BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Friday, May 24, 2019
SHAUKU NI NGUVU ITAKAYOKUWEZESHA KUPATA CHOCHOTE KATIKA MAISHA YAKO.
Shauku ndiyo nguvu ya kwanza ya kukuwezesha kupata kile ambacho unataka kwenye maisha yako. Shauku ni ule msukumo wa ndani wa kukutaka upate kile unachotaka. Msukumo ambao hauondoki wala kupungua. Shauku ina nguvu kubwa ya kukusukuma kufanya mambo ambayo wengine wanaogopa, lakini kwako yanaonekana kawaida.
Watu
wengi wamekuwa wanategemea hamasa iwafikishe kwenye mafanikio makubwa,
lakini tatizo la hamasa ni huwa haidumu, mara kwa mara inabidi uchochee
upya hamasa yako. Lakini
shauku huwa haipungui wala kuhitaji kuchochewa, shauku unakuwa nayo
muda wote na hii ndiyo inakusukuma wewe kupiga hatua zaidi.
Shauku inatokana na ile sababu kubwa inayokusukuma kupata unachotaka, ile KWA NINI inayokufanya wewe upambane kupata unachotaka. Kwa
nini zinatofautiana kwa watu, wapo ambao wanafanya kwa sababu wamejitoa
kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi, wapo ambao wanafanya ili
kuwaonesha wengine wanaweza na kadhalika.
Hakikisha
una msukumo mkubwa ndani yako wa kukupeleka kwenye kile unachotaka, kwa
sababu bila ya msukumo huu, hakuna nguvu nyingine itakayoweza
kukusaidia kupata unachotaka.
UNAHITAJI KUWA NA KOCHA , MENTA AU MSHAURI ILI UWEZE KUPATA CHOCHOTE UNACHOHITAJI KATIKA MAISHA YAKO
Ili kupata unachotaka, unahitaji kupata mwongozo kutoka kwa mtu mwingine. Mtu huyo anaweza kuwa kocha, menta au mshauri ambaye anakusimamia ufike kule unakotaka kufika.
Iko hivi rafiki, sisi binadamu ni wavivu na hatupendi kujitesa. Tunaweza
kuweka mipango mikubwa na mizuri sana, lakini tunapokutana na ugumu ni
rahisi kuacha na kujiambia haiwezekani au hatuwezi.
Lakini
unapokuwa na mtu wa pembeni ambaye anakuangalia na kukusimamia, kwanza
hutataka kumwangusha, hivyo utajisukuma zaidi na pili yeye mwenyewe
hatakubaliana na wewe kirahisi, hivyo itakubidi ujaribu tena na tena na
tena kabla hujasema haiwezekani.
Watu wengi wamekuwa wanajiwekea malengo peke yao, na asilimia 99 wamekuwa hawayafikii. Ila wale wanaoweka malengo na kuwa na mtu wa kuwasimamia kwenye malengo yao, zaidi ya asilimia 90 wanayafikia.
Hii
ndiyo nguvu kubwa iliyopo kwa kuwa na mwongozo. Kwa sababu pia mtu
anayekuongoza anaweza kukushauri vizuri pale ambapo unakuwa umekwama. Ni rahisi kuona makosa ya mchezaji aliyepo uwanjani ukiwa nje ya uwanja, lakini yule aliyepo uwanjani anaweza asione kwa urahisi. Kuna
makosa unaweza kuwa unafanya kwenye maisha yako lakini huyaoni, ila
unapokuwa na mtu anayekusimamia, atakuonesha makosa hayo kwa urahisi na
utaweza kupiga hatua sana.
Unahitaji kuwa na mtu wa kukusimamia kwenye malengo na mipango uliyonayo ambaye atakusukuma kuyafikia.
WATU WANAOKUZUNGUKA WANA MCHANGO MKUBWA SANA KATIKA KUPATA CHOCHOTE UNACHOTAKA
Watu wanaokuzunguka wana nguvu kubwa sana kwako, hata kama hujui. Watu
hao, hasa wale wa karibu, wana ushawishi mkubwa kwako. Kama
wanaokuzunguka wana mtazamo hasi wa kuona mambo hayawezekani, na wewe
pia utajikuta umebeba mtazamo huo, hata kama utakuwa unapingana nao
kiasi gani.
Na kama watu wanaokuzunguka wana mtazamo chanya wa inawezekana, na wewe pia utabeba mtazamo huo. Nguvu hii ya wanaokuzunguka ni nguvu kubwa sana unayopaswa kuwa nayo makini. Wengi wamekuwa wanapuuza nguvu hii, wakiamini wanaweza kuzungukwa na watu wa aina yoyote lakini wakafanikiwa.
Hicho kitu hakipo kabisa, kama haujazungukwa na watu sahihi, huwezi
kufanikiwa. Ni asili ya binadamu, hatuwezi kwenda juu zaidi ya wale
ambao wanatuzunguka.
Hivyo ili kupata kile unachotaka kwenye maisha, tafuta watu wanapiga hatua kwenye maisha yao na uwe nao karibu.
Watu ambao wanaamini kwenye ndoto kubwa na wasiokata tamaa. Watu hawa
watakupa nguvu ya kuendelea hata pale unapokutana na magumu na
changamoto.
UNAPOSHIKWA NA HASIRA , JIPE MUDA WA KUTAFAKARI.
Ukishagundua
kwamba upo kwenye hasira, basi kaa kimya, jipe muda wakutafakari na
kutulia na utajiepusha na makosa makubwa unayoweza kufanya ukiwa na
hasira.
Hasira ni moja ya hisia zenye nguvu sana, na hisia zinapokuwa juu uwezo wetu wa kufikiri unakuwa chini. Hivyo unapokuwa na hasira, unakuwa umetawaliwa na hisia na siyo fikra. Na
ni wakati mbaya sana wa kufanya chochote, kwa sababu unaposukumwa na
hisia, hujui kipi sahihi kufanya, kwa kuwa hufikiri sawasawa.
Hivyo rafiki, unapogundua kwamba una hasira, usifanye chochote.
Kama kuna mtu amekukosea na umepatwa na hasira usimjibu wakati una hasira hizo.
Kama kuna mtoto wake amekosea usimwadhibu ukiwa na hasira.
Ukiwa na hasira usifanye chochote, jipe muda wa kukaa mbali na kile kinachokupa hasira na akili zako zitarudi.
Thursday, May 23, 2019
Saturday, May 18, 2019
KILA MTU ANA HAIBA HIZI TATU : UJASIRIAMALI, UMENEJA , UFUNDI , ZIIBUE NA ZIFANYIE KAZI UTAFANIKIWA KATIKA BIASHARA YAKO
( 1 ). MJASIRIAMALI.
Hii
ni haiba ambayo inabeba nafsi ya mjasiriamali. Mjasiriamali ni mtu wa
kuja na mawazo mapya ya kuzitumia fursa mbalimbali ambazo zinapatikana.
Mjasiriamali ni mtu wa ndoto na maono makubwa, mtu wa kutengeneza picha
za mambo yasiyoonekana. Mjasiriamali anaangalia mambo yalivyo na
kujiuliza vipi kama yangekuwa tofauti.
Bila ya mjasiriamali hakuna mawazo mapya, hakuna ugunduzi na wala hakuna maono makubwa ya kibiashara.
Nafsi
ya ujasiriamali ndiyo inawasukuma wengi kuingia kwenye biashara, lakini
nafsi hii imekuwa haidumu kwa muda mrefu, inazidiwa nguvu na nafsi
nyingine na ndiyo maana tunasema mtu anakuwa amepatwa na kifafa cha
ujasiriamali. Wazo la ujasiriamali linamjia kwa muda mfupi na nafsi hii
kuondoka kabisa.
( 2 ). MSIMAMIZI/MENEJA.
Hii
ni haiba inayobeba nafsi ya usimamizi au umeneja kwenye biashara.
Meneja ndiye mtu ambaye anaisimamia biashara kwa ukaribu, kuhakikisha
kwamba kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa. Huyu ni mtu ambaye
anahakikisha rasilimali za biashara zinatumika vizuri. Pia meneja
anahakikisha kilichofanywa kwenye biashara jana ndiyo kinafanywa leo.
Mameneja hawapendi kujaribu vitu vipya kwa sababu hawana uhakika navyo.
Tofauti
kubwa ya mjasiriamali na meneja ni mabadiliko, mjasiriamali anatafuta
mabadiliko na kuwa tayari kuyafanyia kazi. Lakini meneja hataki kabisa
mabadiliko, anataka kuendelea kufanya mambo kama ambavyo amekuwa
Meneja
ndiyo nafsi inayoiwezesha biashara kufanya kazi. Mjasiriamali anakuwa
na mawazo mapya na makubwa, lakini hawezi kuyafanyia kazi mawazo hayo
kwa muda. Hivyo anahitaji kuwa na meneja ambaye anafanyia kazi mawazo
hayo mapya.
( 3 ).FUNDI/MTAALAMU.
Hii
haiba inayobeba nafsi ya ufundi au utaalamu unaohitajika kwenye
biashara. Huu ni ule ujuzi au utaalamu ambao mtu anaingia nao kwenye
biashara. Fundi kazi yake ni kutengeneza vitu na anapenda sana
kutengeneza vitu. Haiba hii ya ufundi inapenda kufanya yale yanayopaswa
kufanywa kwenye biashara.
Wakati
mjasiriamali anakuja na mawazo mapya, meneja anaweka mfumo mzuri wa
kufanyia kazi mawazo hayo, fundi ndiye anayefanya kazi kwenye biashara
hiyo na kuzalisha matokeo yanayohitajika. Fundi ndiye anayezalisha
matokeo kwenye biashara.
Subscribe to:
Posts (Atom)