Watu
huwa hawapendi kubadilishwa, na wakigundua mtu anataka kuwabadilisha
basi wanaleta upinzani mkubwa kuhakikisha hilo halitokei.
Watu
huwa wanaweza kubadilika kama watachagua kubadilika wao wenyewe, lakini
siyo kulazimishwa kubadilika, hivyo ndivyo saikolojia ya binadamu
ilivyo.
Hivyo usijisumbue kumbadili mtu yeyote yule, hutaweza, utaishia kuibua tu migogoro isiyo na manufaa.
Kama
unataka mtu mwenye sifa fulani, mtafute mtu mwenye sifa hizo na siyo
kumchukua yeyote na kujiambia utambadilisha, unajidanganya.
Kwenye
mahusiano, iwe ni ya mapenzi au ndoa, chagua mtu ambaye sifa alizonazo
sasa unaweza kwenda nazo na siyo kujiambia utambadilisha.
Kwenye ushirikiano wa biashara au kazi, chagua kushirikiana na mtu ambaye sifa unazoziona sasa kwake unaweza kwenda nazo.
Na hata unapoajiri, angalia sifa ambazo mtu anazo na kama unaweza kwenda nazo.
Usijidanganye kwamba sifa fulani ambayo mtu anayo unaweza kuibadili, unatafuta matatizo wewe mwenyewe.
Mtu
mmoja amewahi kuulizwa anawezaje kuwafanya wafanyakazi wake kuwa na
tabia nzuri, alijibu kwa kusema; “siwaambii wafanyakazi wawe na tabia
nzuri, bali naajiri watu ambao tayari wana tabia nzuri”.