Thursday, May 20, 2021

MATAPELI NI WENGI SANA JIFUNZE MBINU ZAO NA UWAKIMBIE NA FURSA ZAO FEKI KAMA UKOMA.

Zama tunazoishi sasa ni zama ngumu mno ambapo mtu usipokuwa na msingi imara utaishia kuanguka vibaya.

Fursa ni nyingi mno, lakini nyingi siyo fursa za kweli.

Fursa hizo zinahamasisha na kutamanisha kwa sababu unaona kabisa wengine wakinufaika nazo.

Kumbe hiyo ni sehemu ya mtego wa kukunasa ili uweze kuingia kwenye fursa hizo na utapeliwe.

Siku chache zilizopita nilipokea simu kutoka kwa mtu aliyejitambulisha kama msomaji ambaye amekuwa anafuatilia kazi zangu kwa muda mrefu.

Akaendelea kueleza kwamba kuna fursa nzuri angependa kunishirikisha. Ana watu anaofahamiana nao ambao wako nchi za nje na wapo tayari kumfadhili kiasi kikubwa cha fedha (mabilioni) ila hajui afanye nini.

Hivyo anataka tushirikiane, tuandike mradi wa mabilioni na kuwatumia hao watu wake na wapo tayari kutoa fedha hizo kama mradi ukionekana ni mzuri.

Kama tukifanya hivyo na mimi nitakuwa sehemu ya mradi huo na hivyo kunufaika nao.

Baada ya kumsikiliza akijieleza kwenye hayo nilimjibu HAPANA, SITAWEZA. Alionekana kushangaa kwa nini nakataa fursa kubwa hivyo. Nikamwambia atafute watu wengine.

Rafiki, kama kwa kusoma hapo umeshangaa iweje nikatae fursa kubwa ya mabilioni, kama umeiona hiyo ni fursa basi jua wewe ni rahisi sana kutapeliwa.

Kwenye makala hii nitakushirikisha mbinu za kuwajua matapeli na fursa zao za kukunasa ili uepuke kutapeliwa. Kisha mwisho nitakuonesha utapeli ulio kwenye hiyo 'fursa' niliyoshirikishwa.

(1). UTAINGIZA  PESA  BILA  KUFANYA  KAZI.

Kiashiria cha kwanza cha utapeli ni ahadi kwamba utaingiza pesa bila kufanya kazi yoyote ile. Na katika maelezo ya fursa husika, huoni jinsi fedha unayoweka inakwenda kufanya kazi.

Wewe unaambiwa tu weka kiasi fulani na baadaye utavuna faida kubwa. Huelezwi jinsi gani fedha hiyo uliyoweka inakwenda kuzalisha thamani ambayo ndiyo inaleta faida.

Rafiki, hii dunia imekuwepo kwa miaka mingi na katika kipindi chote hicho pamoja na wagunduzi wakubwa waliowahi kuishi, haijawahi kujulikana njia ya kupata pesa bila kufanya kazi, bila kuzalisha thamani kubwa kwa wengine.

Hivyo usidhani wewe una akili sana kuweza kujua fursa za aina hiyo, kama unaambiwa weka tu fedha na uje uvune faida, hapo kuna utapeli.

(2). UNAELEZWA  FAIDA  TU ,HUELEZWI    HASARA.

Kila kazi, biashara na hata uwekezaji huwa una faida na hasara.

Ukipata kazi inayolipa sana inakunyima muda kabisa. Ukipata kazi inayokupa muda haikulipi vizuri.

Huwezi kupanda shamba la mahindi au maharage na mbegu zote ulizoweka zikaota na kuzaa vizuri, haijawahi kutokea hata kwa sayansi ya juu kiasi gani.

Hivyo ndivyo asili ilivyo na ndivyo itaendelea kuwepo. Kuna faida na hasara, kuna kupata na kupoteza. Iko hivyo.

Wanaokuja kwako na fursa za kitapeli wanakueleza kitu kimoja tu, faida. Hadithi zao zimetengenezwa vizuri mno kiasi kwamba ukizisikiliza unaona pesa nje nje.

Umewahi kusikia hadithi za kulima matikiti au mapapai na ukapigiwa hesabu ya heka moja inaingia miche mingapi na kila mche unatoa matunda mangapi na ukapigiwa bei ya kila tunda ukauona utajiri si ndiyo huu?

Nenda shambani ndiyo utakutana na asili isiyokuwa na huruma na ndiyo utaelewa kwamba umetapeliwa.

(3). UNAONESHWA  MIFANO  YA  WACHACHE  WALIOFANIKIWA.

Ni vizuri kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa, lakini ni vizuri zaidi kujifunza kutoka kwa walioshindwa.

Maana huwa unafundishwa siri nyingi za mafanikio, ila kubwa kabisa moja umekuwa hufundishwi, ambayo ni; BAHATI.

Ndiyo, kuna wengi ambao wamefanikiwa kwa bahati tu, japo wanaweza wasijue hilo na wakaona ni ujanja au juhudi zao.

Kama watu 100 wanafanya kitu kimoja, kwa namna moja na eneo moja, halafu mmoja akafanikiwa huku 99 wakishindwa, mafanikio ya mtu huyo ni bahati zaidi kuliko juhudi binafsi.

Matapeli huwa wana mifano michache ya watu waliotumia njia zao wakafanikiwa lakini huwa wanaficha mifano ya wengi waliotumia njia zao na wakashindwa vibaya.

Hivyo unapopewa hadithi za waliofanikiwa, usikimbilie kuziamini kwa sababu wanaonekana wazi, bali kazichimbe zaidi na ona kama kuna kitu cha tofauti kimewawezesha kufanikiwa. Angalia wengine wengi ambak pia walikuwa wanafanya kama wao lakini hawajafanikiwa.

Tenganisha bahati na juhudi ili uweze kujua kweli kinacholeta mafanikio.

4. Unapaswa kuchukua hatua haraka la sivyo utaikosa fursa.

Fursa za kitapeli huwa hazitaki upate muda wa kutafakari kitu, hivyo unalazimishwa uchukue hatua haraka la sivyo utaikosa fursa.

Huwa wanafanya hivyo kwa makusudi, wakati wanakuambia kuhusu fursa, wanaibua hisia kali za tamaa ndani yako na tamaa ikishakuwa juu ni rahisi kwako kufanya maamuzi yasiyo sahihi. Hilo ndiyo wanataka.

Wanajua ukipata muda hisia zako zitashuka, utaweza kufikiri kwa usahihi na utaona utapeli ulio kwenye fursa husika.

Richard Branson amewahi kusema fursa ni kama daladala, ukikosa moja jua kuna nyingine inakuja.

Hivyo unapoelezwa kuhusu fursa yoyote ile, jibu lako la kwanza linapaswa kuwa ni wakupe muda uifikirie na kuitafiti kwa kina. Ukiona wanakuambia unapaswa kuchukua hatua sasa au hupaswi kufikiria sana kwa sababu kuna wengine waliofanikiwa tayari wameichukua fursa hiyo, jua hapo kuna utapeli, kaa mbali.

(5 ). UNALAZIMISHWA   UPTAE  MANUFAA.

Tangu kugunduliwa kwa fedha na kutumika kama njia ya kubadilishana thamani, hakuna mtu amewahi kutaka mtu mwingine apate fedha kuliko yeye.

Ndiyo maana ukienda kununua kitu na ukaambiwa bei, huwa unauliza kama kuna punguzo.

Ukipewa kazi na kutajiwa malipo, huwa unaomba upewe nyongeza.

Sasa anakuja mtu kwako, ambaye hata siyo ndugu au rafiki yako, ila ana fursa nzuri kwako ya kukuwezesha kupata fedha nyingi.

Unapokuwa humuelewi anaonekana kuumia sana kwa sababu anaona jinsi unavyokosa fedha nyingi.

Na wewe unaamini na kuingia kwenye mtego huo.

Huwa nasema ukiona mtu anakulazimishia sana fursa, jua wewe ndiyo fursa kwake.

Hakuna anayekupenda sana kwenye fedha kiasi cha kuumia pale anapoona huchangamkii fursa.

Swali jingine la kujiuliza kwa hao waleta fursa, je ndugu zao na watu wao wa karibu wameshawapa fursa hiyo ili wanufaike?

Jibu huwa ni hapana, sasa wanawezaje kukupenda wewe mtu wasiyekujua kuliko wanavyowapenda watu wao wa karibu?

Umeshapata jibu hapo, hawawezi kuwatapeli watu wa karibu.

 ( 6 )KILA   MTU  ANAIZUNGUMZIA  FURSA.

Ukishaanza kusikia kila mtu anazungumzia kitu fulani ni fursa nzuri, jua tayari umeshachelewa.

Hata kama fursa ni ya kweli kabisa, kama unaisikia kwa kila mtu, dirisha la kunufaika kwa kiwango kikubwa limeshakupita.

Inakuwa imebaki kuwa fursa kwa wale wapiga debe ambao wanashawishi wengine wajiunge na fursa hiyo maana wao ndiyo watanufaika.

Na hapa ndipo njama kubwa ya utapeli unaofanana na ukweli inapotengenezwa.

Chukua mfano wa fursa kama ya sungura. Mtu anaanza kufuga sungura kwenye mazingira ambayo ufugaji wa sungura siyo wa kiwango kikubwa.

Kwa kuwa upatikanaji ni mdogo, uhitaji unakuwa mkubwa.

Hivyo mtu huyo anaweza kuuza sana kwa sababu hakuna mwingine anayezalisha kama yeye.

Na hapo anaanza kutangaza hiyo ni fursa nzuri na inayolipa.

Anakuonesha wazi kwamba uhitaji upo, soko lipo na faida ni nzuri.

Wewe kwa kuona hivyo unashawishika kuingia kwenye fursa, sasa basi mbegu utanunua kwake, chakula kwake, madawa kwake na ushauri mwingine kutoka kwake.

Mpaka inakuja kufika wakati wa kwenda sokoni, unakuta wenzako wengi walioingia kama wewe nao wanapeleka bidhaa sokoni. Upatikanaji unakuwa mkubwa kuliko uhitaji na bei inapungua sana.

Unajipa moyo ni soko halijakaa vizuri, usichoweza kukiri ni umetapeliwa kwa njama ya hali ya juu kabisa.

Rafiki yangu mpendwa, umepata mwanga mkubwa kuhusu utapeli kwa haya niliyokushirikisha hapa. Haya ni ya msingi kabisa na ambayo huwa yako wazi kwenye kila aina ya utapeli kama utatumia fikra zako badala ya hisia zako kufanya maamuzi.

Ili uepuke kuingia kwenye utapeli mbalimbali, endelea kujifunza na kujijenga kuwa imara.

Ndimi  KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU , DAR  ES SALAAM , 

WhatsApp + 255 716924136 / 

 

Saturday, May 15, 2021

NAFASI YA BAHATI KATIKA MAFANIKIO----NA MUNGA TEHENAN---( PDF )

JIFUNZE IMANI SAHIHI ITAKAYOKUSAIDIA ULIPWE ZAIDI. USITEGEMEE MSHAHARA PEKEE UTAKUFA MASKINI.

 Sio siri tena kwenye hii karne ya 21,

Mambo yamebadilika sana.

Sahau kila kitu ulichowahi kusikia kuhusu kulipwa.

Sasa kuna njia bora ya kulipwa zaidi kuliko ilivyokuwa imezoeleka karne ya 20.

Ni njia ambayo haizungumzwi sana lakini inafanya kazi kwenye hii karne ya 21.

Haijalishi umeajiriwa au umejiajiri,

Inafanya kazi kwenye hali zote mbili.

Ukweli ni kwamba,

Kwa sasa haulipwi kutokana na masaa unayofanya kazi,

Bali unalipwa kulingana na matokeo unayozalisha.

Unapozalisha matokeo makubwa zaidi unalipwa kiasi kikubwa cha fedha.

Unapozalisha matokeo madogo zaidi unalipwa kiasi kidogo cha fedha.

Angalia huu u tofauti hapa chini,

Kuhusu imani walizonazo matajiri na masikini kuhusu kulipwa.

Matajiri huwa wanachagua kulipwa kwa matokeo wanayozalisha na hapo wanazalisha matokeo makubwa zaidi na kulipwa kiasi kikubwa cha fedha.

Masikini wanachagua kulipwa kwa muda wanaotumia kufanya kitu na kwa kuwa muda una ukomo,

Wanajiwekea ukomo kwenye kipato chao.

Matajiri wote wamepata utajiri wao kupitia njia ambazo hazitegemei muda wao.

Kwa mfano kumiliki biashara inayojiendesha yenyewe ,

Kufanya uwekezaji maeneo yanayozalisha na kadhalika.

Kulipwa kwa muda ni kupitia mshahara au huduma binafsi ambazo mtu anatoza gharama kwa muda.

Hakuna mtu amewahi kufikia utajiri mkubwa kwenye maisha yake kwa kutegemea mshahara pekee.

Hata mshahara uwe mkubwa kiasi gani, bado unakuwa na ukomo.

Na mbaya zaidi, kadiri mshahara unavyokuwa mkubwa, ndivyo makato yanavyokuwa makubwa pia.

Kulipwa kwa muda ni kujiwekea ukomo na kanuni ya kwanza na muhimu kwenye fedha ni kuhakikisha huweki ukomo kwenye kipato chako.

Chagua kulipwa kwa matokeo na thamani unayozalisha ambayo haina ukomo,

Badala ya kutaka ulipwe kwa muda ambao una ukomo.

Je, ungependa ulipwe zaidi kwa kile unachofanya?

Kama ni ndio, KARIBU  UJIUNGE , " DARASA ONLINE "

Ujifunze njia na hatua za kuchukua ili ulipwe zaidi.

Utajiri ni mchezo,

Mchezo ambao una kanuni zake na sheria zake,

Na ili uweze kushinda mchezo huu,

 Lazima uzijue kanuni na uzishike sheria.

Haiwezekani kabisa kwa mtu ambaye hajui kanuni za mpira wa miguu,

Hana mazoezi akaenda uwanjani na kushinda.

Wengi wamekuwa wanaingia kwenye mchezo wa utajiri kama vile ni kitu cha kubahatisha,

Hawajui kanuni wala sheria,

Hawana maandalizi na kinachotokea ni kushindwa vibaya sana.

Karibu sana  UJIUNGE  " DARASA  ONLINE " UJIFUNZE  TABIA ZA KITAJIRI ILI  KUFIKIA  MAFANIKIO  MAKUBWA.

Ujifunze kwa kina na kuyaelewa maarifa haya muhimu sana kwako,

 Kisha uchukue hatua ili maisha yako yaweze kubadilika, ufike kwenye utajiri, mafanikio na furaha.

 

TUWASILANE  SASA, 

Ndimi  Rafiki   yako

Kocha  Mwl  Japhet  Masatu , Dar es  salaam , Tanzania.

 (WhatsApp + 255 716 924136 ) / + 255 755 400128  / + 255 688  361  539 / + 255 629748 937

EMAIL : japhetmasatu@gmail.com

 

Thursday, May 13, 2021

TABIA KUMI ( 10 ) ZA KUISHI KWA SIKU 30.

JARIBIO LA SIKU 30 LA KUUFANYA KILA MWAKA  KUWA WA MAFANIKIO MAKUBWA.

Mafanikio yetu yanajengwa au kubomolewa na tabia tunazoziishi kila siku.

Siku zetu zinaendeshwa zaidi na tabia ambazo tayari tumeshajijengea.

Ndiyo maana huwa unasikia huwa tunajenga tabia na kisha tabia zinatujenga.

Kwa siku 30 za mwezi, unakwenda kufanya jaribio la kuziishi tabia 10 ninazokwenda kukushirikisha hapa.

Kila siku kamilisha tabia hizo kumi bila kuacha hata siku moja, kisha siku 30 zinapoisha, jifanyie tathmini ya mabadiliko unayoyaona kwenye maisha yako.

TABIA KUMI ZA KUISHI KWA SIKU 30.

1. Kila siku amka mapema, saa moja kabla ya muda wako uliozoea kuamka. Ukishaamka usiangalie simu wala usumbufu wowote, bali anza kwa kufanya sala na/au tahajudi (meditation) kisha chukua notebook yako na andika vipaumbele vya siku hiyo, mambo ambayo utakwenda kufanyia kazi (To Do List). Hayo ndiyo mambo utakayoyapa kipaumbele kwenye siku yako, usifanye mengine kabla hayo hayajaisha.

2. Kila siku fanya mazoezi kwa dakika zisizopungua 30, mazoezi mazuri ni ya kukimbia.

3. Kila siku soma kitabu kwa angalau dakika 30, chagua kitabu chochote unachotaka kusoma, iwe ni cha maendeleo binafsi au maendeleo ya kitaaluma kisha soma kwa angalau dakika 30 kila siku.

4. Kila siku pangilia na dhibiti ulaji wako, punguza kabisa vyakula vya wanga na sukari, kula mboga mboga na matunda kwa wingi, kula nyama kwa kiasi na kunywa maji mengi. Pia dhibiti sana vilevi unavyotumia.

5. Kila siku mpigie simu mteja mmoja ambaye amewahi kunufaika na biashara au kazi yako na ongea naye kuhusiana na biashara au kazi yako na changamoto alizonazo unazoweza kumsaidia kutatua. Pia mpigie mteja tarajiwa mmoja, ambaye bado hajanunua ila ana uhitaji ambao unaweza kumsaidia, mwoneshe jinsi unavyoweza kutatua tatizo lake.

6. Kila siku mpigie simu mtu mmoja wa karibu, ndugu jamaa na marafiki na kuwa na maongezi naye ya kuboresha mahusiano yenu.

7. Kila siku jaribu kitu kipya na ambacho umekuwa unahofia kufanya au umekuwa unaona huwezi, hata kama ni kidogo, fanya. Hii inajenga ujasiri wako na kukuwezesha kuvuka hofu.

8. Kila siku kuwa na fikra chanya, fikra za mafanikio na utajiri mkubwa. Pata muda wa kuwa peke yako na jenga taswira ya ndoto kubwa ulizonazo, jione kama tayari umeshazifikia na amini ni kitu ambacho tayari kipo. Jenga taswira hii kwenye fikra zako na pia kuwa na picha ya ndoto ulizonazo unayotembea nayo au iliyo kwenye simu yako na iangalie mara kwa mara.

9. Kwa kila kipato unachoingiza, iwe ni kwa siku, wiki au mwezi, weka pembeni angalau asilimia kumi ya kipato hicho na iweke mahali ambapo huwezi kuitumia. Fedha ya ziada unayoipata ambayo hukuitegemea, yote iweke kwenye fungu hilo.

10. Kila siku unapoimaliza siku yako, jipe muda wa kutafakari jinsi siku hiyo ilivyokwenda. Jua yapi umefanya vizuri, yapi umekosea na wapi unapaswa kuboresha zaidi. Andika kwenye notebook yako yale uliyojifunza kwenye tafakari hiyo ya jioni. Kwa kufanya tafakari hii kila siku, utaendelea kuwa bora zaidi kwa kila siku mpya unayokwenda kuanza.

Rafiki, ni mambo hayo kumi tu ya kufanya kila siku kwa siku 30 bila kuacha hata siku moja, kisha siku 30 zikiisha jifanyie tathmini, kama matokeo ni mazuri fanya hiyo kuwa sehemu ya maisha yako.

NA KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU

 

 

ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA ITAKAYOKUPA MAFANIKIO MAKUBWA NDANI YA MWAKA MMOJA KULIKO WASHINDANI WAKO.

Nenda shule, soma kwa bidii na ufaulu vizuri.

Utapata kazi inayokulipa vizuri na utakuwa na maisha mazuri.

Huu ulikuwa ushauri maarufu na uliofanya kazi kwenye karne ya 20 na muongo wa kwanza wa karne ya 21.

Lakini sasa mambo yamebadilika kabisa,

Waliofuata ushauri huo ni wengi, wameenda shule, wamesoma kwa bidii,

Wakahitimu na ufaulu mkubwa, lakini kazi hakuna.

Karne ya 21 imekuwa na mapinduzi makubwa ya kiteknolojia kiasi kwamba nafasi za kazi ni chache kuliko wahitaji wanaozitaka nafasi hizo.

Hivyo licha ya juhudi mbalimbali zinazofanyika na serikali mbalimbali duniani,

Bado tatizo la kukosekana kwa ajira linaendelea kukua kila siku.

Pamoja na tatizo la kukosekana kwa ajira kuwepo,

Bado ushauri unaendelea na vyuo vinaendelea kuzalisha wahitimu anaotegemea kupata ajira.

Wanafunzi wanapohitimu na kukaa mtaani kutafuta kazi bila mafanikio,

Wanapewa ushauri mwingine ambao unawachanganya zaidi.

Wanaambiwa usisubiri tu kuajiriwa,

Jiajiri mwenyewe, anzisha biashara.

Hapo ndipo wanachanganyikiwa zaidi,

Mtu amekaa darasani kwa zaidi ya miaka 15 na miaka yote hiyo alikuwa anafundishwa kuja kuwa mwajiriwa.

Halafu amehitimu anaambiwa ajiajiri?

Mtu hana maandalizi yoyote katika kujiajiri au kuanzisha biashara,

Hivyo hata pale wanaposaidiwa mtaji wa kuanza biashara,

 zinaishia kufa.

Ukweli ni kwamba, ushauri wa karne ya 20 haufanyi tena kazi kwenye karne ya 21 na watu hawajaandaliwa kukabiliana na mabadiliko haya.

Njia ya uhakika kabisa ya kuingiza kipato kwenye karne hii ya 21 ni kufanya biashara.

Njia hii haina ukomo kwenye ukuaji au kipato,

Lakini siyo njia rahisi ambayo mtu atafanikiwa kwa kuambiwa tu mara moja.

Unahitaji kupata mafunzo sahihi ndiyo uweze kufanikiwa kwenye kuanzisha na kukuza biashara inayokupa kipato kisicho na ukomo na pia kukupa uhuru wako.

Miaka 15 uliyokaa darasani, haikukufundisha hilo.

Lakini una bahati, kuna njia ya kujifunza yale ya msingi kabisa kuhusu biashara kwa njia rahisi,

Huku ukielewa na kuwa na hatua za kuchukua.

 

JIUNGE     NA   " DARASA   ONLINE " SASA  HUJACHELEWA.

 

Wasiliana  na  KOCHA  MWL.  JAPHET  MASATU

WhatsApp + 255 716  924 136 /  + 255 755 400 128 /  + 255 688 361 539  /  + 255 629748  937

EMAIL :  japhetmasatu@gmail.com

 

NJIA RAHISI ITAKAYOKUSAIDIA KUKABILIANA NA RAFIKI HASI KWENYE MAISHA YAKO.

Njia Rahisi Itakayokusaidia Kukabiliana Na Rafiki Hasi Kwenye Maisha Yako.

Kulingana na takwimu inaonyesha,

Wastani wa watu wanne (4) unaojihusisha nao kwa siku wana mitazamo hasi.

Unaye rafiki yeyote ambaye ni hasi?

Je, unaye rafiki ambaye ukikaa naye unaishia kujisikia vibaya?

Je, unaye rafiki ambaye anapenda kulalamika?

Je, unaye rafiki ambaye ukikaa naye unahisi kukata tamaa?

Je, unaye rafiki anayeamini kutowezekana kuliko kuwezekana?

Kama umejibu ndio ,

Kabla ya kujifunza njia rahisi itakayokusaidia kukabiliana na rafiki hasi.

Tuangalie kwanza utofauti uliopo kati ya matajiri  na masikini wanavyojihusisha na rafiki hasi.

Matajiri huwa wanajenga mahusiano na watu wenye mitazamo chanya na waliofanikiwa.

Watu wanaoamini kwenye uwezekano na wanaohamasisha na kutoa matumaini.

Masikini huwa wanajenga mahusiano na watu wenye mitazamo hasi na walioshindwa.

Watu waliokata tamaa na wanaoamini haiwezekani na wanaondoa matumaini.

Watu wanaokuzunguka wanayaathiri sana maisha yako.

Pale ulipo kimaisha sasa ni wastani wa walipo wale unaotumia nao muda wako mwingi.

Matajiri wanajua ili wawe matajiri na wabaki kwenye utajiri, wanapaswa kujihusisha na watu matajiri.

Hivyo marafiki zao huwa ni matajiri wenzao, tena wale waliowazidi utajiri.

Masikini hubaki wakiwa wamezungukwa na masikini na hilo kuwafanya wabaki kwenye umasikini wao.

Ili ufikie utajiri, chagua kujenga mahusiano na watu matajiri au wanaoelekea kwenye utajiri.

Pia lazima uwapunguze watu hasi kwenye maisha yako,

Wale ambao ukikaa nao unaishia kujisikia vibaya na kukata tamaa.

Zungukwa na watu chanya,

 Ambao ukikaa nao unajisikia vizuri na kupata hamasa na matumaini ya kupata utajiri zaidi.

 

Saturday, May 8, 2021

HII NDIYO NJIA YA UHAKIKA YA KUONGEZA MSHAHARA WAKO.

Je wewe ni mwajiriwa lakini mshahara unaoupata hautoshelezi kuyaendesha maisha yako?

Je umekuwa kwenye ajira kwa miaka mingi, lakini kikubwa ulicho nacho ni madeni na mishahara haikutani?

Je mwajiri wako amekuwa hakuongezi mshahara licha ya gharama za maisha kupanda?

Na je ungependa kuwa na njia ya uhakika ya kukuza kipato chako ili uweze kuyaendesha vizuri maisha yako?

Kama umesema NDIYO kwenye swali lolote hapo juu, basi kuna habari njema kabisa kwako hapa.

Njia moja ya uhakika ya wewe kuongeza kipato chako ili uweze kuyamudu maisha yako, ni kuwa na kipato cha ziada badala tu ya kutegemea mshahara wako.

Kuna njia mbalimbali za kutengeneza kipato hicho cha ziada, na moja wapo ni kuanzisha biashara ya pembeni huku ukiwa unaendelea na biashara yako.

Najua unajua hili, siyo geni kwako, na huenda umekuwa unafikiria kufanya hivyo lakini kuna vikwazo mbalimbali vinakuzuia.

Au umeshawahi kuanzisha biashara ya pembeni, lakini ikafa kwa sababu ulishindwa kuisimamia vizuri kutokana na kazi kukubana.

Zipo changamoto kubwa tano zinazowazuia wengi kuanzisha biashara wakiwa kwenye ajira.

Changamoto ya kwanza ni mtaji, wengi wanakwama kwa sababu hawana mtaji wa kuanzisha biashara wanazotaka kuanzisha.

Kama hii ndiyo changamoto yako, basi leo unakwenda kupata majibu ya jinsi ya kuanza biashara bila hata ya mtaji kabisa.

Changamoto ya pili ni wazo sahihi la biashara. Wengi hawajui ni biashara gani nzuri wanayoweza kufanya.

Hii pia utapata jawabu lake kwa sababu kuna mawazo ambayo wengine wameshayafanyia kazi na yakawa na manufaa kwao.

Changamoto ya tatu ni muda wa kuiendesha biashara, kwa kuwa ajira zinawabana sana watu, muda unakuwa changamoto.

 Hapa utajua jinsi ya kuwa na siku mbili ndani ya siku moja.

Changamoto ya nne ni kupata wasaidizi sahihi kwenye biashara hasa kwa kipindi unachokuwa kwenye ajira.

 Kupata watu sahihi imekuwa kikwazo kwa wengi, wapo walioamini ndugu wa karibu na wakaishia kuwaangusha. Hapa unakwenda kujifunza jinsi ya kupata watu sahihi.

Changamoto ya tano ni kujua wakati sahihi wa kuachana na ajira ili uweke nguvu zako zote kwenye biashara.

Wapo wanaowahi kufanya hivyo na baadaye wanajikuta wakilazimika kurudi kwenye ajira na wapo wanaochelewa na kujikuta wakidumaza biashara zao. Hapa utajifunza wakati sahihi wa kuacha ajira na kuweka nguvu kwenye biashara.

Kama umekuwa unatamani sana kuanza biashara ukiwa kwenye ajira au umeshaanza na unasuasua, basi leo unapata majibu ya uhakika ya changamoto zote unazokutana nazo na hatua za kuchukua.

Majibu hayo yako kwenye  "  DARASA   ONLINE  " mwongozo sahihi wa kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwe kwenye ajira utajifunza yote  kwa  kina  zaidi  UTAFANIKIWA  SANA.

NA KOCHA  MWL.  JAPHET  MASATU, DAR  ES SALAAM

WhatsApp + 255 716 924136  /  + 255 755400 128 / + 255 688 361 539


 

ACHA KUMLAUMU MTU YEYOTE BALI KUMBUKA WAJIBU WAKO NI UPI ??

Ni kawaida ya watu kulaumu pale mambo yanapoenda vibaya. Kulaumu kunampa mtu kuona jambo lilotokea hahusiki au kujiondoa katika wajibu fulani. Kulaumu ni kwa watu wasiojua ukweli wa maisha kuwa katika mambo wanayolaumu nao ni sehemu ya matokeo hayo. Kukosa kujua hili kunafanya kundi kubwa la watu mambo yanapotokea vibaya basi kutafuta wa kuwatwika lawama na wao wawe salama kuwa hawahusiki kwa chochote.

Jamii yetu ina watu wachache ambao mambo yakitokea yameenda vibaya basi wanajua kwa namna moja wamesababisha yawe hivyo na wana wajibu wa kufanya kitu kurekebisha, kukubali na kuandaa mpango wa kuchukua hatua ili kuepusha matatizo kama hayo wakati mwingine. Kufanya hivi ni kipimo cha ukomavu na ukuaji ndani ya mtu anapoachana na lawama bali kuwajibika na kuchukua hatua fulani dhidi ya jambo liliotokea.

Mara ngapi umekuwa mtu wa lawama na kulaumu watu ?, umejikuta katika kulaumu hujaongeza chochote zaidi ya kuharibu zaidi au pengine kutochukua hatua zozote zile maana anayelaumu hutaka kuonewa huruma na wengine. Ni mara ngapi tumekua hatuchukui hatua fulani katika maisha kwa kubaki kulaumu asingekuwa mtu fulani ningekuwa sehemu fulani, asingekuwa mtu fulani ningekuwa nimefanikiwa. Kulaumu kunafanya mtu awe mzembe na mvivu kufanya kazi akifikiria kwa kulaumu mambo yatabadilika yenyewe.

Lolote linalotokea jifunze kuangalia ni kwa namna gani na wewe umechangia utokeaji wake. Usibaki upande mmoja kulaumiwa bila kujua na wewe unachangia vipi hali hiyo hadi imejitokeza. Kuna sehemu ukitulia na kufikiria utaona na wewe unahusika katika utokeaji wa mambo mengi. Usiishie tu kulaumu haraka haraka bali angalia upande wako na kuwa tayari kuchukua hatua stahiki. Hili litakusaidia kuvuka vikwazo vya watu wengi wanalaumu tu bila kujua wajibu wao ni upi. 

NA  KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU

WhatsApp + 255 716 924136 / + 255 755 400128  

EMAIL : japhetmasatu@gmail.com


 

KWA NINI WENZAKO WANAFANIKIWA NA WEWE UNABAKI ULIPO ??

Rafiki yangu mpendwa,

Huenda hili ni swali umekuwa unajiuliza kwa muda mrefu.

Unapoona wenzako ambao mmeanza kazi pamoja, kazi ambayo ni sawa na malipo yanalingana, ila wao wanapiga hatua huku wewe unabaki nyuma.

Au ni kwenye biashara ambapo unaona wengine wanaofanya biashara ya aina hiyo na mlioanzia kwa kiwango sawa wanapiga hatua wewe unabaki ulipo.

Watu wa kawaida, ambao hawawezi kufanikiwa huwa wanatafuta sababu za kuhalalisha hali zao.

Wanajiambia wale waliopiga hatua wamependelewa au wamepata bahati au kuna njia zisizo sahihi wanazotumia.

Ni kweli hivyo vinaweza kuchangia kwa namna fulani, lakini siyo sababu hasa.

Wale waliopiga hatua kuliko wewe kuna mambo mawili yanayowatofautisha na wewe ambayo kama hutayajua na kuyafanyia kazi, utaendelea kubaki hapo ulipo.

Jambo la kwanza ni namna wanavyofikiri.

Kuna watu wanapewa urithi na wanaweza kuuendeleza na kufanikiwa. Wakati kuna wengine wanapewa urithi na kuupoteza wote.




Kinachowatofautisha watu hau siyo wanachopewa, bali namna wanavyokichukulia.

Namna mtu anavyofikiri inaathiri sana yale anayofanya kwenye maisha yake. Wanaopiga hatua wanafikiri kwa uchanya, uwezekano na ukuaji.

Kwenye fikra zao wanaona picha kubwa ambayo wanapambana kuifikia. Wanaamini bila ya shaka yoyote kwamba watafikia picha hiyo.

Na pale wanapokutana na vikwazo mbalimbali, wanajua siyo mwishi wa safari, bali wanaimarishwa ili waweze kupokea makubwa.

Wasiofajikiwa wao hufikiri kwa udogo, uhasi na kutokuwezekana. Hawana picha kubwa, wanaona mengi ni mabaya na wanapokutana na changamoto wanaona ni mwisho.

Kama hutabadili namna unavyofikiri hutaweza kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Jambo la pili ni namna watu wanavyofanya.

Kama watu wawili wanafanya kazi au biashara ya aina moja na mmoja akapiga hatua kuliko mwingine, ukimuangalia utaona wazi kuna vitu anafanya tofauti.




Wanaofanikiwa na kupiga hatua wanafanya mambo yao kwa namba ya tofauti kabisa.

Wana viwango walivyojiwekea katika kufanya, viwango ambavyo ni vya tofauti kabisa na wengine.

Wanakwenda hatua ya ziada na kutoa thamani kubwa tofauti na wanavyotegemewa kufanya.

Wanajua mafanikio ni mbio za muda mrefu na hivyo hujipanga vizuri kwenye ufanyaji wao.

Kamwe hawaahirishi yale waliyopanga kufanya, wana nidhamu kubwa ya kutekeleza kama walivyopanga.

Wale wasiofanikiwa huwa wanafanya mambo yao kwa mazoea, hawawezi kujituma wenyewe mpaka wasukumwe na ni wazuri sana kwenye kuahirisha yale waliyopanga kufanya.

Kama hutajifunza namna waliofanikiwa wanavyofanya na wewe kufanya kwa namna hiyo, utaendelea kubaki pale ulipo.

Habari njema kwako rafiki yangu ni una nafasi nzuri ya kujifunza kwa kina namna ya kufikiri na kutenda ili uweze kufanikiwa sana.

JIUNGE   NA  DARASA  ONLINE  --UJIFUNZE    KWA   KINA    NA  VITENDO

JIFUNZE  ,ELIMIKA   NA   CHUKUA  HATUA.

TUWASILIANE  SASA    KWA  MAELEKEZO  ZAIDI

NA  KOCHA  MWL.  JAPHET   MASATU

WhatsApp  + 255 716  924 136  /   +  255  755 400 128  /  + 255 688 361  539

EMAIL : japhetmasatuy@gmail.com




JIFUNZE HAPA : JINSI YA KUZIVUTA FURSA NA KUZITUMIA NDANI YA MUDA MFUPI.

Unakwama Wapi Mpaka Sasa Hujui Jinsi Ya Kuzivuta Fursa?

Huzioni fursa lakini wenzako wanaziona na kuzitumia je, unajua tatizo ni nini?

Ulichofichwa kwa muda mrefu leo unakwenda kukifahamu na kukitumia ipasavyo.

Angalia huu mfano hapa chini;

MARAFIKI  WAWILI  WAKIVUA.

Kulikuwa kuna wavuvi wawili ambao ni marafiki wa karibu.

Walitumia wikiendi kuvua samaki pamoja.

Pale wanapokuwa wametingwa na shughuli zao na familia zao ilikuwa ngumu kuonana.

Ilikuwa ni siku ya juma mosi waliamua kuongozana  pamoja karibu na ziwa kufurahia shughuli za uvuvi kwenye siku yao.

Wote walibeba nyenzo muhimu za uvuvi pamoja na vikorombezo vingine kwa ajili ya kupikia samaki.

Walifika kwenye bwawa.

Walikaa kwa mbali na kuanza kuwinda samaki.

Mvuvi wa kwanza alipata samaki mkubwa na mzuri ndani ya dakika chache.

Alifurahi akamuweka samaki ndani ya jokofu la plastiki lenye mabonge ya barafu na kumuhifadhi.

Alitumia muda kidogo kuwanasa samaki wengine wachache.

Aliamua kuwapika wachache,

Pia aligandisha samaki wachache na wengine aliwaacha kwa ajili ya kuwapeleka nyumbani.

Ilichukua zaidi ya li saa wakiwa wanavua.

Mvuvi wa kwanza  akamfuata mvuvi wa pili na kumuuliza kama anahitaji msaada.

Mvuvi wa pili akamjibu hapana.

Dakika chache , mvuvi wa pili anakamata samaki mkubwa.

Ata hivyo, alimrudisha tena ndani ya ziwa.

Mvuvi wa kwanza alishangazwa na iko kitendo.  

Mvuvi wa pili akawa ana kamata samaki wakubwa , lakini anawarudisha wote ndani ya maji.

Mvuvi wa kwanza anachukizwa sana na iko kitendo cha mwenzake, anamuuliza kwa hasira “ Una wazimu?

Kwanini unawarudisha samaki wote ndani ya maji?

Walikuwa wazuri na wakubwa.

Mvuvi wa pili anajibu, “ Najua walikuwa wakubwa, bali sina kikaango kikubwa cha kupikia hao samaki wakubwa.

Kwa hiyo natafuta samaki wadogo ambao wataenea kwenye kikaango changu kidogo.

Akasema mungu ananisumbua sana leo.

Baada ya kusikia hilo, mvuvi wa kwanza anashangazwa na hilo jibu.

Anamshauri mvuvi wa pili kumkata samaki mkubwa vipande vipande ili aweze kuenea kwenye kikaango na wapike bila shida.

Somo;

Watu wengi wapo kama mvuvi wa pili.

Wanazungukwa na fursa nyingi lakini wanashindwa kuzitumia , na hii ni kwa sababu hawazioni  na hawajui jinsi ya kuzivuta.

Wanachokiona ni vikwazo, uchache, matatizo na hatari ya kupoteza.

Ata wewe mwenyewe unajishangaa unazungukwa na fursa nyingi lakini unashindwa kuziona na kuzitumia, lakini wenzako wanaziona na kuzitumia.

Na hiki ndicho kinachowatofautisha matajiri na maskini.

Matajiri wanajua jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ipasavyo lakini masikini wanafanya kinyume chake.

Ata wewe leo hii unaweza kujifunza jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ndani ya muda mfupi.

Kwa kusoma na  kujifunza , unakwenda kujifunza jinsi ya kuzivuta fursa na kuzitumia ndani ya muda mfupi.

Unakwenda kufahamu vizuizi vinavyokuzuia usizione  fursa.

Karibu sana UJIUNGE  NA    " DARASA  ONLINE "--ujifunze  TABIA ZA KITAJIRI na FURSA  MBALIMBALI   ZINAZOKUZUNGUKA  na Mengine  mengi  YANAYOHUSU FALSAFA , SAIKOLOJIA, MAHUSIANO ,

Ujifunze kwa kina na kuyaelewa maarifa haya muhimu sana kwako,

 Kisha uchukue hatua ili maisha yako yaweze kubadilika, ufike kwenye utajiri, mafanikio na furaha.

 

Kwa  Maelekezo  Tuwasiliane 

NA  KOCHA   MWL.  JAPHET  MASATU

WhatsApp + 255 716 924 136 ,  + 255 755 400 128 

EMAIL : japhetmasatu@gmail.com

 

JINSI YA KUPATA WAZO LA BIASHARA ILI LIWEZE KUKULETEA MAFANIKIO MAKUBWA SANA---NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU---( PDF )

JINSI YA KUPATA MTAJI WA BIASHARA NA VYANZO VYAKE---NA KOCHA MWL. JAPHET MASATU-----( PDF )

Saturday, May 1, 2021

UNASHINDWA NINI ?? NI RAHISI SANA KUOKOA MUDA WAKO

Angalia, Jinsi Ilivyorahisi Kuokoa Muda Wako.

 Unajua ni nini cha kikawaida kati yako na Jeff Bezos, Mark Zuckerberg, Bill Gates, Mukesh Ambani, Warren Buffett

Rasilimali ya kikawaida ambayo mnayo wote sawa ni MUDA.

Kila mmoja amepewa MUDA sawa kama mwenzake.

Hakuna aliyependelewa.

Wote mna sekunde 86,400 kwenye siku moja.

Matumizi mazuri ya muda ndiyo yanaleta tofauti iliyopo kati ya waliofanikiwa sana na wale wenye maisha ya kawaida.

Leo nitakushirikisha stori fupi inayohusu matumizi mazuri ya muda.

Siku moja niliudhuria semina pale mkufunzi alipokuwa anafundisha juu ya MUDA.

Kabla hajaanza kutufundisha  akasema “ Huu ni muda wa kufanya zoea”

Akaenda chini ya meza na kuvuta  jagi kubwa lenye upana wa wastani.

Akaliweka juu ya meza karibu na mawe makubwa ambaye yalikuwepo pale mezani.

Akauliza unafikiri ni mawe mangapi yataweza kuenea ndani ya hili jagi?

Wakati tukiendelea kukisia na kutafakari,

Akasema “Sawa, acha tutafute“.

Akaweka jiwe la kwanza ndani ya jagi... likafuatia  lingine... na lingine tena.

Sikumbuki aliweka mawe mangapi kwenye jagi, lakini alijaza lile jagi.

Akauliza tena “ Hili jagi limejaa?”

Kila mmoja akaangalia yale mawe na kusema “ NDIYO”.

Mkufunzi akacheka kwa sauti, “ahhh”.

Akaingia chini ya meza na kuvuta ndoo ya kokoto.

Halafu  akamimina kokoto kwenye jagi na kuanza kutikisa na kokoto zote zikaenea kwenye jagi na kuziba mianya yote iliyoachwa wazi na mawe makubwa.

Hapo baadae akalitikisa lile jagi na kuuliza tena “ Hili jagi limejaa”

Kwa muda huu ,washiriki tukawa tunakisia jibu na kuogopa kujibu tusije tukakosea tena huku tukiwa tunajisemea “ Pengine sio”.

 Kiukweli  tulikuwa hatujiamini.

Mkufunzi akaitikia kwa kusema ”VIZURI!”.

Akaingia tena chini ya meza na kutoka na ndoo ya mchanga na akaanza kumwaga ndani ya jagi.

Baada ya kumwaga mchanga ndani ya jagi ikaonekana kuna mianya midogo imebaki kati ya mawe na kokoto ndani ya jagi.

Mkufunzi kwa mara nyingine akaangalia na kuuliza, “ Hili jagi limejaa?”

Tulinguruma na kusema “Hapana!”.

Akasema, “SAFI!” na akachukua jagi lingine lenye maji na kuanza kumwagilia ndani ya jagi lenye mawe, kokoto na mchanga.

Akauliza mmeelewa nini?

Mmoja wetu akasema , “ Kuna mianya mingi, na kama utafanya kazi kwa bidii utaweza kukabiliana na chochote kile kinachojitokeza kwenye maisha yako”.

Mkufunzi akasema “ HAPANA”  hicho sicho nilichomaansha.

Nimemaansha hivi.

“WEKA JIWE KUBWA KWANZA”.

Mkufunzi aliendelea,  “ Sasa hivi, nataka uelewe kwamba hili jagi ni maisha yako.

Jiwe kubwa ni vile vitu vyote kwenye maisha vyenye umuhimu mkubwa kwenye maisha yako- chochote ambacho ni muhimu kwako, kama kikipotea  kitaweza kuletea madhara makubwa kwenye maisha yako au kukuharibia maisha yako kabisa.

Mawe makubwa yanawakilisha vitu kama Afya ya mwili, Afya ya akili, Familia yako, Mke wako, Watoto wako.

Kokoto ni vile vitu vyenye umuhimu kwenye maisha yako lakini sio sana kama hivo hapo juu.

 Kokoto inawakilisha vitu kama Kazi, Nyumba, Marafiki, Gari, Koneksheni ulizonazo.

Mchanga ni kila kitu ambacho ni kidogo na hakina umuhimu wowote kwenye maisha yako.

“Kama utaweka mchanga kwanza ndani ya jagi, mawe makubwa yatakosa nafasi ya kukaa ndani ya jagi.

“Ndio maana nilisema, hivi – “WEKA MAWE MAKUBWA KWANZA”.

Aliendelea , “ Natumaini sasa hivi umeelewa, hii ni sawa na kwenye maisha yako”.

Kama utatumia nguvu zako zote na muda wako kwenye vitu ambavyo havina umuhimu mkubwa na ni vidogo, utakosa muda wa kufanya vitu vikubwa na vyenye umuhimu mkubwa kwenye maisha yako.

Kuwa makini na vitu vyote vyenye umuhimu mkubwa kwenye maisha yako na tumia muda wako mwingi kwenye vitu vyenye umuhimu mkubwa.”

Lilikuwa somo zuri kubwa sana na lilibadilisha fikra zetu kwa wale wote tuliohudhuria.

Kuanzia siku hiyo nilibadili kwa kiasi kikubwa namna ninavyotumia muda wangu.

Kupitia stori hii natumaini umejifunza  jinsi ya kutunza muda wako, kwa kuanza kwa kufanya mambo yenye umuhimu mkubwa kwanza.

Vipaumbele vitakusaidia sana kuamua na kujua ni kipi kianze kwanza kabla kingine.

Unahitaji kuweka msawazo kwenye maisha yako.

Unapoweka msawazo kwenye maisha yako hutosumbuka na mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa.

Muda ni dhahabu, tumia kwa hekima na acha kupoteza muda kwa mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa.

Pambana na yale yenye umuhimu mkubwa, acha kupoteza muda.

Kujua kuweka vipaumbele kwenye siku yako haitoshi, unahitaji zaidi ya hilo na hii ni kwa sababu kama hujua vitu vinavyokupotezea muda na kuweza kuvidhibiti.

Utaendelea kutumia nguvu nyingi na mwisho utakuwa unapata matokeo sisimizi.

Hutoweza kuanza kufanya yale yenye umuhimu mkubwa kwanza, kama hutoweza kuvidhibiti vinavyo kupotezea muda.

Hatua unayotakiwa kuchukua sasa hivi ni kuanza kuvidhibiti vitu vyote vinavyokupotezea muda na ikiwezekana uachane navyo kabisa kwa sababu vimekuwa vinachukua muda wako na kukuchosha mwisho unashindwa kufanya mambo yenye umuhimu mkubwa.

Na ipo njia rahisi ambayo kila siku nimekuwa nakushauri unayoweza kuifuata kuanzia sasa hivi ,ili usiendelee kupoteza muda wako kwenye mambo ambayo hayana umuhimu mkubwa na yanaendelea kukuchosha.

 

Na   KOCHA  MWL,  JAPHET   MASATU,DAR  ES  SALAAM , TANZANIA,

 WhatsApp +255 716 924 136 /  + 255 755 400 128

EMAIL :  japhetmasatu@gmail.com