Mwanamuziki chipukizi Diamond wa Tanzania anaendelea kupata mafanikio makubwa katika sanaa ya Muziki . Mungu ambariki.
Nyanja ya muziki ni pana sana na inawagusa watu wengi. Ni fani nzuri na inaleta AJIRA kwa wengi kwa vile ina mvuto hasa pale ambapo panakuwepo mfumo mzuri wa ubunifu wa nyimbo , utunzi wake na uhitaji wa sanaa hii kwa jinsi invyotoa burudani na mvuto wa hisia nyingi na nzuri. Muziki kama sanaa HAIJAPEWA Kipaumbele hapa TANZANIA kwa maana ya kukuzwa tangu watoto wetu wakiwa makinda, hadi utoto udogo hadi umri wa kwenda shule pindi wawapo mashuleni , wawapo nyumbani na kupewa ushindanishi sawa na fani na sanaa nyingine.Muziki ni sanaa ya ajabu sana.Upo Katika viini vya ujuzi za tafakari katika bongo za binadamu na kwa namna fulani hata viumbe vingine.Ni muhimu sana kutambua UTAJIRI unaoweza kupatikana kwa Watanzania wengi kwa kupitia nyanja hii ya muziki kwa kukuzwa vipaji kwa jamii yetu ya kuienzi kwa kila namna inayofaa na hivyo kuithamini.Baada ya kukuza vipaji, tutahitaji kuwa na sheria kali ya hati miliki.
Mfano mzuri
ni katika nchi
zilizoendelea Ulaya na
Marekani ambapo walio
wengi wamekuwa matajiri
kwa kufanya biashara
hii. SIRI YA MAFANIKIO
ni kuendesha biashara
kitaalamu na kibiashara
zaidi. Hapa kwetu
wanamuziki hutoa burudani
tu wakati hawalipwi
chochote au wanapata
malipo kidogo na
kuambulia sifa tu.. Biashara ya
MUZIKI ikiendeshwa vizuri
inaweza kutoa AJIRA
na kipato kwa
watu wengi sana
kama vile , wanamuziki
wenyewe , wamiliki wa
bendi , wamiliki wa
kumbi za muziki,wamiliki wa
studio za kurekodia
, studio za video
na luninga , wahandisi wa
sauti, wazalishaji , wasambazaji
na wauzaji wa
kanda za muziki.
Je, unahisi una
kipaji cha Kuimba ??
Fanya hivi :
Ni rahisi tu. Unakwenda
studio na wimbo
wako, unamweleza mwenye studio—Producer. Una
REKODI. {Siyo lazima
ujue kupiga vyombo
vya muziki }. Kuuza na
Kusambaza nakala atakueleza
Producer. Anza na single
kisha ALBAMU. We imba
soko lipo. Siyo kwamba
wasanii wote wa
muziki unaowajua wanaweza kuimba
vizuri zaidi yako. Unaweza kuwazidi
wengi tu, ni kwa
kuwa hujaamua kufanya
hivyo. JIAMINI !! UNAWEZA
VIZURI SANA !! Imba muziki
wa kidunia {circular music }
au wa kidini { religious music } kama wewe
ni mtu wa
imani.
Bila shaka
mtakubaliana nami kuwa
katika sanaa, muziki ni
eneo lenye kupendwa
na watu wengi
zaidi.
Mfano wa wanamuziki waliofanikiwa katika Sanaa hii ya muziki ni Diamond { Tanzania } , Mzee Yusufu { Tanzania}, Elton John , Whitney Houston n.k.
Japo kila mtu anaweza, lakini siyo wote tunapenda kufanya biashara. Mwingine ukimpeleka katika uimbaji kwa mfano au maigizo , anafurahia na kujisikia kafika kuliko kufanya biashara.
Hivyo ndivyo tulivyo.Mtu unatakiwa kufanya kile unachokipenda na kukifurahia. HAPO UTAFIKA MBALI.
Katika Sanaa kama ilivyo katika biashara , kuna vitu vingi vya kufanya.Angalia Kipaji , upenzi , soko na mazingira mengine ya Kiutendaji kwa ujumla.
Mfano wa wanamuziki waliofanikiwa
katika Sanaa hii ya muziki ni Diamond { Tanzania } , Mzee Yusufu { Tanzania},
Elton John , Whitney Houston n.k. Japo kila mtu anaweza, lakini siyo wote
tunapenda kufanya biashara. Mwingine ukimpeleka katika uimbaji kwa mfano au
maigizo , anafurahia na kujisikia kafika kuliko kufanya biashara. Hivyo ndivyo
tulivyo.Mtu unatakiwa kufanya kile unachokipenda na kukifurahia. HAPO UTAFIKA
MBALI. Katika Sanaa kama ilivyo katika biashara , kuna vitu vingi vya
kufanya.Angalia Kipaji , upenzi , soko na mazingira mengine ya Kiutendaji kwa
ujumla.