Mtu mmoja amewahi kusema kwamba jukumu huwa linachukua muda
uliopangwa lifanyike. Akimaanisha kama kuna jukumu ambalo linapaswa
kufanywa kwa masaa mawili, litakamilika ndani ya masaa mawili. Jukumu
hilo hilo likipangwa kufanyika ndani ya masaa matano, litachukua masaa
matano.
Huwa tunasukumwa kufanya zaidi pale ambapo muda unakuwa mdogo, na
tunaahirisha mambo pale muda unapokuwa mwingi. Ndivyo maana wanafunzi ni
vigumu sana kusoma siku za kawaida, lakini mtihani unapokaribia, hamasa
ya kusoma inakuwa juu.
Jiwekee muda wa ukomo kwa chochote unachopanga kufanya, na muda huo
uwe mfupi kuliko muda uliozoeleka. Kwa kuwa na muda huu na kuufuata,
utaweza kujisukuma kufanya zaidi. Kadiri unavyokuwa na muda mfupi wa
kutekeleza jambo, ndivyo mawazo ya kuahirisha yanavyopotea kwenye akili
yako. Waahidi watu kwamba jukumu litakamilika mapema kuliko kawaida, na
tekeleza hilo uliloahidi.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment