Monday, September 15, 2014

TAMBUA KIPAJI CHAKO.

                    ANAYEFANIKIWA     NI    YULE     ANAYEJIJUA ,   ANAYEJITAMBUA

MAFANIKIO   YA  PESA    kwa     asilimia  kubwa   yako  ndani   ya    KIPAJI  CHAKO.


Hapa    duniani ,  watu    waliofanikiwa   wana   kitu   kinachofanana.  WANAPENDA   WANACHOFANYA.  Huwezi   kuwakuta    watu     waliofanikiwa    WAKICHUKIA   WANACHOFANYA.   Tabia   hii   wanayo  watu   wanaojiona    ni   MASKINI.  Unafikiri  ni    MASKINI  WA   NINI ?     NI    MASKINI   WA  AKILI .  Tabia  yao    hawa     WANACHUKIA   WANACHOFANYA.


UNAWEZAJE    KUFAHAMU  KIPAJI  CHAKO ?

---Fikiria  MICHEZO  uliyokuwa  unapendelea    utotoni. Nini    ulikuwa   unapendelea  pindi    ulipokuwa  mdogo.  Ulifikiria   kuwa   nani   ukubwani  ?


---Waambie    rafiki   zako    wa    karibu    kuwa , unataka    KUTAFITI   KUJUA   KIPAJI     CHAKO    na    unahitajji   MAWAZO     YA   KWELI  KUTOKA  KWAO.


--TUNAJINYIMA    Wenyewe  FURSA   ya  kupata    PESA   kwa   sababu  ya    KUPUUZA   VIPAJI   VYETU.   Kila    MTU   ana   jambo  analoliweza ,  pia  kukiwa   na   MAMILIONI   YA     MAMBO  ASIYOYAWEZA

---TUWACHUNGUZE    WATOTO   WETU  WANAPENDELEA  NI NI  ?WANAWEZA  NINI  ?
---GUNDUA  KITU  UNACHOKIPENDA !!

Friday, September 12, 2014

KUWA JASIRI NA MMAIZI---SIFA KUU MBILI PINZANI ZA MAFANIKIO KATIKA BIASHARA NA KAZINI.

Ukiwa   na    UJASIRI    pekee   hutaweza    kufanya   kazi   barabara. Vilevile    ukiwa    na  UMAIZI  peke   yake , huwezi  kuwa   na   UJASIRI   wa   kutosha   kukabiliana   na    mambo  mapya.
       KAZINI   tunahitaji  mtu    mwenye   sifa   kinzani  za    UJASIRI    NA  UMAIZI  na    mwenye    kujua    jinsi   ya  kutumia   vyema    kila   moja  ya   sifa  hizo  katika   mazingira   tofauti .
     
     NI   MATUMAINI    YANGU    KWAMBA    MTU  TIMILIFU   NI  YULE   MWENYE  UMAIZI  MKALI  MITHILI  YA  WEMBE , NA  ALIYEKWISHAPATA  UJASIRI  WA   DHATI   KUPITIA   TAJIRIBA  ZA  VIWANGO  MBALIMBALI.

    USHAURI   WANGU   TUJITAHIDI    KUIMARISHA  VIPAJI VYA   AMA  UJASIRI   AU   UMAIZI   SAMBAMBA  NA  VILE   TULIVYORITHI.

EWE MWANAFUNZI / KIJANA ISHINDE NAFSI YAKO.

UWEZO  WETU   wa    KUFANIKIWA   katika   Safari   yetu   ndefu   ya   MAISHA   hautegemei  uwezo  wa    AKILI  peke  yake.
     
Tunapofikiria   kuhusu  UWEZO   WA   MTU  hatuna    budi    kujumuisha   pia    UTASHI   WAKE. Kama   mtu ameshindwa  kuishinda    NAFSI  yake  na    kuamua   kuchukua  NJIA  RAHISI  bila  shaka  UWEZO  wake   kamili  utakuwa   pia    UMEPUNGUZWA  SANA.

UNAPOKUWA   SHULENI    utagundua  ya   kwamba  kuna  aina  mbili {2} za    WANAFUNZI :-
      AINA  YA   KWANZA  ni  wale   ambao  hawana  UWEZO    SANA  KIAKILI  lakini  hujitahidi   sana   SHULENI  ili   wahitimu   wakiwa  wamefanya   vizuri  katika   MASOMO   YOTE.
       AINA   YA   PILI   ni    wale    wenye    AKILI    NYINGI     lakini     hupenda    STAREHE  na  katika   MUDA  wao  wote   chuoni   huwa   hawana  nafasi    hata   ya   kufungua   kitabu.
        HUYU wa   pili   angesema   " yule   MBUKUZI  maefaulu    Vizuri ,  lakini    kama   ningekuwa  nimesoma   kama   yeye ,   ASINGEWEZA   KUNISHINDA  AU   ASINGEWEZA   KUFUA   DAFU   KWANGU ".
     BAADA  ya   kuhitimu , yule   mpenda   starehe  anakutana  na   rafiki   yake    mwingine    mwenye   MAFANIKIO    katika   biashara , na    kusema   "  HAKUWA   NA   AKILI   SHULENI. ALAMA  ZANGU   ZILIKUWA   NZURI   KULIKO  ZAKE "  akimaanisha  kwamba  kama    YEYE   angekuwa   ndiye   mwenye   BIASHARA ile   bila    shaka  angekuwa    AMEFANYA   VIZURI  ZAIDI.
  JE, LAKINI   HUO   NDIO  UKWELI   WENYEWE  ?Kujisomea   sana   ni   kuishinda  ILE  SEHEMU  MOJA  YA   NAFSI  YAKO   INAYOTAMANI   STAREHE   ZILIZOPO-----KUJINYIMA  SHEREHE  NA  HATA  KUTAZAMA  RUNINGA.  BILA   SHAKA  PIA  RAFIKI  ALIYEFANIKIWA  AMEJINYIMA   MAMBO  HAYO. 

        ILIMBIDI  AJIZUIE   NA  TAMAA  ZA  STAREHE  NA   KUUTUMIA  MUDA  WAKE   WOTE KWENYE    SHUGHULI  ZAKE.  INAHITAJI   UAMUZI   MKUBWA  ILI   KUISHINDA  NAFSI .

Wednesday, September 10, 2014

JE, WEWE NI MJASIRIAMALI ? USIKWEPE KODI , LIPA KODI .

KATIKA   MAZINGIRA    YA   SOKO    HURIA , FAIDA    inayopatikana  katika   BIASHARA  inatakiwa   kuwa     " TUZO  tu   ya   uendeshaji   wa    BIASHARA  katika   njia  inayokubalika.. "  Kwa  wale   wanaopenda  kukwepa   KULIPA  KODI , WAEPUKE    HISIA  MBAYA   dhidi   ya   KODI ,  NA   KUIFIKIRIA   KODI   kama   matumizi  ya  lazima  ya    biashara  , ,  tunayopaswa  KULIPA  kwa    lengo   la  KUSAIDIA JAMII  tunayofanya   nayo   BIASHARA   ZETU.   HATUPASWI KUFICHA  FAIDA  YETU   KICHOYO   ETI   ISIKATWE  KODI !!

    FAIDA   YA   KWELI   katika  BIASHARA    ni  ile    inayotokana   na   Ongezeko   la   MAUZO  pamoja   na   UPUNGUZAJI  WA   GHARAMA  ZA   UZALISHAJI , SIYO  KWA    KUUZA   BIDHAA  KWA   BEI  YA  JUU.

     SIRI   YA     MAFANIKIO  IKO    KWENYE   KUPATA   HESHIMA   KUTOKA  KWA   WATEJA  WAKO  PAMOJA  WALE   UNAOWAONGOZA.    WATEJA  wako  wanapaswa  kuridhika   kuwa   PESA  wanayolipa   inalingana  na   thamani  halisi  ya  bidhaa   au  huduma   wanazopata   toka   kwako .

KANUNI MUHIMU YA MAFANIKIO KATIKA MAISHA.




                " MAFANIKIO == UWEZO   X     JUHUDI    X    MTAZAMO."



 " UWEZO  ni     talanta   ambayo   kila    mmoja     wetu  huzaliwa     nayo.

" MAFANIKIO   yanapatikana   pale   tunapoweka    JUHUDI    katika   kutumia    UWEZO   tulionao , vyote      vikizidishwa   na      MATAZAMO  tunaokuwa    nao.


"MTAZAMO "  hupimwa  kwenye    KIWANGO  kutoka     --100    hadi    +100.    MATOKEO  YA   MAISHA  YETU   hutegemea  zaidi   MTAZAMO    WETU       NI    HASI {--}   AU     CHANYA{ +}
, na   hivyo    KUFANIKIWA     AU   KUTOFANIKIWA  hutegemea  zaidi    MTAZAMO    WETU   WENYEWE.

VITABU VIZURI NILIVYOSOMA KATIKA MAISHA YANGU NA MWL. JAPHET MASATU.


 {1}.  "Passion  for  Success "  by  Dr.  kazuro   Inamori

{2}.  "Jinsi  ya  Kupata   Pesa " Na  Khamisi  Ibrahim  Zephania.

{3}. " Mbinu   za  Mjasiliamali "  Na  Gwakisa  Balele

{4}.  " Elimu   ya   Ujasiliamali  "  Na Emmanuel   Maige.



Monday, September 8, 2014

JITAHIDI KUFANYA VIZURI SANA.

KAMA  UNATAKA  KUFANYA  VIZURI  SANA  KATIKA  MAISHA , HUNA  BUDI  KUWA   TAYARI  KUPAMBANA  NA  VIKWAZO  VINGI.  Kikwazo  kikubwa    kuliko  vyote   NI    MAWAZO  YAKO    MWENYEWE ,  Yanayokusukuma   kwenye  Kwenye   STAREHE   na   MAMBO  RAHISI.


     Kujinyima   hukuwezesha    KUSHINDA  VIZUIZI   NA   KUFANYA   VIZURI  SANA.  Ni   vigumu   kupata    MAENDELEO  YETU  WENYEWE  KWA   SABABU    KWA   KAWAIDA   TUNAPENDA   NJIA   RAHISI. LAKINI  KWA  KULITAMBUA    HILI , TUNAIFANYA  FURAHA  YETU   Kuwa   kubwa   zaidi   pale    tunapobaini  JITIHADA   ZETU   ZIKITOA   MATUNDA.





UWEZO----  Uwezo   mkubwa  kuliko   wote   ni  ule   wa   kuishinda  nafsi   yako   mwenyewe.