Maisha ya watu yamebadilika katika wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa
wa Corona. Biashara yako pia inapaswa kubadilika ili kuweza kuwahudumia
vizuri wateja wako.
Kama watu wanatumia muda mwingi nyumbani kuliko kutoka, usiendelee
kusubiri wateja waje kwenye biashara yako, badala yake wafuate huko
majumbani.
Badili mfumo wa biashara yako kutoka kusubiri wateja waje eneo la
biashara na kufanya wateja waweze kuagiza wakiwa nyumbani na kupelekewa
au kutumiwa kile walichoagiza.
Hatujui lini hali hii itaisha kwa hakika, hivyo usijiambie unasubiri
mambo yatulie, badala yake chukua hatua sahihi ili uendelee kuwahudumia
wateja wako.
Mfano; biashara ambazo zimekuwa zinategemea wateja
waje kwenye biashara, ni wakati sahihi sasa kuweka mfumo wa wateja
kuweza kuagiza wakiwa nyumbani na kisha kupelekewa au kutumiwa
walichoagiza.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE. JIFUNZE ---ELIMIKA --CHUKUA HATUA---FANIKIWA
Saturday, April 4, 2020
MFANYABIASHARA / MJASIRIAMALI : WAPE WATEJA WAKO MATUMAINI SAHIHI.
Wakati wa mlipuko kama huu, hakuna anayejua nini kitatokea kesho, na
kadiri mambo yanavyozidi kuwa mabaya, ndivyo watu wanaendelea kutabiri
kwamba mambo yatakuwa mabaya zaidi.
Watu wanatishana na kupeana wasiwasi mkubwa. Wapo wanaosema huu ndiyo mwisho wa dunia. Kila mtu ana maoni yake. Lakini tunajua kitu kimoja kuhusu maoni, siyo ukweli.
Hakuna aliyeweza kutabiri ujio au madhara ya mlipuko huu, na hakuna anayeweza kutabiri kwa uhakika mambo yataendaje. Tunachojua ni kwamba tutavuka hili, kama ambavyo jamii ya binadamu imevuka mengi siku za nyuma.
Hivyo wewe kuwa chanzo cha matumaini sahihi kwa wateja wako. Katika hali ya wasiwasi kama hii, watu wanapenda kuwasikiliza wale wanaoleta habari njema, lakini siyo habari njema hewa. Bali habari njema sahihi.
Usiwe mtu wa kutoa habari mbaya kwa wateja wako, utawatisha na kuwafanya waahirishe kununua. Badala yake kuwa mtu wa kutoa habari njema, mtu wa kuwapa wateja wako moyo na hapo watajisikia vizuri na kununua. Ukiweza kuwaonesha jinsi kile unachouza kinawasaidia kupunguza makali ya mlipuko, wateja wanakujali zaidi.
Mfano; biashara za ushauri na mafunzo zinapaswa kuwa chanzo cha matumaini kwa wateja wake. Kwa kuwaonesha kwamba hili linaloendelea siyo mwisho wa dunia na mambo yatakwenda vizuri baada ya hili.

MFANYA BIASHARA / MJASIRIAMALI : JUA THAMANI NA WAELEZE WATEJA WAKO
BIASHARA pekee zitakazovuka kipindi hiki cha Mlipuko wa ugonjwa wa CORONA salama ni
zile ambazo zinatoa thamani kubwa kwa wateja wake na jamii kwa ujumla.
Zile biashara ambazo watu hawawezi kuishi bila ya kuwa na kile
kinachouzwa.
Hivyo huu ni wakati wa wewe kukaa chini na kujiuliza ni thamani gani unayoitoa kwa wateja wako. Huenda umezoea kuuza na kupokea fedha na umesahau thamani ipi unatoa.
Jiulize ni tatizo au hitaji gani la wateja ambalo biashara yako inatoa. Kisha waeleze wateja thamani hiyo vizuri, waoneshe jinsi ambavyo wanaihitaji thamani hii wakati huu wa mlipuko.
Mfano; biashara za huduma za kifedha zinatumia nafasi hii kuonesha jinsi ilivyo salama kutuma na kupokea fedha kwa mtandao na siyo fedha taslimu. Hii ni thamani kubwa ambayo mteja au mfanyabiashara hakuwa anaiona, lakini kwa sasa iko wazi.

Subscribe to:
Comments (Atom)