TUKO WAPI ? Mazingira
yale yale yanazua
swali kwetu. Bila kujali
tunapogeukia , bado tuna swali
la kujibu na
kwa jibu lolote
tutakalotoa, bado kuna HOFU
katika mioyo yetu.
TATIZO
lenyewe ni zaidi
ya ile la
kisiasa. Ni tatizo la
KIMAADILI na KIROHO. Haliwezi kutatuliwa
na mtu yeyote
Yule.
Hali ya
MAISHA inatutaka TUSONGE
MBELE. Je, tutapata
USHINDI ? Vipi , kila
mmoja wetu akiwa
peke yake au
ni kama jamii
au ni watu
walioungana KUELEKEA MAISHA
YA UTAJIRI au kuteleza
kwenye lindi la
KUSHINDWA?
KIPI
NI SAHIHI ? Katika ngazi
ya taifa , jibu letu
huenda likapambwa na
vishawishi vya KISIASA. Kama mtu
binafsi , mawazo yetu juu
ya suala hilo
yataathiriwa na MATUMAINI
au kukatishwa tama
na miundo yetu
wenyewe.
Hebu
tusahau kwa MUDA
mambo makubwa
yanayohusu MAISHA YA KITAIFA
AU KIMATAIFA , kisha tujiulize wenyewe
maswali. Je, sisi ni kama
mtu binafsi anayesonga mbele
kwa KUJIAMINI kuelekea
MAISHA YA KITAJIRI
NA KIFAHARI ?
Jibu letu
kwa swali hilo
huweza kutolewa kwa
namna mbalimbali. Wengine wanaweza
kudhani kwamba hawawezi
KUVISHINDA VIKWAZO. Dhana hii
ina nafasi kubwa
zaidi kuliko watu
wengi wanavyofahamu.
MATATIZO yanaweza
kumsukuma mtu chini , hali
dhamiri yake ikibamizwa
kwenye uzito wa
makosa yake, Si rahisi
kuelewa kesho inaweza
kuwa siku yenye
mafanikio makubwa au
inaweza ikatukuta tukiwa
tumetekwa , kwani jibu
bado halijaandikwa.
HAIJAPANGWA
kuwa TUTASHINDWA au
TUTAFANIKIWA. Jibu litapatikana katika
MIOYO yetu , katika
MATUMAINI yetu , katika
IMANI yetu NA
KUJIPA MOYO na
katika kujaribu kufikia
KILELE CHA MAISHA.
YOTE yanatutegemea SISI. Ni
maneno matatu tu
lakini hayo ndiyo
TEGEMEO LA HATIMA
YETU. Kitabu kinachozungumzia MAISHA
YA BAADAYE bado
hakijaandikwa. Leo ndiyo tunakiandika. Hakuna
anayeweza kusema kuwa
sura ya mwisho
itakuwa ipi .
KAZI YA
LEO ndiyo itakayotoa MAFANIKIO
YA KESHO , KUJITOA
MHANGA kwa leo
ndiko
kutakakotuthibitishia ushindi mkubwa
wa kesho. TULITAFAKARI
VIZURI JAMBO HILI. Ni
muhimu kwa FURAHA
yetu na kwa
ustawi wa jamii
na taifa.
Mnaonaje kama
kila mmmoja atajiendeleza mwenyewe
kwanza ? MTAZAMO WA
MAISHA yetu uwe
kwa ajili ya
wote lakini ukionesha kiwango
cha tabia ya
mtu binafsi.
KADRI WATU
WAZURI walivyo wengi
katika jamii , ndivyo maisha
ya jamii yatakavyozidi kuwa
mazuri . Kadri jamii inavyozidi
kuwa na watu
wengi wenye BUSARA , ndivyo wawakilishi watakavyozidi kuwa
na BUSARA.
MASHIRIKA yote
ya kijamii lazima
yashughulikie ustawi wa
jamii. MASHIRIKA lazima yawanufaishe watu
binafsi na si
watu binafsi kuyanufaisha mashirika.
CHOCHOTE tunachokiwazia kuhusu
MAISHA YA LEO
lazima kiambatane na
IMANI , lakini IMANI
hiyo izingatie MAISHA
YA MTU KIROHO
NA KIMWILI.
Haiyumkiniki tuna
upeo gani wa
kufikiri , ukweli hubakia kuwa
kwa kiasi kikubwa
tumeyatelekeza mambo ambayo
yanachangia kuwa katika
mazingira mazuri ya
kuishi. Ukweli wetu umetusababishia maisha
yaliyokamilika , lakini maisha yetu
ya KIROHO yana
upungufu na hatuwezi
kujiendeleza kiasi cha
kuwiana na wakati.
HICHO ndicho
kilio chetu. TUJIULIZE
wenyewe ni kitu
gani kinasababisha TUSIRIDHIKE NA
MAISHA. Ni wakati
wetu sasa
wa kuwa WACHUNGUZI
WA MAMBO , badala
ya kuwa watafutaji tu , hatua
ambayo inahitaji kufanya
mambo kwa undani
zaidi kuliko kijuu
juu.
Asante mdau wangu kwa
kusoma MAKALA haya , mshirikishe mwenzako.
MAKALA hii imeandikwa
na MWL. JAPHET
MASATU anapatikana kwa
EMAIL: japhetmasatu@yahoo.com. MOBILE : +255
716 924 136 . WhatsApp
+255 755 400 128 .
No comments:
Post a Comment