BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Thursday, July 4, 2019
Wednesday, July 3, 2019
Tuesday, July 2, 2019
FURSA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI, UCHUKUZI NA UTALII
Sekta
ya Usafirishaji ni sekta ya mamilioni ya PESA duniani kote .
Kila kukicha watu wanasafiri : kuwe na mdororo wa kiuchumi watu
watasafiri hivyohivyo. Sasa ni kwanini usitupie jicho lako
kwenye sekta hii na uanze kutengeneza PESA ? Kama unataka
kufanya uwekezaji kwenye sekta hii.
Biashara ya Usafirishaji ni biashara pana ambayo inajumuisha magari ya abiria na magari ya mizigo. Ni biashara yenye faida sana , inayohitaji MTAJI mkubwa na usimamizi wa hali ya juu ili kudhibiti WIZI WA MAPATO.
Kwa Kujifunza Zaidi na Kugundua FURSA zilizojificha katika SEKTA hii ya " USAFIRISHAJI , UCHUKUZI NA UTALII JIUNGE NA " DARASA LA SEMINA AU " FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " KWA KULIPA ADA YA UANACHAMA ili uweze Kuzifanyia Kazi na KUFANIKIWA.
Ndimi Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Afrika Mashariki , Tanzania
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
EMAIL : fursaafrikamashariki@gmail.com
Biashara ya Usafirishaji ni biashara pana ambayo inajumuisha magari ya abiria na magari ya mizigo. Ni biashara yenye faida sana , inayohitaji MTAJI mkubwa na usimamizi wa hali ya juu ili kudhibiti WIZI WA MAPATO.
Kwa Kujifunza Zaidi na Kugundua FURSA zilizojificha katika SEKTA hii ya " USAFIRISHAJI , UCHUKUZI NA UTALII JIUNGE NA " DARASA LA SEMINA AU " FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " KWA KULIPA ADA YA UANACHAMA ili uweze Kuzifanyia Kazi na KUFANIKIWA.
Ndimi Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Afrika Mashariki , Tanzania
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
EMAIL : fursaafrikamashariki@gmail.com
Monday, July 1, 2019
VITU VIWILI VINAVYOITOFAUTISHA BIASHARA YAKO NA ZINGINE.
“The
core values and the purpose of a business are what distinguish it from
every other business and mark it, throughout its lifetime, as special.
Economies cycle, technology marches on, customer tastes change, and
industries come and go, but the DNA of great businesses, regardless of
how they evolve over time, stay the same, just as we humans remain the
same as we transition from infancy through adolescence to maturity and
old age.” – Dick Cross.
Biashara
zinazofanikiwa huwa zina upekee ambao haupo kwenye biashara nyingine
yoyote ile. Hata kama kwa nje biashara hiyo inaonekana kufanana na
nyingine, lakini kwa ndani ipo tofauti kabisa. Na utofauti huo wa ndani
ndiyo unaoifanya biashara ifanikiwe sana.
Kuna
vitu viwili ambavyo vinatofautisha biashara yoyote ile, vitu hivyo ni
misingi au maadili ya biashara na kusudi la biashara. Misingi ni kile
ambacho biashara inasimamia, ile miiko ambayo biashara inasimamia katika
uendeshaji wake. Na kusudi la biashara ni ile sababu ya biashara
kuwepo, kile kitu cha tofauti ambacho biashara hiyo inafanya kwa wateja
wake.
Vitu
hivi viwili, miiko na kusudi ndiyo DNA ya biashara yoyote ile. Hivi
ndiyo vinaifanya biashara iweze kusimama licha ya kuwepo kwa changamoto
mbalimbali. Kama ambavyo mtu akikatwa mkono hazai mtoto aliyekatika
mkono, ndivyo hivyo pia biashara inaweza kuendelea vizuri licha ya
changamoto za nje, kwa sababu msingi wa ndani ni imara.
Kwa
biashara unayofanya au kutegemea kufanya, anza kujiwekea msingi au
miiko ambayo utaisimamia kwenye biashara hiyo. Kisha jua kusudi la
biashara hiyo kuwepo, inatatua tatizo au kutimiza mahitaji gani ambayo
watu wanayo. Ukiwa na vitu hivi viwili, utakuwa na biashara yenye
mafanikio makubwa.
VIPANDE VIKUU VINNE VYA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.
(1). WATEJA.
Wateja
ndiyo kipande cha kwanza muhimu sana cha biashara yako. Kama hakuna
wateja basi hakuna biashara. Lazima uchague biashara yako inakwenda
kuwahudumia watu gani, wanaopatikana wapi na unawafikiaje. Biashara
lazima ijenge wateja ambao wanaotegemea kwa kile inachofanya.
Unapoingia
kwenye biashara anza na kitu ambacho tayari watu wanajihitaji, hivyo
wewe unakuja na suluhisho na kuhakikisha watu wanajua uwepo wako kwenye
biashara hiyo. Hivi ndivyo unavyoweza kutengeneza wateja wa biashara
yako.
(2). MAHITAJI YA WATEJA.
Ukishachagua
aina ya wateja ambao biashara yako inawahudumia, unapaswa kujua yale
mahitaji yao ya msingi. Yale mahitaji yanayowasukuma kununua kile
ambacho wewe unauza. Ukishayajua mahitaji hayo, jipange kuyatimiza kwa
namna ambayo hakuna mfanyabiashara mwingine anayeweza kuyatimiza hivyo.
Kuna
vitu viwili muhimu sana unapaswa kujua kuhusu mahitaji ya wateja wako,
hofu na tamaa. Wateja wa biashara yako wanafanya maamuzi kwa kutumia
hisia hizo mbili, labda wana tamaa ya kupata kitu fulani au wana hofu ya
kupoteza kitu fulani. Jua hisia hizo mbili za wateja na zitumie katika
mauzo.
(3). NAFASI YAKO KATIKA SOKO.
Biashara
yoyote unayofanya, kuna nafasi ambayo upo kwenye soko, unaweza kuwa
ndiyo namba moja yaani wateja wanakufikiria wewe kwanza au ukawa haupo
kwenye namba za juu, yaani wateja hawakufikirii kabisa. Ili kukuza
biashara yako, unapaswa kuwa kwenye nafasi ya juu kwenye soko lako.
Unapaswa kuwafanya wateja wako wakufikirie wewe kwanza inapokuja kwenye
mahitaji yao.
Matangazo,
alama za kibiashara, rangi za kibiashara, kauli mbiu na hata utamaduni
wa tofauti wa biashara yako ni vitu vinavyowafanya wateja wakukumbuke na
kukufikiria muda mrefu. Tengeneza picha ya tofauti ya biashara yako
ambayo inawafanya wateja wakufikirie wewe mara zote.
(4). UBOBEZI WA BIASHARA YAKO.
Je
biashara yako imebobea kwenye nini? Biashara yako inajulikana kwa kipi?
Je ni kitu gani wateja wanapata kwako ambacho hawawezi kupata kwa
wafanyabiashara wengine?
Hayo
ni maswali muhimu ya kupima ubobezi wa biashara yako. Biashara
iliyobobea kwenye kile inachofanya ndiyo biashara ambayo inapata
mafanikio makubwa sana.
Jua
ni aina gani ya biashara unayofanya, na kipi cha tofauti unachotoa kwa
wateja wako kisha kazana kutoa kitu hicho kwa namna ambayo wateja
hawawezi kupata sehemu nyingine na utaweza kufanikiwa sana kwenye
biashara unayofanya. Bobea kwenye vitu vichache na hilo litakufanya
kinara kuliko kung’ang’ana kufanya vitu vingi.
Sunday, June 30, 2019
ASILI YA BIASHARA NI KUKUA NA KUFA.
Biashara
ni kiumbe hai. Inatungwa, inazaliwa, inakua, inafikia makamo na kisha
kufa. Hivi ndivyo mifumo yote ya maisha inavyokwenda. Kuanzia kwetu sisi
binadamu, kabla hujazaliwa mimba inatungwa, anazaliwa mtoto, anakua,
anafikia makamo na kisha anakufa.
Katika
mfumo huu wa ukuaji wa biashara, utungwaji wa mimba ya biashara ni yale
mawazo ya kuanza biashara ambayo mtu anakuwa nayo. Kisha kuanza kwa
biashara ni sawa na mtoto anayezaliwa, kukua na kisha kufa. Sasa kama
ilivyo kwenye asili, siyo mimba zote zinazotungwa zinazaliwa, nyingine
zinaharibika kabla ya kufikia kuzaliwa. Na hata watoto wadogo
wanaozaliwa, wengi hawafiki utu uzima, wanakufa kabla. Na wachache
wanafika utu uzima na kufa.
Kwenye
biashara, biashara nyingi huwa zinashindwa kabla hata ya kuanza, nyingi
zinaishia kwenye mawazo pekee. Kwa zile ambazo zinaanza, nyingi huwa
zinakufa kwenye uchanga, hazikui kufikia ukomavu. Na zile ambazo
zinakua, huwa zinafikia ukomavu na kufa.
Lakini
zipo biashara chache sana ambazo zimeweza kuondoka kwenye mfumo huo wa
ukuaji na kufa. Biashara hizi zimekuwa zinajua kinachopelekea biashara
kufa baada ya kukomaa ni bidhaa au huduma kuzoelekea na kutokuwa na kitu
kipya.
Ili
kuondokana na hali hiyo ya biashara kufika ukingoni na kufa,
wafanyabiashara hao ambao biashara zao hazifi, wamekuwa wanakuja na
bidhaa mpya au huduma mpya kila mara ambapo bidhaa au huduma ya zamani
imefikia kilele chake cha mauzo. Hawasubiri mpaka mauzo yaanze kupungua
na biashara kufa. Badala yake wanakuja na bidhaa au huduma mpya
inayowafanya waendelee kuwa sokoni.
Huu
ndiyo mfumo unaotumiwa na makampuni makubwa ya teknolojia, chukulia
mfano wa kampuni ya Apple ambayo inazalisha simu aina ya Iphone. Kila
mwaka huwa wanakuja na toleo jipya la simu zao, ambalo halitofautiani
sana na toleo lililopita. Yote hii ni kuhakikisha kwamba wanaendelea
kuwa sokoni. Kwa sababu kampuni ikishatoa toleo jipya, na watu wote
wakawa nalo, hakuna tena fursa ya ukuaji. Lakini wanapokuja na toleo
jipya, wale waliokuwa na toleo la zamani wanatamani kuwa na toleo jipya
na hapo mauzo yanaanza upya.
Kwa
biashara unayofanya, angalia jinsi unavyoweza kutumia njia hiyo ya kuwa
na toleo jipya la bidhaa au huduma kila wakati ili biashara yako isife.
Subscribe to:
Posts (Atom)