Angalia, Jinsi Ilivyorahisi Kuokoa Muda Wako.
Unajua ni nini cha kikawaida kati yako na Jeff Bezos, Mark Zuckerberg, Bill Gates, Mukesh Ambani, Warren Buffett
Rasilimali ya kikawaida ambayo mnayo wote sawa ni MUDA.
Kila mmoja amepewa MUDA sawa kama mwenzake.
Hakuna aliyependelewa.
Wote mna sekunde 86,400 kwenye siku moja.
Matumizi mazuri ya muda ndiyo yanaleta tofauti iliyopo kati ya waliofanikiwa sana na wale wenye maisha ya kawaida.
Leo nitakushirikisha stori fupi inayohusu matumizi mazuri ya muda.
Siku moja niliudhuria semina pale mkufunzi alipokuwa anafundisha juu ya MUDA.
Kabla hajaanza kutufundisha akasema “ Huu ni muda wa kufanya zoea”
Akaenda chini ya meza na kuvuta jagi kubwa lenye upana wa wastani.
Akaliweka juu ya meza karibu na mawe makubwa ambaye yalikuwepo pale mezani.
Akauliza unafikiri ni mawe mangapi yataweza kuenea ndani ya hili jagi?
Wakati tukiendelea kukisia na kutafakari,
Akasema “Sawa, acha tutafute“.
Akaweka jiwe la kwanza ndani ya jagi... likafuatia lingine... na lingine tena.
Sikumbuki aliweka mawe mangapi kwenye jagi, lakini alijaza lile jagi.
Akauliza tena “ Hili jagi limejaa?”
Kila mmoja akaangalia yale mawe na kusema “ NDIYO”.
Mkufunzi akacheka kwa sauti, “ahhh”.
Akaingia chini ya meza na kuvuta ndoo ya kokoto.
Halafu akamimina kokoto kwenye jagi na kuanza kutikisa na kokoto zote zikaenea kwenye jagi na kuziba mianya yote iliyoachwa wazi na mawe makubwa.
Hapo baadae akalitikisa lile jagi na kuuliza tena “ Hili jagi limejaa”
Kwa muda huu ,washiriki tukawa tunakisia jibu na kuogopa kujibu tusije tukakosea tena huku tukiwa tunajisemea “ Pengine sio”.
Kiukweli tulikuwa hatujiamini.
Mkufunzi akaitikia kwa kusema ”VIZURI!”.
Akaingia tena chini ya meza na kutoka na ndoo ya mchanga na akaanza kumwaga ndani ya jagi.
Baada ya kumwaga mchanga ndani ya jagi ikaonekana kuna mianya midogo imebaki kati ya mawe na kokoto ndani ya jagi.
Mkufunzi kwa mara nyingine akaangalia na kuuliza, “ Hili jagi limejaa?”
Tulinguruma na kusema “Hapana!”.
Akasema, “SAFI!” na akachukua jagi lingine lenye maji na kuanza kumwagilia ndani ya jagi lenye mawe, kokoto na mchanga.
Akauliza mmeelewa nini?
Mmoja wetu akasema , “ Kuna mianya mingi, na kama utafanya kazi kwa bidii utaweza kukabiliana na chochote kile kinachojitokeza kwenye maisha yako”.
Mkufunzi akasema “ HAPANA” hicho sicho nilichomaansha.
Nimemaansha hivi.
“WEKA JIWE KUBWA KWANZA”.
Mkufunzi aliendelea, “ Sasa hivi, nataka uelewe kwamba hili jagi ni maisha yako.
Jiwe kubwa ni vile vitu vyote kwenye maisha vyenye umuhimu mkubwa kwenye maisha yako- chochote ambacho ni muhimu kwako, kama kikipotea kitaweza kuletea madhara makubwa kwenye maisha yako au kukuharibia maisha yako kabisa.
Mawe makubwa yanawakilisha vitu kama Afya ya mwili, Afya ya akili, Familia yako, Mke wako, Watoto wako.
Kokoto ni vile vitu vyenye umuhimu kwenye maisha yako lakini sio sana kama hivo hapo juu.
Kokoto inawakilisha vitu kama Kazi, Nyumba, Marafiki, Gari, Koneksheni ulizonazo.
Mchanga ni kila kitu ambacho ni kidogo na hakina umuhimu wowote kwenye maisha yako.
“Kama utaweka mchanga kwanza ndani ya jagi, mawe makubwa yatakosa nafasi ya kukaa ndani ya jagi.
“Ndio maana nilisema, hivi – “WEKA MAWE MAKUBWA KWANZA”.
Aliendelea , “ Natumaini sasa hivi umeelewa, hii ni sawa na kwenye maisha yako”.
Kama utatumia nguvu zako zote na muda wako kwenye vitu ambavyo havina umuhimu mkubwa na ni vidogo, utakosa muda wa kufanya vitu vikubwa na vyenye umuhimu mkubwa kwenye maisha yako.
Kuwa makini na vitu vyote vyenye umuhimu mkubwa kwenye maisha yako na tumia muda wako mwingi kwenye vitu vyenye umuhimu mkubwa.”
Lilikuwa somo zuri kubwa sana na lilibadilisha fikra zetu kwa wale wote tuliohudhuria.
Kuanzia siku hiyo nilibadili kwa kiasi kikubwa namna ninavyotumia muda wangu.
Kupitia stori hii natumaini umejifunza jinsi ya kutunza muda wako, kwa kuanza kwa kufanya mambo yenye umuhimu mkubwa kwanza.
Vipaumbele vitakusaidia sana kuamua na kujua ni kipi kianze kwanza kabla kingine.
Unahitaji kuweka msawazo kwenye maisha yako.
Unapoweka msawazo kwenye maisha yako hutosumbuka na mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa.
Muda ni dhahabu, tumia kwa hekima na acha kupoteza muda kwa mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa.
Pambana na yale yenye umuhimu mkubwa, acha kupoteza muda.
Kujua kuweka vipaumbele kwenye siku yako haitoshi, unahitaji zaidi ya hilo na hii ni kwa sababu kama hujua vitu vinavyokupotezea muda na kuweza kuvidhibiti.
Utaendelea kutumia nguvu nyingi na mwisho utakuwa unapata matokeo sisimizi.
Hutoweza kuanza kufanya yale yenye umuhimu mkubwa kwanza, kama hutoweza kuvidhibiti vinavyo kupotezea muda.
Hatua unayotakiwa kuchukua sasa hivi ni kuanza kuvidhibiti vitu vyote vinavyokupotezea muda na ikiwezekana uachane navyo kabisa kwa sababu vimekuwa vinachukua muda wako na kukuchosha mwisho unashindwa kufanya mambo yenye umuhimu mkubwa.
Na ipo njia rahisi ambayo kila siku nimekuwa nakushauri unayoweza kuifuata kuanzia sasa hivi ,ili usiendelee kupoteza muda wako kwenye mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa na yanaendelea kukuchosha.
Na KOCHA MWL, JAPHET MASATU,DAR ES SALAAM , TANZANIA,
WhatsApp +255 716 924 136 / + 255 755 400 128
EMAIL : japhetmasatu@gmail.com
No comments:
Post a Comment