| Chochote kile kinaweza kutokea au kumpata yeyote katika maisha yetu ya kila siku. Hii ndilo somo pana la maisha na asili linavyotuandaa kuwa lolote linaloweza kujitokeza bila kujali mtu, cheo au mazingira. Tumekuwa tunaona mfano kifo kinavyoweza kumkuta yeyote yule na wakati mwingine hata bila kutarajia tunasikia habari za vifo vya watu ambao tulifikiria huenda hawakutakia kufa sasa. Hilo ni moja linalojitokeza ambalo linatufundisha kuwa kwa yeyote yule kifo kinaweza kujitokeza. Maisha ni mfululizo wa matukio ambayo yanaendelea kutokea na kutufundisha kuwa yale ambayo tulikuwa tukiamini hayawezi kujitokeza hujitokeza. Kuna namna huwa tunafikiria sisi kuwa mambo yataenda vizuri kwa kuwa tumejiandaa vizuri ila huwa tunashuhudia namna mambo yanavyoenda vibaya licha maandalizi yalikuwa mazuri. Asili wakati mwingine inatufundisha tuone mambo kwa sura mpya kabisa. Maisha yetu yanapokaribia nafasi ya ujana na utu uzima huwa ni masomo mengi tunayoendelea kuyapitia kupitia visa na watu. Kuna mambo huwatokea watu wengine na hili linatuzindua akili kuwa hata kumbe watu wengine nao wanapitia magumu, wanaanguka, wanashindwa au wanafeli. Ukijifunza hili utajiandaa kuwa maisha yataenda kufundisha masomo magumu na kutuondoa ujuaji wetu wa mambo. Falsafa inatuandaa kwa hili kuwa tutaenda kushuhudia mengi ambayo tulidhani hayawezekani kutokea yatakatokea. Hili litagusa pia hata maisha yetu moja kwa moja kuwa mengine ambayo tutafikiria kuwa hayawezi kujitokeza kwetu basi yatajitokeza. Maandalizi ya kuwa mambo yanaweza kwenda tofauti ni muhimu mno ili uepuke kushangaa au kushangazwa na mambo yatakavyokuwa tofauti. Wengi huwa hawaamini hili mpaka pale ambapo mambo hujitokeza na kugundua kuwa maisha mambo hujitokeza si vile tutakavyo sisi ila hujitokeza namna yalivyo yenyewe tu. Katika kusubiri au kushuhudia wakati unaokuja mambo yaloonekana hayawezekani yakawezekana linaweza kujitokeza hata katika magumu au matatizo ambayo yapo sasa kuja kuwa na majibu wakati ujao. Magumu yalokuwepo jana na kuonekana ilikuwa ngumu kumalizika basi leo yamepata majibu. Ndivyo inavyojitokeza kuwa magumu ya sasa yataenda kupata majibu na njia itapatikana siku zijazo. Maisha ni mchezo wa ajabu usoacha kutufunza na kutubadilisha namna tulivyokuwa tukichukulia mambo yalivyo. NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU , DAR ES SALAAM , TANZANIA ( WhatsApp + 255 716 924 136 / ) / + 255 755 400128 / + 255 688361 53 9 EMAIL : japhetmasatu@gmail.com |
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Sunday, March 28, 2021
MCHEZO UITWAO MAISHA.
KUWA TAYARI KUISHI UHALISIA WAKO , UACHE ALAMA NJEMA.
Maisha yetu mengine huanza pindi tunapomaliza maisha haya ya mwili. Awamu hii ya pili ya maisha ni kuishi katika mioyo ya watu wakikumbuka namna tulivyogusa maisha yao kipindi uhai wetu ulipokuwepo. Nafasi hii ya kushuhudia kila kitu ambacho kimeachwa kama alama tuachayo huchipua pindi ukomo wa maisha yetu ufikapo na hivyo huwa hatuoni namna alama iloachwa bali waloachwa hushuhudia.
Maisha yetu ni alama na nyayo tunazoacha kuwa tulikuwepo wakati fulani wa maisha. Alama za maisha yetu zinabebwa na kumbukumbu ambazo zinaachwa mioyoni mwa watu ambao huwa tayari kubeba masimulizi kwa vizazi vingine. Watu wenye alama njema alama ya matendo yao huchipua na kuendelea kuishi kwa muda mrefu.
Kuishi katika vipawa na vipaji ulivyopewa kwa ukubwa au kutojibakiza ndivyo alama njema inavyoacha katika mioyo ya watu. Jina la mtu atendaye mambo mema hudumu na kukua zaidi. Mtu hukumbukwa kwa vile alivyowagusa watu kwa namna mbalimbali
Moja ya mambo niaminiyo kuwa uwepo wetu wa maisha ni kuacha alama ya vipawa, vipaji, ujuzi na uzoefu kwa kuandaa njia kwa ajili ya watu wengine. Tulipo leo ni kwa sababu ya majitoleo ya watu wengi ambao majitoleo yao hawakuweza kuona matokeo ya mbegu walizopanda, majitoleo yao ndio unafuu ambao tunao sasa na majitoleo yao ni njia ambazo leo tunapita kwa sababu yao. Tupo tuishi na kuacha Dunia katika nafasi nzuri zaidi tofauti na vile tulivyoikuta.
Kuishi bila kujibakiza ni maisha yatakayo moyo, ni maisha ya kujitoa sadaka, ni maisha ya kujisahau wakati mwingine ili uwe daraja kwa watu wengine. Kuacha alama njema ni gharama na hugharimu hata watu maisha yao. Kujitoa usiku na mchana kuishi kikamilifu ni kujikana kuwa hutafanya kila kitu katika maisha haya bali utawekeza nguvu maeneo muhimu katika maisha ili kuandaa njia njema kwa wengine. Yataka moyo, yataka moyo thabiti, yataka ustahimilivu kujitoa na kuishi kitoshelevu.
Alama njema unayoweza kuitengeneza na kutoa zawadi yenye manukato kwa dunia ni kuwa tayari kuishi uhalisia wako, u tayari wa kujimimina kwa vipaji ulivyojaliwa, mawazo, ujuzi, uzoefu, maarifa kuisaidia jamii kujitambua, kukua na kuendelea. Hii alama huyapa maisha ya mtu kuwa marefu hata baada ya kufa kwake. Maisha ya mashujaa ambao tunawasoma na kuwakumbuka ni kwa sababu ya alama za matendo yao yasofutika mioyoni mwetu. Mimi na wewe tuna nafasi sasa tukiwa hai kuendelea kufanya mambo bila kujibakiza tukijitoa kadri tuwezavyo kuifanya Dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.
KOCHA MWL. JAPHET MASATU , DAR ES SALAAM
WhatsApp + 255 716924136 / + 255 755 400128 / + 255 688 361 539
Friday, March 26, 2021
NYUMA YA PAZIA , KUNA MAUMIVU MAKALI , SI VILE ULIVYOKUWA UKIFIKIRIA.
Jambo lolote lile unaloweza kuliona kwa wengine unaweza kufichwa uhalisia wake na ukachukulia huenda ni jepesi au watu hao wanaofanya hivyo hawapitii changamoto zozote zile. Ni rahisi sana watu kutamani kuishi kama wengine ila wanapoanza kuishi kama hao watu wanakuja kugundua ukweli kuwa si vile walivyofikiria itakuwa. Unachokiona na unachokutana nacho huenda visiwe vinafanana kabisa na hili limefanya watu wengi wagundue kuwa maisha si vile wanavyoona kwa juu juu bali yana siri kubwa mno.
Unaweza kuona ni rahisi kusikia mtu ambaye kila siku anaamka asubuhi na mapema na kufanya mazoezi bila kuacha ukadhania kujenga nidhamu ya namna hiyo ni vyepesi. Ikiwa huna utamaduni huo na ukajisemea siku basi ngoja nianze kufanya mazoezi kila asubuhi bila kuacha utakuta umeanza siku ya kwanza vizuri, ya pili vizuri, ya tatu unaanza kukutana na vikwazo, ya nne unasema ngoja leo nipumzike, ya tano unapendezwa na mapumziko, siku zinapita hufanyi tena mazoezi. Unapotafakari haya unakuja kugundua kuwa wale wanaofanya mazoezi ya mwili au akili kila siku kwa kufanya matendo kama kukimbia au kusoma vitabu kila siku si rahisi na si wa kubezwa hata kidogo.
Unapopitia mwenyewe kufanya kitu ndivyo unavyoweza kuwa na uzoefu na kuweza kukielezea vizuri katika ugumu wake tofauti na unaposema mambo kwa nadharia au kuyasikia sikia tu. Jamii zetu nyingi hupenda kuona mambo rahisi huku hakuna ambaye ana uzoefu nayo bali ni kwa kusikia au kujifanya kujua ila inapotokea mtu inabidi ahusike kuyapitia ndipo anapokuja kugundua si rahisi kama alivyodhani au kuambiwa na watu wengine.
Wengine wanaweza kusema hiyo biashara unayofanya mbona ni rahisi au kama ni jambo la kuandika au kusoma kitabu mtu anaweza kuona anayefanya ni rahisi. Ila inapotokea mtu huyo aingie kuandika, kusoma au kufanya biashara ndipo anapokuja kugundua namna ilivyo ngumu kufanya hivyo vitu. Kuna msemo unaosema kama ingekuwa mambo rahisi basi watu wengi wangekuwa wameyapata isitoshe ni asili ya binadamu kuishi vizuri na kwa furaha. Ndivyo ambavyo hata njia ya kufanikiwa inavyotamaniwa na wengi ila si rahisi kama vile watu wanavyoingia katika mitego ya kuambiwa toa fedha sasa na utapata mara mbili yake au toa fedha na utajirike haraka. Wengi wameingia katika matatizo kwa kutamani kupita njia rahisi au wakijaribu kurahisisha mambo huku kiuhalisia mambo huwa si rahisi kama yanavyodhaniwa na wengi.
Usiwe mwepesi kuvunja moyo watu au kuchukulia vitu kirahisi hasa kama hujawahi kuvipitia au huvijui kiuzoefu wake. Inawezekana ukijaribu hutaweza kuvifanya kama wengine wanavyofanya.
KOCHA MWL. JAPHET MASATU.
WhatsApp + 255 716924136 / + 255 755 400128
EMAIL : japhetmasatu@gmail.com
Monday, March 22, 2021
JE , NI ALAMA GANI UTAKAYOIACHA UKISHAMALIZA SAFARI YA KUISHI KWAKO HAPA DUNIANI ?
Kifo ni kufunga kwa ukurasa wa maisha ya mtu ya kimwili. Baada ya kufa kwa mtu kinachoanza kuelezwa ni juu ya matendo aloyaacha mtu nyuma yake au alama alizoacha katika namna mbili. Moja ni alama katika mioyo ya watu, hapa tunaona namna watu walikufa zamani ila bado unazo kumbukumbu zao namna walivyogusa maisha yako kiasi huwezi kuwasahau. Pili ni alama za vitu kama majengo, viwanda, vitabu, picha, nyimbo na kadhalika. Tatu ni watoto walowaacha nyuma baada ya kufa kwa mtu. Hizi ni alama kubwa ambazo hubakia na mtu kuendelea kukumbukwa.
Hatujui lini siku tutakayokufa na ikiwa wanaojua siku ya kufa kwao basi ni wale wenye bahati kupata kugundua kuwa hizi ni dakika zangu za mwisho wa maisha basi huandaa wosia, kuandaa msimamo au wengine huandika hata vitabu. Ila kwa watu wengi kifo hutokea kama ajali wakati mwingine. Mtu hajui hili wala lile maisha yanapotea kupitia ajali, kuvamiwa, ghafla, magonjwa na kadhalika. Hili ndilo lifanyalo kuwa kifo kionekane ni FUMBO. Hatujui ni kwa namna gani tumebakiza siku zetu za kuishi.
Kifo ni njia yetu sote ambayo hakuna aliye hai ataiepuka kuwa ataondoka katika Dunia bila kufa. Kifo kipo na kila mmoja kwa nafasi yake na namna yake atamaliza siku alizopewa za kuishi. Nini kitakachobakia baada ya mtu kufa ndilo jambo la muhimu pia tunapoendelea kuishi na tukiwa tungali bado hatujafikia mwisho wa maisha yetu.
Wengi hatuna utaratibu wa kutafakari ukomo wa maisha yetu maana ni habari zenye kutisha mno, tunaziogopa na huwa hatudhanii kuwa tutakufa. Ukweli ni kuwa hata tusipowazia bado njia ya kifo hatuwezi kuiepuka maana ni njia halisi katika maisha yetu ya kila siku baada ya kuisha maisha haya.Tukifa ndipo huwa tunaanza kuishi katika mioyo ya watu, watu huanza kutukumbuka baada ya kufa kwetu. Ni wakati ambao watu huanza kukufuatilia juu ya kazi ulizowahi kufanya, urithi uloacha au alama yoyote uloiacha kipindi uko hai. Maisha ya mtu huelezwa sana pindi anapokufa kuliko anapokuwa hai. Wengi watafahamu mengi kukuhusu wewe pale watakaposikia umefariki. Alama unazoacha sasa iwe ni kitabu, biashara, namna ya utu wako ulivyogusa watu ni nafasi ya maandalizi itakayosimulia sana ukishamaliza safari ya kuishi kwako hapa duniani.
Je ni alama gani ukatayoiacha katika nafasi ambayo bado ipo sasa ukiwa hai ?. Swali zito ila litakupa maana kubwa ya kuanza kuishi kitoshelevu.
TUMEUMBIWA MASIKIO MAWILI NA MDOMO MMOJA. KUWA MSIKILIZAJI SANA KULIKO KUONGEA.
Tumeumbiwa masikio mawili na mdomo mmoja ambapo masikio mawili tusikilize zaidi na mdomo mmoja kuongea kidogo. Wale wanaosikiliza zaidi hupata mengi kupitia wale wanaongea. Kuongea sana ni kujipa nafasi ya kurudiwa na kile unachoongea na kujikuta unachoongea kisiwe halisia na kile unachokifanya. Tafiti fulani zilifanyika na kuonesha kuwa kadri unavyoongea juu ya mipango yako au kitu chochote ndivyo ilivyo nafasi ndogo ya kukifanya au kukitenda. Hili ndo limezalisha na kuwa ukiona mtu ni muongeaji sana basi ni mtendaji kidogo. Watendaji wengi si waongeaji ukilichunguza hili utaona.
Akiba ya maneno ni ya muhimu mno katika zama tuishizo sasa kuliko zile zilizowahi kuwepo. Tunaishi katika mifumo ya kumbukumbu kupitia mitandao ya simu kiasi kwamba yale ambayo tunayaandika au kuyaongea watu huyahifadhi na baadaye huyatumia kama fimbo au hukumu unapokuwa umeyasaliti maneno yako. Watu huwa hawafikirii namna neno huishi zaidi ndani ya wale wanaosikiliza.
Kuongea ni kujiandalia mtego hasa hasa pale unapotaka kuchangia mazungumzo fulani ya mambo. Kuongea sana kunapelekea mtu aanze kuongea vitu visivyo kweli ili wale wanaomsikiliza waendelee kumsikiliza. Watu wengi wamefungwa kwa maneno yao ambayo walishindwa kujizuia kuongea. Kusikiliza kunaepusha migorogoro mingi sana katika maisha ya watu na ndiko kunakozalisha watu kuwa na hekima.
Inaleta maswali mengi kuwa tupo katika zama ambazo kila mtu anasukumwa kuongea, kutoa maoni na tunakosa watu ambao huwa kimya na wasikivu kipindi ambacho kila mmoja anasukumwa kuongea ongea. Utaona namna katika majukwaa mbalimbali ya mtandaoni watu wasivyo na subira katika kuyazungumza mambo au kuyaongea. Kila mmoja anaona atapitwa kuongea juu ya jambo fulani au tukio fulani. Katika kufanya hili watu wengi wamepoteza utulivu wa maisha na kujikuta wanahangaishwa na kile walichokiongea kinapoenda tofauti na namna wanavyoishi sasa.
Huwa ninafaidika sana katika mazungumzo ninapokuwa msikilizaji. Ninapokuwa nasikiliza iwe ni mazungumzo ya watu, mijadala au watu watoa maoni napata mengi mno nilokuwa sijajui kupitia kusikiliza watu wanaozungumza au kuongea. Kusikiliza kunatengeneza yule anayeongea aone anathaminiwa tofauti na mtu mmoja anaongea na mwingine analeta mazungumzo kati kati.
Kama wanafalsafa tujiepushe na kuongea kama watu wengine ambao wanakosa udhibiti wa kujizuia kuongea kwa kila wanachokiona. Pili ni kuongeza nafasi ya kuwa wasikilizaji maana hata katika kusikiliza ndipo kunakozaliwa ufahamu wa mambo. Mtu anayesikiliza vizuri huweza hata kufafanua alichokisikia. Si lazima uongee kwa kila kinachotokea hususani zama hizi tuishizo za usumbufu, kelele na mihemko kila kona.
NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU , DAR ES SALAAM , TANZANIA.