Umakini wako ndiyo utajiri wako, kama utaweza kuweka umakini wako wote kwenye kile unachofanya, kwa hakika utaweza kuongeza kipato chako maradufu.
Mtaalam Mmoja Aliwahi Kusema Hivii.”Siku zijazo, kutakuwa na makundi makuu mawili ya watu duniani.
Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wanaruhusu umakini wao kudhibitiwa na watu wengine, ambao wanaruhusu kila aina ya usumbufu kuwaingia. Kundi hili litakuwa na watu wengi sana, na mara zote watakuwa wamevurugwa na wasiweze kufanya makubwa kwenye maisha yao.
Kundi la pili litakuwa la wale ambao wanadhibiti umakini wao na kutoruhusu usumbufu wa aina yoyote ile kuwavuruga. Kundi hili litakuwa na watu wachache sana, na hawa ndiyo watakaoweza kufanya makubwa na kufanikiwa sana.”
Swali kwako, je kwa hali inavyokwenda sasa kwenye maisha yako, unajiona ukielekea kwenye kundi lipi kati ya hayo mawili?
Na je ungependa kuwa kwenye kundi lipi? Kama ungependa kuwa kwenye kundi la kwanza huna cha kufanya, endelea kufuata mkumbo na kila aina ya kelele.
Lakini kama ungependa kuwa kwenye kundi la pili, basi yale yote ambayo umejifunza kwenye kitabu cha juma hili yafanyie kazi.
Jua usumbufu wako wa ndani na wa nje na tenga muda wa kufanya yale muhimu na kuepukana na usumbufu.
Maarifa tayari unayo, kama hutachukua hatua huna wa kumlaumu, utakuwa umechagua wewe mwenyewe.
Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.
Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.
USICHANGANYE VIPAUMBELE.
ReplyDelete" Mafanikio makubwa ndiyo kipaumbele cha kwanza kabisa kwenye maisha yako, hupaswi kuruhusu kitu kingine kuingilia kipaumbele hicho. Utaona wengine wakihangaika na mambo mbalimbali kwenye maisha na kutamani kufanya kama wao. Lakini jua wengi hawafiki kwenye mafanikio makubwa na sababu kuu ni kuhangaika na mambo mengi badala ya kuweka vipaumbele sahihi."
USIIGE ANASA ZISIZO SAIZI YAKO.
ReplyDeleteUsiige anasa zisizo saizi yako... Kama bado hujafikia uhuru wa kifedha, anasa yako ni moja tu, kazi. Usidanganyike na mlinganyo wa maisha na kazi. Usidanganyike na kufanya kazi kwa akili na siyo kwa nguvu