Saturday, September 20, 2014

MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI---BIASHARA YA DUKA LA KANDA ZA MUZIKI.

      BIASHARA     YA    DUKA   LA     KANDA   ZA     MUZIKI
Biashara   ya    kanda   za   muziki   ni    biashara  nzuri  kwani   SOKO  LA   MUZIKI  ni  kubwa  kwa  sasa. Bidhaa   za    biashara  hii   zimekuwa    nyingi    kutokana    na     MAENDELEO    YA   TEKNOLOJIA.

DUKA  LA  KANDA  ZA  MUZIKI   linaweza   kuwa     na    bidhaa  kama :---  Kanda   za   kaseti ,  Kanda    za   Video , CD  na   DVD.  Mmiliki  wa   duka    la   kanda   za    Muziki   lazima    awe   na    mapenzi      na    Muziki. 

 ASIKILIZE   MATANGAZO , AFUATILIE   MAENDELEO  YA   MUZIKI  ili    ajue  ni   nyimbo  gani   zinapendwa    ili   AENDE    NA    WAKATI.

 MATATIZO   ya   biashara   hii  ni  ushindani    mkali     uliopo    kwani   watu   wengi    wanapenda   kuifanya   biashara   kwa    sababu     ni  rahisi.

MATATIZO  mengine   ni   WIZI   WA    KAZI   ZA    WASANII   kwa    kudurufu    Kanda    zao   bila    KIBALI    kwa   bei   rahisi. 

NI    KOSA   KUDURUFU / BURN  KANDA  BILA   IDHINI   YA  MTUNZI. 



Friday, September 19, 2014

MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI ----BIASHARA YA DUKA

MADUKA yapo  aina   nyingi. Bidhaa   tofauti  tofauti. Unataka   la   aina  gani  ? ,  bidhaa   gani ?  NGUO , VIATU , VIPODOZI , VYAKULA ----  VIFAA  VYA   UJENZI ,  UMEME ,  VYOMBO  VYA  NDANI , n.k.  SPEA / VIPURI   VYA   PIKIPIKI ,  BAISKELI ,  MAGARI    bado  ni  biashara   nyingine.

UNANUNUA , UNAUZA , UNANUNUA ,  UNAUZA -----  UGUMU    HAKUNA.   UPO  HAPO ?  NDUGU   YANGU ?

NENDA  TRA   WAMBIE  NATAKA   KUFANYA   BIASHARA  YA   DUKA   FULANI.   WATAKUPATIA   UTARATIBU   MZIMA.   HAPO   NDIPO   KWA   KUANZIA.


Unaweza  kuanza   na   KIOSK /  GROCERY.   SABUNI   KIDOGO ,  VIBERITI ,  MAFUTA   YA  KULA , PIPI , N.K.  Baada   ya  muda   utakuwa   na  DUKA  NA   MADUKA  MAKUBWA  na   KUUZA  BIDHAA   UNAZOZITAKA.



MUNGU   AKUBARIKI   KWA  KUSOMA  MAKALA  HAYA.



MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI ---- HUDUMA ZA KITAALAMU.

BIASHARA  ya   kutoa  huduma   za    kitaalamu   ni  nzuri  sana  na  ina  mapato   mazuri , inaweza  kuleta  UTAJIRI   na  MAISHA  BORA. Ili   ufanye  biashara   hii  unapaswa   kwanza     KUSOMEA   TAALUMA  HUSIKA  kwa   kiwango   kinachohitajika   na     WAHITAJI   WA  SOKO.

TAALUMA    ambazo  zina   malipo   mazuri   ni   UALIMU , UANASHERIA, UDAKTARI, UFAMASIA ,  UHASIBU ,  UFUNDI  WA   VIFAA   VYA   ELECTRONIKI   N.K.

Unaweza   kuanza  kwa    KUAJIRIWA  kwenye   ofisi  inayotoa   huduma   ya  fani  yako    ili  UPATE   UZOEFU  NA   SIRI  YA  BIASHARA  HIYO.

kisha   tafuta  kuanza   taratibu   KUFANYA  KAZI   ZAKO  BINAFSI. UKIONA   BIASHARA     YAKO   INAENDA   VIZURI  ACHA  KAZI   NA  UENDE  KUFANYA  BIASHARA  YAKO   KWA    JUHUDI      NA    MAARIFA   YAKO   YOTE    UTAFANIKIWA.



      MUNGU    AKUBARIKI    MSOMAJI   WA  MAKALA   HII.


MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI ----KUWA NA UKUMBI WA KUKODISHA.

Ukipata   MTAJI    WA  KUTOSHA  jenga  au  tengeneza   ukumbi   kwa   ajili   ya   kukodisha --- SHEREHE , MIKUTANO , SEMINA  n.k.  kila   siku   mambo  hayo    yapo na   yanafanyika. Ni   wewe   kuchangamka !! Unagaharamia  mwanzo   tu   baada  ya  hapo  unabaki   kuzivuna  FEDHA   siku   nenda   rudi. 

Kwa   ukumbi   wa   kawaida  ni  kati  ya   shs.  50,000  hadi   100,000  kwa   siku.  Kumbi  kubwa {  hasa  za   sherehe } ni  laki  tano   hadi  milioni   kwa   siku    kwa   maeneo  ya  mijini  kama   DAR--ES--SALAAM. 

Ukiwa  na   KUMBI   kama   tatu   hivi  na  zaidi   PIGA  mahesabu    mwenyewe       una shilingi   ngapi  ?  FEDHA   NYINGI SANA!!  ACHA   KUBWETEKA  !!!  CHANGAMKA   SASA !!!  

Thursday, September 18, 2014

MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI ----BIASHARA YA KUKODISHA VITI

KUKODISHA  VITI      kwa     ajili   ya    SHEREHE  , HARUSI , MIKUTANO , KIPAIMARA  n.k .   ni  biashara   ambayo   haikugharimu   kitu    zaidi    ya    KUNUNUA     VITI    na     KUAZIMISHA.


TAFUTA   CHUMBA ,  hata   kimoja  tu    KINATOSHA.   NUNUA   VITI   VYA  PLASTIKI     KAMA   MIA   TATU   HIVI    VYA   KUANZIA.  Kila  kiti  kinauzwa   ELFU   KUMI.    kodisha  kila   kiti     kimoja    kwa     shs.  300 /=   kwa    siku   moja { saa  24 }.

 Kwa  mfano , Ukiazimisha    viti   200   kwa   siku   moja tu   utakuwa    una   shs.  60,000/ =.  Hii   ni    mojawapo     ya     shughuli    ya    KUKUINGIZIA   MAPATO   AINA   YA  TULI (  PASSIVE   INCOME ).  Baadaye   waweza  kupanua biashara   kwa   kununua  na   MEZA , STULI , MATURUBAI ,  VYOMBO  n.k.


MAPATO  TULI  ni  mapato   anayoyapta    mtu  pasipo   kuwa   na   ulazima  wa   kushughulika  au  kufanya  kazi  kwa   wakati  huo. Yanatokana  na  kazi  au  shughuli  uliyokwisha  kufanya  kitambo   na  kuendelea    kupata  mapato  haya  kimya  kimya.  Unayapata  kutokana  na  vitega  uchumi   ulivyo  weka.

Wednesday, September 17, 2014

MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI ----- BIASHARA YA MAZAO.

UNANUNUA     Kipindi  cha    MAVUNO    na    KUUZA  bei  zinapokuwa     juu, MCHELE , MAHARAGE , MAHINDI   kwa   mfano    ni   baadhi   ya   MAZAO    YENYE   UHAKIKA   ZAIDI.                                                                            .

MAARIFA YA KUPATA PESA NA UTAJIRI-- UANDISHI NA UTUNZI WA VITABU NA MASHAIRI

UANDISHI  na  UTUNZI   wa       VITABU , MASHAIRI , RIWAYA , VITABU   VYA   KITAALUMA ( MASOMO )     ni    njia    na    sanaa     ya   kukupatia   PESA.   Waandishi   maarufu   kama   akina   CHINUO    ACHEBE ,  SOCRATES ,  SHAABAN    ROBERT   , NAPOLEON   HILL ,  CARL   MAX ,  HERODOTUS   na    PINDAR   wanakumbukwa   na   kuenziwa   hadi  dakika  hii   kwa    kazi  zao. Hata  sasa  wapo   waandishi   wengi  tu ,  ukipenda  hata  wewe   unaweza   kuwa  mmoja  wao.

Unaweza   kutunga   kitabu  kuhusu suala   lolote   ambalo  linaweza   kuelimisha   jamii  au    kuburudisha   jamii.  Kwa   mfano  unaweza   kutunga  kitabu   cha   hadithi  na   unaweza    kueleza kuhusu   jambo   lolote   lile.


KUANDIKA   KITABU   inagharimu   sana    MUDA   na   KICHWA ---   AKILI.  UNAWAZA   NA    KUWAZUA.  UANDIKE  NINI  /  KIPI  UACHE   KIPI  !  NI   SANAA    NGUMU   LAKINI    MWISHO   WA   SIKU   INALIPA.   TAFUTA    mada --- kitu   unachoona   kitaifaa   jamii    yako   ya  sasa    na    vizazi   vijavyo   kisha    kiweke    katika    MAANDISHI.