BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Friday, August 30, 2019
Saturday, August 24, 2019
Sunday, August 18, 2019
HAKUNA ANAYEKOSEA KWA MAKUSUDI.
Upo
msingi wa ustoa ambao utakuwezesha kuishi maisha yako kwa utulivu bila
ya kujali wengine wanasema au kufanya nini. Moja ya vitu ambavyo
vinatusumbua sana zama hizi ni mambo ambayo wengine wanasema au
wanafanya. Huwa tunayaruhusu yatuumize, tukiamini kwamba watu hao
wanafanya mambo hayo kwa makusudi ili kutuumiza.
Lakini
wastoa wanatuambia kwamba, watu wanaofanya mambo ambayo yanatuumiza,
hawafanyi hivyo kwa makusudi, bali wanafanya hivyo kwa sababu hawajui
kulicho sahihi kufanya. Hivyo hupaswi kuumia kwa sababu yao, badala yake
unapaswa kuwaonea huruma na kuona kama kuna namna unaweza kumsaidia ili
asiendelee kukosea.
Mfano
mzuri ni pale mtoto mdogo anapokupiga kofi, je utarejesha kwa kumpiga
kofi pia? Je utakasirika? Je utamnunia? Je utasema amekudharau? Majibu
hapo ni hapana. Lakini vipi mtu mzima mwenzako akikupiga kofi? Hapo
mambo yanabadilika, unaona amekudharau, utataka kulipiza, utakasirika na
hata kumnunia. Lakini kama utachukulia mtu huyo amekupiga kofi kwa
kutokujua au kwa bahati mbaya, hutapata hisia hizo.
Hivyo
cha kujifunza hapa, tusikimbilie kuhukumu pale watu wanapofanya vitu
kwamba ni vibaya au wamedhamiria kutuumiza. Badala yake tuchukulie
kwamba watu hao hawajui wanachofanya au wamefanya kwa bahati mbaya, na
hilo litatuzuia sisi kuumia.
Mfano
mzuri ni kwenye wizi au utapeli, mtu akikuibia, badala ya kuumia,
unapaswa kumwonea huruma, kwa sababu kwanza hajui njia sahihi ya
kutengeneza kipato ambayo itampa maisha ya utulivu na pili, kwa tabia
yake hiyo, ataishia jela au kaburini, maana ataiba akamatwe na wananchi
wenye hasira kali hadi kufa, au apelekwe polisi na baadaye kufungwa.
Unaona jinsi ambavyo unaondoka kwenye upande wa lawama na kuwa upande wa
utulivu!
CHAGUA SHUJAA WA MAISHA YAKO.
Wastoa
wamekuwa wanaelewa umuhimu wa kuwa na mashujaa, watu ambao tunayapima
maisha yetu kupitia wao. Lakini hili ni eneo ambalo limekuwa na
changamoto kubwa sana zama hizi, kwa sababu kumekuwa na mashujaa wengi
feki. Siku hizi watu wanaoweza kutengeneza umaarufu rahisi kupitia
mitandao ya kijamii, sanaa, michezo au siasa ndiyo wanaonekana mashujaa
kwa wengi. Na wengi wanawafuata watu hao, lakini hakuna wanachojifunza
kwa sababu mwisho wa siku umaarufu wa watu hao huanguka, kwa sababu
haujajengwa kwenye misingi sahihi.
Ni
muhimu uchague mashujaa sahihi wa maisha yako, kutokana na misingi
wanayoiishi au waliyoiishi ambayo unaweza kujijengea kwenye maisha yako
na ukaweza kupiga hatua pia. Kadiri unavyojifunza falsafa hii na
kujifunza wengine walioiishi falsafa hii, utavutiwa na maisha ya baadhi
ya wanafalsafa na kuwachagua kuwa mashujaa wako.
JINSI YA KUKABILIANA NA MABADILIKO MAKUBWA YA MAISHA KIAFYA.
Kuna
wakati tunakutana na mabadiliko makubwa kimaisha kwenye afya zetu.
mabadiliko haya yanaweza kutuyumbisha sana kama hatuna msingi sahihi
tunaouishi. Mfano ni pale mtu anapopata ulemavu wa mwili ambao unaathiri
maisha na hata kazi za mtu. Wengi huvurugwa sana na mabadiliko ya aina
hii, kitu ambacho hupelekea maisha yao kudorora na hata kufa mapema.
Wastoa
wanatupa njia sahihi ya kukabiliana na mabadiliko ya aina hii, kwa
kutuambia tunapaswa kufikiria na kutumia kile tulichonacho na siyo
kuangalia tumekosa nini. Kama umepata ulemavu wa miguu, kumbuka bado una
mikono, macho, masikio, na viungo vingine, ambavyo kama utaweza
kuvitumia vizuri maisha yako yatakuwa bora.
Mmoja
wa wanafalsafa wa Ustoa, Epictetus, ambaye alikuwa mwalimu bora sana wa
falsafa hii, alikuwa mtumwa. Katika maisha yake ya utumwa, aliumizwa na
kupata ulemavu wa miguu. Hili lilimpa ulemavu wa maisha, lakini
hakuruhusu ulemavu huo uathiri maisha yake, aliangalia mambo gani
mengine anayoweza kufanya, kama kujifunza na kufundisha falsafa na siyo
kuangalia alichokosa.
Somo
muhimu la kuondoka nalo hapa ni usiweke nguvu zako kwenye yale
uliyokosa au kupoteza, badala yake weka nguvu zako kwenye yale uliyonayo
na jinsi unavyoweza kuyatumia kwa ubora zaidi.
FALSAFA YA USTOA NA UTAJIRI.
Kwenye Falsafa ya Ustoa, vitu vimegawanyika katika makundi matatu;
Kundi la kwanza ni vitu vizuri kufanya au kuwa navyo (virtues), ambavyo ni vinne; hekima, ujasiri, haki na kiasi.
Kundi
la pili ni vitu vibaya kufanya au kuwa navyo (vices), ambavyo ni
kinyume na hivyo vizuri, yaani, upumbavu, woga, udhalimu na tamaa.
Kundi
la tatu ni vitu ambavyo siyo vizuri na wala siyo vibaya (indifferent),
ambavyo hakuna ubaya kuwa navyo, lakini pia hupaswi kujitesa ili kuwa
navyo. Hapa vitu vingine vyote kwenye maisha vinaingia hapo, kuanzia
afya, kazi, biashara, fedha na kadhalika.
Sasa
kwa misingi ya ustoa, wengi hufikiri inawataka wawe masikini, watu
wasiojali fedha wala utajiri. Lakini katika historia, moja ya
wanafalsafa waliokuwa na maisha mazuri basi ni wastoa. Seneca alikuwa
tajiri mkubwa enzi zake na mwanasiasa, Marcus Aurelius alikuwa mtawala
wa Roma. Kwa kifupi wastoa walijihusisha na maisha ya kila siku na ya
kawaida, wakifanya yale ambayo kila mtu anafanya.
Na
hii ni sababu nyingine nzuri kwa nini tunapaswa kuwa wastoa, kwa sababu
ni falsafa ambayo haipingi mtu kuwa na fedha, au kujihusisha na mambo
mengine, kama tu hayavunji msingi wa wema.
Zipo
baadhi ya dini na falsafa ambazo zinawafundisha wafuasi wake kuachana
kabisa na mambo ya dunia, kutoa maisha yao kwa ajili ya falsafa au Mungu
pekee. Lakini wote tunajua maisha yana mahitaji yake, hutaenda kulipa
ada za watoto kwa falsafa, na wala hutaenda dukani kupata chakula kwa
kusema wewe ni mwanafalsafa.
Hivyo
kwa kuishi kwa falsafa ya ustoa, unakuwa huru kufanya upendacho, ila tu
kiwe sahihi kwako na kwa wengine, na pia unakuwa huru kujikusanyia
fedha utakavyo, ila tu ufanye hivyo kwa usahihi na kwa manufaa ya
wengine pia.
Na
kikubwa nilichojifunza ni kwamba ukiishi misingi ya falsafa ya ustoa,
una nafasi kubwa ya kuwa tajiri, lakini pia utakuwa huru na utajiri huo.
Kwa sababu kwanza utakuwa unafanya kilicho sahihi na kuachana na yasiyo
sahihi, pia utaepuka kufanya mambo ambayo yatakupotezea fedha, kwa
kudhibiti vizuri hisia zako. Lakini kilicho muhimu zaidi ni kwamba
hutafungwa na utajiri wako, hata kama utapoteza kila kitu, bado utabaki
imara na maisha yako yataendelea.
Naweza
kuhitimisha kwa kusema, Ustoa ni falsafa ya watu wakuu na matajiri,
najua unapenda kuwa mkuu, unapenda kuwa tajiri na kuwa huru na maisha
yako, hivyo basi, ijue na kuiishi misingi ya ustoa.
Subscribe to:
Posts (Atom)