Monday, July 15, 2019

JINSI YA KUPATA WAZO LA TOFAUTI NA WENGINE NA KUFANIKIWA

Katika kupata wazo bora, zingatia mambo yafuatayo;
Moja; anza na chochote unachojali sana.
Watu wengi wamekuwa wanafikiria kwamba ili uweze kuleta mabadiliko makubwa kwako na kwa wengine basi inabidi uwe na wazo kubwa na la kipekee sana. Wazo ambalo wengine hawajawahi kuwa nalo. Huo siyo ukweli, unaweza kuanza na wazo lolote na ukaweza kulijenga kwa utofauti na ukajitofautisha sana.
Anza na chochote unachojali, unachopenda, unachoamini, unachojua, ulichozoea au ambacho umesomea. Chochote kile ambacho unaona kinaweza kuwa bora zaidi ya kilivyo sasa, unaweza kukichukua kama wazo lako la kufanyia kazi.
Mbili; uliza maswali ambayo hayaulizwi.
Watu wamekuwa wanafanya mambo kwa mazoea kwa sababu wanafanya kile ambacho kila mtu anafanya, na hawathubutu kujaribu vitu vya tofauti. Sasa kwa wazo unalotaka kufanyia kazi kuliboresha zaidi, anza kwa kuuliza maswali ambayo watu wengine hawaulizi.
Maswali hayo yanaweza kuwa, vipi kama.... vipi kinyume cha... Hapa unajaribu kupata picha ya tofauti na wengi walivyozoea, kwa kuona upande wa pili wa vitu au kwa namna ya tofauti.
Tatu; angalia uzoefu wako binafsi.
Baada ya kujiuliza maswali ya tofauti kwenye wazo unalotaka kufanyia kazi, angalia uzoefu wako binafsi kwenye wazo hilo. Usijidharau kwa sababu labda huna elimu kubwa au uzoefu mkubwa kwenye jambo hilo. Labda siku za nyuma umewahi kujaribu kufanya tofauti na ukapata matokeo ya tofauti, hiyo inatosha kukuonesha kwamba kuna uwezekano wa kupata matokeo tofauti na ambayo watu wanapata sasa.
Nne; chagua eneo la ubobezi kwenye wazo lako.
Wazo unalokuwa nalo linaweza kuwa pana, sasa unahitaji kuchagua eneo ambalo utabobea kwenye wazo hilo ili kujitofautisha kabisa na wengine. Badala ya kutaka kufanya kila kitu, unachagua eneo moja ambalo utaweka muda na nguvu zako na kuweza kutengeneza ubobezi mkubwa. Ni kupitia ubobezi huu ndiyo unaweza kupiga hatua kubwa kwenye wazo hilo.
Tano; fanya utafiti.
Watu wengi wamekuwa wanapata mawazo mapya ya kuboresha zaidi, lakini hawanufaiki nayo kwa sababu huwa hawaweki kazi inayopaswa kuwekwa ili mtu kubobea kwenye kitu hicho. Moja ya kazi kubwa unayopaswa kuweka ni kufanya utafiti. Siyo kusoma tafiti, badala yake kufanya utafiti mpya, kwa kuangalia yale maeneo ambayo unataka yawe bora kisha kuja na njia bora za kuyaboresha kutoka kwenye tafiti mbalimbali zinazogusa wazo hilo.
Sita; unganisha mawazo.
Kuna maeneo mengine ambayo yameweza kupiga hatua kubwa, ambayo ni tofauti na wazo unalofanyia kazi wewe. hii haikuzuii wewe kujifunza kutoka maeneo hayo. Jifunze kupitia maeneo mbalimbali kwa hatua ambazo watu wameweza kupiga, kisha unganisha mawazo hayo na wazo unalofanyia kazi kuweza kuona jinsi gani ya kuboresha wazo unalofanyia kazi. Kumbuka misingi ya mafanikio kwenye kila eneo inafanana, hivyo kwa kuangalia jinsi ambavyo mawazo mengine yamefanikiwa, utaweza kufanikisha wazo lako pia.
Saba; tengeneza nguzo ya kubeba wazo lako jipya.
Baada ya kuchagua wazo unalotaka kuboresha, ukauliza maswali ya tofauti, ukatumia uzoefu wako, ukafanya utafiti na hata kujifunza kutoka maeneo mengine, unakuwa umejifunza mambo mengi sana kuhusiana na wazo lako jipya. Hapa unakuwa na maarifa na taarifa nyingi ambazo mtu mwingine siyo rahisi kuyaelewa. Hivyo ili wazo lako la kuboresha liweze kueleweka na kutumiwa na wengine, unahitaji kutengeneza nguzo ya kubeba wazo lako. Hapa unatengeneza mfumo unaobeba wazo lako jipya, kwa namna ambayo watu wengine wanaelewa jinsi linavyofanya kazi na matokeo ya tofauti yanavyopatikana.
Kwa hatua hizo saba, unakuwa umekamilisha wazo lako la tofauti, ambalo linaleta matokeo bora kuliko yale ambayo yamezoeleka. Baada ya hapo sasa unakwenda kwenye hatua ya pili ambayo ni kujenga wafuasi kwenye wazo lako.

FURAHA ZAO LA FEDHA-------------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

Ile kauli kwamba matajiri hawana furaha au huwezi kuwa na fedha na ukawa na furaha, ni mtego ambao watu wamekuwa wanajitengenezea wenyewe bila ya kujua.
Ipo hivi rafiki, wengi tunapokuwa tunaanzia chini, huwa tunafikiri tutakapopata fedha basi ndiyo zitakuwa jawabu la kila kitu. Hivyo tunaahirisha maisha yetu yote mpaka pale tutakapopata fedha.
Na hata kwa upande wa furaha, tunaahirisha furaha yetu tukiamini tukishakuwa na fedha basi ndiyo tutakuwa na furaha. Tunaacha kufanya yale mambo madogo madogo ya kila siku ambayo yanatuletea furaha, tukiamini kwamba tukishakuwa na fedha nyingi, basi furaha itakuja yenyewe.
Lakini hilo ni kinyume kabisa na msingi wa furaha, fedha haileti furaha, bali furaha inaleta fedha. Kwa kifupi ni kwamba fedha ni zao la furaha, na siyo kama wengi wanavyofikiri kwamba furaha ni zao la fedha.
Hivyo basi, usiahirishe furaha yako sasa kwa sababu unatafuta kwanza fedha na unafikiri ukishakuwa nayo basi utapata furaha. Badala yake ishi maisha yako kamili sasa, fanya vile vitu vidogo vidogo vinavyoleta furaha kwenye maisha yako na hivi vitakuwezesha kupata fedha zaidi na kwa kutokutumia nguvu kubwa kama unavyofanya unapokuwa huna furaha.
Usipuuze kitu chochote muhimu kwenye maisha yako kwa sababu unakazana kupata fedha, weka kipaumbele chako kwenye furaha na fedha itakuwa matokeo.
Jipende wewe mwenyewe kwanza, fanya kile unachopenda na zungukwa na wale wanaokupenda, haya yatakuletea furaha na furaha yako itavutia fedha zaidi kwako.
Fuata hili na hutafikia kwenye hali ya wengi ambao wana fedha lakini hawana furaha, wewe tayari unayo kanuni ya kuwa na furaha na kuwa na utajiri kwa wakati mmoja. Ifanyie kazi.

FEDHA KAMA WAZO ----------------------------" Fursa Afrika Mshariki Blog "

TENGENEZA GEREZA LA AKIBA --------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "

MBINU YA KUONGEZA KIPATO 2019 ----------- " Fursa Afrikan Mashariki Blog.

USIOGOPE KUWAAMBIA WATU WAKULIPE.

Watu wengi wanaofanya biashara za huduma, hasa za ushauri au mafunzo, huwa wanaanza kutoa huduma hizo bure ili watu wawajue. Ni vigumu sana kuanza kwa kuwachaji watu fedha ndiyo uwashauri au kuwafundisha mambo mbalimbali.
Hivyo mtu anapoanza kutoa huduma zake bure, watu wengi wanamfuatilia na kujifunza au kunufaika na huduma hizo kama ni za ushauri au nyinginezo.
Sasa mtu anaweka juhudi kubwa kutengeneza wafuasi wengi, akiwa na lengo kwamba watu wanaomfuatilia wanapokuwa wengi na wengi zaidi kuhitaji huduma zake, basi anaweza kuwatoza ada na kutengeneza kipato.
Lakini unapofika wakati wa kuwaambia watu wakulipe ili kuendelea kupata huduma ambazo umekuwa unawapa bure, wengi huwa wanaogopa. Wengi wanajenga hofu hii pale wanapoanza kuwaambia watu kuhusu malipo na watu hao wakawaambia hawakutegemea kulipia ushauri au mafunzo yanayotolewa.
Watu wengi ambao wamekuwa wananufaika na mafunzo hayo ya bure watapinga sana pale mtu aliyekua anatoa mafunzo hayo bure anapoanza kutoza ada. Na hili limekuwa linawafanya wengi kushindwa kuendelea na huduma zao na hivyo huduma hizo zinakufa.
Nikuambie leo rafiki yangu, kama unaendesha huduma yoyote ile, iwe ni ushauri, uandishi, ukocha, au huduma ya kiimani, lazima ujue kwamba ili huduma hiyo iendelee unahitaji njia ya kukuingizia kipato. Hivyo basi usiogope kuwatoza watu fedha pale wanapohitaji huduma zaidi kutoka kwako.

Wednesday, July 10, 2019

FURSA 28 KATIKA SEKTA YA MICHEZO NA BURUDANI -------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "

 SEKTA YA  MICHEZO  ina  fursa  nyingi  sana  ambazo  zinaweza  kumnufuaisha  MJASIRIAMALI  mwenye  hari  ya  kuwekeza  kwenye  sekta  hii. Gundua  fursa  unazoweza  kufanya  kwenye  sekta  ya  michezo.

Je, wewe  ni  mpenzi  wa  BURUDANI  ? Je,  umewahi  kujiuliza  watu  kwenye sekta  hii  wanapataje  pesa ? Basi  hilo  lisikupe  maswali  mengi  sana  kwa  sababu mimi   MJASIRIAMALI  nipo  wewe  katika  kila  jambo.Fuatilia " Darasa  la  Semina  kujua   fursa  unazoweza  kuwekeza  kwenye  sekta  hii  ya  burudani.


MUHIMU : Ili   kuendelea  Kujifunza  Zaidi na  Kugundua  FURSA  mbalimbali zilizojificha katika  
'SEKTA   YA MICHEZO & BURUDANI "jiunge   na   "FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG "  na    " DARASA  LA  SEMINA "   kwa  kulipa  ADA  YA  UANACHAMA ( Tshs 10000  kwa  Mwezi ) ili   uweze  Kuzigundua na  kujifunza " FURSA  ZINAZOKUZUNGUKA " na  Kuzifanyia  Kazi na  KUFANIKIWA.

Ndimi  Rafiki na  Kocha  Wako  Mwl    Japhet  Masatu , Dar  es  salaam ,Tanzania , Afrika   Mashariki , 

Kama   hujajiunga  na  "  FURSA  AFRIKA  MASHARIKI  BLOG " na  "DARASA  LA  SEMINA "  tuwasiliane   Kwa  Maelekezo  Zaidi


WhatsApp /  Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539


ULIZA  MASWALI , TOA  MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO  kwa  Email  hii:-  EMAIL fursaafrikamashariki@gmail.com