Kubadili tabia ambayo umeshazoea kuiishi kila siku ni kitu kigumu 
mno. Watu wamekuwa wanatumia motisha mbalimbali kwao na hata kwa wengine
 ili waweze kubadili tabia. Moja ya motisha ambayo imekuwa inatumika ni 
zawadi, kwamba mtu akibadili tabia yake basi anapata zawadi, labda ni 
ongezeko la mshahara au kupewa bonasi fulani.
Lakini motisha hii ya zawadi imekuwa haina nguvu sana. Kwa wengi 
ambao wameshazoea tabia za zamani, zawadi haiwasukumi kubadilika. Mfano 
kama una wafanyakazi ambao wanachelewa kukamilisha majukumu yao, unaweza
 kuwapa motisha kwamba atakayewahi kukamilisha anapewa ongezeko la 
fedha, lakini wachache sana watakaokamilisha kwa muda.
Ipo motisha nyingine ambayo ina nguvu sana ya kubadili tabia, kwa 
sababu ni motisha inayoumiza. Motisha hii ni mtu kupoteza fedha iwapo 
ataendelea na tabia ya zamani. Hakuna mtu anayepoteza fedha na hivyo 
tishio la kupoteza fedha linawafanya watu walazimike kubadilika. Kwa 
mfano huo hapo juu, ukiwaambia wafanyakazi kwamba yule anayechelewa 
kukamilisha majukumu yake kwa muda, anakatwa fedha kwenye malipo yake, 
utashangaa jinsi ambavyo wote wanakamilisha kwa muda.
Tafiti za kisaikolojia zinaonesha kwamba watu wanasukumwa zaidi pale 
panapokuwa na hatari ya kupoteza fedha kuliko panapokuwa na uwezekano wa
 kupata kiasi kile kile cha fedha. Hii ni nguvu unayoweza kuitumia kwa 
mabadiliko yako mwenyewe.
Kwa mfano kama kuna tabia ambayo umegundua ni sugu kwako, na ambayo 
unajitahidi kuibadili huwezi, basi waambie watu wako wa karibu 
wakufuatilie kwa karibu na kila utakapofanya tabia hiyo basi wakudai 
kiasi fulani cha fedha.
Mfano kama una tabia ya kuwakatisha watu wakiwa wanaongea, waambie 
watu wote wa karibu kwamba kila unapomkatisha mtu akiwa anaongea basi 
akudai shilingi elfu 10. Ukishalipa watu wawili au watatu, 
nakuhakikishia hutarudia tena, kupoteza fedha kutakuumiza na 
kukushikisha adabu.
Kadhalika kwenye tabia nyingine kama ulevi au uvutaji wa sigara, 
kutokufanya mazoezi, kula hovyo, kutumia maneno ya matusi na kadhalika. 
Tabia yoyote inayokupa shida kubadili, ingiza fedha na utabadilika 
haraka sana.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE. JIFUNZE ---ELIMIKA --CHUKUA HATUA---FANIKIWA
Saturday, June 22, 2019
ELIMU YA FEDHA : MUDA WAKO NI PESA YAKO
Ndugu  yangu mpendwa, nimekuwa napenda kukuambia sana kauli hii, 
HAKUNA KITU CHA BURE. Ukiona mtu anakupa kitu bure, jua kuna namna 
unalipia ambayo wewe hujui au kuna mtu ameshalipa kwa ajili yako. Huu ni
 msingi ambao ukiweza kuuishi na kuusimamia kwenye maisha yako, 
utajiepusha na matatizo mengi mno. Mfano huwezi kutapeliwa kama utaishi 
kwa msingi kwamba hakuna kitu cha bure. 
Sasa tuje kwenye mitandao ya kijamii, orodhesha mitandao yote ya kijamii ambayo unaitumia. Je ni Instagram? Facebook? Whattsapp? Twitter? Snapchat? Na mingine zaidi. Swali ni je umekuwa unalipa kiasi gani ili kutumia mitandao hii ya kijamii?
Ukiacha bando (data) unazonunua ili kuweza kuingia mtandaoni, hulipi hata senti moja kutumia mitandao hii. Lakini unaweza kuitumia muda wowote, masaa 24 kwa siku, siku 7 za wiki.
Swali jingine unalopaswa kujiuliza ni je mitandao hii inapataje fedha za kujiendesha. Maana mitandao hii ina wafanyakazi wengi, na ambao ni wasomi kweli kweli, ina rasilimali nyingi na wamiliki wake ni matajiri wakubwa sana duniani. Ukichukua mfano wa mmiliki wa Facebook na Instagram, ambaye ni bilionea mkubwa duniani, ambaye yupo kwenye watu 10 matajiri zaidi duniani. Hizo fedha wanazitoa wapi?
Kama hujawahi kujiuliza swali hili basi leo unakwenda kupata mwanga, na utakufanya uangalie kwa mtazamo tofauti kabisa mitandao hii ya kijamii.
Mitandao ya kijamii inaingiza kipato kupitia MATANGAZO. Mfumo wao wa biashara uko hivi, kusanya watu wengi watumie huduma yako ya mtandao wa kijamii, kisha nenda kwa mtu mwenye biashara na mwambie unaweza kutangaza biashara yako kwenye mtandao wangu ambao una watumiaji wengi, na wanaotumia huduma hiyo kwa muda wao mwingi wa siku.
Sasa kama unavyojua tabia yetu binadamu, huwa tunafanya zaidi kile tunacholipwa ili kufanya. Kwa kuwa makampuni haya yanapata fedha kwa watu kutangaza kupitia mitandao yao, na kwa sababu wingi wa fedha unaamuliwa na wingi wa watembeleaji na muda ambao watembeleaji wanatumia kwenye mitandao hiyo, basi mitandao hii imekuwa inahakikisha inatumiwa na wengi, na ukishaitumia huachi, kila muda unataka kuitembelea. Kama nilivyokuambia kwenye kipengele namba moja, hujavutiwa kutembelea mitandao hii, umesukumwa kuitembelea kila wakati, kwa sababu unavyoitembelea zaidi, ndivyo wenye mtandao wanatengeneza kipato zaidi.
Hivyo basi, MUDA WAKO = PESA ZAO. Muda unaotumia kwenye mitandao ya kijamii ndiyo fedha ambazo zinawafanya wamiliki wa mitandao hiyo kuwa mabilionea wakubwa.
Swali jingine muhimu sana ni je, kwa matumizi yako makubwa ya mitandao ya kijamii, ni manufaa gani unayapata? Najua wengi mnajiambia naungana na marafiki na kujua yanayoendelea. Kama jibu hilo ni kweli, swali jingine litakuwa je unahitaji zaidi ya masaa mawili kwa siku kutembelea mitandao hii? Je kweli unahitaji kila baada ya nusu saa au saa moja kutembelea tena mitandao hii?
Rafiki, nafikiri unapata picha ni jinsi gani tumechagua kuharibu na kupoteza maisha yetu, kuwafaidisha wengine, huku sisi wenyewe tukibaki hatuna kitu.
Nikuache na mbinu moja ya kupima matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwako. Chukulia hili, kama kila dakika unayotumia kwenye mitandao ya kijamii ulikuwa unailipia shilingi elfu moja, je ungekuwa tayari kulipa shilingi ngapi kwa siku kutembelea mitandao hii?
Je ungekuwa tayari kulipa tsh 120,000/= kila siku ili tu utumie mitandao ya kijamii? (kwa wastani mtumiaji wa mitandao ya kijamii anatumia masaa mawili kila siku). Kama jibu ni hapana basi jua muda unaoweka kwenye mitandao hiyo unaupoteza. Kama kweli unatumia mitandao ya kijamii kuungana na marafiki na kujua yanayoendelea, utahitaji dakika 10 tu kwa siku kwa ajili ya hilo. Muda mwingine utakuwa na manufaa kwako kama utatumia kwenye mambo yenye tija.
Kila unapoingia kwenye mitandao ya kijamii jikumbushe hili, MUDA WAKO = PESA KWAO na jiulize kama kweli unataka kuendelea kuwa bidhaa inayouzwa.
Na mwisho kabisa, pima umuhimu wa mitandao hii kwa kujiuliza kama ungekuwa tayari kulipia ili kuitumia, maana bure inakudanganya na kukupotezea muda wako.
Sasa tuje kwenye mitandao ya kijamii, orodhesha mitandao yote ya kijamii ambayo unaitumia. Je ni Instagram? Facebook? Whattsapp? Twitter? Snapchat? Na mingine zaidi. Swali ni je umekuwa unalipa kiasi gani ili kutumia mitandao hii ya kijamii?
Ukiacha bando (data) unazonunua ili kuweza kuingia mtandaoni, hulipi hata senti moja kutumia mitandao hii. Lakini unaweza kuitumia muda wowote, masaa 24 kwa siku, siku 7 za wiki.
Swali jingine unalopaswa kujiuliza ni je mitandao hii inapataje fedha za kujiendesha. Maana mitandao hii ina wafanyakazi wengi, na ambao ni wasomi kweli kweli, ina rasilimali nyingi na wamiliki wake ni matajiri wakubwa sana duniani. Ukichukua mfano wa mmiliki wa Facebook na Instagram, ambaye ni bilionea mkubwa duniani, ambaye yupo kwenye watu 10 matajiri zaidi duniani. Hizo fedha wanazitoa wapi?
Kama hujawahi kujiuliza swali hili basi leo unakwenda kupata mwanga, na utakufanya uangalie kwa mtazamo tofauti kabisa mitandao hii ya kijamii.
Mitandao ya kijamii inaingiza kipato kupitia MATANGAZO. Mfumo wao wa biashara uko hivi, kusanya watu wengi watumie huduma yako ya mtandao wa kijamii, kisha nenda kwa mtu mwenye biashara na mwambie unaweza kutangaza biashara yako kwenye mtandao wangu ambao una watumiaji wengi, na wanaotumia huduma hiyo kwa muda wao mwingi wa siku.
Sasa kama unavyojua tabia yetu binadamu, huwa tunafanya zaidi kile tunacholipwa ili kufanya. Kwa kuwa makampuni haya yanapata fedha kwa watu kutangaza kupitia mitandao yao, na kwa sababu wingi wa fedha unaamuliwa na wingi wa watembeleaji na muda ambao watembeleaji wanatumia kwenye mitandao hiyo, basi mitandao hii imekuwa inahakikisha inatumiwa na wengi, na ukishaitumia huachi, kila muda unataka kuitembelea. Kama nilivyokuambia kwenye kipengele namba moja, hujavutiwa kutembelea mitandao hii, umesukumwa kuitembelea kila wakati, kwa sababu unavyoitembelea zaidi, ndivyo wenye mtandao wanatengeneza kipato zaidi.
Hivyo basi, MUDA WAKO = PESA ZAO. Muda unaotumia kwenye mitandao ya kijamii ndiyo fedha ambazo zinawafanya wamiliki wa mitandao hiyo kuwa mabilionea wakubwa.
Swali jingine muhimu sana ni je, kwa matumizi yako makubwa ya mitandao ya kijamii, ni manufaa gani unayapata? Najua wengi mnajiambia naungana na marafiki na kujua yanayoendelea. Kama jibu hilo ni kweli, swali jingine litakuwa je unahitaji zaidi ya masaa mawili kwa siku kutembelea mitandao hii? Je kweli unahitaji kila baada ya nusu saa au saa moja kutembelea tena mitandao hii?
Rafiki, nafikiri unapata picha ni jinsi gani tumechagua kuharibu na kupoteza maisha yetu, kuwafaidisha wengine, huku sisi wenyewe tukibaki hatuna kitu.
Nikuache na mbinu moja ya kupima matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii kwako. Chukulia hili, kama kila dakika unayotumia kwenye mitandao ya kijamii ulikuwa unailipia shilingi elfu moja, je ungekuwa tayari kulipa shilingi ngapi kwa siku kutembelea mitandao hii?
Je ungekuwa tayari kulipa tsh 120,000/= kila siku ili tu utumie mitandao ya kijamii? (kwa wastani mtumiaji wa mitandao ya kijamii anatumia masaa mawili kila siku). Kama jibu ni hapana basi jua muda unaoweka kwenye mitandao hiyo unaupoteza. Kama kweli unatumia mitandao ya kijamii kuungana na marafiki na kujua yanayoendelea, utahitaji dakika 10 tu kwa siku kwa ajili ya hilo. Muda mwingine utakuwa na manufaa kwako kama utatumia kwenye mambo yenye tija.
Kila unapoingia kwenye mitandao ya kijamii jikumbushe hili, MUDA WAKO = PESA KWAO na jiulize kama kweli unataka kuendelea kuwa bidhaa inayouzwa.
Na mwisho kabisa, pima umuhimu wa mitandao hii kwa kujiuliza kama ungekuwa tayari kulipia ili kuitumia, maana bure inakudanganya na kukupotezea muda wako.
ELIMU YA FEDHA : CHANGAMOTO YA FEDHA
Fedha
 imekuwa changamoto kubwa sana kwenye zama tunazoishi sasa. Tunapoteza 
muda na maisha yetu kwenye kufanya kazi ngumu, lakini fedha tunazozipata
 tunazipoteza kwa kununua vitu ambavyo siyo mahitaji ya msingi.
Makampuni
 makubwa yanatumia mbinu za kisaikolojia kututangazia bidhaa na huduma 
zao kwa namna ambayo tunajisikia vibaya kama hatuna wanachouza.
Pia
 taasisi za fedha zimerahisisha sana matumizi yetu, hata kama mtu huna 
fedha za kununua kitu, basi ni rahisi kukopa fedha ili kununua 
unachotaka. Na hapo sasa mtu analipa mkopo pamoja na riba kubwa.
Yote haya ni matatizo ya kujitakia, kwa kushindwa kudhibiti tamaa zetu na kujilinganisha na wengine.
Ili kuondokana na changamoto hii ya fedha, fanya yafuatayo;
- Jua mahitaji yako ya msingi ambayo utayagharamia na yale ya anasa ambayo utaachana nayo. Mahitaji ya msingi ni manne, maji, chakula, moto na malazi. Mengine yoyote nje ya hapo ni anasa, yanaweza kusubiri.
- Kuwa na bajeti ya matumizi yako ya fedha, usitumie tu fedha kwa sababu unazo, bali weka bajeti na ifuate hiyo.
- Usikope fedha kwa ajili ya matumizi, ni kuchagua kupoteza fedha.
- Kwenye kila kipato unachoingiza, sehemu ya kumi hupaswi kuitumia kabisa, hivyo ni fedha unayojilipa kwa ajili ya uwekezaji wako wa baadaye.
- Usishindane na watu wengine wala kujilinganisha na yeyote kwenye mali, mavazi na hata maisha.
- Fanya tahajudi rahisi kabla hujanunua kitu. Kabla hujalipia jiulize je unachotaka kulipia ni hitaji la msingi au anasa. Hii itakuepusha kufanya manunuzi yasiyo muhimu.
- Fanya mfungo wa matumizi. Kwa mwezi mmoja, usinunue kabisa kitu ambacho siyo cha msingi. Jizuie kabisa kununua chochote ambacho siyo lazima kwa kipindi cha mwezi mzima, kisha ona jinsi maisha yako yatakuwa bora zaidi.
- Wekeza akiba yako kwenye maeneo ambayo yanazalisha zaidi baadaye.
- Usinunue vitu ambavyo thamani yake inashuka kadiri muda unavyokwenda.
- Ongeza kipato chako kwa kuwa bora zaidi kwenye kile unachofanya, toa huduma bora zaidi, wahudumie wengi zaidi na utaweza kuongeza kipato zaidi.
ELIMU YA FEDHA : MAISHA ULIYOPOTEZA
Watu
 wengi wamekuwa wanakutana na hali hii, akiwa hana fedha anakuwa na 
mawazo na mipango mizuri sana ya kutekeleza anapopata fedha. Anakuwa 
mpole na mwenye akili nzuri juu ya matumizi ya fedha. Akiona wengine 
wanatumia fedha vibaya anajiambia kama mimi ningepata fedha hizo, basi 
ningefanya mambo mazuri sana.
Lakini
 mtu huyo huyo anapopata fedha, anajikuta anafanya vitu ambavyo hata 
hakupanga kufanya. Mtu akishapata fedha zile akili nzuri na mipango 
aliyokuwa nayo anasahau kabisa. Anajikuta ananunua vitu ambavyo 
hakupanga kununua, mahitaji muhimu ambayo hayakuwepo awali yanaanza 
kujitokeza. Ni mpaka fedha hiyo inapoisha ndiyo mtu anarudi kwenye akili
 zake na kujiuliza zile fedha zimeishaje bila kufanya mambo mazuri.
Kama
 umewahi kukutana na hali kama hii usijione kama una bahati mbaya, au ni
 mjinga sana inapokuja kwenye fedha. Jua hiyo ni hali inayowakumba watu 
wengi kwenye fedha, na inatokana na wengi kutokuielewa vizuri saikolojia
 ya fedha. Fedha ni nguvu, na nguvu yoyote isipodhibitiwa na kutumiwa 
vizuri inaleta uharibifu.
Leo
 nakwenda kukushirikisha dhana itakayokuwezesha kuwa na udhibiti mzuri 
kwenye fedha zako, dhana itakayokuzuia usitumie hovyo fedha pale 
unapokuwa nazo.
Dhana
 hii ni kuhesabu fedha kwa kulinganisha na maisha ambayo umepoteza 
kupata fedha hizi. Wote tunajua kwamba muda ni fedha, na pia tunajua 
kwamba muda ni maisha, hivyo basi maisha pia ni fedha.
Sasa
 chukua kipato chako unachopata kwa mwezi, kisha gawa kwa masaa 
unayofanya kazi. Mfano kama kipato chako ni milioni moja, halafu 
unafanya kazi masaa 8 kwa siku, siku 5 au 6 za wiki, kwa mwezi unafanya 
kazi kwa masaa 160 mpaka 200. Ukigawa milioni moja kwa masaa 200 utapata
 shilingi elfu 5. Hii ina maana kila saa unayofanya kazi unalipwa 
shilingi elfu 5.
Sasa
 kwa sababu muda ni fedha na maisha ni muda hivyo maisha ni fedha, kila 
elfu 5 unayoipata, unapoteza saa moja ya maisha yako. ukipata elfu 10 
umepoteza masaa mawili.
Sasa
 kila unapotaka kununua kitu, kabla hujafanya maamuzi ya kukinunua 
jiulize kwanza swali hili, je kitu hiki ninachokwenda kununua, kina 
thamani sawasawa na maisha niliyopoteza?
Kwa
 mfano umekutana na nguo ambayo inauzwa shilingi elfu 20, umeipenda 
kweli na unataka kuinunua. Jiulize kwanza je nguo hii ina thamani sawa 
na masaa manne ya maisha yangu? Je kama nikiambiwa nichague kupata nguo 
hii na kupata masaa manne zaidi kwenye maisha yangu nitachagua nini?
Kwa
 kuchukulia fedha zako kama maisha ambayo unapoteza, utajijengea nidhamu
 kubwa sana ya fedha na kuacha matumizi ya hovyo, yasiyo na manufaa 
kwako. Pia utapata muda zaidi wa kufanya yale muhimu kwako, pamoja na 
kuwekeza fedha zako maeneo ambayo yanazalisha na hivyo kukusaidia 
usifanye kazi muda mrefu kupata fedha za kupoteza.
Linganisha
 kila fedha unayotaka kutumia na maisha unayopoteza, na utaona jinsi 
gani vitu vingi unavyopenda kununua havina thamani unayovipa.
KWANINI UTAKE KUUZA BIASHARA YAKO ?
"John  Warrillow "  katika  Kitabu   Chake  " BUILT  TO  SELL " anatuambia zipo sababu mbalimbali za wewe kutaka kuuza biashara unayokuwa umeianzisha.
- Biashara yako inaweza kuwa ndiyo chanzo chako cha mafao unapostaafu, hivyo kuweza kuiuza kunakupa kiasi kikubwa cha fedha cha kustaafu bila ya shida.
- Unaweza kuwa unataka kuanzisha biashara nyingine. Wajasiriamali huwa wanachoka kitu haraka, hivyo ukianzisha biashara na kuona tayari umeichoka na kuna biashara nyingine unapenda kuingia, unaweza kuuza ile uliyonayo sasa.
- Unaweza kuwa na uhitaji mkubwa wa fedha kutatua matatizo mbalimbali yanayokukumba. Biashara yako inaweza kuwa kama akiba au uwekezaji wako, ambao unaweza kuuza pale unapokuwa na uhitaji mkubwa wa fedha kutatua changamoto mbalimbali za maisha yako.
- Unaweza kuwa unahitaji kupata muda zaidi kwa ajili yako na familia yako. Pale unapoona biashara yako inachukua muda kuliko unavyoweza kuipa, unaweza kuchagua kuiuza.
- Unaweza kuwa unahitaji kulala vizuri usiku bila ya wasiwasi, kwa sababu unapokuwa mjasiriamali, unakuwa na usiku mwingi ambao hulali, unafikiria biashara itakuaje, ushindani utaushindaje, mishahara utalipaje, mikopo unarejeshaje na mengine mengi ambayo yatakunyima usingizi. Lakini unapojua kwamba unaweza kuiuza biashara hiyo muda wowote, unakuwa na utulivu mkubwa wa akili.
KWANINI BIASHARA NYINGI HAZIFAI KUUZA ?
Biashara
 nyingi hazifai kuuza kwa sababu zinaendeshwa kwa vurugu. Kwa nje 
biashara inaweza kuonekana inakwenda vizuri, lakini kwa ndani mambo ni 
vurugu. Hakuna mpangilio wowote wala mfumo ambao unafuatwa. Kila kitu 
kinafanywa kwa namna ambavyo mtu anajisikia kufanya. Hakuna viwango 
vyovyote vinavyofanyiwa kazi.
Wateja
 wanaokuja kupata huduma kwenye biashara, hawaji kwa sababu ya biashara,
 bali wanakuja kwa sababu ya mtu. Na wengine wanasema wazi kwamba 
wanataka kuhudumiwa na fulani tu.
Wafanyabiashara
 wengi hufurahia pale wateja wanapotaka wahudumiwe na wao tu, wakiona ni
 wateja wanawaamini na kuwakubali sana. Lakini wasijue kama hicho ndiyo 
kifungo chao.
Huwezi kuuza biashara ambayo haiendeshwi kwa mfumo na kila kitu kinamtegemea mmiliki wa biashara hiyo.
Na biashara ya aina hii inakuwa mzigo kwa mmiliki na kumnyima uhuru.
Karibu
 tujifunze jinsi ya kutengeneza biashara inayokupa uhuru na unayoweza 
kuiuza muda wowote na hili litakuwezesha kuwa na biashara bora na 
isiyokutegemea kwa kila kitu. Na hata kama hutaki kuuza biashara yako, 
kitendo cha biashara kuweza kujiendesha yenyewe bila ya wewe kuwepo, 
utakuwa ushindi mkubwa sana kwako.
HATUA NANE (8 ) ZA KUTENGENEZA BIASHARA INAYOJIENDESHA YENYEWE NA UNAYOWEZA KUIUZA MUDA WOWOTE
Kutoka
 kwenye kitabu "BUILT TO SELL", mwandishi " John Warrillow " anatushirikisha hatua nane za 
kufuata katika kutengeneza biashara ambayo inaweza kujiendesha yenyewe 
bila ya kuwepo kwa mwanzilishi wa biashara hiyo na pia inaweza kuuzwa 
muda wowote.
(1). Chagua bidhaa au huduma yenye uwezo wa kukua.
Hatua
 ya kwanza kabisa kwenye kutengeneza biashara inayojiendesha yenyewe na 
unayoweza kuiuza ni kuchagua bidhaa au huduma ambayo ina uwezo wa kukua.
Bidhaa au huduma yenye uwezo wa kukua ina vigezo vitatu;
Moja, inafundishika. Ni rahisi kumfundisha mtu mwingine jinsi ya kufanya kitu hicho na akaelewa.
Mbili;
 ina thamani kwa mteja. Hivyo mteja anakuwa tayari kulipa bei ambayo 
umeiweka. Kama kitu kinapatikana kwa wengine, mteja ataenda kwenye bei 
rahisi. Lakini kama kinapatikana kwako tu na mteja anakihitaji kweli, 
atakuwa tayari kulipa bei uliyopanga.
Tatu;
 manunuzi ni ya kujirudia. Mteja anahitaji kuwa anarudia tena na tena 
kununua. Isiwe ni kitu ambacho mteja ananunua mara moja kwenye maisha 
yake.
Baada
 ya kuchagua bidhaa au huduma ambayo inafundishika, ina thamani na 
manunuzi yake ni ya kujirudia, unahitaji kukaa chini na kuandika 
mchakato mzima wa jinsi unavyofanya biashara yako. Kila kitu 
kinachohusika kwenye biashara kinapaswa kuandikwa kwa namna ambayo mtu 
mwingine anaweza kufundishwa na akaelewa na kufuata. Huu unakuwa ndiyo 
mwongozo mkuu wa ufanyaji wa biashara yako.
Baada
 ya kuwa na mwongozo, unapaswa kuipa jina bidhaa au huduma yako. Unaipa 
jina kuitofautisha na bidhaa au huduma nyingine, hivyo inakuwa ya 
kipekee kwa wateja wako. Kadiri bidhaa au huduma inavyokuwa ya tofauti 
na zinazopatikana sokoni, ndivyo inakuwa na thamani kubwa kwa wateja 
wako.
Baada
 ya kuwa na jina linaloitofautisha bidhaa au huduma yako, andika maelezo
 mafupi kuhusu bidhaa au huduma hiyo ambayo yanajumuisha faida zake na 
jinsi inavyotatua changamoto za wateja wako, na tumia maelezo hayo 
kwenye masoko.
Katika
 hatua hii ya kwanza unachagua bidhaa au huduma moja au chache ambao 
unaweza kuweka nguvu zako zote na ukawafikia wateja wengi na biashara 
kukua pia. Ukifanya hatua hii kwa bidhaa au huduma nyingi utashindwa.
(2). Tengeneza mzunguko chanya wa fedha kwenye biashara.
Mzunguko
 wa fedha ndiyo uhai wa biashara yako. Yeyote anayetaka kununua biashara
 yako, akishaangalia kama inajiendesha yenyewe, anakwenda kuangalia 
mzunguko wa fedha wa biashara hiyo.
Mzunguko
 wa fedha kwenye biashara unaweza kuwa chanya au hasi. Mzunguko unakuwa 
chanya pale mapato ni makubwa kuliko matumizi na hasi pale matumizi ni 
makubwa kuliko mapato.
Ili
 kutengeneza mzunguko chanya wa fedha kwenye biashara yako, bidhaa au 
huduma unayouza inapaswa kuwafanya wateja walipe kwanza kabla ya 
kuipata. Epuka kuendesha biashara ambayo mteja anapata bidhaa au huduma 
kwanza halafu analipa baadaye. Hii inaifanya biashara ikae muda mrefu 
bila ya fedha na hivyo kuwa na mzunguko hasi wa fedha.
Biashara
 inapokuwa na mzunguko chanya, yule anayetaka kuinunua atakulipa zaidi 
kwa sababu tayari biashara inazalisha, tofauti na biashara yenye 
mzunguko hasi ambayo inahitaji kupokea fedha nyingi ili kujiendesha.
(3 ). Ajiri timu ya mauzo. 
Baada
 ya kutengeneza bidhaa au huduma ambayo utaiuza kwa wateja kulipa kabla 
ya kuipata, unahitaji kujiondoa kwenye kuiuza bidhaa au huduma hiyo. Na 
hapa ndipo unapohitaji timu ya mauzo, watu ambao wanaenda kuuza bidhaa 
au huduma kwa niaba yako.
Hii
 ni hatua muhimu sana ambayo wengi hukwama, unapouza bidhaa au huduma 
yako mwenyewe, unawafanya wateja wakutegemee wewe. Lakini unapokuwa na 
mfumo wa mauzo, ambao unaendeshwa na watu wa mauzo, wateja hawakutegemei
 wewe bali wanategemea mfumo wa biashara.
Kazi
 yako kama mjasiriamali ni kuuza kampuni yako, siyo kuuza bidhaa au 
huduma za kampuni hiyo. Ajiri na tengeneza timu bora ya mauzo na ipe 
mwongozo wa kuuza bidhaa au huduma yako na wewe utapata muda mwingi wa 
kuikuza zaidi kampuni yako.
Unapoajiri
 watu wa mauzo, ajiri ambao wana uzoefu wa kuuza bidhaa na epuka sana 
watu ambao wana uzoefu wa kuuza huduma. Hii ni kwa sababu wauzaji wa 
bidhaa huwa wanamuuzia mteja kile kilichopo, wakati wauzaji wa huduma 
wanabadilika kulingana na mahitaji ya mteja. Kwa sasa biashara yako 
inauza bidhaa, hata kama ni huduma, unapaswa kuiuza kama bidhaa, hivyo 
watu waliozoea kuuza bidhaa watakusaidia kuuza vizuri bila ya kutaka 
kubadili chochote.
Pia
 unapoajiri watu wa mauzo, ajiri angalau wawili. Hii inaleta hali fulani
 ya ushindani baina yao na inawasukuma kujituma zaidi. Mfano kama mmoja 
ameuza kwa wateja 10 kwa wiki, na mwingine akauza kwa wateja 7, yule wa 
wateja saba atakazana naye afike wateja 10. Kadhalika wa wateja kumi 
atakazana zaidi ili asipitwe. Watu wa mauzo huwa wanapenda kujipima kwa 
namba, unapokuwa na wawili na kuendelea, wanakuwa na ushindani ambao 
unawasukuma zaidi.
(4 ). Acha kuuza vitu vingine vyote.
Tumeona
 chanzo cha biashara nyingi kutokuuzika ni zinaendeshwa kwa vurugu, kila
 kitu kinauzwa na mteja akisema anataka kitu cha tofauti anapatiwa. Sasa
 hutaweza kuikuza wala kuiuza biashara kama inaendeshwa kwa vurugu kiasi
 hicho.
Hivyo
 baada ya kuchagua bidhaa au huduma moja kuu unayouza kwenye biashara 
yako, acha kuuza vitu vingine vyote. Inawezekana kuna vitu vingine 
ulikuwa unauza ambavyo vinakuingizia faida. Lakini kama vipo nje ya ile 
bidhaa au huduma uliyoiainisha kama msingi mkuu wa biashara yako, basi 
unapaswa kuacha kuuza vitu hivyo vingine.
Unahitaji
 kuweka nguvu zako zote kwenye kuikuza biashara yako kupitia bidhaa au 
huduma yenye fursa ya ukuaji zaidi. Unapojihusisha na kuuza vitu 
vingine, unawapa wateja wako wakati mgumu kukuelewa na kukutegemea.
Wateja
 wana tabia ya kujaribu wafanyabiashara, watakujaribu kwenye kutaka bei 
ya chini zaidi, watakujaribu kwenye kutaka kitu cha tofauti na unachotoa
 na watakujaribu kwa kutaka uboreshe zaidi kile unachotoa kiendane na 
wao. Epuka sana mitego na majaribu haya ya wateja, simamia kile 
ulichopanga na wateja wanapojifunza kwamba unasimamia nini, 
wanakuheshimu kwa hilo na kuwa tayari kununua kile unachouza.
Muhimu
 ni uzingatie hatua ya kwanza ya kuwa na bidhaa au huduma yenye thamani 
kwa wateja na ambayo hawawezi kuipata sehemu nyingine yoyote.
(5). Kuwa na mpango bora wa motisha kwa mameneja wako.
Kadiri
 biashara yako inavyokwenda, inazidi kukua. Timu ya mauzo inaleta wateja
 na biashara inakuwa kwenye mzunguko chanya wa fedha. Kwa kuwa wewe 
huhusiki moja kwa moja kwenye mauzo na wala kuandaa bidhaa au huduma, 
unahitaji kutengeneza viongozi kwenye biashara yako.
Hata
 mtu anayetaka kununua biashara yako, anaanza kuangalia uongozi uliopo 
kwenye biashara hiyo. Hivyo utahitaji kuwapandisha cheo wafanyakazi wako
 na kuwafanya kuwa mameneja, kisha kuajiri wafanyakazi wengine 
watakaofanya kazi chini ya usimamizi wao.
Ili mameneja hawa wajitume kweli unahitaji kuwa na mpango bora wa motisha kwao.
Zipo
 njia mbalimbali za kutoa motisha kwa mameneja wako, ipo njia ya 
kuwalipa bonasi mwisho wa mwaka kutokana na ongezeko la faida, hii 
inawasukuma kujituma zaidi ili kutengeneza faida kubwa.
Lakini
 pia baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wanawapa mameneja wao sehemu ya 
umiliki wa biashara hiyo, kwa kuwapa hisa. Kama lengo lako ni kuuza 
biashara yako, usitumie njia hii, kwa sababu ukishawapa umiliki, 
mchakato wa kuiuza biashara hiyo unakuwa mgumu zaidi.
Tumia
 mfumo wa kulipa bonasi kutokana na ongezeko la faida. Na pale biashara 
inapouzwa, basi wape zawadi ya bonasi kutokana na mauzo hayo.
(6).Tafuta dalali sahihi kwako.
Baada
 ya biashara yako kuwa inajiendesha yenyewe, kwa kuwa na timu bora ya 
uongozi na mzunguko chanya wa fedha, sasa unaanza kuangalia uwezekano wa
 kuiuza.
Hapa
 ndipo unapohitaji kutafuta dalali au wakala ambaye atakuunganisha na 
wanunuaji wa biashara. Zipo kampuni ambazo hizi ndiyo kazi zake, 
kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji au wanunuaji wa biashara.
Unahitaji
 kuchagua kampuni ambayo utafanya nayo kazi, ambayo itakuwa upande wako.
 Hivyo ongea na watu mbalimbali mpaka upate ambaye unaona anaweza 
kukuwakilisha vizuri kwa wanunuzi wa biashara hiyo.
Kampuni
 hizi za udalali huwa zinalipwa kwa asilimia ya mauzo bada ya mauzo 
kufanyika, lakini zinakusaidia sana kukutana na wanunuzi na kuweza kuuza
 biashara yako.
(7). Iambie timu yako ya uongozi kuhusu mpango wa kuuza biashara.
Timu
 ya uongozi wa biashara yako ni watu ambao wana imani kubwa sana na 
wewe. Ni watu ambao wanajitoa sana ili biashara yako ikue zaidi. Hivyo 
unahitaji kuwa makini sana pale unapotaka kuuza biashara yako.
Kwanza
 unahitaji kufanya mchakato huo kwa siri mwanzoni wakati unatafuta 
mteja. Ukishapata mteja sasa, unahitaji kuiambia timu yako kuhusu mpango
 wako wa kuuza.
Inaweza
 kuwa wakati mgumu sana kwako kuiambia timu ambayo inakuamini kwamba 
unapanga kuuza biashara hiyo, wapo ambao watakuchukulia wewe ni msaliti 
na huwajali wao bali unajali fedha tu.
Hivyo
 unapopanga kuwaambia, waoneshe kwamba biashara inapouzwa, hata wao pia 
wananufaika. Mfano biashara ikinunuliwa na kampuni ambayo ni kubwa 
zaidi, wao wanapata nafasi ya kukua zaidi. Wanakuwa kwenye mazingira 
bora zaidi ya kufanya kazi na pia wanaweza kupata nafasi za juu zaidi.
Pia
 waahidi kupata bonasi pale ambapo biashara itauzwa. Kwa njia hii 
watakubaliana na wewe na watakuwa tayari kusaidia ili mchakato wa mauzo 
ukamilike vizuri.
Ni
 muhimu uiambie timu yako kwa sababu anayenunua atahitaji kukutana na 
timu yako ya uongozi na pia kuna ukaguzi wa kina utakaofanyika kwenye 
biashara yako, ambao utahusisha kila aliyepo kwenye timu ya uongozi.
Hatua ya nane; geuza ofa kuwa makubaliano ya kisheria.
Wale
 wanaoonesha nia ya kununua biashara yako huwa wanatoa ofa ya kiasi 
wanachopanga kulipa ili kununua biashara hiyo. Lakini ofa siyo 
makubaliano, wakati wowote wanaweza kubadilika.
Na
 katika makubaliano ya kibiashara, watu huwa wanakuwa na mbinu 
mbalimbali za kupata kitu kwa bei ya chini. Mfano kwenye kuuza biashara,
 mtu atatoa ofa yake, kisha atafanya uchunguzi kwenye biashara na 
baadaye atakuja na matokeo ya uchunguzi na kukuambia kuna mambo ambayo 
ameyaona na hataweza kulipa ofa ya kwanza na hivyo kupunguza.
Ili
 kuepuka kujikuta kwenye hali hiyo, kwanza chagua ni kiasi gani upo 
tayari kupokea kwa kuuza biashara yako. Hivyo wanapokuja na ofa ya juu 
ya kiasi hicho kubali. Lakini pia wape muda wa ukomo, la sivyo zoezi 
litachukua muda mrefu zaidi.
Wanapofanya
 uchunguzi na kuja na majibu yao, ambapo watapunguza ofa yao, angalia 
kama bado inaendana na mpango wako wa awali. Kama ndiyo basi kubaliana 
nao na kamilisheni dili. Kama ofa yao iko chini ya mpango wako wa awali 
kataa na tafuta mnunuzi mwingine.
Zoezi
 la kutengeneza biashara ambayo inaweza kujiendesha yenyewe linategemea 
zaidi mfumo unaoweka kwenye biashara hiyo, unapokuwa na mfumo bora 
ndivyo kazi inakuwa rahisi kwako.
Zoezi
 la kuuza biashara yako huwa ni gumu na linalokuweka kwenye wakati mgumu
 mno. Hivyo kama unachagua kuuza biashara, lazima ujue una kipindi 
kigumu mbele yako, kuanzia kupata mnunuzi mpaka kufikia makubaliano.
Iwe
 unapanga kuuza biashara yako au la, bado utanufaika sana kama biashara 
yako inaweza kujiendesha yenyewe bila ya kukutegemea wewe moja kwa moja.
 Hivyo fuata hatua hizi nane na utaweza kutengeneza bishara bora sana 
kwako.
Subscribe to:
Comments (Atom)
