Baada ya kutangaza biashara yako, utakuwa na watu wengi wanaojua
kuhusu biashara yako, hawa ni wateja tarajiwa. Sasa unahitaji kuwabadili
hawa na kuwa wateja halisi wa biashara yako. Kadiri unavyowageuza wengi
kuwa wateja halisi, ndivyo gharama ya kuwapata inakuwa ndogo na ndivyo
faida inakuwa kubwa kwako.
Kuongeza kiwango cha wateja wapya, fanya yafuatayo;
- Toa uhakika wa kile unachouza, mpe mteja uhakika kwamba kama
anachonunua hakitafanya kazi basi anaweza kurudisha na akapata kitu
kingine au akarudishiwa fedha zake.
- Tumia shuhuda za wateja walionunua kwako siku za nyuma na wakanufaika sana. shuhuda zina nguvu kubwa ya ushawishi.
- Kuwa na kitu cha tofauti ambacho kinapatikana kwako tu na mteja
hawezi kukipata kwa wafanyabiashara wengine, na mweleze wazi kwamba
atakipata kwako tu.
- Uza viti vya thamani kubwa, ambavyo upatikanaji wake siyo rahisi.
- Tengeneza mwonekano mzuri wa kile unachouza, ikiwa ni pamoja na unavyopakia kile unachouza. Mwonekano mzuri unaongeza mauzo.
- Weka majaribio ambapo mteja anaweza kujaribu kitu kabla hajakinunua.
Njia ambazo unapaswa kuziepuka sana kuwashawishi watu kununua ni
kupunguza bei au kutoa zawadi zenye thamani kubwa. Kwa kufanya hivi
utapunguza faida na pia utavutia wateja ambao baadaye watakuwa wasumbufu
sana kwako.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Rafiki, kwenye eneo la fedha, ukuaji unapimwa kwa ongezeko lako la
kipato. Na ongezeko siyo la mwaka, bali la mwezi. Kila mwezi, inabidi
kipato chako kiwe kinaongezeka.
Kama kipato chako kinabaki pale pale kila mwezi, kama ilivyo kwa
waajiriwa na hata wafanyabiashara wengi, siyo kwamba unabaki pale pale,
bali unarudi nyuma kwa upande wa kipato.
Kwa sababu kila siku gharama za maisha zinaongezeka, hivyo kipato kisipoongezeka, unazidi kurudi nyuma.
Njia pekee ya kuongeza kipato chako kila mwezi ni kutoa thamani zaidi
kwa wengine. Kama upo kwenye biashara hilo ni rahisi, uzia wateja wengi
zaidi kila mwezi, hata kupata mteja mmoja wa ziada kila mwezi ni hatua
nzuri. Wauzie wateja ulionao zaidi kila mwezi, na pia ongeza bidhaa na
huduma ambazo wateja wako wanahitaji pia.
Kwa walioajiriwa, pia unaweza kuongeza thamani zaidi kwenye kazi yako
au nje ya kazi yako na ukaongeza kipato chako. Kama una utaalamu
fulani, tumia utaalamu huo nje ya kazi yako kwa kutoa huduma za utaalamu
huo. Unaweza kutoa huduma za ushauri kulingana na utaalamu ulionao na
watu wakalipia msaada ambao unakuwa umewapatia.
Chochote unachofanya, hakikisha kila mwezi kipato chako kinaongezeka
zaidi. Na hivyo ni muhimu kila mwezi ukapiga hesabu za kujua kipato
chako ni kiasi gani.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
‘Be miserable. Or motivate yourself. Whatever has to be done, it’s always
your choice.’ – Wayne Dyer
kama unajisikia vibaya, hilo ni tatizo lako ninafsi. Wala usitafute
mtu wa kumlaumu, hakuna anayeharibu siku yako ila wewe mwenyewe. Hakuna
anayeharibu maisha yako ila wewe mwenyewe. Wewe ndiye unayechagua
ufikirie nini, usikilize nini, uangalie nini, uambatane na nani na
ufanye nini.
Sasa kama unachagua kufikiria vitu vinavyokufanya ujisikie vibaya,
unataka kumlaumu nani? Kama umechagua mwenyewe kusikiliza na kuangalia
habari hasi, halafu unajisikia kukata tamaa na maisha, unataka kumlaumu
nani? Kama umechagua kukaa na watu ambao hawana wanakoelekea, watu
waliokata tamaa na maisha yao, na wewe unaanza kuona maisha yako hayana
maana, unafikiri nani wa kulaumiwa?
Kama unajisikia vibaya, umekata tamaa na maisha au unakosa hamasa ya
kuchukua hatua, anza kuangalia maamuzi uliyofanya kwenye maisha yako, na
utaona jinsi yale uliyochagua wewe mwenyewe yanakuweka kwenye hali
hiyo.
Na uzuri ni kwamba wewe ndiye unayechagua, hivyo usijaribu kumlaumu
yeyote. Kama hupendi pale ulipo sasa badili kitu, wewe siyo mti kwamba
lazima uendelee kuwa hapo ulipo sasa.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Ili biashara yako ikue vizuri na uweze kupata faida, lazima ufukuze baadhi ya wateja.
Kwanza kabisa unahitaji kuwapanga wateja wako kwenye makundi A, B, C, na D.
Kundi A ni wale wateja ambao wanalipa fedha nyingi na siyo wasumbufu.
Kundi B ni wale wateja ambao wapo tayari kulipia, lakini siyo
walipaji wa fedha nyingi, ila ni wateja wenye msimamo, ambao unaweza
kwenda nao muda mrefu, na hawana usumbufu mkishakubaliana.
Kundi C ni wale wateja ambao wanataka punguzo kwenye kila kitu, na
watakusumbua sana, wanaweza kununua kwa bei ya punguzo na bado wakarudi
tena kulalamika kwamba haikuwa sawa kwao.
Kundi D ni wale wateja ambao ni matatizo kwa biashara yako, kwanza
hawalipi kwa wakati, na kwenye kila kitu wanatafuta njia ya kubishana au
kugombana. Hawa ni wateja ambao wanakuja wakiwa wamejipanga kukusumbua,
ili wanufaike zaidi wao.
Ukishawagawa wateja wako kwenye makundi hayo manne, wahudumie vizuri
wateja wa kundi A na B, na fukuza wateja wa kundi C na D, kwa sababu
hawa ni wateja mabao hawana faida, na pia wanakuzuia usiwahudumie vizuri
wateja wa kundi A na B.
Swali ni unawafukuzaje wateja hao?
Zipo njia mbili;
Ya kwanza ni kuwapa utaratibu mpya wa kufanya biashara na wewe,
kwamba yale waliyozoea hayapo tena. Bei ni moja na haipungui na malipo
ni kwanza na siyo baadaye. Kama hawawezi hilo wanaweza kwenda kwenye
biashara nyingine.
Njia ya pili ni kuongeza bei ya bidhaa au huduma unayouza, na moja kwa moja watakimbia wenyewe.
Ukishaachana na wateja hao wasumbufu, nguvu zako peleka kwa wale wateja wazuri wa biashara yako.
Pia unapotangaza biashara yako, hakikisha unatumia lugha inayowavutia
wateja wa kundi A na B, badala ya kundi C na D. Kwa mfano kama tangazo
lako linasema kuna punguzo la bei au zawadi ya bure, utajikuta unavutia C
na D wengi, maana ndiyo wanaopenda rahisi na bure.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA.
(1). KUJIDHIBITI
Eneo la kwanza kabisa unalohitaji kulifanyia kazi kila siku ili kuwa
na maisha bora ni kwenye udhibiti. Unahitaji kujidhibiti wewe mwenyewe,
la sivyo utawapa wengine nafasi ya kukudhibiti wewe. Unahitaji
kujipangia nini utafanya na kipi hutafanya na kufuata mpango huo.
Muda ulionao kila siku ni mfupi sana, ni muda ambao kama ukiweza
kujidhibiti utaweza kufanya makubwa. Lakini ukishindwa kujidhibiti,
utashangaa muda unaisha na hakuna ulichofanya. Lazima uweze kujiambia
HAPANA wewe mwenyewe, pale unapojiona unakosa udhibiti. Pia lazima uweze
kujiadhibu wewe mwenyewe pale unapokwenda kinyume na mipango
uliyojiwekea wewe mwenyewe.
Jidhibiti wewe mwenyewe na kila siku yako itakuwa siku ya ushindi, kwa sababu utafanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwako.
(2). KUWA HALISIA / ACHA MAIGIZO
Kitu kimoja ambacho dunia inakazana sana kufanya kwako ni wewe uwe
kama wengine. Kwa sababu dunia inajua ukiwa wewe, utakuwa msumbufu,
hutafaa kutawaliwa na hivyo inakazana sana uwe kama wengine, uwe ndani
ya kundi ili uweze kutawaliwa na kutumiwa vizuri na wengine.
Hivyo eneo la pili la kufanyia kazi kila siku ili kuwa na maisha bora
ni uhalisi. Unapaswa kukazana kuwa halisi kila siku, kuishi maisha yako
kwa uhalisia, kuacha kuigiza na kuacha kufanya vitu ili kuwaridhisha
wengine au uonekane na wewe unafanya.
Hutaweza kufanikiwa kama huishi maisha halisi kwako, hata kama
utapata vitu vingi kiasi gani, kama maisha unayoishi siyo halisi kwako,
kila mara utasikia sauti inakuambia wewe bado sana. Na hapa ndipo wengi
husema wamefanikiwa lakini hawana furaha.
Shida yao ni moja tu, maisha wanayoishi siyo halisi kwao, ni maisha
feki na hivyo mafanikio yoyote wanayopata yanakuwa yanaonekana na
wengine lakini siyo ndani yao binafsi.
Kuwa halisi kwako, jua uimara wako, jua madhaifu yako, jua yapi yenye
maana kwako na jua kusudi la maisha yako ni lipi. Kisha tumia kila
dakika ya siku yako kuishi maisha ambayo ni halisi kwako. Utafanikiwa
kariri unavyoishi maisha halisi kwako.
(4). JITAMBUE.
Kujitambua ni eneo muhimu sana la kufanyia kazi, na linatangulia
uhalisia. Kwa sababu bila ya kujitambua, hutaweza kuishi uhalisia wako.
Na changamoto ya kujitambua ni kwamba ni zoezi endelevu.
Watu wengi wamekuwa wakifikiri wakishajua wanataka nini kwenye maisha
yao, wakishaweka malengo makubwa basi wamemaliza. Hiyo siyo sahihi,
unachojua leo kuhusu wewe, kinaweza kuwa tofauti kabisa na
utakachotambua kesho kuhusu wewe.
Kubadili mazingira, kukutana na changamoto, kote huko kutakufunulia
kwa undani kuhusu wewe. Mara nyingi huwezi kujua una uwezo wa kufanya
makubwa kiasi gani mpaka pale unapokutana na changamoto kubwa kwenye
maisha yako.
Hivyo zoezi la kujitambua ni endelevu, kila siku, kwa kila
unachopitia, jiulize ni kipi kipya umejua kuhusu wewe. Na wakati mzuri
wa kujipima ni pale unapopitia mambo magumu. Utaweza kupima uwezo wako
wa kudhibiti hasira pale unapokasirishwa hasa. Unaweza kujua unaweza
kuvumilia ugumu kiasi gani pale unapokutana na ugumu zaidi.
Kila siku mpya ya maisha yako ni siku ya kujitambua zaidi, ishi kila
siku kwa kutaka kujitambua na maisha yako yatakuwa bora sana.
(4).KUJIENDELEZA.
Eneo la nne ambalo unapaswa kulifanyia kazi kila siku ni kujiendeleza
wewe binafsi. Kila siku lazima ukazane kuwa bora zaidi kuliko siku
iliyopita. Kila siku unapaswa kujifunza kitu kipya. Usikubali siku iishe
ukiwa kama siku ya jana ilivyoisha.
Weka kipaumbele kwenye kujifunza. Jifunze kupitia kusoma, kusikiliza,
kuangalia na hata kufanya. Soma vitabu, sikiliza mafundisho mbalimbali,
waangalie wengine kwa namna wanavyofanya na jaribu vitu vipya kwa ajili
ya kujifunza kwa kufanya.
Jinsi unavyojifunza kila siku, unazidi kuwa bora na kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Rafiki yangu mpendwa, maeneo haya manne ni muhimu sana kwako
kuyafanyia kazi kila siku. Ninaposema kila siku, namaanisha kila siku ya
maisha yako. Na usiache hata siku moja, mpaka siku unaondoka hapa
duniani.
Kama unajiambia huwezi kila siku, kama unajiambia utajisahau au
kupitiwa na maisha mengine, ninayo nafasi ya kukumbusha hili kila siku,
na kukushirikisha fursa za kujifunza na kujitambua kila siku. Karibu
kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utapata nafasi ya kuingia kwenye kundi
la wasap, na kila siku utajifunza kwenye maeneo hayo manne na mengine
mengi.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
Kwa chochote ambacho unafanya kwenye maisha yako, kuna misukumo au hamasa za aina mbili.
(2):-
Aina ya kwanza ni msukumo au hamasa inayotoka ndani yako. Hapa ni
pale unapofanya kitu kwa sababu umechagua kufanya, kwa sababu unajua ni
kitu muhimu kwako kufanya na kwa sababu unajua kuna thamani unaongeza
kwenye maisha ya wengine.
Aina ya pili ni msukumo au hamasa inayotoka nje. Hapa ni pale
unapofanya kitu ili kuonekana unafanya, au kwa sababu wengine wanafanya,
au kwa sababu watu wanakutegemea ufanye hivyo. Pia unaweza kuwa
unafanya ili upate kitu fulani unachotaka.(BENDERA FUATA UPEPO ).
(1) .MSUKUMO AU HAMASA KUTOKA NDANI
Msukumo wa ndani yako ndiyo wenye
nguvu sana, kwa sababu utafanya licha ya kinachoendelea nje yako. Lakini
msukumo wa nje hauna nguvu kubwa, kwa sababu mazingira ya nje
yakibadilika, basi na msukumo unabadilika.
Sasa kama unataka kupata fedha zaidi, tafiti zinaonesha kwa kutumia
msukumo wa ndani unaweza kutengeneza fedha mara tatu zaidi ya
unavyotumia msukumo wa nje.
Pale unapofanya kitu kwa sababu umechagua kufanya, kwa sababu unataka
kuwasaidia wenye uhitaji au unataka kutoa mchango wako, utatengeneza
kipato kikubwa kuliko pale unapofanya ili tu upate fedha ya kulipa
gharama za maisha yako.
Unapofanya kitu kwa sababu tu unataka
fedha, unapata fedha kidogo, kuliko kama utafanya kitu hicho hicho kwa
msukumo kutoka ndani yako.
Na pale unapofanya kitu kwa msukumo wa ndani, haimaanishi kwamba
hujali fedha, unajali sana, ila msukumo wa wewe kufanya ni mkubwa kuliko
fedha, hivyo unakuwa umejiweka juu ya fedha, kitu ambacho kinakuwezesha
kupata fedha kama unavyotaka.
(2).MSUKUMO AU HAMASA KUTOKA NJE
Lakini unapofanya kwa ajili ya fedha pekee, utapata fedha, lakini
utakuwa umeweka fedha juu yako, hivyo unakuwa umejiwekea ukomo wewe
mwenyewe, ukishafika kiwango fulani cha fedha utaacha kufanya kwa sababu
hamasa yako ilikuwa fedha pekee.
Kuwa na msukumo wa ndani kwenye kila unachofanya, penda fedha na
ihitaji, lakini isiwe msukumo pekee wa wewe kufanya kitu. Fanya
unachofanya kwa msukumo wa ndani na utaweza kupata fedha kadiri
utakavyo, na hutakuwa na ukomo wowote kwenye kipato unachoweza
kutengeneza.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker, MC,Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com