BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE. JIFUNZE ---ELIMIKA --CHUKUA HATUA---FANIKIWA
Thursday, May 22, 2025
Sunday, May 18, 2025
MAKALA : NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA NA NDOTO ZAKO UMEIBEBA WEWE MWENYEWE NA SI MTU MWINGINE--------NA MWL. JAPHET MASATU -------CALL / SMS / WHATSAPP + 266 716 924 136
Kakaa/Dadaa Yangu...
Umesahau wewe ni nani.
Umesahau kuwa ndani yako kuna nguvu ya kutikisa dunia.
Umejikatia tamaa kimya kimya.
Kila siku unasema *labda mimi sina bahati.*
Umeanza kuamini maisha ni magumu na huwezi kubadilisha chochote.
Lakini ukweli ni huu: UNA NGUVU YA MIUJIZA NDANI YAKO ,
Unaitumia vibaya.
Au hujui hata ipo.
Ulishawahi kumuona mtu aliyeanzisha biashara kwa buku 5 akafika juu?
Ulishawahi kumuona mtu aliyefeli shule lakini leo anaajiri waliopata division one?
Ulishawahi kumuona mtu aliyetelekezwa, akasota, lakini leo anajenga nyumba yake?
Wote hawa hawakuwa na miujiza ya mbinguni.
Walitumia nguvu ya ndani waliyoamka nayo kila siku.
Na hiyo nguvu wewe pia unayo.
Lakini... unaitumia kuskroll TikTok.
Unaitumia kulalamika.
Unaitumia kutafuta huruma badala ya suluhisho.
Una nguvu lakini hauna mwelekeo.
Miujiza sio kupasuliwa mbingu.
Sio malaika kushuka.
Miujiza ni pale mtu wa kawaida anapoamua kuamka na kuchukua hatua isiyo ya kawaida.
Ni pale mtu anapoamua kuamka kabla ya wengine.
Kuanza kuandika ndoto zake.
Kuanza kusoma vitabu badala ya magazeti ya udaku.
Kuanza kuomba kazi kwa bidii badala ya kuomba msaada.
Miujiza ni matokeo ya msimamo.
Suluhisho Lipo. Na Lipo Ndani Yako.
Badilisha namna unavyofikiri.
Acha kusema “sina mtaji” sema “naanza na hiki kidogo.”
Acha kusema “nimechelewa” sema “leo ndiyo siku yangu ya kwanza.”
Acha kujificha nyuma ya visingizio.
Toka uvunguni.
Toka kwenye comfort zone ya umaskini wa mawazo.
Chukua hatua.
Anza leo.
Fanya kitu.
Kwa sababu NGUVU YA MIUJIZA UMEIBEBEA WEWE MWENYEWE.
Bado namkumbuka....
Kuna bro mmoja alichoka na maisha.
Alikuwa hana kazi. Hana mtaji. Hana cheti.
Alikaa chini akaandika: “Mwaka huu lazima niwe mtu mwingine.”
Akaanza kuuza karanga mtaani.
Akaweka akiba ya mia mia.
Alikuwa anasoma vitabu alivyokopeshwa.
Alifungua YouTube kujifunza marketing.
Miaka mitatu baadaye...
Ana biashara ya kuuza nafaka.
Ana familia.
Ana ndoto mpya kila mwaka.
Aliniambia hivi:
“Miujiza haikunitokea, niliitengeneza mwenyewe.”
Sasa Wewe Una Sababu Gani Ya Kukata Tamaa?
Huna sababu.
Una kila sababu ya kusimama.
Chukua kalamu na kuandika ndoto zako.
Zima data saa tatu usiku na kupanga kesho yako.
Na anza kutenda miujiza ya kweli kupitia nguvu yako ya ndani.
Kumbuka: Miujiza Haiporomoki.
Miujiza hutengenezwa.
Na hutengenezwa na watu kama wewe.
Watu wa kawaida lakini walioamua kuishi maisha ya ajabu.
ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII UTAJIFUNZA MENGI " MAISHA NA MAFANIKIO ( LIFE & YOU ) BLOG " PENDA KUNUNUA VITABU NA KUVISOMA UTAGUNDUA SIRI NYINGI ZA DUNIA HII.
Friday, May 16, 2025
MAKALA : SHERIA 100 ZA MAISHA NA MAFANIKIO -----NA MWL JAPHET MASATU ---- CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
Kakaa/Dadaa Yangu...
Watu wengi wanakufa maskini si kwa sababu walizaliwa maskini…
Wanabaki maskini kwa sababu wanaishi bila sheria.
Wanapiga hatua moja mbele… halafu wanarudi tatu nyuma.
Siku zinaenda, miaka inasonga… maisha yanabaki pale pale.
Unaamka, unaenda kazini… lakini huna cha maana unaweka mezani.
Kila ukijaribu kusonga, kuna kitu kinakuvuta nyuma.
Unajua ni nini?
Huna ramani.
Huna sheria.
Huna mwelekeo.
Na Hapo Ndio Unatupwa Katika Kundi la “Wanaojitahidi Tu”
Unahangaika sana, lakini hakuna matokeo.
Unasoma vitabu, unaenda semina… lakini maisha yako hayabadiliki.
Una marafiki wanafanikiwa, lakini wewe bado unahaha.
Una ndoto, lakini hazina miguu.
Una malengo, lakini hayatimizwi.
Una nia nzuri, lakini hakuna mbinu.
Inachosha.
Inaumiza.
Inavunja moyo.
Unaweza ukajiona kama vile maisha yamekuchoka.
Kila kitu kinagoma.
Kila mtu anakupita.
Wewe unabaki unaangalia… ukiwa na maswali kuliko majibu.
Na Tatizo Halipo Kwenye Bahati… Lipo Kwenye Mfumo Wako
Wengi wanangoja bahati.
Wanasema: “Siku moja nitapanda juu.”
Hiyo siku haiji.
Kwa sababu hawafuati sheria.
Sheria za maisha.
Sheria za mafanikio.
Hakuna mafanikio bila sheria.
Kama vile gari halisafiri bila barabara.
Kama vile mti hauoti bila mizizi.
Maisha yanahitaji misingi.
Na misingi hiyo ni sheria.
Na sio sheria ngumu.
Ni zile rahisi.
Zenye mantiki.
Zenye mpangilio.
Lakini wengi hawajui.
Wengine wamewahi kusikia, lakini hawafuati.
Na ndio maana maisha yao ni kama gari lililoharibika breki, linaenda tu... bila mwelekeo.
Sasa Hii Ndio Dawa – Sheria 100 Za Maisha Ya Mafanikio
Nimekuandalia sheria hizi kwa jasho na damu.
Zimetoka kwa tajiri aliyewahi kulala kwenye dari la mabati.
Zimetoka kwa kijana aliyekua anauza vocha, leo ana kampuni.
Zimetoka kwa mwanamke aliyetelekezwa, leo ana biashara tano.
Sheria hizi ni silaha.
Zikupatie mwelekeo.
Zikupatie nguvu ya kupambana.
Zikusaidie kuachana na maisha ya mdundo mmoja.
Ukitaka kubadilisha maisha yako…
Ukitaka kuamka kutoka usingizini...
Sheria hizi ni Biblia / Juzuu yako mpya.
Sikiliza Story ya Kelvin Kijana Aliyeamua Kubadilika
Kelvin alikua anaishi Tandale, kwa mama wa kambo.
Alikua anafukuzwa shule kila siku —si kwa sababu ni mjinga, bali hakuwa na sare.
Alikua anaota kuwa mtu mkubwa, lakini mtaa ulimcheka.
Siku moja akapewa kitabu kidogo tu kilikua na "Sheria 100 Za Maisha Ya Mafanikio"
Akakisoma.
Akaanza kubadili tabia.
Akaanza kuamka mapema.
Akaanza kujifunza kila siku.
Akaacha kulalamika.
Leo Kelvin ni mkurugenzi wa kampuni inayouza bidhaa mitandaoni.
Analipa kodi.
Anasaidia mama yake.
Anafundisha vijana wenzie.
Na yeye anasema hivi:
"Maisha yanabadilika pale unapofuata sheria za maisha, si pale unapongoja msaada."
Sasa Ni Zamu Yako
Sheria 100 hizi si hadithi za kuburudisha.
Ni mashine ya kukutoa kwenye maisha ya hovyo hovyo.
Ni mwelekeo mpya wa mafanikio.
Ukiamua kuzifuata, hakuna kitakachokuzuia.
Ukiamua kuzipuuza, usilalamike maisha yanapokuchezea.
ENDELEA KUPERUZI NA KUSOMA BLOG HII " MAISHA NA MAFANIKIO ( AND LIFE ) BLOG "
ILI UJIFUNZE SHERIA/ KANUNNI ZA KUFANIKIWA KATIKA MAISHA YAKO.
Thursday, May 15, 2025
MAKALA : USILAUMU WAZAZI , SI KOSA LAKO HATUKUFUNDISHWA KUHUSU ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA NA MAUZO---JIFUNZE UINUKE---BIASHARA NI AKILI NA MAARIFA------------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136
*Siyo Kosa Lako, Hujafundishwa TU!*
Kakaa/Dadaa..
Unajua kuna watu wanawacheka wajasiriamali wadogo?
Huku wakiwasema vibaya:...
*Mbona kila biashara unayoanzisha haifiki miezi mitatu?*
*Unapenda kulalamika sana!”
*Wewe huwezi fanikiwa kamwe!*
Na huwa naumia nikisikia haya maneno.
Kwa sababu…
Watu hawajui mateso yanayomfanya mtu aamue kuuza maandazi saa 12 asubuhi bila hata chai.
Hawajui…
Maumivu ya kutafuta mtaji wa elfu 20 kwa kuazima mia mia.
Kunyanyaswa na maneno ya jamaa zako:
“Kama ni biashara ya maandazi si kila mtu anafanya?”
Kukesha ukitengeneza sabuni halafu asubuhi mvua inanyesha, hakuna mtu hata mmoja kununua.
Sasa leo nakuambia ukweli:
Siyo Kosa LAKO.
Haujafundishwa TU!..
Tatizo Si Wewe, Ni Mfumo Wetu.
Shule zetu hazikufundisha namna ya kuuza.
Hazikufundisha namna ya kujua faida.
Hazikufundisha namna ya kumshawishi mteja.
Tulifundishwa 1+1=2.
Lakini hatukufundishwa jinsi ya kutengeneza buku kwa kuuza karanga.
Ukatoka shule ukiwa na degree.
Au ukiwa form four.
Au hata bila cheti.
Lakini wote mko sokoni mnaanza biashara kama vipofu wanaovuka barabara.
Na Ndio Maana…
Unajikuta unafungua duka la vocha,
Unaanza kuuza na sabuni tano, pipi za mchina, na airtime ya mia.
Mwishoni mwa mwezi…
Umeuza elfu 50.
Umebakiwa na 10.
Na hata hujui imepotelea wapi.
Wewe si mzembe.
Wewe si mjinga.
Wewe ni mtu jasiri lakini hujapewa silaha.
Sasa Sikiliza Hii:
Kabla hujaanza biashara yoyote…
Unahitaji kujua vitu vitano tu vya msingi:
1. Shida ya watu ni ipi?
Watu hawataki bidhaa, wanataka suluhisho.
2. Unawauzia kina nani?
Hakuna biashara ya “kila mtu”
3. Unawafikiaje?
Kama hawaitwi hawaji. Kama hawajui hawanunui.
4. Bei yako inasemaje?
Bei nzuri haimaanishi rahisi inamaanisha INAOANA na thamani.
5. Faida yako iko wapi?
Si pesa inayoingia, ni pesa inayobaki baada ya gharama.
Stori Ya Kweli Ya Dada Zawadi Wa Gongo La Mboto....
Zawadi alikuwa anafua nguo kwa watu.
Kila siku jua likitoka, anajitwika ndoo, anazunguka mtaani akitafuta wateja wa kuwafulia hadi jioni.
Analipwa elfu mbili elfu tatu.
Anaondoka na macho mekundu, mikono iliyochubuka,
Lakini hana hela hata ya sabuni.
Siku moja alihudhuria semina ya biashara.
Akaambiwa kitu kimoja tu:
*Fungua huduma yako. Uisajili. Toa package. Weka namba zako mitandaoni.*
Leo Zawadi haendi nyumba hadi nyumba.
Anapokea simu.
Wateja wanamfuata.
Anatoza elfu kumi hadi elfu ishirini kwa huduma ya kitaalamu.
Na bado anafua nguo.
Lakini kwa akili.
Tunaambiwa tukomae. Lakini hatuambiwi namna.
Tunaambiwa tufanye kazi kwa bidii. Lakini bidii bila maarifa ni kama kukata mti kwa kijiko.
SULUHISHO?
Sihitaji nikuambie uache biashara.
La hasha.
Nakuheshimu.
Ninachokuambia ni hivii…:
Chukua hatua ya kutafuta elimu ya msingi ya biashara.
Elimu inayoeleweka.
Elimu ya mtaani.
Elimu ya kweli.
Kabla hujapoteza muda tena,
Kabla hujakataliwa tena,
Kabla hujachoka kujaribu jifunze.
Kwa Nini?
Kwa sababu:
Huwezi kufanikiwa kwa kukurupuka.
Na
Siyo kosa lako kuwa hujui.
Lakini litakuwa kosa lako ukikataa kujua.
Kama makala hii imekuongelea wewe, huna haja ya kujionea aibu.
Kila shujaa alianza akiwa hajui.
Lakini waliamua KUJIFUNZA.
Nataka nikupe silaha mbili za siri.
Ni silaha za kumtokomeza ujinga,
Silaha hizo ni Elimu Ya Msingi Ya Biashara na CHUO CHA MAUZO, Kwa Mtu Wa Mtaa.
#SioKosaLako
#JifunzeUinuke
#BiasharaNiAkiliNaMaarifa