USIMPIGE
MKE WAKO
KATIKA maisha
ya kila siku , mume
na mke waweza
kuwa wanaishi kwa
kuheshimiana na kuonyeshana
UPENDO wa kila
hali. Kuna baadhi ya
watu wamekuwa na
IMANI kwamba mwanamke
bila kupigwa bado
hajaoneshwa UPENDO.Hata hivyo
IMANI hii mara
nyingi imekuwa ikijitokeza
katika baadhi ya
makabila ilhali watu wengine
, hasa wale wanaokwenda
na mabadiliko ya
SAYANSI na TEKNOLOJIA , wakijitahidi kuyaepuka
katika familia zao.
Matatizo
huweza kuzuka pale
nyumba inapofikiwa na
mgeni ambaye ana
uhusiano na mume
au mke. Kwa wenye
nyumba wastaarabu, hata kama
tayari wamekwishaanza kuwa
na tofauti , hujitahidi kwa
kila hali , kuzificha
mpaka pale mgeni
huyo atakapoondoka ili
kulinda SIFA na
HESHIMA yao nje
ya nyumba.
Hata
hivyo, wapo wale wanaoona
kwamba huo ndio
wakati mwafaka wa
kuonesha ubabe kwamba
wana uwezo wa
kuzimiliki nyumba
zao ikiwa ni
pamoja na kuwafanya
jambo lolote wake
zao bila kujali , kwani ni
mali yao. Wakati mwingine, huweza kuanzisha
kisa kidogo sana
ambacho humsababisha mume
huyo kumpiga mkewe
huku mtazamaji akibakia
hana la kufanya ,
kwani WAPENDANAO WAGOMBANAPO
ukaingilia , siku
wakipatana watakuona mchonganishi
wao.
Kuna
wanaume wengine wenye
tabia ya kuchukia
pindi wanaporudi nyumbani
na kukuta WAGENI. Tena
cha ajabu zaidi ,
ni pale wanapowarushia mzigo
WAKE zao kwa
madai kwamba wao
ndio wamewaalika. Ikumbukwe
kwamba WAGENI nyumbani
ni BARAKA
na mnatakiwa mjitahidi
kwa kila hali
kuwakirimu kwa kilichopo. Pindi unapoonesha
kuwa na shaka
na mgeni ikiwa atagundua
hali hiyo , yawezekana kabisa
AKAONDOKA nyumbani kwenu
akiwa amebeba mzigo
wenye sifa mbaya
juu ya maisha
yenu ambao huenda
na kuutua huko
aendako.
Tabia ya
kugombana na kutaka
KUJIKWEZA ili KUONEKANA
kuwa UNA NGUVU
katika nyumba imekuwa
ikijitokeza mara nyingi
pindi wanaume wanapoona
kuna ujio ndani
ya nyumba zao. Huamua
kufanya hivyo, kwa ajili
ya kujionesha wana
nguvu na hawatawaliwi
na wake zao ,
kwa kuwagombeza bila misingi hata
mbele ya watoto
wao , si hivyo tu bali
pia huweza hata
kuwapiga mbele ya wageni
wakiwa na malengo
ya kutafuta sifa.
Si kwamba
wanaume wote wana
tabia hii , la hasha !!
Bali ni muhimu
kwa wale wenye
tabia hizi , KUJIFAHAMU AU
KUJITAMBUA MWANAMKE HAFUNZWI
WALA KUREKEBISHWA KWA
FIMBO !! ONGEA NA
MKE WAKO !!
ACHA UBABE WEWE
MWANAUME !! JISHUSHE WAKATI
WOTE KWA MKEO. FANYA
LEO UONE UTANIAMBIA
BABA !! ONYESHA MAPENZI YA
DHATI KWA MKEO
SIYO NGUVU ZA
MWILI. MWANAKE ANAHITAJI UPENDO TOKA
KWAKO BABA !!
Si kwamba
mke ni mnyama
au mtoto mdogo
kiasi kwamba akielezwa
tu kwa maneno
hukosa uwezo wa kuelewa
anachoambiwa ni nini
na anapaswa kutekeleza
vipi. Kibaya zaidi ni
pale unapompiga mkeo
mbele ya mtu
ambaye ana uhusiano
naye wa karibu
zaidi. Moja kwa moja
hata kama ulikuwa
na nia nzuri
ya kumwonya atachukulia
kuwa unamnyanayasa ndugu
yake huku anakuona. Yawezekana akawa
hajapanga kuondoka na
kulazimisha kuondoka kwa
hasira ya yale
uliyomfanyia ndugu yake.
Anapofika kwa
wazazi ama walezi
huweza kukupakazia ikiwa
ni pamoja na
kutia chumvi dhidi
ya uhusiano mlionao
na wakati mwingine
shutuma huweza kuwa
nyingi zaidi hata
kama uliwafanyia kitendo
kizuri kiasi gani
kwa nia ya
kuwapoza. La ya hivyo , huo
waweza kuwa mwanzo
wa kuvurugika kwa
ndoa yenu. Mpaka hapo
hakutakuwa na wa
kumlaumu kwani awali
MUME kama muhimili
wa nyumba , alikuwa
na NIA ya
ajabu.
Kwa WANAUME
ambao bado wana
tabia ya kutumia
FIMBO kama njia
pekee ya KUWAELIMISHA
wake zao , ni vema
wakafahamu kuwa njia hiyo
SASA IMEPITWA NA
WAKATI. Hali kadhalika
kwa kufanya hivyo
mbele ya watoto ,
ina maana kwamba
UNAMDHALILISHA MKEO na
kumjengea ukuta wa
kutokuwa na maamuzi
na watoto hasa
katika masuala ya
KUWAKANYA.Kwani daima atakapowapiga hawatasita
kumwambia “ mbona
na wewe Baba
huwa anakupiga !!”Hata kama
mbele za watu.
EWE BABA
ACHA KUMPIGA MKEO ,
ONGEA NAYE !! JIFUNZE KUMSIKILIZA!
ASANTE MSOMAJI WANGU
KWA KUSOMA MAKALA
HII , KARIBU KWA MAONI , USHAURI , CHANGAMOTO !!
WEWE WAONAJE SUALA
HILI LA KUPIGA
WANAWAKE KATIKA NDOA ?
Makala hii
imeandikwa na MWL.
JAPHET MASATU ,
Mwelimishaji na mhamasihaji
katika masuala ya
Elimu ya maisha
na Mafanikio , Mahusiano, biashara / ujasiriamali, anapatikana kwa namba
+ 255 755 400 128 { WhatsApp} /
+ 255 716 924136
/ + 255 785
957077. EMAIL : japhetmasatu@yahoo.com