Kila mwaka malengo ya watu yamekuwa ni
kuweka akiba kwa ajili ya uwekezaji. Na kweli wanaweka sana akiba,
wanajinyima na kuanza kutengeneza akiba zao.
Lakini haupiti muda inajitokeza dharura
ambayo inawapelekea kutumia zile akiba walizokuwa wamejiwekea, hivyo
wanarudi sifuri kabisa, wanakuwa hawana akiba yoyote.
Rafiki, iwe una fedha au huna, dharura
hazitaacha kutokea kwenye maisha yako. Hivyo njia pekee ya kulinda akiba
yako siyo kuombea usipate dharura, badala yake ni kutengeneza gereza
kwa ajili ya akiba yako.
Gereza hili ni kuweka akiba eneo ambalo
huwezi kuitoa hata ardhi ipasuke. Na ukishaweka huko unasahau kabisa,
hivyo kama dharura itakuja, utaangalia njia nyingine za kuitatua na siyo
kuangalia akiba hiyo.
Magereza ya fedha yapo mengi, unaweza
kuziweka kwenye akaunti maalumu, ambayo huwezi kutoa fedha hiyo mpaka
muda uliochagua uishe. Pia unaweza kufungua akaunti ya pamoja na mtu
mwingine na makubaliano yakawa ni hakuna kutoa hata iweje. Pia unaweza
kutumia mitandao ya simu, ukapoteza namba ya siri ya mtandao wa simu
unaotumia kuweka fedha ili isiwe rahisi kwako kutoa.
Angalia njia bora kwako ni ipi na
itumie, usiache akiba yako ikakaa kirahisi rahisi kiasi kwamba ukiwa na
shida kidogo tu unaitumia. Iweke kwenye gereza ambalo hutaweza kuitumia
kabisa.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Monday, January 14, 2019
SIFA YA WASHINDI KATIKA MAISHA.
“Victory belongs to the most persevering.” - Napoleon Bonaparte
Ushindi unaenda kwa wale ambao ni ving’ang’anizi na wavumilivu.
Huwa tunawaangalia wale waliofanikiwa na kupenda sana kufika walipofika. Lakini sisi wenyewe kuna vitu vingi ambavyo tulishawahi kuanza kwenye maisha yetu, lakini havikutufikisha mbali, kwa sababu tulikosa ung’ang’anizi na uvumilivu.
Sasa chagua kitu kimoja au vichache unavyotaka kwenye maisha yako, kisha weka juhudi zako zote na usikate tamaa mpaka umekipata, na ninakuhakikishia utakipata. Maana washindi wote wameng’ang’ana na kupata walichotaka.
Ushindi unaenda kwa wale ambao ni ving’ang’anizi na wavumilivu.
Huwa tunawaangalia wale waliofanikiwa na kupenda sana kufika walipofika. Lakini sisi wenyewe kuna vitu vingi ambavyo tulishawahi kuanza kwenye maisha yetu, lakini havikutufikisha mbali, kwa sababu tulikosa ung’ang’anizi na uvumilivu.
Sasa chagua kitu kimoja au vichache unavyotaka kwenye maisha yako, kisha weka juhudi zako zote na usikate tamaa mpaka umekipata, na ninakuhakikishia utakipata. Maana washindi wote wameng’ang’ana na kupata walichotaka.
Tuesday, January 8, 2019
HEKIMA.
Bila
ya hekima, fedha na afya tunazopigania kuwa nazo, zitatupoteza kabisa.
Hekima ndiyo inayotuongoza vizuri kwenye maisha yetu, ndiyo
inayotuwezesha kufanya maamuzi sahihi kwetu ambayo yanafanya maisha yetu
yawe bora zaidi.
KUSOMA;
kila siku ya maisha yako, soma angalau kwa dakika 30, na soma vitabu
vinavyoongeza maarifa na uelewa wako kwenye kile unachofanya na hata
maisha kwa ujumla. Tenga na linda sana muda huu wa kujisomea, ndiyo
utakaokutoa hapo ulipo sasa na kukufikisha mbali zaidi.
UZOEFU WA WENGINE;
chagua watu ambao utajifunza kupitia wao, hawa tunawaita menta.
Unapaswa kuwa na mtu ambaye unataka kufikia hatua ambazo amefikia yeye,
kisha kujifunza kila kitu kuhusu yeye. Kama yupo hai na yupo karibu
unaweza kutafuta nafasi ya kuonana naye. Na kama yupo mbali huwezi
kumfikia au alishafariki basi jifunze kupitia maandiko yake na hata
maandiko yaliyoandikwa kuhusu wewe. Mazuri aliyofanya na pia jifunze
makosa aliyoyafanya ili uweze kuyaepuka.
KUTAFAKARI;
Unapaswa kuwa na muda wako mwenyewe, muda wa kutafakari, kuyatafakari
maisha yako na kutafakari kila unachofanya, kuanzia ulikotoka, ulipo
sasa na kule unakokwenda. Kila mwisho wa siku yako tafakari kila hatua
uliyochukua kwenye siku hiyo na angalia wapi umefanya vizuri, wapi
umekosea na wapi unahitaji kurekebisha na kuboresha zaidi. Majibu ya
maswali mengi uliyonayo kuhusu maisha tayari unayo, ni wewe kutafakari
na kujisikiliza na utapata majibu mengi sana.
UTAJIRI.
Fedha
ni sehemu muhimu sana ya maisha yetu, ukiondoa pumzi ambayo kila mtu
anaipata bure, kila kitu kinahitaji fedha. Na hata hiyo pumzi unapoumwa
inaacha kuwa bura na unaanza kuilipia. Fedha ni hitaji muhimu sana
kwenye maisha yetu, kwa sababu ndiyo inatuwezesha kupata kila
tunachotaka.
KIPATO;
ongeza kipato chako kwa kutoa thamani zaidi, kujituma zaidi na
kuwafikia wengi zaidi. Kama umeajiriwa tekeleza majukumu mengi zaidi na
magumu zaidi. Kama unafanya biashara wafikie wateja wapya na wengi
zaidi. Fanya zaidi ya ulivyozoea kufanya huko nyuma na kipato chako
kitaongezeka.
MATUMIZI;
Dhibiti sana matumizi yako, peleka fedha zako kwenye yale mambo ambayo
ni muhimu pekee kwenye maisha yako, kama kitu siyo muhimu, achana nacho.
Matumizi huwa yana tabia ya kukua kadiri kipato kinavyokua,
usipoyadhibiti yatakurudisha nyuma.
UWEKEZAJI;
Hutakuwa na nguvu za kufanya kazi kama unavyofanya sasa miaka yako
yote. Hivyo unahitaji kuifanya fedha yako ikufanyie kazi na kukiingizia
kipato. Na hapa ndipo uwekezaji unapokuwa muhimu. Weka akiba na wekeza
akiba hiyo kwenye maeneo ambayo yanazalisha zaidi kwa baadaye.
AFYA
Afya
ndiyo mtaji wa kwanza na muhimu sana kwenye maisha yetu, bila ya afya
bora na imara huwezi kufanya chochote kikubwa kwenye maisha yako. Afya
unaweza kuichukulia kirahisi sana unapokuwa nayo, lakini ukishaipoteza
gharama zake ni kubwa sana.
KULA VYAKULA
vya kiafya kwa kuepuka sukari, kupunguza wanga na kuongeza zaidi
mbogamboga, matunda, mafuta na protini. Sumu namba moja kwenye afya zetu
ni wanga na sukari, ukiweza kudhibiti hili utakuwa na afya bora.
KUFANYA MAZOEZI,
kila siku fanya mazoezi ya kukimbia kwa angalau nusu saa. Mazoezi ya
kukimbia ni mazoezi bora kabisa na yasiyo na gharama kwako. Hakikisha
unafanya haya kila siku.
KUPUMZIKA,
pata muda wa kutosha wa kulala kulingana na uhitaji wa mwili wako. Kwa
wastani binadamu tunahitaji masaa 6 mpaka 8 ya kulala kwa siku. Jua
mwili wako unahitaji kiasi gani na kila siku upe muda huo. Hili
litakufanya uwe imara na kuweza kuweka juhudi kwenye shughuli zako.
Sunday, January 6, 2019
JINSI UTAJIRI UNAVYOKUJA KWAKO.
Utajiri unakuja kwako kwa njia ya thamani. Unapaswa kutoa thamani kubwa zaidi ya matumizi kuliko thamani ya fedha ambayo mtu anakupa. Ili kupata zaidi lazima uwe tayari kutoa zaidi.
Usiwalangue watu, wala usitumie mbinu kuwashawishi wanunue kitu ambacho hakitawasaidia. Wape watu kitu ambacho kitakuwa na msaada kwenye maisha yao na wewe utaweza kupata kile unachotaka.
USIWE MTU WA KULALAMIKA AU KUKOSA SHUKRANI.
Tumeona kwamba kuna mfumo wa fikra ambao unatupa kila ambacho tunakifikiri kwa muda mrefu. Njia pekee ya kushirikiana na mfumo huu ni kuwa na shukrani.
Kwa kushukuru, mfumo huu wa fikra unajua kwamba upo tayari kupokea zaidi na hivyo kukuwezesha kupata zaidi.
Usiwe
mtu wa kulalamika au kukosa shukrani, mara zote shukuru na utaweza
kupata zaidi. Shukuru kwa kidogo na utafungua milango ya kupata kikubwa
zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)