Kila mtu ana masaa 24 kwa siku ila kuna wanaofanikiwa
sana na kuna ambao wanaishia kulalamika kwamba hawana muda. Kama una
jambo ambalo ni muhimu kwako lazima utapata muda wa kulifanya. Tumia
njia hizi hapa chini kuokoa muda unaopoteza kila siku na uanze kuwekeza
kwenye maisha yako.
Hebu fikiria unaambiwa ujisomee kila siku, ufanye mazoezi, ufanye meditation,
utenge muda wa kuweka mipango yako kwa siku, upate muda wa kupitia
mipango yako, upate muda wa kupumzika na pia upate muda kwa ajili ya
wale unaowapenda na wanaokupenda. Kwa mambo hayo tu tayari siku imeisha
na bado hujaweka muda wa kufanya kazi na muda wa kulala.
Kwa muda mfupi tulio nao ni vigumu sana kufanya
mambo yote hayo kila siku. Unaweza kujiaminisha hivyo ila ni uongo
mkubwa sana ambao umekuwa unajidanganya kila siku.
Ili uache visingizio visivyo na maana leo ninakupa
njia ya kupata masaa mawili ya ziada kila siku ambapo unaweza kufanya
mambo hayo ambayo yatabadili maisha yako na kuwa bora zaidi.
Kwanza hebu tuangalie muda wetu kwa siku. Kila
binadamu ana masaa 24 kwenye siku moja. Wapo wengi ambao wameyagawa
masaa yao kwa masaa nane ya kulala, nane ya kazi na nane ya kupumzika.
Kwa vyovyote ulivyoyagawa wewe haijalishi, ila unaweza kuokoa masaa
mawili ili kufanya mambo yako.
Ili kupata masaa mawili ya ziada kila siku fanya mambo yafuatayo;
1. Amka nusu saa kabla ya muda uliozoea kuamka kila
siku. Utumie muda huo kufanya jambo lenye manufaa kwenye maisha yako
kama kujisomea au kuweka MALENGO NA MIPANGO. Na ili uweze kuamka nusu saa kabla ni vyema ulale mapema na ulale usingizi mzuri.
2. Punguza nusu ya muda unaotumia kusikiliza redio,
kuangalia tv na kuangalia filamu. Asilimia 80 ya vipindi unavyofuatilia
kwenye tv au redio havina msaada wowote kwenye malengo yako ya maisha.
Asilimia kubwa ya taarifa zinazokushtua kila siku sio za kweli au
zimeongezwa chumvi mno. Hivyo punguza muda huu unaotumia kwenye vyombo
vya habari na uutumie kubadili maisha yako.
3. Punguza muda unaotumia kwenye
mitandao ya kijamii hasa facebook na twitter. Mitandao hii ina ulevi
fulani, unaweza kusema unaingia kuchungulia ujue ni nini kinaendelea ila
ukajikuta saa nzima unashusha tu kuangalia zaidi. Na asilimia 90 ya
unayofuatilia kwenye mitandao hii hayana msaada kwenye maisha yako.
Tenga muda maalumu kwa siku wa kutembelea mitandao hii ili kujua nini
kinaendelea.
4. Zima simu yako au iweke kwenye hali ya kimya
kabisa(wala isitetemeshe). Hapa najua utanipinga sana na unaweza kudhani
nimechanganyikiwa. Tumehamishia fikra zetu kwenye mawasiliano hasa ya
simu. Mtu unakaa na simu ikiita kidogo tu unakimbilia kujibu bila ya
kujali ni kitu gani cha muhimu unafanya. Inaingia meseji ambayo haina
hata maana ila inakuhamisha kutoka kwenye jambo la muhimu unalofanya.
Najua una madili mengi yanayokuhitaji kupatikana kwenye simu ila kuiweka
simu yako mahali ambapo huwezi kuiona kwa masaa mawili kwa siku haiwezi
kukupotezea dili lolote. Muda ambao unafanya kazi inayokuhitaji ufikiri
sana na uwe na utulivu hakikisha simu yako haiwezi kukuondoa kwenye
kazi hiyo. Hivyo izime au iwe kimya kabisa na iwe mbali.
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Wednesday, May 1, 2019
USISUBIRI KUSTAAFU, NDIO UFANYE UJASIRIAMALI USIJE UKAFA MAPEMA.
Wengi
wameingia kwenye mtego huo, kazi wanaifanya kweli, na wanafikia umri wa
kustaafu, wanastaafu, mafao wanayapata, lakini maisha hayawi mazuri
bali yanakuwa yamejaa msongo. Na wengi, hawavuki miaka mitano, wanafariki ndani ya miaka mitano baada ya kustaafu.
Hivyo kama hutaki kufa mapema, basi usikubali kustaafu. Kila
siku ya maisha yako ifanye kuwa siku ya kazi, na kadiri mwili
unavyokuwa kwenye kazi, unakuwa imara zaidi ya mwili uliopumzika.
Hivyo chagua kufanya kazi au biashara ambayo utaendelea kuifanya hata ukiwa na miaka 80, 90 na hata 100. Chagua kufanya kazi mpaka siku unayokufa, na utakuwa na maisha marefu, na yaliyo bora zaidi.
Kama
umeajiriwa na ukifika miaka 60 au 65 ni lazima ustaafu, hakikisha
unatengeneza mazingira ya kukuwezesha kuwa na kazi ya kuendelea kufanya
hata baada ya kustaafu kwenye ajira. Na hapo siyo ukatafute tena ajira za muda, badala yake uwe umeshajenga kitu chako ambacho utakifanyia kazi kwa miaka yako yote.
Friday, April 26, 2019
JIWEKE KWENYE VIATU VYA MWINGINE HUTAKUWA NA SABABU YA KUUMIZWA NA CHOCHOTE TOKA KWA WENGINE
Njia ya kuondokana na msongo na kupata utulivu kwenye maisha yako ni kujiweka kwenye viatu vya wengine, kukaa kwenye nafasi ya mwingine ili kuweza kuelewa kwa nini mtu amefanya kile ambacho amefanya.
Chanzo kikubwa cha hasira, msongo na hata migogoro kwenye maisha yetu ni mahusiano yetu na wengine. Pale wengine wanapofanya vitu ambavyo hatukutegemea wafanye, tunapatwa na hasira na msongo. Tunaona kama wamefanya kwa makusudi au wamepanga kutuumiza kwa namna fulani.
Lakini mara nyingi sana watu wanafanya vitu kwa nia njema, hasa kwa upande wao. Ni wachache sana ambao wanafanya kitu kwa makusudi ili kumuumiza mtu mwingine. Ukitaka kuelewa kwa nini mtu amefanya kile alichofanya, jaribu kwanza kujiweka kwenye nafasi yake.
Kila mtu huwa ana sababu nzuri ya kufanya kile ambacho amefanya, iwe ni kizuri au kibaya kwako. Ukichukua nafasi ya kuelewa sababu hiyo, hasa kwa kujiweka kwenye nafasi yako, utagundua huna sababu ya kuwa na hasira au msongo. Kwa sababu huenda na wewe ungekuwa kwenye nafasi kama yake ungefanya kama alivyofanya yeye.
Tambua kwamba watu wana mitazamo tofauti, vipaumbele tofauti, uelewa tofauti na hata imani tofauti. Ukichukua nafasi ya kuelewa hayo kuhusu wengine, utaona huna sababu ya kuumizwa na chochote ambacho wengine wanafanya.
BADILI MPANGILIO WA VIPAUMBELE PALE MAMBO YANAPOKWENDA TOFAUTI.
Njia ya kuondokana na msongo na kuwa na utulivu kwenye maisha yako ni kubadili mpangilio wa vipaumbele vyako kulingana na mazingira unayojikuta upo. Kila mmoja wetu ana mpangilio wake wa vipaumbele, na tunapenda mpangilio huo uende hivyo bila ya kubadilika. Inapotokea hali inayobadili mpangilio huo tunapatwa msongo na kuona hatuna udhibiti wa maisha yetu.
Hatua bora za kuchukua hapa ni kubadili mpangilio wa vipaumbele vyako. Mfano inawezekana familia kwako ni kipaumbele cha kwanza, kazi au biashara ni kipaumbele cha pili. Sasa unajikuta kwenye kazi au biashara ambayo inataka muda wako mwingi na kukunyima muda wa kukaa na familia, ambayo ndiyo kipaumbele cha kwanza. Hali hii inaweza kukuletea msongo mkubwa na kukosa utulivu, kwa sababu vipaumbele vyako vinavurugwa. Lakini unaweza kuchukua hatua ya kubadili mpangilio wa vipaumbele vyako kulingana na hali uliyonayo. Kwa kipindi fulani kuweka kipaumbele cha kwanza kuwa kazi au biashara kabla ya familia, na baada ya kujijengea msingi mzuri ukarudi kwenye vipaumbele vyako vya awali.
Hilo pia linakwenda kwa vipaumbele vingine kwenye maisha, mfano kama umekuwa unapendelea kufanya kazi mwenyewe, lakini ukajikuta kwenye kazi inayokutaka ushirikiano na wengine, kama hutabadili kipaumbele kuwa kufanya kazi na wengine utakuwa na msongo kipindi chote cha kazi. Kadhalika kwenye mahusiano na maeneo mengine ya maisha, pale mazingira yanapobadilika au unapokutana na uhitaji tofauti, kuwa tayari kubadili vipaumbele vyako.
Unapobadili vipaumbele kulingana na mazingira au hali inapobadilika, unakuwa tayari kutumia kila hali unayokutana nayo badala ya kupambana nayo.
Tuesday, April 23, 2019
KUWA KING"ANG"ANIZI NA MVUMILIVU UTAFANIKWA SANA.
Kila
kitabu kinachohusu mafanikio kinasisitiza sana ung’ang’anizi na
uvumilivu ili kuweza kufanikiwa. Lakini siyo kila ung’ang’anizi na
uvumilivu utakufikisha kwenye mafanikio. Bali unahitaji ung’ang’anizi
sahihi, na kukubali pale ambapo umekosea ili kuboresha zaidi.
Tunapaswa
kuwa ving’ang’anizi ili kupata utajiri na mafanikio, tunapaswa kujaribu
tena na tena na tena kila tunaposhindwa. Lakini tunapaswa kukumbuka
kwamba kufanya jambo lile lile kwa njia ile ile halafu kutegemea kupata
matokeo tofauti ni maana sahihi ya ujinga.
Tunapaswa
kung’ang’ana kwa njia sahihi, tunapaswa kubadili njia tunazotumia,
ambacho hatupaswi kubadili ni lengo ambalo tumejiweka. Tunapaswa
kuendelea na mapambano mpaka pale tutakapopata tunachotaka.
Wote
tunajua jinsi ambavyo dunia ina uangalifu, haikubali kutoa kitu kwa mtu
ambaye hajaonesha kweli anakitaka na yupo tayari kulipa gharama
kukipata. Jioneshe kwamba wewe unautaka utajiri kweli, kuwa tayari
kulipa gharama na ng’ang’ana kwa njia sahihi na utapata unachotaka.
JIAMINI WEWE MWENYEWE.
Kama hujiamini wewe mwenyewe, hakuna yeyote anayeweza kukuamini na hutaweza kufanikiwa kwenye jambo lolote maishani mwako.
Unapaswa
kujiamini wewe mwenyewe, unapaswa kuamini kwamba una uwezo mkubwa ndani
yako wa kukuwezesha kupata chochote unachotaka, unapaswa kuamini hakuna
kinachoweza kukuzuia kupata kile unachotaka. Tunaambiwa imani inaweza
kuihamisha milima, na hii ndiyo imani unayopaswa kuwa nayo ili
kufanikiwa na kufikia utajiri.
Katika
safari yako ya kusaka utajiri utakutana na vikwazo vya kila aina,
utapatwa na hofu nyingi, wapo watakaokukatisha tamaa kwa kukupa mifano
ya wengi walioshindwa. Kitu pekee kinachoweza kukuvusha kwenye hali hizo
ni kujiamini wewe mwenyewe.
Pia
hakuna utakachopanga na kikaenda kama ulivyopanga, utashindwa kwenye
mambo mengi licha ya kufanya kila unachopaswa kufanya. Kujiamini ndiyo
kutakupa nguvu ya kuamka kila unapoanguka ili uweze kuendelea na safari
ya mafanikio.
Jiamini wewe mwenyewe na hakuna kitakachoweza kukuzuia kufanikiwa.
AMINI SAUTI YAKO YA NDANI.
Kila
mmoja wetu ana sauti iliyopo ndani yake, hisia fulani unazozipata
ambazo huwezi kuzielezea, ambazo zinakuashiria kama kitu ni kibaya au
kizuri, kama ni sahihi au siyo sahihi. Mara nyingi huwa tunapuuza sauti
hii na matokeo yake tunafanya makosa makubwa. Kuna wakati ndani yako
unapata msukumo wa kufanya au kutokufanya kitu, lakini ushawishi wa nje
unakufanya uende kinyume na sauti hiyo na unakuja kugundua
ungejisikiliza ungekuwa sahihi zaidi.
Jifunze
kuamini sauti yako ya ndani, hata kama inaendana na uhalisia wa nje.
Kuna kitu kwa nje kinaweza kuonekana ni sahihi, lakini sauti yako ya
ndani ikakuambia siyo sahihi, au kitu kwa nje kikaonekana siyo sahihi,
lakini sauti yako ya ndani ikakuambia ni sahihi. Jifunze kusikiliza
sauti yako ya ndani, inajua zaidi kuliko wewe na itakuongoza kwa usahihi
mara zote.
Watu
wote ambao wamefikia utajiri na mafanikio makubwa, kuna hatua ambazo
wamewahi kuzichukua, ambazo watu wa nje waliwaambia wanakosea, lakini
wao walifanya, kwa sababu sauti ya ndani iliwaambia ndiyo kitu sahihi
kufanya.
Unapojikuta
njia panda na hujui hatua ipi sahihi kuchukua, isikilize sauti yako ya
ndani, inajua njia sahihi na utaweza kufanya kilicho sahihi.
Subscribe to:
Posts (Atom)