HAKIKISHA! Siku Zote Unapopambana Na Changamoto Yoyote Ile Usisahau Kutumia Mbinu Hizi Muhimu Zenye Matokeo Ya Haraka…!
Rafiki yangu mpendwa,
Katika maisha lazima ujue kila wakati unaweza kukutana na changamoto.
Na
watu wanasema kila ukitoka kwenye changamoto moja utaingia kwenye
changamoto nyingine, duniani hapa kama hauko kwenye changamoto basi
utakuwa umetoka kwenye changamoto au unaelekea kwenye changamoto
nyingine.
Shida
sio changamoto unazokutana nazo, tatizo kubwa ambalo watu linawakabili
ni namna ya kushughulika na changamoto ambazo zile zinatokea katika
maisha yao.
Na
Leo lingependa nikwambie namna ambavyo unaweza kutoka kwenye changamoto
yoyote inayokukabili, inawezekana leo upo kwenye changamoto kwenye
taaluma yako inawezekana leo upo kwenye changamoto ya mahusiano yako au
upo kwenye changamoto ya kiuchumi, au upo kwenye changamoto ya kazi,
kazi unayofanya au eneo lako la kiofisi au kwenye biashara yako.
Bila
kujali upo kwenye changamoto ipi kuna maeneo manne ukiweza kuyazingatia
yatakusaidia sana kutoka kwenye changamoto yako tena kwa haraka.
Kumbuka tena washindi ni wale ambao wakipita kwenye changamoto wanaondoka kwenye changamoto zao kwa haraka sana bila kuchelewa.
Jambo
La Kwanza; Ambalo unatakiwa kulifahamu katika maisha yako ni kwamba
unapopitia changamoto USIKUBALI ile hali ya kujiambia changamoto yako ni
SPESHO.
Changamoto
SPESHO, maana yake ni kuna watu wanafikiri wanapopitia matatizo ni wao
ndio wa kwanza kupitia katika matatizo hayo na hakuna mtu mwingine
yeyote aliyepitia katika changamoto hiyo.
SI KWELI, ukiwa na fikra ya namna hiyo utashindwa kabisa kukabiliana na changamoto yako.
Changamoto
yoyote leo unayokutana nayo, cha kwanza ambacho ningependa nikuambie.
Kuna mtu ameshawahi kukutana na changamoto kama hiyo, na katika wale
waliokutana na changamoto kama hizo hakika wako ambao wameshinda hizo
changamoto.
Lakini
kuna mtu leo anapitia changamoto kama ya kwako na hakika anaweza
akashinda pia, wewe ukajua na kufikiri kwamba changamoto yako ni SPESHO
na hakuna mtu ambaye anachangamoto kama ya kwako, hakika hautavuka,
hautatoka katika hiyo changamoto.
Kuna
watu ambao wakipitia matatizo wanaona changamoto yao hakuna mtu
mwingine yeyote mwenye nayo. Wanaona kama lile tatizo ndio mara yao ya
kwanza wanalipitia duniani yaani ni kama limevumbuliwa hakuna mtu
mwingine ambaye amekutana nalo.
SI
KWELI, usikubali hata siku moja kwamba changamoto yako ni SPESHO hakuna
mtu mwenye changamoto kama hiyo, ukiwa na fikra kwamba changamoto yako
ni spesho , hautapata uvumbuzi mapema na utaona hakuna msaada.
Cha
kwanza kabisa kataa fikra inayokuambia changamoto yangu ni spesho
hakuna mtu kama mimi, mtu aliyopo kama mimi, hakuna mtu aliyepata
matatizo kama mimi.
SI KWELI, wako wengi na wameshinda na wewe unaweza kuishinda.
Jambo
La Pili; Unalotakiwa kulifahamu ni kwamba changamoto yoyote unayopitia
ni SAIZI YAKO, watu wengi ambao changamoto zinawazidi sio kwa sababu
wanashindwa kuzitatua kwa sababu walikata tamaa.
Ningependa
nikuambie changamoto yoyote ile unayokabiliana nayo leo ya KIFEDHA, ya
KIMAHUSIANO, ya KITAALUMA, KAZINI KWAKO au kwenye BIASHARA, inawezekana
kabisa umekosa usingizi kabisa kwa sababu ya changamoto inayokukabili.
Ninachotaka nikuhakikishie ni kwamba changamoto hiyo unayokutana nayo leo ni SAIZI YAKO.
Ukiwa
na fikra ya namna hiyo tafsiri yake ni kwamba utafanya kila unachoweza,
kuweza kukabiliana nayo, unapokubali kwamba changamoto hii ni SAIZI
YAKO. Unaulazimisha ubongo wako kutafuta suluhisho unaposema changamoto
hii imenizidi umri unauambia ubongo wako ila tu kwa sababu hakuna kitu
ninaweza kufanya.
Ninachotaka kukuambia ni kwamba changamoto ni saizi yako, ya mambo unayopitia leo.
Jambo
La tatu; Ambalo ni la msingi sana, kulijua katika kutoka kwenye
changamoto unayokutana nayo ni kujua katika kila changamoto KUNA MLANGO
WA KUTOKEA, kuna njia za wewe kutoka kwenye changamoto ukweli ni kwamba
hukuuona huo mlango wakutokea.
Ukweli
ni kwamba haujaona njia za kutoka kwenye changamoto zinazokukabili
haimaanishi kwamba changamoto yako imekosa suluhisho, kuna suluhisho
kwenye changamoto yako inawezekana haujaiona ndio maana tunasema kama
leo unapitia changamoto usikubali tu kukaa nyumbani, usikubali tu kukaa
ndani, usikubali kujifungia, tafuta watu uzungumze nao, nenda mahali
toka nje fuatilia kitu fulani utapata suluhisho.
Hakuna
changamoto ambayo haina suluhisho katika maisha hata ya kwako, iwe
inawezekana umefika sehemu unasema kwamba nimejaribu kila nilichofanya
kupata suluhisho.
SI KWELI, changamoto uliyonayo ina suluhisho kama hutokata tamaa utapata suluhisho ya changamoto yako.
Jambo
La Mwisho; Ambalo litakusaidia kutoka kwenye changamoto ambayo
inakukabili sasa hivi kwa haraka sana nikijua kwamba changamoto
zinapokuja saa zingine zinatuepusha na mabaya makubwa ambayo hatuyaoni.
Kuna
watu wengi sana wanapitia changamoto za mahusiano na kusema yule
nilimpenda sana, nikajitolea na leo hayupo tena kwenye maisha yangu,
kuja kugundua kwamba hapana kumbe ni sababu ya wao kupata watu sahihi
zaidi, kuna watu walifukuzwa kazi, kuna watu waliondolewa ofisini kwa
kudhalilishwa lakini leo wanamiliki makampuni yao au wengine wamepata
kazi kubwa zaidi.
Kwa
hiyo kila wakati unapokutana na changamoto uwe na jicho la ziada la
kuangalia usiangalie kile tu ulichokosa lakini pia kuna kitu ambacho
kiko leo.
Kwa
nini inakuwa hivyo mara nyingine tukiambiwa tuache vya sasa hivi
tulivyonavyo ili tupate bora, tulivyoandaliwa mbele yetu hatutakuwa
tayari kufanya maamuzi magumu ya namna hiyo kwa sababu yanatuumiza,
lakini changamoto zinakuja pia kutuepusha na mabaya ambayo kwa macho ya
kawaida hatuyaoni, ndio maana changamoto unayopitia leo ni mbaya na
inakuumiza sana.
Lakini kesho utamshukuru mungu na kusema afadhali nimepitia hii changamoto. Kwa sababu imenisaidia kuwa hivi nilivyo sasa.
KAZI KWAKO MDAU WANGU .
TUWASILIANE KWA
( WhatsApp + 255 716924136 ) kwa USHAURI NA MAONI YAKO WEWE UNASEMAJE ??