Wednesday, January 14, 2015

BIASHARA YA DUKA LA VYAKULA NA BIDHAA MCHANGANYIKO.



  DUKA  LA   VYAKULA  NA   BIDHAA  MCHANGANYIKO
 
 
 
Biashara   ya  duka  ni  biashara  nzuri.Inahitaji  mtaji  mdogo  japo  faida  ya  biashara  hii  ni  ndogo  sana na   inahitaji  umakini  na  udhibiti  mkubwa  ili  uweze  kuendelea  na  kufanikiwa.Matatizo  ya  biashara  hii   ni :-  ushindani  wa  kibiashara    kwani  watu  wengi   wanapenda   kuifanya  biashara   hii , udokozi  wa  fedha  na  bidhaa   toka  kwa  muuzaji  na  mmililki  wa  duka, kuchukua  fedha  dukani   bila  kuzirejesha, ukosefu  wa  ubunifu ,  hivyo   kufanya   biashara   kushindwa  kuendelea ,  na  kadhalika. Ili  kukabiliana  na   matatizo  hayo   unapaswa  kuwa   mbunifu.Penye  ushindani  mkubwa   toa  huduma   nzuri  kwa   wateja.Vile  vile  wateja  wako  waaminifu  unaweza kuwafungulia  daftari  na  kuwakopesha   walipe  mwisho  wa  mwezi.Ukiwa   umezungukwa  na   maduka   mengi  ya  rejareja , lifanye  duka  lako  liwe  la  mchanganyiko  la  kuuza  bidhaa  kwa  jumla  na   reja  reja , hivyo  hata  wale  wapinzani  wako  wawe  wateja  wako. Usichukue  vitu  na  fedha  kiholela  toka  dukani, UKICHUKUA  KITU  CHOCHOTE  AU  FEDHA  MWAMBIE  MUUZAJI   AKUANDIKIE  DENI   NA  LAZIMA  ULILIPE  DENI. Kama  UMEJIAJIRI  mwenyewe  na   wewe  ndiyo  unauza   hilo  duka  JIPANGIE  MSHAHARA.  Usichanganye  fedha  za   duka   na   fedha   zako   za  matumizi  ya  nyumbani.