Leo nimeamua nikusogezee mada hii kwenye macho yako kwani imekuwa changamoto na kuathiri utendaji kazi wa watu wengi.
Ukweli ni kwamba akili zetu sisi binadamu ni kitu cha ajabu sana, ni kitu ambacho kina nguvu ya kufanya makubwa kuliko tunavyoweza kutegemea.
Lakini cha kushangaza ni kwamba, mtu anaweza kuitawala akili yake akafanya makubwa, au akatawaliwa na akili yake na kuwa mtumwa maisha yake yote.
kuhusu ubongo wa binadamu ni kwamba una nguvu za ajabu lakini watu wengi hutumia sehemu ndogo sana ya nguvu hiyo.
Asilimia kubwa ya watu huishia kufanya mambo ya kawaida, hivyo hupata matokeo kawaida na kuishi maisha ya kawaida (routine life).
Lakini kundi lingine ni watu ambao ni asilimia ndogo ambao hufikia viwango vya juu vya ufanisi/ nguvu za ubongo wao.
Kundi hili hufanya mambo makubwa na huwa na maisha tofauti na kundi la kwanza.
Tofauti ipo kwenye namna tunavyotumia bongo zetu, uamuzi upo mikononi mwako.
Ujenge au ubomoe.
Uzuri mpaka hapa umeshajua upo kundi gani.
Kama tayari tuendelee…
Ubongo wetu unaweza kutunza taarifa mbalimbali kwa muda, ambazo baadae huenda kwenye subconscious mind.
Ili taarifa zivuke kwenye subconscious mind, hupita kwenye mfumo RAS ( Recuticular Activating System) ambapo taarifa huchujwa.
Ili kundi lingine huruhusu vitu vya kimazingira kuingia ambavyo huathiri maamuzi na kisha utendaji.
Kwa bahati mbaya huwezi kufikia viwango vya juu vya ufanisi ikiwa muda mwingi umezungukwa na usumbufu.
Hivyo unapaswa uwe na ufahamu juu ya vitu gani vinavyokuletea usumbufu na kuweza kuvidhibiti mara moja.
Kuna maelfu ya watu walipitia hali kama hii na wakafanikiwa kutoka mimi ni miongoni mwao, hata wewe leo hii unaweza kutoka kwenye hali hii.