Kauli ya Seneca kuhusu kuishi kwa furaha;
“What is a happy life? It is peacefulness and lasting tranquillity,
the sources of which are a great spirit and a steady determination to
hold fast to good decisions. How does one arrive at these things? By
recognizing the truth in all its completeness, by maintaining order,
moderation and appropriateness in one’s actions, by having a will which
is always well-intentioned and generous, focused on reason and never
deviating from it, as lovable as it is admirable.” – Seneca, Letters, 92.3
Seneca anauliza maisha ya furaha maana yake nini? Ni maisha ambayo
yana amani na utulivu, ambayo chanzo chake ni imani kuu na maamuzi ya
kushikilia maamuzi sahihi. Na je mtu anawezaje kufikia hili? Ni kwa
kugundua ukweli kamili, kwa kuenda kulingana na mipango, kuwa na kiasi
katika matendo na kuwa na nia njema na ukarimu, kuongozwa na fikra
sahihi na kutokupotoka.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Sunday, October 7, 2018
FALSAFA YA USTOA NI NINI ???
USTOA ni falsafa ya matendo, ni falsafa ambayo imelenga kumwezesha
mtu kuwa na maisha bora, kwa kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi
kwenye maisha yake. Falsafa ya ustoa siyo kama falsafa nyingine za
kubishana na kutaka kuonekana unajua zaidi, badala yake ni falsafa ya
kufikiri sahihi na kuchukua hatua sahihi. Falsafa ya ustoa inalenga
kudhibiti hisia zetu na kuishi kulingana na asili. Kwa njia hiyo,
tunakuwa na maisha bora wakati wote.
Falsafa ya ustoa ilianzishwa na Zeno wa Citium miaka ya 301 K.K na baadaye kupokelewa na kukuzwa na wanafalsafa Cato, Seneca, Epictetus na Marcus Aurelius. Hawa wote ni wanafalsafa walioishi zaidi ya miaka 2000 iliyopita, wakati wa utawala wa Roma.

Saturday, September 22, 2018
KILA MTU APAMBANE NA HALI YAKE,USINUNUE MATATAIZO YA WATU.
Chukua
mfano una ndugu wa karibu au mtoto ambaye bado hajaweza kutengeneza
maisha yake vizuri, lakini wewe maisha yako yameshakaa vizuri.
Yeye hana kazi na ni mlevi. Hivyo unaamua kumsaidia awe na kipato, kwa
sababu maisha yake siyo mazuri. Unampa mtaji wa kuanzisha biashara,
anatumia vibaya na biashara inakufa. Unaona kwa kuwa una uwezo, basi unaweza kuwa unampa fedha ya kujikimu, lakini ukimpa fedha anaenda kulewa. Unakwama,
usipompa fedha maisha yake yanakuwa magumu na unaonekana umemtenga
ndugu yako, ukimpa anaenda kulewa na kuzitumia vibaya.
Wawezeshe watu kutatua matatizo yao wenyewe, na usisukumwe kufanya vitu kwa sababu unataka kuonekana una roho nzuri.
Wale utakaowawezesha kutatua matatizo yao, utawasaidia hata wakati wewe
haupo. Ila wale unaobeba matatizo yao, utawaandaa kuanguka vibaya pale
ambapo wewe hutakuwepo. Na
nikukumbushe tu, haijalishi unampenda mtu kiasi gani, hutakuwa naye kwa
maisha yako yote, hivyo mpende kwa kumfanya aweze kutatua matatizo yake
mwenyewe.
Katika
kukazana kwetu kuwasaidia wengine, hasa wale wa karibu kwetu, watoto,
wenza, ndugu tuliozaliwa nao, tumekuwa tunakazana kuwaibia matatizo yao. Tunayachukua kabisa matatizo yao na kuyafanyia kazi na wao wanabaki hawana cha kufanya.
Hii ni njia mbovu sana ya kutaka kumsaidia mtu, kwa sababu unakuwa humsaidii, badala yake unamsababishia matatizo zaidi. Kwa sababu unapomchukulia matatizo yake, anabaki hana cha kufanya, hivyo anaenda kutengeneza matatizo zaidi.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Kwa sababu ukikimbilia kuyabeba ili uonekane una roho nzuri, utaishia kumharibu zaidi yule mwenye matatizo. Kwa sababu maisha yetu yanatoa maana kwenye matatizo na changamoto tunazokutana nazo mara kwa mara na kuzitatua.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Friday, September 21, 2018
JE, WAIJUA AKAUNTI YA FEDHA YA SAIKOLOJIA ?
Unahitaji kujizoesha kifikra na kisaikolojia kuwa na fedha nyingi, hata
kama bado hujazishika kwenye mikono yako au kuwa nazo kwenye akaunti
yako ya benki. Na unaweza kuanza kwa kufikiria mara kumi ya kipato
unachopata sasa, kisha kufikiria kipato hicho mara kwa mara, kukiwekea
mipango na kuweka lengo lako la kipato liwe ni kukua kufikia mara kumi
ya kipato chako cha sasa. Kwa njia hii utaongeza kiwango chako cha fedha
kisaikolojia.
Watu wengi wanajua aina moja ya akaunti ya kifedha, ambayo ni akaunti ya benki, au akiba na uwekezaji ambao wamekuwa wamefanya. Hivyo ukitaka kuangalia utajiri wa mtu, unaangalia ni kiasi gani cha fedha anacho kwenye akaunti zake za benki na uwekezaji kiasi gani amefanya.
Aina ya pili ya akaunti ya kifedha, ukiacha akaunti ya benki, ni akaunti ya fedha ya kisaikolojia. Kila mmoja wetu, ana kiwango chake cha kifedha kwenye fikra zake, ambacho ndiyo ameshajiambia anapaswa kupata kiwango hicho. Yaani kila mmoja wetu, kuna kiwango chake cha fedha, ambacho ameshakiweka kwenye fikra na mawazo yake, na akishapata kiwango hicho basi akili yake inatulia na hakazani tena kupata fedha zaidi.
Waangalie watu wote ambao wamepata fedha nyingi kwa mkupuo, kiasi kikubwa cha fedha ambacho hawajawahi kukishika kwenye maisha yao. Waangalie watu ambao wameshinda bahati nasibu, waangalie watu ambao wamerithi mali, waangalie watu ambao wamepokea mafao. Wengi haiwachukui muda wanakuwa wameshapoteza fedha nyingi walizopata na kurudi kwenye maisha yao ya kawaida.
Wanakuwa wamepata fedha nyingi kwenye akaunti ya benki, lakini akaunti yao ya kisaikolojia inasoma kiwango cha chini. Hivyo wanaacha kufikiria kabisa kuhusu fedha, wanaanza kupoteza fedha, mpaka zinapofika kwenye kile kiwango chao cha kisaikolojia ndiyo wanastuka na kuanza kufikiria kuhusu fedha.
Pia unaweza kufikiria mara 100, mara 1000 na hata zaidi ya kipato unachopata sasa. Fikra zote hizo zitaiandaa akili yako kupokea fedha zaidi na kuweza kutulia na fedha zaidi unazopata. Unapofikiria mara elfu moja ya kipato unachopata sasa, ongezeko kidogo halitakusumbua kama linavyokusumbua sasa.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Watu wengi wanajua aina moja ya akaunti ya kifedha, ambayo ni akaunti ya benki, au akiba na uwekezaji ambao wamekuwa wamefanya. Hivyo ukitaka kuangalia utajiri wa mtu, unaangalia ni kiasi gani cha fedha anacho kwenye akaunti zake za benki na uwekezaji kiasi gani amefanya.
Aina ya pili ya akaunti ya kifedha, ukiacha akaunti ya benki, ni akaunti ya fedha ya kisaikolojia. Kila mmoja wetu, ana kiwango chake cha kifedha kwenye fikra zake, ambacho ndiyo ameshajiambia anapaswa kupata kiwango hicho. Yaani kila mmoja wetu, kuna kiwango chake cha fedha, ambacho ameshakiweka kwenye fikra na mawazo yake, na akishapata kiwango hicho basi akili yake inatulia na hakazani tena kupata fedha zaidi.
Waangalie watu wote ambao wamepata fedha nyingi kwa mkupuo, kiasi kikubwa cha fedha ambacho hawajawahi kukishika kwenye maisha yao. Waangalie watu ambao wameshinda bahati nasibu, waangalie watu ambao wamerithi mali, waangalie watu ambao wamepokea mafao. Wengi haiwachukui muda wanakuwa wameshapoteza fedha nyingi walizopata na kurudi kwenye maisha yao ya kawaida.
Wanakuwa wamepata fedha nyingi kwenye akaunti ya benki, lakini akaunti yao ya kisaikolojia inasoma kiwango cha chini. Hivyo wanaacha kufikiria kabisa kuhusu fedha, wanaanza kupoteza fedha, mpaka zinapofika kwenye kile kiwango chao cha kisaikolojia ndiyo wanastuka na kuanza kufikiria kuhusu fedha.
Pia unaweza kufikiria mara 100, mara 1000 na hata zaidi ya kipato unachopata sasa. Fikra zote hizo zitaiandaa akili yako kupokea fedha zaidi na kuweza kutulia na fedha zaidi unazopata. Unapofikiria mara elfu moja ya kipato unachopata sasa, ongezeko kidogo halitakusumbua kama linavyokusumbua sasa.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Sunday, September 16, 2018
JE, WAJUA NJIA ZA KUONGEZA THAMANI YA MAISHA YA WATEJA WAKO ?? JIFUNZE HAPA .
Wateja wako wanapokaa na wewe kwa muda mrefu ndivyo
unavyonufaika zaidi. Hivyo unahitaji kuweka juhudi kuhakikisha wateja
wanabaki na wewe kwa muda mrefu. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia
ili wateja wakae na wewe kwa muda mrefu.
Hatua ya kwanza ni wapitaji tu, wanaisikia au kiona biashara yako lakini hawajawahi kuuliza chochote.
Hatua ya pili ni wateja tarajiwa, wamesikia na wamefuatilia kutaka kujua zaidi kuhusu biashara yako.
Hatua ya tatu ni wanunuaji, hapa wamejua, wakafuatilia na wakajaribu kununua kile unachouza.
Hatua ya nne ni wateja, hapa mtu amejaribu kununua kwa mara ya kwanza, na amerudi tena kununua. Mtu kununua mara moja haimfanyi kuwa mteja, na wala haikufanyi wewe kuwa mjanja. Ni mpaka mtu atakaporudi tena kununua ndiyo utajua umefanya kazi nzuri.
Hatua ya tano ni mwanachama, hapa mteja anakuwa mnunuaji wa mara kwa mara na unaweza kumpa manufaa ya kadiri anavyonunua. Labda akifika kiwango fulani anapata zawadi, au akinunua mara tano, ya sita anapata bure. Hapa mwanachama anakuwa na kielelezo cha kuonesha idadi ya manunuzi yake.
Hatua ya sita ni mtetezi wa biashara yako, hapa mteja anakuwa tayari kuwaambia watu wengine kuhusu biashara yako, anatoa shuhuda kwa wengine na hasiti kuwaalika wengi waje kununua.
Hatua ya saba ni shabiki kindakindaki, hawa ni wale wateja ambao hawaambiwi chochote kuhusu biashara yako, yaani wao wameshachukulia biashara yako kama sehemu ya maisha yako. Hawa ni wateja ambao wanaiongelea biashara yako muda wote, na wakikutana na mtu ambaye hanunui kwako wanaona anakosa kitu kikubwa sana.
Katika kuboresha thamani ya maisha ya wateja wako, kazana kuwapandisha wateja wako ngazi mpaka wafikie kiwango cha watetezi na mashabiki wa biashara yako.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
- Toa huduma bora sana kwa wateja wako, ambazo hawawezi kuzipata sehemu nyingine yoyote ila kwako tu.
- Kutengeneza mahusiano mazuri na wateja wako, wafanye wateja kuwa rafiki kwako na kwa biashara yako, waone siyo tu wanakuja kununua, bali wanakuja kwa rafiki yao, anayewajali na kuwapa kile kilicho sahihi kwao.
- Weka mbele maslahi ya wateja wako na siyo faida unayotaka kupata.
- Waelimishe wateja wako, washauri vizuri, hata kama utapoteza mauzo, lakini hilo litawajengea imani zaidi na hivyo kuendelea kununua zaidi.
- Wafanye wateja wako kuwa mashabiki wa biashara yako.
Hatua ya kwanza ni wapitaji tu, wanaisikia au kiona biashara yako lakini hawajawahi kuuliza chochote.
Hatua ya pili ni wateja tarajiwa, wamesikia na wamefuatilia kutaka kujua zaidi kuhusu biashara yako.
Hatua ya tatu ni wanunuaji, hapa wamejua, wakafuatilia na wakajaribu kununua kile unachouza.
Hatua ya nne ni wateja, hapa mtu amejaribu kununua kwa mara ya kwanza, na amerudi tena kununua. Mtu kununua mara moja haimfanyi kuwa mteja, na wala haikufanyi wewe kuwa mjanja. Ni mpaka mtu atakaporudi tena kununua ndiyo utajua umefanya kazi nzuri.
Hatua ya tano ni mwanachama, hapa mteja anakuwa mnunuaji wa mara kwa mara na unaweza kumpa manufaa ya kadiri anavyonunua. Labda akifika kiwango fulani anapata zawadi, au akinunua mara tano, ya sita anapata bure. Hapa mwanachama anakuwa na kielelezo cha kuonesha idadi ya manunuzi yake.
Hatua ya sita ni mtetezi wa biashara yako, hapa mteja anakuwa tayari kuwaambia watu wengine kuhusu biashara yako, anatoa shuhuda kwa wengine na hasiti kuwaalika wengi waje kununua.
Hatua ya saba ni shabiki kindakindaki, hawa ni wale wateja ambao hawaambiwi chochote kuhusu biashara yako, yaani wao wameshachukulia biashara yako kama sehemu ya maisha yako. Hawa ni wateja ambao wanaiongelea biashara yako muda wote, na wakikutana na mtu ambaye hanunui kwako wanaona anakosa kitu kikubwa sana.
Katika kuboresha thamani ya maisha ya wateja wako, kazana kuwapandisha wateja wako ngazi mpaka wafikie kiwango cha watetezi na mashabiki wa biashara yako.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
JE, WAJUA AINA ZA GHARAMA ZA KUWAPATA WATEJA WA BIASHARA YAKO ?? JIFUNZE HAPA.
Kuna aina mbili za gharama ya kupata wateja wa biashara yako.
Aina ya kwanza ni GHARAMA ZINAZORUHUSIWA za kupata mteja. Hapa unatumia gharama ambazo mteja akinunua mara moja basi gharama ile inarudi. Chukua mfano umetengeneza tangazo ambalo limekugharimu tsh 100,000/= na tangazo hilo limewafikia watu 1000. Katika hao 1000 ndiyo wamenunua. Na kwa kila unayenunua unapata faida ya shilingi elfu moja. Inamaana kwa watu 100, faida unayopata ni tsh 100,000/= sawa sawa na gharama ulizoingia kutoa tangazo. Hivyo hiyo ni gharama inayoruhusiwa ya kupata mteja. Kama utaandaa tangazo kwa gharama kubwa kuliko faida unayopata, hiyo sasa siyo GHARAMA INAYORUHUSIWA kupata wateja.
Aina ya pili ni GHARAMA UWEKEZAJI KWA WATEJA. Hapa unatumia gharama kubwa, ambayo inakuletea wateja, lakini manunuzi ya mwanzo ya mteja hayalipi gharama hiyo. Lakini kwa kuwa mteja ataendelea kununua, basi huko mbeleni ile gharama inarudi. Hivyo hapa unakuwa umewekeza kwa mteja, ukijua kwamba atafanya biashara na wewe kwa muda mrefu na gharama zako zitarudi.
Kwa biashara ndogo, ni vyema kutumia gharama zinazoruhusiwa, kwa biashara kubwa, ambazo zina rasilimali nyingi, zinaweza kuwekeza kwa wateja na baadaye zikanufaika zaidi. Usikimbilie kununua wateja kabla hujajua ni gharama kiasi gani unaingia na kama zinalipwa na idadi ya wateja watakaonunua.

JE, WAJUA JINSI YA KUNUNUA WATEJA WA BIASHARA YAKO ??? JIFUNZE HAPA !!
Kazi kubwa ya kila biashara ni kununua wateja wa biashara hiyo. Sasa
ili biashara iweze kufanikiwa, lazima iweze kununua wateja bora kwa
gharama ambazo siyo kubwa. Kitu ambacho wafanyabiashara wengi siyo tu
hawakifanyii kazi, ila hata hawakijui.
Inawezekana upo kwenye biashara, lakini hujui kama biashara yako inanunua wateja. Sasa nikuambie tu, kila biashara huwa inatumia fedha kununua wateja, na biashara yako pia inatumia fedha kununua wateja.
Labda nikuulize swali, biashara yako inatumia gharama kiasi gani kununua wateja? Na je gharama ambazo biashara yako inatumia kununua wateja zinarudi? Najua maswali haya yanaweza kukuacha ukiwa umeduwaa kwa sababu hujawahi kufikiria kuhusu kununua wateja.
Sasa kwenye kitabu nilichosoma ; BUYING CUSTOMERS, kilichoandikwa na kocha wa biashara Bradley Sugars, mwandishi ametushirikisha njia sahihi za kununua wateja bora wa biashara zetu na kwa gharama nafuu ambazo biashara inaweza kumudu.
Kwa kuanza, kila biashara huwa inanunua wateja. Kila hatua unayotumia kuwafanya wateja wajue kuhusu uwepo wa biashara yako, ni kununua wateja. Kama umewahi kutangaza biashara yako, umewahi kuandaa vipeperushi, kama umetengeneza bango, au kuuza vitu kwa pamoja kwa bei ya punguzo, kama umewahi kupunguza bei ili mteja anunue, au kutoa zawadi kwa mteja anayenunua. Kama umewahi kutoa usafiri kwa mteja, au kumpelekea alichonunua, au kumwomba mteja wako akuletee wateja zaidi. Zote hizo ni harakati za kununua wateja unazotumia kwenye biashara yako.
Sasa kuna ambazo zinakuletea wateja bora, nyingine hazikuletei wateja wazuri. Nyingine ni za gharama kubwa kwako, nyingine ni za gharama ndogo.
Kupitia kitabu cha BUYING CUSTOMERS, tunakwenda kujifunza jinsi ya kununua wateja bora kwa gharama nafuu kwenye biashara zetu.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Inawezekana upo kwenye biashara, lakini hujui kama biashara yako inanunua wateja. Sasa nikuambie tu, kila biashara huwa inatumia fedha kununua wateja, na biashara yako pia inatumia fedha kununua wateja.
Labda nikuulize swali, biashara yako inatumia gharama kiasi gani kununua wateja? Na je gharama ambazo biashara yako inatumia kununua wateja zinarudi? Najua maswali haya yanaweza kukuacha ukiwa umeduwaa kwa sababu hujawahi kufikiria kuhusu kununua wateja.
Sasa kwenye kitabu nilichosoma ; BUYING CUSTOMERS, kilichoandikwa na kocha wa biashara Bradley Sugars, mwandishi ametushirikisha njia sahihi za kununua wateja bora wa biashara zetu na kwa gharama nafuu ambazo biashara inaweza kumudu.
Kwa kuanza, kila biashara huwa inanunua wateja. Kila hatua unayotumia kuwafanya wateja wajue kuhusu uwepo wa biashara yako, ni kununua wateja. Kama umewahi kutangaza biashara yako, umewahi kuandaa vipeperushi, kama umetengeneza bango, au kuuza vitu kwa pamoja kwa bei ya punguzo, kama umewahi kupunguza bei ili mteja anunue, au kutoa zawadi kwa mteja anayenunua. Kama umewahi kutoa usafiri kwa mteja, au kumpelekea alichonunua, au kumwomba mteja wako akuletee wateja zaidi. Zote hizo ni harakati za kununua wateja unazotumia kwenye biashara yako.
Sasa kuna ambazo zinakuletea wateja bora, nyingine hazikuletei wateja wazuri. Nyingine ni za gharama kubwa kwako, nyingine ni za gharama ndogo.
Kupitia kitabu cha BUYING CUSTOMERS, tunakwenda kujifunza jinsi ya kununua wateja bora kwa gharama nafuu kwenye biashara zetu.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Subscribe to:
Posts (Atom)