JIULIZE Kipi kipaumbele kikuu cha biashara Yangu ?
Hakuna
kitu kinachowapoteza wafanyabiashara wengi kama fursa mpya na nzuri
zinazojitokeza kila wakati. Iwapo mfanyabiashara atakuwa mtu wa
kukimbizana na kila fursa inayojitokeza, hawezi kufanikiwa kabisa kwenye
biashara.
Hii
ni kwa sababu fursa mpya huwa ni nyingi na haziishi, na ili upate
mafanikio kwenye jambo lolote, unahitaji kuweka muda na kazi.
Jukumu
lako kama mfanyabiashara ni kuweka kipaumbele kikuu cha biashara yako,
yaani ni aina gani ya biashara utafanya na kisha kuachana na kelele
nyingine zozote.
Ukishachagua
biashara utakayofanya, funga masikio kuhusu biashara nyingine
zisizoendana na biashara hiyo. Hata uambiwe kuna biashara mpya na yenye
faida kubwa, usidanganyike kuondoka wenye vipaumbele vyako na kwenda
kwenye biashara hiyo mpya, utajipoteza mwenyewe.
Ukichagua
nini unataka na kuweka nguvu zako zote kwenye kitu hicho, lazima
utakifikia. Lakini ukigawa nguvu zako kwenye kila kitu kipya
kinachojitokeza, unajizuia mwenyewe kufanikiwa.
Kama
biashara uliyoanzisha imekuwa na unaona fursa ya kuingia kwenye
biashara nyingine, fanya hivyo kwa mipango na maono yako na siyo kwa
kusukumwa na tamaa zako na za wengine.