BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Monday, July 15, 2019
USIOGOPE KUWAAMBIA WATU WAKULIPE.
Watu
wengi wanaofanya biashara za huduma, hasa za ushauri au mafunzo, huwa
wanaanza kutoa huduma hizo bure ili watu wawajue. Ni vigumu sana kuanza
kwa kuwachaji watu fedha ndiyo uwashauri au kuwafundisha mambo
mbalimbali.
Hivyo
mtu anapoanza kutoa huduma zake bure, watu wengi wanamfuatilia na
kujifunza au kunufaika na huduma hizo kama ni za ushauri au nyinginezo.
Sasa
mtu anaweka juhudi kubwa kutengeneza wafuasi wengi, akiwa na lengo
kwamba watu wanaomfuatilia wanapokuwa wengi na wengi zaidi kuhitaji
huduma zake, basi anaweza kuwatoza ada na kutengeneza kipato.
Lakini
unapofika wakati wa kuwaambia watu wakulipe ili kuendelea kupata huduma
ambazo umekuwa unawapa bure, wengi huwa wanaogopa. Wengi wanajenga hofu
hii pale wanapoanza kuwaambia watu kuhusu malipo na watu hao
wakawaambia hawakutegemea kulipia ushauri au mafunzo yanayotolewa.
Watu
wengi ambao wamekuwa wananufaika na mafunzo hayo ya bure watapinga sana
pale mtu aliyekua anatoa mafunzo hayo bure anapoanza kutoza ada. Na
hili limekuwa linawafanya wengi kushindwa kuendelea na huduma zao na
hivyo huduma hizo zinakufa.
Nikuambie
leo rafiki yangu, kama unaendesha huduma yoyote ile, iwe ni ushauri,
uandishi, ukocha, au huduma ya kiimani, lazima ujue kwamba ili huduma
hiyo iendelee unahitaji njia ya kukuingizia kipato. Hivyo basi usiogope
kuwatoza watu fedha pale wanapohitaji huduma zaidi kutoka kwako.
Wednesday, July 10, 2019
FURSA 28 KATIKA SEKTA YA MICHEZO NA BURUDANI -------------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "
SEKTA YA MICHEZO
ina fursa nyingi sana ambazo zinaweza kumnufuaisha MJASIRIAMALI
mwenye hari ya kuwekeza kwenye sekta hii. Gundua fursa
unazoweza kufanya kwenye sekta ya michezo.
Je, wewe ni mpenzi wa BURUDANI ? Je, umewahi kujiuliza watu kwenye sekta hii wanapataje pesa ? Basi hilo lisikupe maswali mengi sana kwa sababu mimi MJASIRIAMALI nipo wewe katika kila jambo.Fuatilia " Darasa la Semina kujua fursa unazoweza kuwekeza kwenye sekta hii ya burudani.
MUHIMU : Ili kuendelea Kujifunza Zaidi na Kugundua FURSA mbalimbali zilizojificha katika
'SEKTA YA MICHEZO & BURUDANI " , jiunge na "FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na " DARASA LA SEMINA " kwa kulipa ADA YA UANACHAMA ( Tshs 10000 kwa Mwezi ) ili uweze Kuzigundua na kujifunza " FURSA ZINAZOKUZUNGUKA " na Kuzifanyia Kazi na KUFANIKIWA.
Ndimi Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam ,Tanzania , Afrika Mashariki ,
Kama hujajiunga na " FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na "DARASA LA SEMINA " tuwasiliane Kwa Maelekezo Zaidi
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
ULIZA MASWALI , TOA MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO kwa Email hii:- EMAIL : fursaafrikamashariki@gmail.com

Sunday, July 7, 2019
FURSA 20 ZA BIASHARA ZA KUFANYA UKIWA NYUMBANI -------------- " Fursa Afrika Mashariki Blog "
Kuna
fursa nyingi za kufanya ukiwa nyumbani kwako. Uzuri wa fursa
hizi ni kwamba unakuwa bosi wewe mwenyewe na unapanga MUDA
wa kufanya kazi na faida unayotaka mwenyewe.
MUHIMU : Ili kuendelea Kujifunza Zaidi na Kugundua FURSA mbalimbali zilizojificha ukiwa nyumbani , jiunge na "FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na " DARASA LA SEMINA " kwa kulipa ADA YA UANACHAMA ( Tshs 10000 kwa Mwezi ) ili uweze Kuzigundua na kujifunza " FURSA ZINAZOKUZUNGUKA " na Kuzifanyia Kazi na KUFANIKIWA.
Ndimi Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam ,Tanzania , Afrika Mashariki ,
Kama hujajiunga na " FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na "DARASA LA SEMINA " tuwasiliane Kwa Maelekezo Zaidi
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
ULIZA MASWALI , TOA MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO, MASULUHISHO kwa Email hii :- EMAIL : fursaafrikamashariki@gmail.com

Saturday, July 6, 2019
FURSA 17 KATIKA SEKTA YA AFYA , MADAWA NA MATIBABU------------" Fursa Afrika Mashariki Blog "
AFYA , MADAWA na MATIBABU
ni eneo nyeti sana ambalo sio la kufanyia mzaha.SEKTA hii
ni muhimu sana kwa binadamu ndio maana hata katika kipindi
kigumu sana cha kiuchumi watu wanaweza kupunguza manunuzi ya
vitu vya starehe lakini hawawezi kubana matumizi kwenye sekta
hii. Ukweli ni kwamba mtu akikosa huduma sahihi kipindi cha
ugonjwa wake anaweza kupoteza maisha. Je, una ELIMU juu ya
maswala ya matibabu ? Ungependa kuwekeza kwenye sekta hii HATA
KAMA HAUNA ELIMU YA AFYA ? Mdau wangu , Rafiki Yangu Soma Na
Ujifunze fursa mbalimabali zinazopatikana kwenye sekta hii kwa
KUJIUNGA UANACHAMA.
MUHIMU : Ili kuendelea Kujifunza Zaidi na Kugundua FURSA mbalimbali zilizojificha katika SEKTA hii ya " AFYA , MADAWA NA MATIBABU " , jiunge na "FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na " DARASA LA SEMINA " kwa kulipa ADA YA UANACHAMA ( Tshs 10000 kwa Mwezi ) ili uweze Kuzigundua na kujifunza " FURSA ZINAZOKUZUNGUKA " na Kuzifanyia Kazi na KUFANIKIWA.
Ndimi Rafiki na Kocha Wako Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam ,Tanzania , Afrika Mashariki ,
Kama hujajiunga na " FURSA AFRIKA MASHARIKI BLOG " na "DARASA LA SEMINA " tuwasiliane Kwa Maelekezo Zaidi
WhatsApp / Call / Message + 255 716 924136 / + 255 755 400128 / + 255 688361539
ULIZA MASWALI , TOA MAONI , USHAURI , MAPENDEKEZO , CHANGAMOTO ,MASULUHISHO kwa Email hii :-- EMAIL : fursaafrikamashariki@gmail.com

Friday, July 5, 2019
TOKA KWENYE UMASKINI NA UTEGEMEZI KWA KUCHUKUA HATUA HIZI KUELEKEA UTAJIRI
HATUA YA KWANZA; TAMBUA ASILIMIA 95 HAWATAFANIKIWA.
Hatua ya kwanza ya kutoka kwenye umasikini na kuelekea kwenye utajiri ni kutambua kwamba asilimia95 ya watu hawatafanikiwa. Kwa maneno mengine ni kwamba utajiri siyo kwa kila mtu. Hata watu wote wangepewa fedha sawa au fursa sawa, bado mgawanyo utabaki vile vile, asilimia 5 watafanikiwa sana na asilimia 95 watakuwa na maisha magumu.
Na hili liko wazi ukiangalia kwenye jamii zetu. Mambo kama haya yapo wazi kabisa;
Ukianzia kwenye upande wa afya ya mwili, watu wengi wanakabiliwa na magonjwa sugu kama presha na kisukari, wengi hawapo kwenye afya nzuri inayowawezesha kujituma zaidi kwenye kazi zao.
Ukienda upande wa afya ya akili na roho, wengi wana msongo wa mawazo na sonona, hawawezi kuyakabili maisha yao bila ya kutumia dawa au vilevi vya kuwasahaulisha matatizo yao kwa muda.
Upande wa mahusiano nao una changamoto kubwa kwa wengi, ndoa nyingi zinavunjika na familia kusambaratika.
Kwenye fedha ndiyo mambo ni magumu zaidi. Wengi wapo kwenye madeni, kipato hakitoshelezi matumizi na hivyo wanaendelea kukopa, kitu ambacho kinawaumiza zaidi na kuwaweka kwenye umasikini mkubwa.
Ni muhimu sana utambue hali halisi na jinsi ambavyo wengi wanakwamba kwenye hali hiyo, ili wewe ukatae hali hiyo na kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
HATUA YA PILI; TAMBUA CHANZO CHA WENGI KUBAKI KWENYE UMASIKINI.
Baada ya kukubali kwamba wengi hawatafanikiwa, hata kama kila kitu kitatolewa sawa kwa wote, hatua ya pili ni kutambua chanzo cha wengi kubaki kwenye umasikini.
Siyo bahati nzuri kwamba asilimia 5 pekee ndiyo wanaofanikiwa sana na siyo bahati mbaya kwamba asilimia 95 wanabaki kwenye umasikini mkubwa.
Kila kinachotokea kwenye maisha ya mtu kinasababishwa, na ili kubadili matokeo, unapaswa kubadili kwanza kisababishi.
Ili kuondoka kwenye kundi kubwa la wasiofanikiwa na kwenda kwenye kundi dogo la wanaofanikiwa, jua sababu hizi zinazowaweka watu kwenye umasikini na ondokana nazo mara moja.
Rafiki, epuka sababu hizi saba ambazo zimewaweka wengi kwenye umasikini mkubwa. Huwezi kuondoka kwenye umasikini huo kama utaendelea kukumbatia sababu hizo.
HATUA YA TATU; CHORA MSTARI.
Baada ya kuzijua sababu ambazo zimekuweka kwenye umasikini kwa muda mrefu, sasa kuna hatua ya tatu ya kuchukua, ambayo ni kuchora mstari.
Kuchora mstari maana yake ni kufanya maamuzi kwamba kuanzia sasa mambo yako yote yanabadilika. Unaachana na mambo ya nyuma na kuanza maisha mapya ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Maamuzi hayo unayafanya sasa na hatua unaanza kuzichukua sasa. Siyo baadaye, siyo kesho, siyo wiki ijayo, siyo mwezi ujao na wala siyo mwaka ujao. Ni leo, ni sasa. Kama hutachora mstari sasa hivi na kuanza kuishi maisha mapya, utaendelea kujichelewesha kufanikiwa.
Kataa kuwa wa kawaida, kataa kubaki kwenye umasikini na maisha magumu na chagua kufanikiwa na kufikia utajiri. Chagua kuziishi tabia ambazo zitayafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Usikubali kuendesha maisha yako kwa ukawaida, halafu unapofika ukingoni mwa maisha unagundua hukuishi maisha yako. Chagua leo kuyaishi maisha yako, chagua kuwa bora zaidi ya pale ulipo sasa. Yote yanawezekana na yapo ndani ya uwezo wako.

- Kuangalia nyuma badala ya mbele. Wale wanaoshindwa wanatumia muda wao mwingi kuangalia mambo ya nyuma kuliko pale walipo sasa na kule anakokwenda. Wamekuwa wanatumia matukio ya nyuma kama sababu ya wao kushindwa kupiga hatua zaidi. Wataeleza jinsi ambavyo walidhulumiwa, kuteswa au kunyanyaswa huko nyuma. Wataeleza jinsi ambavyo wamejaribu mambo mengi lakini wameshindwa. Kwa kuangalia zaidi nyuma kuliko mbele kunawafanya kuangalia kushindwa zaidi kuliko kufanikiwa.
- Kukosa kusudi la maisha. Watu wengi wanaendesha maisha yao bila ya kusudi, hawajui nini wanachotaka kwenye maisha yao na wala hawajisukumi kufanya chochote kikubwa. Kwa kukosa kusudi wanajikuta wanakimbizana na kila kitu, mwisho wa siku wanachoka na hakuna hatua wanayokuwa wamepiga.
- Kutenga madhara ya matukio. Watu wengi wanabaki kwenye umasikini kwa sababu hawana nidhamu. Mtu anapanga kufanya kitu fulani, lakini wakati wa kufanya unapofika hafanyi na anajipa sababu. Anachoamini ni kwamba asipofanya kitu mara moja hakuna madhara makubwa, atafanya siku nyingine. Asichojua ni kwamba kila tukio lina madhara kwenye maisha yake. Mfano mtu anapoacha kufanya kile alichopanga, hilo lina madhara makubwa kwake, anajichukulia kama mtu asiye makini na ni rahisi kurudia hilo kwenye maeneo mengine ya maisha yake.
- Kukosa uwajibikaji. Watu wote waliofanikiwa wanajua uwajibikaji ni muhimu sana kwenye mafanikio yao. Ndiyo maana watu hao wana mamenta, makocha na washauri mbalimbali, hawa wanahakikisha watu hao wanatekeleza kile walichopanga. Lakini wasiofanikiwa hawapendi kabisa uwajibikaji, wao wanataka kuendesha maisha kama wanavyojisikia wenyewe. Bila ya uwajibikaji, hakuna hatua mtu anaweza kupiga.
- Kuzungukwa na watu wa kawaida. Utafiti unaonesha kwamba maisha yako ni wastani wa watu watano wanaokuzunguka au unaotumia nao muda wako mwingi. Kinachowafanya watu wengi kubaki kwenye umasikini ni kuzungukwa na watu masikini. Unapozungukwa na watu masikini, fikra zako na hata matendo yako yanakuwa kama yao na hilo linapelekea ubaki kwenye umasikini.
- Kutokujiendeleza binafsi. Watu wanaoshindwa huwa hawajiendelezi wao binafsi. Wakishahitimu masomo ndiyo basi, hawajisumbui tena kuendelea kujifunza hasa kusoma vitabu. Na hata wakisoma vitabu basi ni vya hadithi, na siyo vya kujifunza. Wale wanaofanikiwa wanaweka uzito mkubwa sana kwenye kujiendeleza wao binafsi. Wananunua na kusoma vitabu vinavyowafanya kuwa bora zaidi. Pia wanahudhuria mafunzo na semina mbalimbali zinazowafanya kuwa bora zaidi.
- Kukosa uharaka. Watu wengi hawapigi hatua kwenye maisha yao kwa sababu hawana ile hali ya uharaka wa kuchukua hatua kwenye jambo lolote. Ni watu wa kuahirisha mambo na kusubiri mpaka dakika za mwisho ndiyo wachukue hatua. Kwa kukosa hali hii ya uharaka wengi wamekuwa wanajichelewesha wao wenyewe kufanikiwa.
Rafiki, epuka sababu hizi saba ambazo zimewaweka wengi kwenye umasikini mkubwa. Huwezi kuondoka kwenye umasikini huo kama utaendelea kukumbatia sababu hizo.
HATUA YA TATU; CHORA MSTARI.
Baada ya kuzijua sababu ambazo zimekuweka kwenye umasikini kwa muda mrefu, sasa kuna hatua ya tatu ya kuchukua, ambayo ni kuchora mstari.
Kuchora mstari maana yake ni kufanya maamuzi kwamba kuanzia sasa mambo yako yote yanabadilika. Unaachana na mambo ya nyuma na kuanza maisha mapya ya kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Maamuzi hayo unayafanya sasa na hatua unaanza kuzichukua sasa. Siyo baadaye, siyo kesho, siyo wiki ijayo, siyo mwezi ujao na wala siyo mwaka ujao. Ni leo, ni sasa. Kama hutachora mstari sasa hivi na kuanza kuishi maisha mapya, utaendelea kujichelewesha kufanikiwa.
Kataa kuwa wa kawaida, kataa kubaki kwenye umasikini na maisha magumu na chagua kufanikiwa na kufikia utajiri. Chagua kuziishi tabia ambazo zitayafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Usikubali kuendesha maisha yako kwa ukawaida, halafu unapofika ukingoni mwa maisha unagundua hukuishi maisha yako. Chagua leo kuyaishi maisha yako, chagua kuwa bora zaidi ya pale ulipo sasa. Yote yanawezekana na yapo ndani ya uwezo wako.
Subscribe to:
Posts (Atom)