MAISHA ni mchezo wa kuigiza ambao kila mmoja wetu ana nafasi mahususi ya kushiriki kama MWIGIZAJI. Hata hivyo tunachofanya katika MAISHA yetu wenyewe, ni zaidi ya KUSHIRIKI tu kama WAIGIZAJI----hakika tunaandika Mchezo wenyewe. TOFAUTI na Mchezo ambao tayari tunafahamu kwamba HATIMA yake ni nini , HATIMA YA MAISHA YETU TUMEISHIKILIA MIKONONI MWETU WENYEWE .
BAADHI YA WATU huamini kwamba HATIMA ya MAISHA YETU huwa tayari imeamuliwa hata KABLA YA KUZALIWA KWETU. MIMI SI KAMA hao wanaoamini hivyo. NINACHOAMINI MIMI NI KWAMBA UPO UWEZEKANO WA KUBADILI HATIMA YA MAISHA YETU WENYEWE KWA KUBORESHA NAMNA TUNAVYOZITUMIA FIKRA ZETU.
BADALA YA KUISHI KWA KUTEGEMEA KUDURA TULIVYOPANGIWA , Tupanue FIKRA ZETU ili zituwezeshe KUANDIKA MCHEZO WA MAISHA YETU TUKIWA TUMEJIPANGIA NAFASI TUNAZOPENDELEA KUSHIRIKI KATIKA MCHEZO HUO. Kadiri tutakavyoweza kufanya jambo hili mapema ndivyo tutakavyoharakisha mwanzo wetu sisi wenyewe wa kutawala kikamilifu kila kipengele cha MAISHA yetu ya kila siku.
KATIKA MCHEZO UITWAO MAISHA KUNA TOFAUTI KUBWA SANA BAINA YA WALE WALIOJIPANGIA WENYEWE NAFASI ZA UHUSIKA KWENYE MCHEZO HUO , NA WALE WANAOISHI MAISHA YA MAJALIWA YASIYO NA LENGO.
FURSA mbalimbali zinatusubiri katika mambo mengi yanayohusu MAISHA YETU. Tuna UWEZO WA KUZIPATA FURSA HIZO KAMA TUKIPANIA. HATA HIVYO tusipokuwa na DHAMIRI pamoja na MALENGO BAYANA KATIKA FIKRA ZETU , haitakuwa rahisi kufaulu hata katika FURSA zile za kawaida na bayana kabisa.
KANUNI YA MAFANIKIO----JIPATIE NAMBA KATIKA MCHEZO UITWAO MAISHA.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Monday, September 8, 2014
Saturday, September 6, 2014
KAMWE USIKATE TAMAA.
MAFANIKIO yanapatikana pale ambapo mtu anapokubali kufanya JITIHADA ZA MFULULIZO , HATUA--KWA--HATUA , hata kwenye MAMBO yanayochosha sana. Hili linaweza kusikika kuwa ni jambo lililorahisishwa , lakini mtu anayeendelea KUFANYA KAZI KWA UAMINIFU kuliko mwingine YEYOTE , bila shaka atafanikiwa kwenye LENGO LAKE.
KUBALI UDHAIFU WAKO.
USIJIFANYE KWAMBA UNAWEZA KUFANYA JAMBO USILOLIWEZA . KUBALI USILOLIWEZA KUFANYA , NA ANZIA HAPO.
BUNI KUTATUA MATATIZO YA WATU ! NDIYO NJIA PEKEE YA KUPATA PESA
Huwa tunasema mtu fulani KAFANIKIWA KIMAISHA. ANA PESA NYINGI. Naam ! Ni kweli KAFANIKIWA , Lakini amefanya nini hadi KUPATA PESA HIZO ? JIBU : KATATUA MATATIZO YA WATU ! Naam , ndiyo UKWELI.
NJIA MOJA YA KUPATA PESA NI HII : Chochote unachotaka kufanya wa ajili ya kukuletea PESA , JIULIZE kama kinaweza kuwatatulia watu MATATIZO YAO ? Kama jibu ni ndiyo basi ANZA MARA MOJA , HAKIKA UTAFANIKIWA. LAKINI KAMA JIBU NI HAPANA , KIACHE MARA MOJA. UKIFANYA UTAANGUKA VIBAYA SANA .
Jenga tabia ya kuwa MTAFITI MZURI. Unapofanya UTAFITI utajua WATU wanahitji nini . HATUA YA KUJUA WATU WANATAKA NINI NA WANAHITJI NINI , NI HATUA KUBWA SANA YA KUKUFANYA UPATE PESA TU , PIA UTAPATA HESHIMA KUBWA KATIKA JAMII HIYO. KWANI UTAKUWA UMEWEZA KUTATUA SHIDA YAO.
Hivyo , unapoingia katika uwanja wa kutafuta PESA , Kabla hujaanza kufanya jambo unalotaka likuletee PESA, JIULIZE : "je , jambo hili litawatatulia watu tatizo lao ?" Kama jibu ni HAPANA , LIACHE MARA MOJA ! Huwezi kufanikiwa kwa kuuza sweta wakati wa joto. Ukipata HASARA utalalamika, : " MIE NINA MKOSI !"
KABLA YA KUANZA BIASHARA YOYOTE hata kama ni ndogo , FANYA UTAFITI WA KUTOSHA kama BIASHARA unayotaka kufanya itakuwa na manufaa , au laa ! UTAFITI WAKO WAKO UANGAZE HIVI :
1. Je, jambo ninalotaka kufanya litaleta faida ?
2.

Thursday, September 4, 2014
HESHIMU HISIA ZAKO.
HISIA NI NINI ? Kuna tofauti gani kati ya HISIA na MATAMANIO ?
BINADAMU ana NAFSI MBILI. Nafsi ya kumuelekeza MAZURI na Nafsi ya kumuelekeza MABAYA.
KWA MFANO , unaweza kuwa unataka kutenda JAMBO BAYA. Bila shaka kuna sauti nafsini kwako inakunong"oneza , USIFANYE JAMBO HILI , nyingine inakwambia FANYA ! Inayokwambia "USIFANYE NI HISIA " inayokwambia " FANYA" ni MATAMANIO.
Bila shaka umewahi kusikia MTU akimwambia mwenzake , " UNA MACHALE SANA , VINGINEVYO UNGEIBIWA ! " Je, unafikiri hii inamaanisha NINI ? Hii ni " HISIA " ndiyo iliyomwongoza na kumwepusha na balaa la kuibiwa .
AU unaweza kuwa umezungukwa na watu , unasikia SAUTI INAKUNONG"ONEZA , " KIMBIA HARAKA ! Hawa watu ni HATARI kwako. " Lakini sauti hiyo haiwezi kusikika kwa mtu mwingine yeyote zaidi yako. JE , UNAFIKIRI HUYU ANAYEKUNONG"ONEZA NI NANI ? NI " HISIA " NDIYO INAYOONGEA NA WEWE ! Watu wengi hudharau "HISIA" zao na mwishowe hupata MATATIZO.
KILA MTU ANA HISIA. Watu hutumia lugha: " CHALE ZILIMCHEZA ", wakimaanisha : " HISIA ZILIMWAMBIA."
HISIA ni NGUVU iliyo ndani ya mwili wako ambayo HUKUONGOZA. Zimewekwa katika mwili wako kwa malengo maalumu KUKUSAIDIA. PINDI unapotawaliwa na MATAMANIO , ni hakika kwamba baadaye UTAWEZA KUKOSA FURAHA. HISIA hujaribu KUKUTAARIFU kuwa JAMBO FULANI SI ZURI . HUKUSISITIZA ZAIDI NA ZAIDI.
UKIONA HISIA zinakuzuia KUFANYA JAMBO , LIACHE MARA MOJA. KISHA , TOKA UTAFAKARI AU UWAULIZE WENGINE. Kwa kufnya hivyo , itakusaidia KUPAMBANUA MWELEKEO WA HISIA ZAKO.WANAOHESHIMU HISIA ZAO HAWAJUTI.
ANZA KUHESHIMU HISIA ZAKO , si kwamba UTAPATA PESA TU , BALI kuna mambo mengi ambayo UTAWEZA KUFANIKIWA MAISHANI KUTOKANA NA KUHESHIMU HISIA ZAKO.
HISIA zinavutia. WAPELELEZI hutumia HISIA. HISIA Zinapowambia JAMBO HUSIMAMA. HUZISIKILIZA. kisha huzifanyia kazi.Vivyo hivyo , hata WANASAYANSI , WATABIRI ,MADAKTARI N.K.
KILA SIKU HISIA ZINAZUNGUMZA NA SISI . KINACHOTAKIWA NI KUZIHESHIMU.
HISIA NI KIONGOZI NA MSHAURI WETU TUMHESHIMU ILI TUEPUKANE NA MATATIZO MBALIMBALI.

Wednesday, September 3, 2014
SOMA VITABU VIZURI UPANUE UPEO WAKO.
SOMA VITABU VIZURI UPANUE UPEO WAKO.
Badala ya kusoma tu kwa kujifurahisha , ninaamini sote tunapaswa KUSOMA ili kuboresha na kubadilisha nafsi zetu.HATUNA BUDI kujenga TABIA YA KUJITAFUTIA VITABU VIZURI na KUJIFUNZA kwa makini yale YALIYOMO ndani ya vitabu hivyo.
UNAWEZA KUHISI kuwa na shughuli nyingi MNO kiasi cha kukosa kabisa MUDA WA KUJISOMEA. LAKINI bado inawezekana kutumia MUDA MCHACHE katika ratiba yako yenye shughuli nyingi , POPOTE PALE ULIPO , KUFUNGUA KITABU CHAKO KIZURI na KUVUTIWA SANA NA YALIYOMO.
UZOEFU WAKO na ule wa wengine ambao unaupata KWA KUSOMA VITABU unaweza kukupatia NGUZO YA NAFSI YA MAFANIKIO MAISHANI .

Tuesday, September 2, 2014
TAFUTA SHABAHA / LENGO LA MAISHA.
Watu wengi zaidi hasa VIJANA, wanaonekana kupoteza SHABAHA yao au LENGO lao katika MAISHA. HUISHI maisha ya hapa na pale WAKIFUKUZIA MANUFAA YA MUDA MFUPI. SABABU yao pekee ya kufanya KAZI ni ili kupata HUNDI YA MALIPO kwa madhumuni ya kukidhi MATAMANIO YA KUFANYA ANASA NA STAREHE.Utafutaji wa FURAHA wa namna hii hauwezi kumfkisha mtu popote.
Bila kujali zama tunazoishi , dhati ya UBINADAMU inabaki kuwa ile ile. NI KUTAFUTA MAISHA yenye KUPENDEZA na KUFANIKIWA kufikia hali ya KUTOKUFA KWA KUKIACHIA KIZAZI KIJACHO jambo ambalo LITAENDELEA KUKINUFAISHA.Tunapaswa kutafuta MAISHA yaliyotimia ili siku moja tuweze kusema
"NILIFANYA KAZI KWA BIDII , NILITENDA MAMBO YENYE MANUFAA , NA NINAJISIKIA FURAHA."
Baadhi ya watu wanaweza wasikubaliane na mimi kuhusu WAZO HILI , LAKINI naamini kwa dhati kabisa kwamba njia hii ya KUJIBIDIISHA KATIKA MAISHA NI BORA ZAIDI KULIKO ILE NJIA RAHISI. Watu wenye uzoefu mkubwa zaidi wanaweza kuelewa kile ninachokisema. KWA BAHATI MBAYA , WATU WA AINA HIYO HAWAKO TAYARI KUTOA MAONI YAO KUHUSU MAISHA. SABABU ambayo kwa kawaida wamekuwa wakiitoa ni kwamba, WAKATI umebadilika na HADITHI zao za kale hazina mchango wowote KWA VIJANA WA LEO. LAKINI kama tukizungumza kwa dhati ya moyoni , WATU WENGI WATAJITOKEZA kuzungumzia kile TUNACHOAMINI.
KWA KUHITIMISHA NASEMA " MFUMO wa MAISHA RAHISI MWANZONI UNAWEZA KUONEKANA KAMA WA KUCHANGAMSHA NA KUVUTIA HATA HIVYO HUFIKA WAKATI SISI SOTE TUKATAMANI KUWA NA SHABAHA YA/ LENGO LA JUU ZAIDI KIMAISHA.

Subscribe to:
Posts (Atom)