KAMA tukiangalia jamii
kwa ujumla au
kila mtu binafsi , jambo kubwa
ambalo linadhihirika kwetu
katika zama hizi ,
ni dhana ya
maendeleo ya MALI
inayoambatana na kutoendelea
kwa kiroho. Ni hali
ambayo ipo wazi
sana.
Kuna sauti
nyingi sana zinazodai
kuwa mwanadamu ameendelea
sana katika Nyanja
ya mali , na
bado nguvu anayoionesha
wakati anapodhibiti misingi
ambayo imeelekezwa kiusahihi , huweza kubadilisha
maisha yake ya
ndani.
Si ufahamu
ambao umeshindwa kumwezesha
mwanadamu kupata USHINDI
wa kimaisha. Kama tunayachunguza kwa
undani mawazo ya
zama zetu , yanaonekana kuzingatia
zaidi CHAKULA , MALAZI, MAVAZI ,BURUDANI ,
FARAJA na USALAMA , pamoja na
tabia ya kutojali
hata kidogo “ na ya
“ kujijali mwenyewe tu “
na dhana ya
“ SHAURI YAO
WOTE.”
Mazoea ya
kuzingatia mali tu
katika maisha ambayo
yamekithiri sana siku
hizi , ndiyo yanayochangia kiasi
kikubwa matatizo ya
watu binafsi , KITAIFA na
KIMATAIFA. DUNIA ya leo
imekumbwa na UBINAFSI , UCHOYO , KUTORIDHIKA
na KUTOVUMILIA.
HAKIKA ,
maisha katika ulimwengu
huu mpya huzua
matatizo ya aina
nyingi. Hakuna kinachoaminika. MATUKIO
huambatana na mwendo
wa radi. MAADILI
ya kiubinadamu mara
nyingi hudharauliwa. UKOSEFU WA
USALAMA umetanda kila
mahali.
MAISHA yamekuwa
magumu kupita mategemeo
ya watu wa
karne iliyopita. Kama suluhisho
litaweza kupatikana kwa
matatizo yetu ya
kutatanisha na kusumbua , ni lazima tuzingatie
MAADILI fulani fulani
na viwango vya
KIROHO katika MAISHA.
Mwanadamu hawezi
kuishi kwa MKATE
tu , anahitaji CHAKULA CHA
KIROHO ili maisha
yake ya kiroho
yaweze kustahimili vikwazo
na matatizo ya nyakati hizi
mpya. Moja ya mahitaji
muhimu ya mwanadamu
ni DINI ya
namna fulani , njia ya
kutokea mwelekeo wa
KIROHO.
MWANADAMU ana
msukumo unaomwelekeza kutaka
kuabudu –ni moja ya
misukumo muhimu ambayo
anayo , hitaji linalomtawala.
Huwa pia
na msukumo unaomfunga KIROHO –kutoendelea KIROHO
kunakoambatana na KUPENDA
MALI. Na hiki ndicho
kinachoonekana kutokea siku
hizi –kuhubiriwa kwa INJILI
isiyo na
TOBA ambayo inazingatia
upatikanaji wa MALI
ambazo zinasababisha KUZOROTA
KIROHO.
KATIKA kusisitiza MAISHA YA
KIROHO , kuna mambo mengine
ambayo ni lazima
yazingatiwe. ULIMWENGU WA LEO
unaonekana kuwa PARADISO
inayopotosha watu KIUCHUMI
ambayo huwavuta watu
wengi , dhana ya
USALAMA isiyo sahihi.
Lakini , ili tuweze
kuendelea kuwepo kama
taifa au kufanikiwa
kila mmoja binafsi , ina maana
lazima yawepo mapambano makubwa
ya KUJITOA SANA ,
bila kukata tama.
HUU NI
UKWELI ambao ni
vigumu kukabiliana nao ,
hata hivyo unabaki
kuwa ukweli mtupu. Kwani kuanzia
MTU ANAPOZALIWA HADI KUINGIA
KABURINI , MAISHA MAANA YAKE
NI MAPAMBANO YASIYOKWISHA. HII
SI KWA WANADAMU
PEKEE , BALI PIA KWA
MIMEA NA WANYAMA –KUANZIA MBUMBUMBU
HADI MWENYE AKILI
SANA.
Hakuna kitu
kinachotembea kinachoweza kuepuka
mapambano ya kimaisha , wala hakuna
kinachoepuka mapambano kinachoweza
kutembea.MAHALI ambapo misingi
ya ndani ya
kimaisha inachangamka ,
bidii na kuhangaika
ndiyo njia nzuri
ya maendeleo.
Kama ni
WANAWAKE na WANAUME
tu watakubaliana na
ukweli huu , utawaletea maisha
ya kiutajiri na
kutosheka sana. Lakini
kuna wengi ambao
bado wanaamini jambo
bila sababu yoyote.
Hawajagundua kuwa matatizo yanayotokea
miaka hii yanatoana
na mazingira yanayotaka kuwaamsha
na kuwainua KIMAFANIKIO.
Kuishi kimafanikio ni
kupambana , na kila
anayepambana sana mara
nyingi huwa na
FURAHA nyingi . Tunaweza
tukawa wapiganaji au
tukawa mstari wa
nyuma katika mapambano ;
sifa zetu zinaweza
kuharibiwa kwa KUKATISHWA
TAMAA au KUPATA
MATUMAINI. Uchaguzi ni
wako ndugu yangu !
Asante kwa kusoma
makala hii , mshirikishe mwenzako !!
Makala hii imeandikwa
na MWL. JAPHET
MASATU anapatikana kwa
namba + 255 716 924 136 /
WhatsApp + 255 755 400128 ,
EMAIL , japhetmasatu@yahoo.com.
No comments:
Post a Comment