Wednesday, April 30, 2025

MAKALA : KUWA NA NIDHAMU NA PESA ZAKO !! ANZA KUWEKEZA BUKU ( SH 1000 ) KILA SIKU UJENGE UTAJIRI WAKO WA KESHO ----NA MWL. JAPHET MASATU---------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

Mpendwa Rafiki,

‎Watu wengi wanaamini kuwa ili uanze kujenga utajiri, lazima uwe na hela nyingi ,milioni tano, kumi, au hata zaidi.

‎Wengine wanasema, *Mimi ni wa mshahara wa chini, siwezi kufika mbali.*

‎Lakini ukweli ni kwamba watu wengi hawajui kitu kimoja muhimu: nguvu ya *buku* moja tu.

‎Buku ambayo unaitumia bila mpango kila siku, inaweza kuwa tiketi yako ya kutoka kwenye umaskini hadi kwenye uhuru wa kifedha.

‎Ni mara ngapi umetumia buku kununua soda, chipsi, vocha, au kitu usichohitaji halafu ukaishia kusema, *Ah ni buku tu*?

‎Halafu mwisho wa mwezi unakuta umekopa, umeshindwa kuwekeza, hata akiba huna.

‎‎Inasikitisha, siyo? Sasa fikiria, kama kila siku unapoteza buku moja tu, ndani ya mwezi umepoteza buku 30.

‎Mwaka mzima? Hiyo ni buku  360,000!

‎Na kama ungezitumia kuanzisha biashara ndogo au kuwekeza, ungekuwa mbali.

‎Hiyo ndiyo nguvu tuliyo nayo lakini hatuitumii.

‎Wengi tulifundishwa kwamba hela nyingi ndiyo hujenga utajiri.

‎Tukaanza kusubiri *mshahara mkubwa,* *tenda kubwa za kibiashara," au *mjomba wa Dubai.*

‎Lakini hizo ni hadithi.

‎‎Angalia Uhalisia : Hela hujengeka kwa nidhamu na mpango, siyo kiasi.

‎Watu matajiri hawakuanza na mamilioni.

‎Walitumia kile kidogo walichokuwa nacho kwa akili.

‎Walitunza, wakawekeza, wakaendeleza.

‎Kwa hiyo, tukiachana na dhana ya *nitakapoanza kupata hela kubwa,* tunaweza kuanza safari ya utajiri hata leo,

‎Kwa ile buku tuliyonayo mfukoni.

‎Sasa hebu tuweke wazi, unataka kujenga utajiri kwa kutumia buku?

‎Hizi hapa ni hatua 3 rahisi lakini zenye nguvu:

‎a. Weka akiba ya buku 1 kila siku:

‎Tafuta kopo, lipachike mahali salama. Kila siku, kabla ya kutumia hela yoyote, tengeneza tabia ya kuweka buku moja pembeni.

‎b. Anza kuwekeza kidogo:

‎Baada ya mwezi mmoja, utakuwa na zaidi ya buku 30.

‎Tafuta biashara ndogo, lipia kozi fupi, au nunua bidhaa za kuuza mitandaoni.

c. Wekeza kwenye maarifa:

‎Buku moja inaweza kununua data. Tumia hiyo kusoma makala, kuangalia video za elimu ya fedha, au kusikiliza podcast. Maarifa ni mtaji.

‎Kuna jamaa yangu mmoja anaitwa Mussa,

‎Alikuwa na mshahara wa laki na 20 kwa mwezi.

‎Alikuwa na majukumu mengi lakini alianza kuweka buku moja kila siku.

‎Miezi sita baadaye, alikuwa na buku 180.

‎Akanunua kahawa na kuanza kuuza kikombe ofisini kwao, faida yake ilikuwa buku 2 kwa kila kikombe.

‎Siku moja akaniambia,

‎‎*Bro, ile tabia ya kuweka buku moja kwa siku ilinibadilishia maisha.

‎Sasa hivi nina biashara mbili na bado naendelea kuweka akiba!*

‎Ukweli ni huu:

‎Buku moja inaweza kuwa mtaji wa maisha yako mapya.

‎Usidharau kile kidogo, ndani yake kuna nguvu kubwa sana ya kifedha.

‎Anza leo, anza sasa.

‎Usisubiri mshahara mkubwa, anza na buku!


‎Kumbuka; Buku yako ya leo, ndiyo utajiri wako wa kesho.

MAKALA : MSHAHARA HAUJAWI KUMTOSHA MTU YEYOTE DUNIANI ??? HUJUI PESA YAKO INAPOTELEWA WAPI ?? MATUMIZI NI MAKUBWA KULIKO KIPATO UNACHOPATA ???!!!---- -----NA MWL . JAPHET MASATU---------CALL / SMS / WHATSAPP + 255 716 924 136

 Basi Sikiliza Hii Siri Ya Wale Wanaofanikiwa Na Kipato Kidogo!…

Mpendwa Rafiki,

Wengi wetu tunasoma, tunahangaika, tunachapa kazi usiku na mchana,

...lakini hela inavyopatikana si sawa na inavyopotea.

Kule shule waliwahi kukufundisha (compound interest), lakini hawakuwahi kukufundisha kutokutumia hela hovyo wiki ya mshahara.

Ujuzi wa fedha ni uwezo wa....

Kujua hela yako inaingia wapi na inatoka vipi,

Kujua muda gani ni wa matumizi na muda gani ni wa kuweka akiba,

Kuweza kupangilia matumizi kabla mshahara haujalala kwenye simu.

Na ukweli mchungu ni huu:

Si kiasi cha hela unachopata kinachokufanya uwe vizuri, ni vile unavyotumia hiyo hela.

Ebu Niambie, Wewe Uko Wapi?

Hebu kuwa mkweli...

Umewahi kupata mshahara, halafu wiki ya pili unakopa kwa mpesa?

Umewahi kuwa na hela nzuri mkononi, ukajisikia *bosi* – halafu baada ya wiki mbili ukawa broke kama mwanafunzi wa form one?

Umewahi kujiambia, *Mwezi huu nitapanga matumizi vizuri,* lakini siku ya tarehe 5 mshahara ushakwisha?

Kama jibu lako ni *ndiyo* hata mara moja,

... basi wewe si mgeni kwenye kasheshe hili la kukosa ujuzi wa fedha.

Waliokudanganya Kwamba…

Hela inaisha tu bro, hakuna jinsi ya kuizuia.

Maisha ni magumu kwa kila mtu, hakuna anayefanikiwa bila kuibia watu.

Weka hela benki? Hela ya matumizi si ya kuwekwa tu!

Hizi ni kauli tunazojidanganya nazo kila siku.

Lakini ukweli ni huu....

Hela yako haitoshi si kwa sababu hujui kupata, ni kwa sababu hujui kuitunza.

Na hakuna mtu atakayekuja kukuokoa hadi uanze kujifunza wewe mwenyewe.

Na Hii Ndio Njia....

Ujuzi wa fedha sio somo gumu kama hesabu za algebra.

Ni mambo madogo sana ambayo ukiyajua, unabadilika kama saa.

Zifuatazo Ni Njia Tatu (3) Rahisi Unazoweza Kuanza Kuzitumia.

1. Tenga asilimia 10 ya kipato chako mara tu inapopatikana.

Hata kama ni buku tano, anzia hapo.

2. Andika matumizi yako ya kila siku.

Ukishangaa unavyonunua vinywaji vya 3,000 kila jioni, utajua hela zako zinapotelea wapi.

3. Jifunze njia za kuongeza kipato bila kuongeza kazi.

Huu ndio wakati wa kujua kutumia maarifa yako, sio nguvu zako tu.

Chukua Hatua....

Bro, Dada, ukikaa unasema ‘nitabadilika tu muda ukifika’, muda wenyewe haufiki.

Muda upo, ila wewe ndo hujaamka.

Kumbuka;
Maisha yako ya kesho yanatengenezwa na maamuzi yako ya leo, si mshahara wako wa mwezi ujao.