Friday, May 16, 2025

MAKALA : SHERIA 100 ZA MAISHA NA MAFANIKIO -----NA MWL JAPHET MASATU ---- CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

Kakaa/Dadaa Yangu...

‎Watu wengi wanakufa maskini si kwa sababu walizaliwa maskini…

‎Wanabaki maskini kwa sababu wanaishi bila sheria.

‎Wanapiga hatua moja mbele… halafu wanarudi tatu nyuma.

‎Siku zinaenda, miaka inasonga… maisha yanabaki pale pale.

‎Unaamka, unaenda kazini… lakini huna cha maana unaweka mezani.

‎Kila ukijaribu kusonga, kuna kitu kinakuvuta nyuma.

‎Unajua ni nini?

‎Huna ramani.

‎Huna sheria.

‎Huna mwelekeo.

‎Na Hapo Ndio Unatupwa Katika Kundi la “Wanaojitahidi Tu”

‎Unahangaika sana, lakini hakuna matokeo.

‎Unasoma vitabu, unaenda semina… lakini maisha yako hayabadiliki.

‎Una marafiki wanafanikiwa, lakini wewe bado unahaha.

‎Una ndoto, lakini hazina miguu.

‎Una malengo, lakini hayatimizwi.

‎Una nia nzuri, lakini hakuna mbinu.

‎Inachosha.

‎Inaumiza.

‎Inavunja moyo.

‎Unaweza ukajiona kama vile maisha yamekuchoka.

‎Kila kitu kinagoma.

‎Kila mtu anakupita.

‎Wewe unabaki unaangalia… ukiwa na maswali kuliko majibu.

‎Na Tatizo Halipo Kwenye Bahati… Lipo Kwenye Mfumo Wako

‎Wengi wanangoja bahati.

‎Wanasema: “Siku moja nitapanda juu.”

‎Hiyo siku haiji.

‎Kwa sababu hawafuati sheria.

‎Sheria za maisha.

‎Sheria za mafanikio.

‎Hakuna mafanikio bila sheria.

‎Kama vile gari halisafiri bila barabara.

‎Kama vile mti hauoti bila mizizi.

‎Maisha yanahitaji misingi.

‎Na misingi hiyo ni sheria.

‎Na sio sheria ngumu.

‎Ni zile rahisi.

‎Zenye mantiki.

‎Zenye mpangilio.

‎Lakini wengi hawajui.

‎Wengine wamewahi kusikia, lakini hawafuati.

‎Na ndio maana maisha yao ni kama gari lililoharibika breki, linaenda tu... bila mwelekeo.

‎Sasa Hii Ndio Dawa – Sheria 100 Za Maisha Ya Mafanikio

‎Nimekuandalia sheria hizi kwa jasho na damu.

‎Zimetoka kwa tajiri aliyewahi kulala kwenye dari la mabati.

‎Zimetoka kwa kijana aliyekua anauza vocha, leo ana kampuni.

‎Zimetoka kwa mwanamke aliyetelekezwa, leo ana biashara tano.

‎Sheria hizi ni silaha.

‎Zikupatie mwelekeo.

‎Zikupatie nguvu ya kupambana.

‎Zikusaidie kuachana na maisha ya mdundo mmoja.

‎Ukitaka kubadilisha maisha yako…

‎Ukitaka kuamka kutoka usingizini...

‎Sheria hizi ni Biblia / Juzuu yako mpya.

‎Sikiliza Story ya Kelvin Kijana Aliyeamua Kubadilika

‎Kelvin alikua anaishi Tandale, kwa mama wa kambo.

‎Alikua anafukuzwa shule kila siku —si kwa sababu ni mjinga, bali hakuwa na sare.

‎Alikua anaota kuwa mtu mkubwa, lakini mtaa ulimcheka.

‎Siku moja akapewa kitabu kidogo tu kilikua na "Sheria 100 Za Maisha Ya Mafanikio"

‎Akakisoma.

‎Akaanza kubadili tabia.

‎Akaanza kuamka mapema.

‎Akaanza kujifunza kila siku.

‎Akaacha kulalamika.

‎Leo Kelvin ni mkurugenzi wa kampuni inayouza bidhaa mitandaoni.

‎Analipa kodi.

‎Anasaidia mama yake.

‎Anafundisha vijana wenzie.

‎Na yeye anasema hivi:

‎"Maisha yanabadilika pale unapofuata sheria za maisha, si pale unapongoja msaada."

‎Sasa Ni Zamu Yako

‎Sheria 100 hizi si hadithi za kuburudisha.

‎Ni mashine ya kukutoa kwenye maisha ya hovyo hovyo.

‎Ni mwelekeo mpya wa mafanikio.

‎Ukiamua kuzifuata, hakuna kitakachokuzuia.

‎Ukiamua kuzipuuza, usilalamike maisha yanapokuchezea.

ENDELEA   KUPERUZI    NA   KUSOMA  BLOG  HII  "  MAISHA    NA   MAFANIKIO  (  AND  LIFE  )   BLOG " 

ILI  UJIFUNZE  SHERIA/  KANUNNI   ZA  KUFANIKIWA  KATIKA  MAISHA    YAKO.

Thursday, May 15, 2025

KITABU 339 : KAPTULA LA MARX ---FULL KITABU-----VITO VYA FASIHI-----NA EUPHRASE KEZILAHABI----TANZANIA---1999 , 2010---( PDF )---CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 

MAKALA : USILAUMU WAZAZI , SI KOSA LAKO HATUKUFUNDISHWA KUHUSU ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA NA MAUZO---JIFUNZE UINUKE---BIASHARA NI AKILI NA MAARIFA------------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

*Siyo Kosa Lako, Hujafundishwa TU!*

‎Kakaa/Dadaa..

‎Unajua kuna watu wanawacheka wajasiriamali wadogo?

‎Huku wakiwasema vibaya:...

‎*Mbona kila biashara unayoanzisha haifiki miezi mitatu?*

‎*Unapenda kulalamika sana!”

‎*Wewe huwezi fanikiwa kamwe!*

Na huwa naumia nikisikia haya maneno.

‎Kwa sababu…

‎Watu hawajui mateso yanayomfanya mtu aamue kuuza maandazi saa 12 asubuhi bila hata chai.

‎Hawajui…

‎Maumivu ya kutafuta mtaji wa elfu 20 kwa kuazima mia mia.

‎Kunyanyaswa na maneno ya jamaa zako:

‎ “Kama ni biashara ya maandazi si kila mtu anafanya?”

‎Kukesha ukitengeneza sabuni halafu asubuhi mvua inanyesha, hakuna mtu hata mmoja kununua.

‎‎Sasa leo nakuambia ukweli:

‎Siyo Kosa LAKO.

‎Haujafundishwa TU!..

‎Tatizo Si Wewe, Ni Mfumo Wetu.

‎Shule zetu hazikufundisha namna ya kuuza.

‎Hazikufundisha namna ya kujua faida.

‎Hazikufundisha namna ya kumshawishi mteja.

‎Tulifundishwa 1+1=2.

‎Lakini hatukufundishwa jinsi ya kutengeneza buku kwa kuuza karanga.

‎Ukatoka shule ukiwa na degree.

‎Au ukiwa form four.

‎Au hata bila cheti.

Lakini wote mko sokoni mnaanza biashara kama vipofu wanaovuka barabara.

‎Na Ndio Maana…

‎Unajikuta unafungua duka la vocha,

‎Unaanza kuuza na sabuni tano, pipi za mchina, na airtime ya mia.

‎Mwishoni mwa mwezi…

‎Umeuza elfu 50.

‎Umebakiwa na 10.

‎Na hata hujui imepotelea wapi.

‎Wewe si mzembe.

‎Wewe si mjinga.

‎Wewe ni mtu jasiri lakini hujapewa silaha.

‎Sasa Sikiliza Hii:

‎Kabla hujaanza biashara yoyote…

‎Unahitaji kujua vitu vitano tu vya msingi:

‎1. Shida ya watu ni ipi?

‎Watu hawataki bidhaa, wanataka suluhisho.

‎2. Unawauzia kina nani?

‎Hakuna biashara ya “kila mtu”

‎3. Unawafikiaje?

‎Kama hawaitwi hawaji. Kama hawajui hawanunui.

‎4. Bei yako inasemaje?

‎Bei nzuri haimaanishi rahisi inamaanisha INAOANA na thamani.

‎5. Faida yako iko wapi?

‎Si pesa inayoingia, ni pesa inayobaki baada ya gharama.

‎Stori Ya Kweli Ya Dada Zawadi Wa Gongo La Mboto....

‎Zawadi alikuwa anafua nguo kwa watu.

‎Kila siku jua likitoka, anajitwika ndoo, anazunguka mtaani akitafuta wateja wa kuwafulia hadi jioni.

‎‎Analipwa elfu mbili elfu tatu.

‎Anaondoka na macho mekundu, mikono iliyochubuka,

‎Lakini hana hela hata ya sabuni.

‎Siku moja alihudhuria semina ya biashara.

‎Akaambiwa kitu kimoja tu:

‎‎ *Fungua huduma yako. Uisajili. Toa package. Weka namba zako mitandaoni.*

‎Leo Zawadi haendi nyumba hadi nyumba.

‎Anapokea simu.

‎Wateja wanamfuata.

‎Anatoza elfu kumi hadi elfu ishirini kwa huduma ya kitaalamu.

‎Na bado anafua nguo.

‎Lakini kwa akili.

‎Tunaambiwa tukomae. Lakini hatuambiwi namna.

‎Tunaambiwa tufanye kazi kwa bidii. Lakini bidii bila maarifa ni kama kukata mti kwa kijiko.

‎SULUHISHO?

‎Sihitaji nikuambie uache biashara.

‎La hasha.

‎Nakuheshimu.

‎Ninachokuambia ni hivii…:

‎Chukua hatua ya kutafuta elimu ya msingi ya biashara.

‎Elimu inayoeleweka.

‎Elimu ya mtaani.

‎Elimu ya kweli.

‎Kabla hujapoteza muda tena,

‎Kabla hujakataliwa tena,

‎Kabla hujachoka kujaribu jifunze.

Kwa Nini?

‎Kwa sababu:

‎Huwezi kufanikiwa kwa kukurupuka.

‎Na

‎Siyo kosa lako kuwa hujui.

‎Lakini litakuwa kosa lako ukikataa kujua.

‎Kama makala hii imekuongelea wewe, huna haja ya kujionea aibu.

‎Kila shujaa alianza akiwa hajui.

‎Lakini waliamua KUJIFUNZA.

‎‎Nataka nikupe silaha mbili za siri.

‎Ni silaha za kumtokomeza ujinga,

Silaha hizo ni Elimu Ya Msingi Ya Biashara na CHUO CHA MAUZO, Kwa Mtu Wa Mtaa.

‎#SioKosaLako

‎#JifunzeUinuke

‎#BiasharaNiAkiliNaMaarifa

KITABU 340 : NO FUTURE WITHOUT FORGIVENESS----FULL BOOK---BY DESMOND MPILO TUTU----SOUTH AFRICA----1999----( PDF )-----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

Monday, May 12, 2025

KITABU 340 : 101 WAYS TO MAKE MONEY IN AFRICA---FULL BOOK---LUCRATIVE BUSINESS IDEAS , INSPIRING SUCCESS STORIES , AND INTERESTING BUSINESS OPPORTUNITIES FOR FORWARD THINKING ENTREPRENEURS----BY JOHN AUL LWUOHA & HARNET BOKREZION PHD-----FIRST EDITION , NOVEMBER , 2014-----CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

MAKALA : UMASKINI UNAUTAKA WEWE MWENYEWE , USILALAMIKIE WATU , NDUGU WALA SERIKALI ? ANZA NA BUKU ( TSHS 1000 ) KUWEKA AKIBA .----------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 

Kaka, dada, hebu tuambiane ukweli…

‎Umechoka kuishi kwa mlo mmoja?

‎Au kila mwisho wa mwezi ni stress tupu?

‎Mishahara inapita kama upepo.

‎Biashara haieleweki.

‎Kuna hela, lakini haikai.

‎Unafanya kazi kama punda, lakini mfuko ni kama gunia la mbolea mashimo kila kona.

‎Unajituma, lakini mafanikio yako kama ndoto ya mchana.

‎Kaka, hiyo siyo laana.

‎Ni mfumo mbovu wa maisha.

‎Ni kukosa maarifa sahihi.

‎Tazama wenzako wanaoanza na elfu moja,

‎Leo wanamiliki vibanda, magari, hadi mashamba.

‎Wewe bado unatafuta mtu wa kukukopesha buku la kula.

‎Ni aibu.

‎Lakini sio kosa lako kabisa.

‎Ni kwamba wakati unakuwa uliaminishwa kuwa*Ukiwa na hela nyingi, ndo unaweza kuwekeza.*

‎Na Wewe Ukaamini.

‎Ulimwengu unabadilika, lakini mtazamo wako umebaki kuwa ule wa miaka ya 70.

‎Upo kwenye mduara wa mateso pesa inaingia na kutoka bila faida.

‎Kila mwezi ni kama kuanza maisha upya.

‎Mpaka lini?

‎Watu wengi hudhani kwamba ili uanze kujenga utajiri, lazima uwe na mamilioni.

‎Hapo ndo tunakosea.

‎Ukweli ni huu:

‎Hela kidogo ndiyo mwanzo wa hela nyingi.

‎Tatizo si kwamba huna pesa.

‎Tatizo ni kwamba hujui namna ya kukitumia kile kidogo ulichonacho.

‎Huna mfumo.

‎Huna maarifa.

‎Unakula mtaji, unaua ndoto zako.

Usingoje mshahara mwingine ukufikishe kwenye msongo tena.

‎Usingoje upate milioni ndo uanze.

‎Anza na hiyo buku  YAANI  TSHS  1000

‎Buku yako ya leo inaweza kuwa sababu ya uhuru wako wa kesho.

 ENDELEA  KUSOMA    KILA     SIKU   "  MAISHA     NA  MAFANIKIO  BLOG "  UTAJIFUNZA  MENGI  NA  SIRI    NYINGI  ZA  MAISHA   NA  MENGINEYO  DUNIANI  --- ONGEA  NA   KOCHA    MWL.  JAPHET  MASATU-----CALL  /  SMS   /  WHATSAPP  +  255  716  924 136