Wengi
wanapoingia kwenye safari hii ya utajiri, huwa wanaona mambo mazuri tu
mbele, kwamba wakishapata utajiri maisha yatakuwa mazuri na watakuwa na
furaha.
Felix
anatupa ukweli kuhusu utajiri, kupitia maisha yake binafsi, ili tuelewe
ni kitu gani tunakwenda kukutana nacho mbele, na tujiandae vizuri.
Kwanza
kabisa anasema utajiri haujawahi kumletea yeye furaha, zaidi umemletea
matatizo makubwa ya kiafya baada ya kujihusisha na ulevi, madawa ya
kulevya na uzinzi.
Pili
anasema utajiri unakufanya uwe chambo ambapo kila mtu atatumia kila
njia kupata fedha zako. Wapo watakaotumia njia za kuomba, wengine kuiba
na hata wengine kukushitaki kwa kitu ambacho hujafanya.
Tatu
utajiri utaharibu mahusiano mengi uliyonayo. Mahusiano ya ndoa, kwa
wengi yanaathirika sana. mahusiano ya kifamilia na kindugu nayo
yanaathiriwa sana na safari yako ya utajiri na hata baada ya kufikia
utajiri.
Kwa
kifupi kadiri unavyokuwa tajiri siyo kwamba matatizo uliyonayo
yanaondoka, bali yanakuwa makubwa zaidi. Hivyo jiandae kukabiliana nayo,
na kazana kujijengea busara zaidi kadiri unavyoendelea kutajirika. Kwa
sababu utajiri bila busara utakuwa ni kujichimbia kaburi lako mapema.
No comments:
Post a Comment