Ni kizazi gani
hiki kilichojaa mahangaiko
kwani tumekulia katika
mazingira yenye vurugu
na kizazi kijacho
kinakabiliwa na hali
ngumu ya maisha !
Kwani kila
jambo jipya katika
MAISHA limeongeza uchovu
na fadhaha katika
MWILI, MAWAZO na ROHO. Kuongezeka kwa
mwendo wa jinsi
ya kufanya mambo
mbalimbali kumeongeza HOFU , tunaomba MUDA
wa kufikiri juu
ya ghasia za
sasa.
Tungefurahi sana
kama tungepata mahali
pa kupumzikia kando
ya barabara japo
kwa muda mfupi , lakini hatujapapata mahali
pa namna hiyo.
Hatuna hata
uhakika kama tupo
katika njia sahihi
lakini tunasonga
mbele kwa ushujaa
huku tukihitaji unafuu
au mapumziko na
wengine tukiondoa matatizo
yaliyomo mioyoni mwetu.
Tuna msukumo
mkubwa sana wa
kuwa katika haraka.Ghasia zipo
katika damu zetu
na hali hiyo
ni tofauti na
tabia za vizazi
vilivyopita vilivyoishi kwa
AMANI. Si rahisi kukiri
kwamba kulikuwa na
hali hiyo ama
maisha ya wakati
wao yalikuwa tofauti
na ya kwetu ,
lakini tunawaonea WIVU.
Kuna siku
saba tu katika
wiki na saa
24 kwa siku. Tumebadilisha mambo
mengi sana lakini
hatuwezi kuzidisha siku
wala kurefusha saa, bali
tunajiona hatuna muda
wa kutosha.
Katika misukosuko
yote hiyo tunatafuta kitu
fulani. Hatuna uhakika ni
kitu gani tunakitafuta , lakini
tuna uhakika kuwa
mahali fulani kuna , lakini tuna
uhakika kuwa mahali
Fulani kuna jambo
litatupatia faraja kama
tungefahamu mahali pa
kukipata.
Tunachojua ni
kuwa maisha hayajakamilika lakini
katika kuhangaika kwetu
na kuharakisha kwa
hatua za maisha
yetu kunaambatana na
haraka ya kukata
tamaa ambayo inatufanya
tuendelee kutafuta jambo
ambalo tunafahamu kuwa
tunapaswa kumiliki.
MAADILI ya
zamani hayathaminiwi tena. Tunajikuta tukiwa
tumenasa kwenye shughuli
ambazo tukiwa hatuna
shauku nazo huku
MUDA ukipata pasipo
na jambo la
kufanya.
Tunakosa KUSOMA
VITABU vya kutuwezesha KUTAFAKARI
au KUOANISHA mambo
ambayo wazazi wetu
waliwahi KUVISOMA na
KUFAIDI. Tumechoka kwa kukaa
bila kazi na
kukosa watu wa
kuzungumza nao na
pale tunapojaribu kukaa
kimya ., tunajikuta tukiwa tumechanganyiwa na
kujawa na
hasira kisha kulazimika
kukimbilia kufanya jambo
ambalo litatuangamiza wenyewe.
Hali hii
inanifanya nikumbuke kisa
cha mzee mmoja
aliyetumia siku zake
katika kona ya
chemli na wakati
kijana mmoja alipomwuliza alifanya
nini siku nzima , alijibu : “
Vema , nakaa hapa na
kufikiri , na wakati
mwingine nakaa tu
bila kufanya lolote.”
MZEE huyo
alikuwa na kicheko
cha chinichini ambacho wengi wetu
hatukijui. Tunapaswa
kujifunza kuwa WAPWEKE
na FIKRA zetu
na wakati mwingine
bila fikra zetu.
Kuna mambo ambayo
katika maisha yetu
ni magumu sana
kuyatamka. Kuna hali
ambayo inabidi kuifurahia
na dhana ambazo
husababisha kufarahia hasira.
MAWAZO
na MATENDO ni
mambo mawili ya
sehemu moja. Chukua mambo
yote mazuri yaliyofanyika siku
nzima , SAMEHE MABAYA
yote yaliyofanywa kwetu
na kuwasamehe ndugu
na rafiki zetu
kwa masumbufu yote
waliyotusababishia.
WENGI WETU
hufikiria kupata MAFANIKIO
au mambo mazuri
kirahisi rahisi tu. TUTOE
KIPAUMBELE kwenye mambo mazuri
yanayotokea katika siku.
UZURI huwepo
pia katika dunia
hii ambayo watu
wanakabiliwa na hali
ngumu ya maisha , hivyo tuuabudu
uzuri , hali tukiwa
hatukosi KUFAHAMU UBAYA
WA UKWELI katika
sehemu nyingi za
ulimwengu. Hii ndiyo itakuwa
nguvu yetu ya
kutuimarisha mika iliyosalia katika
maisha yetu.
Asante kwa
kusoma MAKALA hii ,
mshirikishe mwenzako.
MAKALA hii imeandikwa
na MWL. JAPHET
MASATU , anapatikana kwa
+255 716 914136 , WhatsApp + 255
755 400
128. EMAIL :
japhetmasatu@yahoo.mail.
No comments:
Post a Comment