Mipango ni rahisi sana, kila mtu anapanga na msimamishe mtu yeyote
njiani na muulize mipango yake ni ipi, atakupa mipango mizuri sana.
Pamoja na kila mtu kuwa na mipango mizuri, ni wachache sana ambao
wanaweza kufanyia kazi mipango hiyo na ikawa uhalisia kwenye maisha yao.
Wengi wamekuwa wanabaki na mipango tu, lakini haiwi uhalisia.
Kinachowazuia wengi kutekeleza mipango waliyonayo ni tabia ya
kuahirisha mambo. Hii ni tabia ambayo ni asili yetu sisi binadamu, huwa
hatupendi kufanya chochote ambacho kinatuumiza au kinataka tuweke kazi.
Huwa tunapenda kutumia muda wetu kwa vitu visivyo na maana. Kwa muda
ule ule na kwa nguvu zile zile, huwa tunaona ni bora kutumia kufanya
vitu ambavyo vitatupa raha ya muda mfupi, kuliko kufanya vitu ambavyo
havina raha ya muda mfupi lakini kwa muda mrefu vina maana.
Kinachowatofautisha wale wanaopata mafanikio makubwa kwenye maisha
yao na wale wanaoshindwa siyo bahati wala akili wala fursa.
Kinachowatofautisha ni namba wanavyoweza kuishinda tabia ya kuahirisha
mambo.
Wanaofanikiwa na wanaoshindwa wote wanakuwa kwenye mazingira
sana, wanakutana na fursa sawa, lakini wale wanaoshindwa huwa wanasubiri
wakati wanaofanikiwa wanachukua hatua.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment