Watu wengi wanakosea kuweka malengo kwa
sababu wanayaweka kipindi ambacho siyo sahihi. Wakati wa mwaka mpya,
watu wengi huwa wanakuwa na hisia kali za upya wa mwaka na kwa kuwa kila
mtu anasema mwaka mpya mambo mapya, basi na wao wanajiunga na msafara
huo.
Wengi wanajikuta wanaweka malengo ambayo
siyo yao, wanapoona wengine wameweka malengo fulani basi na wao wanaona
wanapaswa kuwa na malengo ya aina hiyo. Kitu kinachowapelekea kushindwa
sana kwenye maisha yao.
Wakati sahihi wa kuyaweka malengo yako
kwa mwaka mpya ni kabla mwaka haujaanza. Hivyo mwezi huu wa disemba,
tenga muda na ukae chini ili kuweka malengo yako kwa mwaka unaofuata.
Kupitia tafakari ya mwezi ulioisha uliyofanya, kupitia vipaumbele vya
mwaka ulivyojiwekea, unaweza kuweka malengo ambayo ni bora sana kwako.
Weka malengo yako ya mwaka mpya mwezi
disemba na wakati wengine wanakimbizana na malengo mwanzo wa mwaka, wewe
unakuwa upo kwenye utekelezaji.
HERI YA X--MASS NA MWAKA MPYA.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Tuesday, December 25, 2018
WEKA VIPAUMBELE ( PRIORITES ) MWEZI DISEMBA VYA MWAKA UNAOFUATA.
Kabla hujaweka malengo yoyote, anza
kwanza na vipaumbele. Watu wengi wanakosea kwenye kuweka malengo kwa
sababu hawajui na pia hawana vipaumbele kwenye maisha yao. Hilo
linawapelekea kuweka malengo ambayo hata hawajui wanayafikiaje, kwa
sababu yanakuwa hayaendani na hayajapangiliwa vizuri.
Chagua vipaumbele vichache kwa mwaka unaofuata, angalia yale maeneo ambayo ni ya muhimu zaidi kwenye maisha yako, ambayo ukiyasimamia vizuri na kuyafanyia kazi, utaweza kupata matokeo bora sana kwenye maisha yako.
Kwa kujua vipaumbele vyako, utaweza kuweka malengo ambayo ni sahihi kwako na yanafikika.

KUWA MAKINI NA MSIMU WA SIKUKUU USIKUACHE MWEUPE PEPEEE !!
Mwezi disemba ni mwezi ambao huwa kuna
sikukuu nyingi, ni mwezi ambao wengi wana mategemeo makubwa ya kupumzika
na kusherekea. Lakini unapaswa kuwa makini sana na kipindi cha sikukuu
kwa sababu wengi hujisahau na kuuanza mwaka wakiwa kwenye madeni
makubwa.
Hakikisha unajiwekea bajeti ya matumizi yako kwenye msimu wa sikukuu, na usizidishe kabisa bajeti hiyo. Hakikisha unaamua mapema kabisa ni vitu gani utagharamia kwenye msimu huo wa sikukuu na vipi utaachana navyo.
Na kama kuna sherehe ambazo hazina ulazima, zisikuumize kichwa, achana nazo. Hakuna utakachokikosa kwa kuachana na baadhi ya sherehe na mapumziko. Pia kama utaanza kufanyia kazi malengo yako mapema, utakuwa bize kupiga hatua na sikukuu hazitakuwa na madhara kwako.

UTAFAKARI MWAKA UNAOKWENDA KUUMALIZA.
Watu wengi huwa wanauanza mwaka kwa
matumaini makubwa, wanaweka malengo makubwa lakini huwa hayamalizi
mwezi, wanaachana nayo na kurudi kwenye maisha ya kawaida.
Unapofika mwezi disemba ni wakati mzuri wa kuutafakari mwaka unaokwenda kuumaliza, kuangalia yale malengo na mipango uliyojiwekea na pia kuangalia kwa kiasi gani umeweza kutekeleza.
Kwa yale malengo uliyoachana nayo, jua tatizo ni nini, uliyaweka vibaya au uvivu na uzembe wako ndiyo umekufanya uachane nayo?
Angalia pia fursa mbalimbali ulizokutana nazo kwenye mwaka wako mzima, zile ulizofanyia kazi na zile zilizokupita.
Kwa kuutafakari mwaka unaokwenda kuumaliza, utaweza kuona wapi umefanya vizuri, wapi umekosea na marekebisho yapi ya kufanya.

JIKUMBUSHE KUSUDI LA MAISHA YAKO MWEZI DISEMBA.
Kwa kelele za dunia ni mihangaiko yetu
ya kila siku ni rahisi sana kusahau kusudi la maisha yako. Na
ukishasahau kusudi la maisha yako, huna tofauti na meli ambayo haina
uelekeo. Unaweza kwenda kasi sana, lakini haitakusaidia, kwa sababu
unakuwa tayari umeshapotea.
Unapofika mwisho wa mwaka jikumbushe kusudi la maisha yako, jikumbushe kwa nini upo hapa duniani, jikumbushe nini kinakusukuma kutoka kitandani kila asubuhi.
Kusudi la maisha yako ndiyo linapaswa kukupa msukumo wa kufanya makubwa. Na unapolikumbuka mara zote, linakuwezesha kuchukua hatua sahihi ili kuweza kulitimiza.
Jikumbushe kusudi la maisha yako na jiulize yale unayofanya yanachangiaje kwenye kufikia kusudi la maisha yako.
HERI YA KRISMASI NA MWAKA MPYA !

Saturday, December 22, 2018
TUMIA VIGEZO HIVI VITANO ( 5 ) KUYAFIKIA MALENGO YAKO.
(1).LENGO LINAPASWA KUWA MAALUMU (SPECIFIC).
Kigezo cha kwanza muhimu kwenye kuweka malengo ambayo utayafikia ni umaalumu wa lengo husika. Unapaswa kuweka lengo ambalo linaeleweka ni nini hasa unachotaka.
Unapaswa kujua ni nini kwa hakika unachotaka kwenye lengo hilo, unakipata wapi, utashirikiana na nani, kwa nini unakitaka na hatua zipi unapaswa kuchukua.
Tukienda kwenye mfano wetu wa fedha, usiweke lengo kwamba nataka fedha zaidi, au nataka kuwa bilionea. Unapaswa kuweka kiasi cha fedha unachotaka na kujua utakipataje kwa hatua zipi unazopaswa kuchukua.
Utaona tofauti kubwa kati ya hali hizo mbili, unaposema unataka fedha zaidi, ukipata elfu kumi ambayo hukuwa nayo ni fedha zaidi. Lakini unaposema unataka milioni 50 au bilioni moja, hapo sasa unakuwa na uhakika nini unataka.
Usiweke malengo yanayoelea hewani, jua kabisa nini unataka na nenda mbali zaidi kujua unakipataje na kwa kufanya nini. Pia unapaswa kuwa na kwa nini inayokusukuma kufikia lengo hilo.
(2). LENGO LIPIMIKE (MEASURABLE).
Kigezo cha pili kwenye kuweka malengo utakayoweza kuyafikia ni kila lengo linapaswa kuwa linapimika. Hapa unapaswa kuona kabisa ni jinsi gani kupata kile unachotaka kutabadili maisha yako.
Pia unapaswa kuligawa lengo lako kubwa kwenye hatua ndogo ndogo ambazo unaweza kuzitumia kupima maendeleo yako kwenye lengo hilo.
Kwa mfano kama lengo lako ni kupata milioni 50 kwa mwaka, unaweza kuligawa kwa miezi 12 na ukapata kama milioni 4 kwa mwezi, hii inakuwa rahisi kwako kujipima kila mwezi kuona unaelekeaje kwenye lango lako.
Kuweza kuligawa lengo lako kubwa kwenye hatua ndogo ndogo zinazopimika kutakuondolea kukata tamaa pale lengo linapoonekana ni kubwa sana.
Hakikisha kila lengo unaloweka unaweza kupata taswira ya ukiwa umelikamilisha kisha ligawe kwenye hatua ndogo ndogo ambazo ni rahisi kwako kupima.
(3). LENGO LIWE NINAFIKIKA (ATTAINABLE).
Kigezo cha tatu ni lengo liwe linafikika. Tumekuwa tunayaelewa sana mafunzo ya maendeleo binafsi ambayo yanatufundisha kwamba ndani yetu tuna uwezo mkubwa na tunaweza kufanya chochote tunachotaka kufanya. Hili ni kweli kabisa kwamba tuna uwezo mkubwa na kuweza kufanya chochote tunachotaka.
Lakini inahitaji muda, nguvu na hata vipaji kufikia lengo lolote tunalojiwekea. Hivyo unapoweka lengo, lazima ujiulize je kwa muda, nguvu, rasilimali na hata vipaji ulivyonavyo utaweza kufikia lengo hilo? Kama siyo unajidanganya.
Kwa mfano kama mwaka huu kipato chako ni shilingi milioni moja kwa mwezi, kujiambia kwamba mwaka kesho unataka upate bilioni moja ni kujidanganya na kujiandaa kushindwa. Ni kweli lengo la bilioni moja linafikika, lakini linachukua muda, na linahitaji jitihada zaidi.
Kwenye kila lengo unalojiwekea, angalia rasilimali ulizonazo kisha weka lengo kubwa ambalo litakusukuma, lakini lisikukatishe tamaa.
(4). LENGO LIWE NA UHUSIANO NA KUSUDI LA MAISHA YAKO (RELEVANT).
Kigezo cha nne kwenye kuweka malengo utakayoyafikia ni lengo liwe na uhusiano na kusudi la maisha yako. Mara nyingi wengi wamekuwa wanaweka malengo ambayo siyo yao. Kwa sababu wamesikia wengine wakiweka malengo hayo basi na wao wanaona inabidi wayaweke la sivyo wataachwa nyuma.
Watu wengi wamekuwa wanafuata mkumbo kwenye uwekaji wa malengo, wanaweka malengo ambao hayahusiani kabisa na lile kusudi walilonalo kwenye maisha. Wanapokuja kugundua hili wanashindwa kuendelea na malengo yao.
Kwenye kila lengo unalojiwekea, hakikisha linaendana na kusudi kubwa la maisha yako. Hata kama ni lengo kubwa kiasi gani, kama halitokani na kusudi lako kubwa, utaishia kushindwa.
Usijiambie unataka kupata mabilioni ya fedha kupitia biashara fulani ambayo inaonekana kuwa yenye faida kubwa, wakati wewe unapenda kufanya kitu kingine tofauti kabisa. Lengo unaloweka liendane na kile unachopenda na kujali kufanya.
(5).LENGO LIWE NA UKOMO WA MUDA (TIMELY).
Kigezo cha tano katika kuweka malengo ambayo utayafikia ni kuwa na ukomo wa muda. Wote tunajua jinsi ambavyo ukomo wa muda unavyotusukuma kuchukua hatua. Watu wanaweza kupewa nafasi ya kufanya kitu kwa muda mrefu lakini wasifanye, inapofikia tarehe ya ukomo ndiyo kila mtu anafanya.
Tumia nguvu hii ya ukomo wa muda kwenye malengo unayoweka, kila lengo liwe na ukomo wake wa muda na ujikumbushe ukomo huo ili uweze kujisukuma kufanya zaidi na kufikia lengo hilo. Kwenye kila lengo ulilogawa kwenye hatua ndogo, jiwekee ukomo kwenye kila hatua na ufuate ukomo huo.
Kama umejiambia unataka kupata bilioni moja ndani ya miaka kumi, basi gawa kiasi cha kupata kila mwaka, kila mwezi, kila wiki na hata kila siku, kisha weka muda wa kufuatilia kila kiwango unachotaka kupata ili kuona maendeleo yako yakoje.
Rafiki, hivyo ndivyo vigezo vitano muhimu unavyopaswa kuvitumia kuweka malengo ambayo kwa hakika utayafikia. Tumia vigezo hivi katika kila lengo unaloweka na utaona jinsi utakavyolielewa lengo lako vizuri, kuona kila hatua unayopaswa kuchukua na kuwa na msukumo wa kuchukua hatua kabla muda uliojiwekea haujaisha.

WATU WENGI HUSHINDWA KUYAFIKIA MALENGO YAO ! KWANINI ----------------- ?
Wapo watu ambao wamekuwa wanayaendesha maisha yako kama saa ya mshale ambayo imeharibika. Kwa nje mishale inaweza kuonekana kama inafanya kazi, lakini kwa hakika imesimama.
Wapo watu ambao kila mwanzo wa mwaka huwa wanaweka malengo makubwa, malengo yanayowahamasisha sana na kuwafanya waone wanaweza kufanya makubwa kwenye maisha yao. Lakini siku chache baada ya kuweka malengo hayo, wanajikuta wamesharudi kwenye maisha ya mazoea na kusahau kabisa malengo waliyojiwekea.
Sasa kinachowafanya watu wafanane na saa iliyoharibika ni kwamba mwaka unapoisha na kuanza mwingine, wanaweka tena malengo yale yale na siku chache baadaye wanajikuta wameshayasahau. Hivyo kinachotokea ni mtu kwa miaka mingi anakuwa anarudi kuweka malengo yale yale lakini hachukui hatua wala kuyafikia.
Watu wengi wanaoweka malengo huwa wanashindwa kuyafikia kwa sababu hawavijui vigezo vitano muhimu sana vya kuweka malengo ambayo mtu ataweza kuyafikia.
Subscribe to:
Posts (Atom)