na ukuaji mkubwa sana wa teknolojia kwenye zama tunazoishi sasa.

Kuna maendeleo makubwa ambayo yametokea tangu kuanza kwa karne ya 21 ambayo hakuna aliyetegemea yangetokea kwa kasi kubwa hivyo.

Nani alidhani angeweza kuwasiliana na mtu aliye bara la mbali kwa kuonana uso kwa uso bila hata ya kutumia gharama kubwa?

Nani alifikiri vitabu vyote duniani vingeweza kuweka mtandaoni na ikawa rahisi mtu kuvipata na kuvisoma?

Nani alifikiri kungekuja simu za mkononi (simu janja) ambazo unaweza kuzitumia kufanya kila kitu kama unavyotumia kompyuta, kuanzia kuwasiliana, kutunza kumbukumbu, kupiga picha, kurekodi sauti na video, kuuza na kununua na hata kujifunza?

Haya ni maendeleo makubwa, ambayo mtu aliyefariki kwenye karne ya 20, akifufuliwa leo atashangaa mno kwa maendeleo haya na angetegemea kuona maisha ya watu yakiwa bora kutokana na maendeleo haya makubwa.

Lakini hapo ndipo atakaposhangazwa zaidi, kwani licha ya maendeleo makubwa ya teknolojia atakayokuwa ameyaona, atagundua maisha ya watu yako hovyo kuliko kipindi ambacho teknolojia hizo hazikuwepo.

Atashangaa kuona watu wakiwa wamechoka, wana msongo na hawana muda kabisa.

Atashangaa kuona watu wakitumia muda wao mwingi kwenye simu zao, kwa mambo ambayo hayana manufaa kwao.

Atashangaa jinsi watu wanaonena wivu kwa mambo ambayo wanayaweka kwenye mitandao ya kijamii.

Ujumbe atakaokuwa ameupata ni mmoja, kwamba teknolojia hizi mpya ambazo zina nguvu ya kufanya maisha ya wengi kuwa bora, zimegeuka kuwa gereza lililowafungia wengi na hawana tena uhuru wa kuyaishi maisha yao.

Ni dhahiri kwamba teknolojia mpya, hasa simu janja na mitandao ya kijamii, vimekuwa tatizo kubwa kwa wengi. Kila mtu analalamika jinsi vitu hivyo vinavyochukua muda mwingi, kuleta uchovu na hata msongo.

Wanaotengeneza na kuendesha teknolojia hizo hawajali kuhusu hilo, kwani kadiri unavyozitumia kwa muda mrefu, ndivyo wao wanavyopata faida. Hivyo wamejipanga kuhakikisha watumiaji wanaendelea kuwa wafungwa kwenye teknolojia hizo.

Na kwa kuwa teknolojia hizi ni mpya, hakuna mwenye uzoefu wa jinsi ya kukabiliana nazo, hivyo watu wanaingia kwenye teknolojia hizo mpya kwa kuhadaiwa watanufaika sana, lakini kinachotokea ni wanageuzwa kuwa wafungwa.


Leo nina habari njema mdau  wangu  , habari hizo ni kupatikana kwa mwongozo wa kuzitumia teknolojia hizi mpya vizuri na ukombozi wa ufungwa ambao teknolojia hizo zimetengeneza kwako.

Kupitia   " DARASA   ONLINE "   MAISHA  NA  MAFANIKIO utajifunza  jinsi  teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia za kuondoka kwenye utumwa huo.

Mungu  akubariki  sana.

WASILIANA  NAMI  HARAKA  NIKUUNGE

 ( WhatsApp  + 255 716924136 ) /  + 255 755400 128  /  + 255 688 361539 / + 255

 

KWANINI WATU WENGI HAWANA FURAHA ??

Unajua Kwa Nini Wanakosa Furaha?

Ili uweze kufanikiwa kwenye malengo ambayo unayo ni lazima uwe mtu mwenye furaha.

Na wapo watu wengi sana ambao wamekosa furaha kwenye maisha yao na inawezekana hii imesababishwa na changamoto mtu anazozipitia mambo anayopitia, inawezekana ni changamoto za kifedha, changamoto za kimahusiano au ni changamoto za kiuongozi.

Lakini kuna jambo ambalo limenyang " anya furaha ya watu wengi sana.

Lakini kitu kimoja ambacho watu wengi sana ambacho hawakifahamu furaha huwa haianzii nje furaha huwa inaanzia ndani yako.

 Na kuna vitu ambavyo watu waliofanikiwa siku zote kuwa na furaha kwenye maisha yao, wamezingatia na wamevifanya siku zote.

Kuna mambo ukiyafahamu utakuwa na furaha kila siku bila kujali nini kinaendelea, bila kujali hauna nini na ndio mambo leo ninataka uyazingatie na kujifunza, ili uweze kuyatumia kama sehemu ya kujenga furaha yako inawezekana kabisa kuwa na furaha kila siku kwenye maisha yako.

Jambo a ambalo mwanasaikolojia leonard ambalo alilisema 1954, ili uwe na furaha usijilinganishe na watu wengine , yeye alitumia concept nzuri sana, upward comparison na downward comparison, kwamba kuna kujilinganisha kwa juu yako au kujilinganisha chini yako, kwa watu wengine wenye mitazamo chanya inawasaidia kama kutamani lakini wengi sana inakuwa kama inawakatisha tamaa, wanajiona kama wamechelewa wanasema kwa kweli najiona kama nimechelewa.

Maana kama Yule kafanikiwa kiwango kile kwa nini mimi sijafanikiwa kwenye hichi.

 Lakini wale wanaojilinganisha na wachini yao tunasema wao wanajiona kama wamefanikiwa sana, wakijilinganisha na wale watu ambao wapo chini yao.

Mwanasaikolojia leonard, anasema ukifanya ulinganifu wako na watu wengine itakupa shida sana kufanikiwa kwako, kwa sababu ukweli ni kwamba (“somebody ten chapter it can be your one chapter”).

Kwamba sura ya kumi ya mtu mwingine unayemwangalia kwako inawezekana ikawa ni sura ya kwanza kwenye kitabu chako, kwa maneno mengine unapojilinganisha unakuwa hujui kinachoendelea kwenye maisha ya mtu mwingine watu wengi kwa ajili ya kujilinganisha wamejikuta wamejikuta wameingia kwenye maisha yenye gharama kubwa sana, wamejikuta wanatumia vitu katika viwango vikubwa kuliko walivyokuwa wanatakiwa.  

Mtu anajilazimisha kufanya mambo yaliyo juu sana ya uwezo wao, kutokana tu na kujilinganisha.

Unachotakiwa kujua ni kwamba watu wengi hawakuonyeshi kitu kilichopo wanakuonyesha kitu wanachotaka wewe ukione.

Rudia ili uelewe vizuri, watu hawaonyeshi kitu kilichopo kwao wanakuonyesha kitu wanachotaka wewe ukione.

Kitakacho tokea ni nini? Wewe utakuwa unajilinganisha na kitu ambacho wanataka wewe ukione lakini hujui uhalisia wa mambo yaliyojificha, lakini ushawahi kukutana na hali au ukasikia kitu cha mtu ukasema aisee nilikuwa sijui kama jamaa ndivyo alivyo kumbe alikuwa anaigiza kumbe maisha yake hayakuwa hivyo, kwa hiyo usijilinganishe na watu wengine, watu wengi ambao wanajilinganisha nao, unawakuta wana struggle kwenye maisha yao, kuna mambo wanaendelea kustruggle kuyapata.

kwa hiyo focus kwenye kitu unachokifanya, focus kwenye maono yako, angali kitu unachopaswa kukifanya , angalia jinsi maisha yako wanavyopaswa kwenda, acha kujilinganisha utajikuta kwenye matatizo makubwa  sana kwenye maisha yako.

Nilishawahi kukutana na mtu mmoja, akawa ananiambia alikuwa na anajilinganisha sana, alikuwa anawatamani sana watu Fulani, lakini siyo kitu kibaya wapo watu ambao wanaishi vizuri lakini mwisho wa siku tunasema lazima urudi kwako wewe mwenyewe kwa sababu yeye mwenyewe anakuja kusema alichokuja kugundua baadae akawa anasema kwa kweli ningekuwa nawajua nisinge watamani wapo ki hivyo.

Kuna watu umekuwa unawatamani wanaendesha magari mazur, unatamani kujifunza vitu vizuri kutoka kwao lakini isifike sehemu ukawa unajiona wewe siyo kitu, hauna maana kwa sababu ya kujilinganisha sana na wengine kwa hiyo cha kwanza acha kujilinganisha badilisha kutoka kwenye kujilinganisha kwenda katika kujifunza, kujifunza alifanya nini akapata alichokipata, alifanya nini au alijifunza nini, au alipita njia gani ili na mimi niweze kupita.

Lakini mtu ambaye anajilinganisha ni Yule anayesema na mimi nataka kuwa kama Fulani bila kujifunza yaliyo nyuma yake.

Unaweza kuwa na FURAHA  kila siku kwa  kujiunga  na  " DARASA   ONLINE "  LA  MAISHA   NA  MAFANIKIO " ,kwawa sababu UTAJIFUNZA   hatua kwa hatua jinsi ya kujijengea tabia zinazoleta   FURAHA   NA   MAFANIKIO  katika  Maisha  yako.

 WASILIANA   NAMI   HARAKA   HUJACHELEWA.  ILI  NIKUUNGE ,  " MAARIFA  NI   NGUVU "

NA  KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU , DAR  E  SALAAM , TANZANIA

 ( WhatsApp  + 255  716 924 136 ) /    + 255 755 400 128 / + 0688  361  539 /  + 255 629 748  937

EMAIL :  japhetmasatu@gmail.com