Ili kuongeza mimea zaidi kwenye vyakula vyako, zingatia mambo yafuatayo;
- Kula mbogamboga na matunda mara nne mpaka sita kwa siku. Kwa kila mlo wa siku, kuwa na matunda na matunda.
- Punguza ulaji wa nyama, kama unaweza acha kabisa, kama huwezi kula siyo zaidi ya mara mbili kwa wiki na kula kiasi kidogo cha nyama.
- Weka matunda sehemu ambayo ni rahisi kuyaona na kuyatumia unapokuwa unaendelea na shughuli zako. Hili litakusukuma kutumia matunda zaidi.
- Kula kunde zaidi. Vyakula vya jamii ya kunde vina virutubisho vya kutosha kwa mwili wako, fanya hivi kuwa sehemu kubwa ya chakula chako.
- Kula karanga kila siku, vyakula vya karanga na jamii yake, kama korosho na lozi vina mafuta mazuri kwa mwili wako na tafiti zinaonesha vinapunguza hatari ya magonjwa ya moyo.
- Kuwa karibu na karanga na vyakula vya jamii ya karanga ili iwe rahisi kwako kutumia mara kwa mara. Unaweza kuziweka kwenye chombo ambacho inakuwa rahisi kwako kutumia.