Chanzo
kimoja cha kipato ni utumwa, iwe ni kazi au biashara, huwezi kutajirika
kwa kutegemea chanzo kimoja pekee. Angalia matajiri wote wakubwa,
hakuna hata mmoja ambaye anategemea chanzo kimoja pekee cha kipato.
Kila
biashara huwa ina changamoto zake, hakuna biashara ambayo inafanya
vizuri wakati wote, kila biashara kuna kipindi inafanya vizuri na
kipindi kingine inafanya vibaya. Unapotegemea biashara moja pekee, kila
wakati utakuwa kwenye kupanda au kushuka.
Dawa
ya kuondoa hali hiyo ya kupanda na kushuka ni kuwa na vyanzo vingi vya
kipato, na ambavyo havitegemeani. Hivyo unapokuwa na changamoto eneo
moja, eneo jingine linakuwa linaenda vizuri.
Kanuni
hii haiwahusu wale wanaoanza, unapokuwa unaanza, anza na kitu kimoja na
kiwekee msingi imara wa kuweza kujiendesha chenyewe. Baada ya
kuhakikisha kitu cha kwanza kimekuwa imara, hapo sasa unaweza kuanzisha
kitu kingine. Kuanza vitu vingi kwa wakati mmoja ni njia ya uhakika ya
kushindwa.
No comments:
Post a Comment