(1). KUJIDHIBITI
Eneo la kwanza kabisa unalohitaji kulifanyia kazi kila siku ili kuwa
na maisha bora ni kwenye udhibiti. Unahitaji kujidhibiti wewe mwenyewe,
la sivyo utawapa wengine nafasi ya kukudhibiti wewe. Unahitaji
kujipangia nini utafanya na kipi hutafanya na kufuata mpango huo.
Muda ulionao kila siku ni mfupi sana, ni muda ambao kama ukiweza
kujidhibiti utaweza kufanya makubwa. Lakini ukishindwa kujidhibiti,
utashangaa muda unaisha na hakuna ulichofanya. Lazima uweze kujiambia
HAPANA wewe mwenyewe, pale unapojiona unakosa udhibiti. Pia lazima uweze
kujiadhibu wewe mwenyewe pale unapokwenda kinyume na mipango
uliyojiwekea wewe mwenyewe.
Jidhibiti wewe mwenyewe na kila siku yako itakuwa siku ya ushindi, kwa sababu utafanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwako.
(2). KUWA HALISIA / ACHA MAIGIZO
Kitu kimoja ambacho dunia inakazana sana kufanya kwako ni wewe uwe
kama wengine. Kwa sababu dunia inajua ukiwa wewe, utakuwa msumbufu,
hutafaa kutawaliwa na hivyo inakazana sana uwe kama wengine, uwe ndani
ya kundi ili uweze kutawaliwa na kutumiwa vizuri na wengine.
Hivyo eneo la pili la kufanyia kazi kila siku ili kuwa na maisha bora
ni uhalisi. Unapaswa kukazana kuwa halisi kila siku, kuishi maisha yako
kwa uhalisia, kuacha kuigiza na kuacha kufanya vitu ili kuwaridhisha
wengine au uonekane na wewe unafanya.
Hutaweza kufanikiwa kama huishi maisha halisi kwako, hata kama
utapata vitu vingi kiasi gani, kama maisha unayoishi siyo halisi kwako,
kila mara utasikia sauti inakuambia wewe bado sana. Na hapa ndipo wengi
husema wamefanikiwa lakini hawana furaha.
Shida yao ni moja tu, maisha wanayoishi siyo halisi kwao, ni maisha
feki na hivyo mafanikio yoyote wanayopata yanakuwa yanaonekana na
wengine lakini siyo ndani yao binafsi.
Kuwa halisi kwako, jua uimara wako, jua madhaifu yako, jua yapi yenye
maana kwako na jua kusudi la maisha yako ni lipi. Kisha tumia kila
dakika ya siku yako kuishi maisha ambayo ni halisi kwako. Utafanikiwa
kariri unavyoishi maisha halisi kwako.
(4). JITAMBUE.
Kujitambua ni eneo muhimu sana la kufanyia kazi, na linatangulia
uhalisia. Kwa sababu bila ya kujitambua, hutaweza kuishi uhalisia wako.
Na changamoto ya kujitambua ni kwamba ni zoezi endelevu.
Watu wengi wamekuwa wakifikiri wakishajua wanataka nini kwenye maisha
yao, wakishaweka malengo makubwa basi wamemaliza. Hiyo siyo sahihi,
unachojua leo kuhusu wewe, kinaweza kuwa tofauti kabisa na
utakachotambua kesho kuhusu wewe.
Kubadili mazingira, kukutana na changamoto, kote huko kutakufunulia
kwa undani kuhusu wewe. Mara nyingi huwezi kujua una uwezo wa kufanya
makubwa kiasi gani mpaka pale unapokutana na changamoto kubwa kwenye
maisha yako.
Hivyo zoezi la kujitambua ni endelevu, kila siku, kwa kila
unachopitia, jiulize ni kipi kipya umejua kuhusu wewe. Na wakati mzuri
wa kujipima ni pale unapopitia mambo magumu. Utaweza kupima uwezo wako
wa kudhibiti hasira pale unapokasirishwa hasa. Unaweza kujua unaweza
kuvumilia ugumu kiasi gani pale unapokutana na ugumu zaidi.
Kila siku mpya ya maisha yako ni siku ya kujitambua zaidi, ishi kila
siku kwa kutaka kujitambua na maisha yako yatakuwa bora sana.
(4).KUJIENDELEZA.
Eneo la nne ambalo unapaswa kulifanyia kazi kila siku ni kujiendeleza
wewe binafsi. Kila siku lazima ukazane kuwa bora zaidi kuliko siku
iliyopita. Kila siku unapaswa kujifunza kitu kipya. Usikubali siku iishe
ukiwa kama siku ya jana ilivyoisha.
Weka kipaumbele kwenye kujifunza. Jifunze kupitia kusoma, kusikiliza,
kuangalia na hata kufanya. Soma vitabu, sikiliza mafundisho mbalimbali,
waangalie wengine kwa namna wanavyofanya na jaribu vitu vipya kwa ajili
ya kujifunza kwa kufanya.
Jinsi unavyojifunza kila siku, unazidi kuwa bora na kuyafanya maisha yako kuwa bora zaidi.
Rafiki yangu mpendwa, maeneo haya manne ni muhimu sana kwako
kuyafanyia kazi kila siku. Ninaposema kila siku, namaanisha kila siku ya
maisha yako. Na usiache hata siku moja, mpaka siku unaondoka hapa
duniani.
Kama unajiambia huwezi kila siku, kama unajiambia utajisahau au
kupitiwa na maisha mengine, ninayo nafasi ya kukumbusha hili kila siku,
na kukushirikisha fursa za kujifunza na kujitambua kila siku. Karibu
kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ambapo utapata nafasi ya kuingia kwenye kundi
la wasap, na kila siku utajifunza kwenye maeneo hayo manne na mengine
mengi.
Na
Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya
Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker(MC), Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL:
japhetmasatu@gmail.com
BADILI FIKRA.FIKIRI TOFAUTI .BADILI MAISHA.JITAMBUE .JIFUNZE ELIMU YA SAIKOLOJIA,TEOLOJIA , FEDHA ,UTAMBUZI(SELF HELP EDUCATION),FALSAFA YA MAISHA,MAISHA NA MAFANIKIO,BIASHARA / UJASIRIAMALI.FURAHIA WASAA WAKO NA MAISHA NA MAFANIKIO BLOGU.THIS IS THE COMMUNITY CAPACITY BUILDING BLOG.ENJOY THE BLOG.STRETCH YOUR MIND. YOU CAN CHANGE YOUR LIFE FOR EVER. YOU CAN ACHIEVE EXCELLENCE.YOU CAN MAKE A DIFFERENCE.
Sunday, September 16, 2018
Saturday, September 15, 2018
UKIFANYA KWA MSUKUMO WA NDANI , UTAPATA PESA SANA.
Kwa chochote ambacho unafanya kwenye maisha yako, kuna misukumo au hamasa za aina mbili.
(2):-
Aina ya kwanza ni msukumo au hamasa inayotoka ndani yako. Hapa ni pale unapofanya kitu kwa sababu umechagua kufanya, kwa sababu unajua ni kitu muhimu kwako kufanya na kwa sababu unajua kuna thamani unaongeza kwenye maisha ya wengine.
Aina ya pili ni msukumo au hamasa inayotoka nje. Hapa ni pale unapofanya kitu ili kuonekana unafanya, au kwa sababu wengine wanafanya, au kwa sababu watu wanakutegemea ufanye hivyo. Pia unaweza kuwa unafanya ili upate kitu fulani unachotaka.(BENDERA FUATA UPEPO ).
(1) .MSUKUMO AU HAMASA KUTOKA NDANI
Msukumo wa ndani yako ndiyo wenye nguvu sana, kwa sababu utafanya licha ya kinachoendelea nje yako. Lakini msukumo wa nje hauna nguvu kubwa, kwa sababu mazingira ya nje yakibadilika, basi na msukumo unabadilika.
Sasa kama unataka kupata fedha zaidi, tafiti zinaonesha kwa kutumia msukumo wa ndani unaweza kutengeneza fedha mara tatu zaidi ya unavyotumia msukumo wa nje.
Pale unapofanya kitu kwa sababu umechagua kufanya, kwa sababu unataka kuwasaidia wenye uhitaji au unataka kutoa mchango wako, utatengeneza kipato kikubwa kuliko pale unapofanya ili tu upate fedha ya kulipa gharama za maisha yako.
Unapofanya kitu kwa sababu tu unataka fedha, unapata fedha kidogo, kuliko kama utafanya kitu hicho hicho kwa msukumo kutoka ndani yako.
Na pale unapofanya kitu kwa msukumo wa ndani, haimaanishi kwamba hujali fedha, unajali sana, ila msukumo wa wewe kufanya ni mkubwa kuliko fedha, hivyo unakuwa umejiweka juu ya fedha, kitu ambacho kinakuwezesha kupata fedha kama unavyotaka.
(2).MSUKUMO AU HAMASA KUTOKA NJE
Lakini unapofanya kwa ajili ya fedha pekee, utapata fedha, lakini utakuwa umeweka fedha juu yako, hivyo unakuwa umejiwekea ukomo wewe mwenyewe, ukishafika kiwango fulani cha fedha utaacha kufanya kwa sababu hamasa yako ilikuwa fedha pekee.
Kuwa na msukumo wa ndani kwenye kila unachofanya, penda fedha na ihitaji, lakini isiwe msukumo pekee wa wewe kufanya kitu. Fanya unachofanya kwa msukumo wa ndani na utaweza kupata fedha kadiri utakavyo, na hutakuwa na ukomo wowote kwenye kipato unachoweza kutengeneza.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki ---Mwl wa Maisha Na Mafanikio, Mshauri, Public Speaker, MC,Mwandishi, Mjasiriamali /
Tuwasiliane kwa :+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com

Sunday, September 2, 2018
JINSI YA KUDHIBITI TABIA YA KUNUNUA VITU OVYO ! KWA KUTUMIA SHERIA YA SIKU 30 KWENYE FEDHA.
Moja ya tatizo kubwa ambalo watu wanalo kwenye fedha ni kushindwa
kudhibiti matumizi. Watu wanapokuwa na fedha, na wakakutana na kitu
kizuri, wanajikuta wameshanunua.
Ndiyo maana watu wanaishia kuwa na nguo ambazo hawazivai, vitu ambavyo hawavitumii, lakini wamenunua. Ukiwauliza kwa nini walinunua hata hawawezi kukupa jibu la wazi. Wengine watakuambia ilikuwa rahisi na wasingeweza kupata kwa bei rahisi vile. Wengine watakuambia wanajua watakuja kuhitaji kitu hicho siku moja.
Haijalishi unajifariji kwa maneno gani, kama umenunua kitu ambacho hukitumii sana, umepoteza fedha. Au kama umenunua kitu, lakini inakulazimu ukitumie ili usijione umepoteza fedha, jua umeshapoteza fedha.
Sasa, ipo sheria inayoweza kukusaidia usirudie tena makosa uliyofanya huko nyuma ya kununua kitu ambacho hukitumii. Sheria hiyo ni sheria ya siku 30.
Sheria hii inasema kwamba, kama umekutana na kitu na ukajishawishi unahitaji kukinunua, usikinunue hapo hapo. Badala yake andika mahali kwamba unataka kununua kitu hicho, kisha subiri kwa siku 30 kabla hujakinunua. Sasa kama siku 30 zitaisha na bado ukawa unauhitaji mkubwa wa kitu hicho, au hata siku 30 hazijaisha uhitaji unakuwa mkubwa mno la sivyo maisha hayawezi kwenda, nunua kitu hicho.
Rafiki, kwa sheria hii, usijidanganye kwamba hii ni bei rahisi na hutapata tena, au kitu hicho ni cha mwisho na hakitapatikana tena. Sheria ni moja, subiri siku 30 zipite na utanunua.
Kitu ambacho utanufaika nacho kwenye sheria hii ni kwamba baada ya siku tatu kupita, wala hata hutakumbuka kama ulipanga kununua kitu hicho.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki /+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com

USIOGOPE KUACHA KITU KAMA HAKINA TIJA.
Usiogope kuacha kitu pale unapoona hakikupi matokeo uliyotaka. Watu wengi huwa wanafikiria kuacha ni kushindwa. Siyo sahihi, unaweza kuacha kitu ambacho hakifanyi vizuri na kufanya kingine ambacho kitakuwezesha kufanikiwa zaidi.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki /+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
FANYA MAAMUZI KWA WAKATI.
Fanya maamuzi wakati unapokutana na hitaji la kufanya maamuzi.
Usijiambie wacha nifikiri nitaamua baadaye. Kama kitu ni muhimu fanya
maamuzi sasa, au hutayafanya kabisa. Maamuzi yanayosogezwa mbele ni
maamuzi ambayo yamekuwa hayafanywi.
Usiogope kukosea pale unapochagua kufanya maamuzi. Ni bora ufanye maamuzi ukosee, kwa sababu utarekebisha makosa yako, kuliko kutokufanya maamuzi kabisa.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki /+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Usiogope kukosea pale unapochagua kufanya maamuzi. Ni bora ufanye maamuzi ukosee, kwa sababu utarekebisha makosa yako, kuliko kutokufanya maamuzi kabisa.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki /+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
USIKIMBIZANE NA VITU VYA KUPITA . WEWE KAZANA NA AMBAVYO SIYO VYA KUPITA.
Weka nguvu zako kwenye vitu ambavyo havitabadilika. Watu wengi huwa
wanakazana kukimbizana na vitu vinavyopita, fursa mpya, fasheni na
habari mpya ya mjini. Wewe kazana na vile ambavyo siyo vya kupita, na
biashara yako itakuwa imara. Achana na vitu ambavyo watu wanataka sasa,
kazana na vitu ambavyo watu wataendelea kuhitaji miaka kumi ijayo.
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki /+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Na Mwl Japhet Masatu , Dar es salaam , Tanzania, Afrika Ya Mashariki /+ 255 755 400 128 / + 255 716 924136(WhatsApp ). EMAIL: japhetmasatu@gmail.com
Saturday, August 18, 2018
Subscribe to:
Posts (Atom)