Nimesikia mara nyingi
sana watu wakilalamika kuwa hawana muda. Kupitia malalamiko haya,
nimejikuta nikijiuliza maswali mengi kama haya;”kwamba muda huwa unatoka
wapi? Nani huwa anagawa muda? Nani ni mmiliki wa muda? Je mimi ndiye
mmiliki wa muda? Au muda unanimiliki mimi.
Katika kutafakari maswali yote haya nimegundua kwamba... MUDA ni dhana ambayo ilitengenezwa na binadamu hasa baada ya kutambua kuwa kuna kifo.
Hii
inasaidia katika kupima utendaji wa shughuli za kimaisha kwa lengo la
kuuambia mwili wako kuwa unatakiwa kukamilisha vitu Fulani kwa muda
Fulani.
Katika
dhana hii ya muda, tunapata kufahamu kuwa kuna makundi ya watu aina
mbili; kundi la kwanza ni lile LINALOMILIKI MUDA na kundi la pili wale
WANAOMILIKIWA NA MUDA – yaani watu wanamilikiwa na muda.
Kundi la wale WANAOMILIKI MUDA, ni watu wanaojua kuwa wana wajibu wa kuwa wachoyo wa muda wao.
Yeyote
anayemiliki muda inamlazimu kuwa mchoyo wa muda wake ili kuutumia
kuzalisha thamani ambayo wanaweza kufaidi hata wale ambao uliwanyima
muda wako mwanzoni.
Kuwa mchoyo wa muda wako ni busara ilimradi unawagawia watu wengine kile kitokanacho na matumizi ya muda wako.
Acha ku-manage muda na badala yake anza KUUMILIKI,
MUDA ni mali ghafi ya kupata kitu chochote cha thamani. MUDA ni kitu pekee duniani ambacho huwezi kirudisha kikishapotea.
Poteza
pesa lakini unaweza kutengeneza pesa nyingi. Poteza ajira lakini
unaweza kupata ajira nyingine. Lakini poteza muda na hautaupata tena.
Kuna
masaa 168 katika wiki. Na una wastani wa dakika 2,400 kila wiki. Huu
ni muda mwingi sana. Unaweza kwenda wapi? Au muda huu wote unautumia
wapi?
Mambo makubwa yanaweza kufanyika kwa siku kama ukijua ni nini cha kufanya kwa muda husika.
Pindi
ukiacha kusimamia MUDA na badala yake chukua umiliki wa muda wako, ni
rahisi sana kuongeza uzalishaji na kuacha kufanya vitu ambavyo
huvipendi.
“Kuna njia nne za kutumia muda wako: Kuwaza, mazungumzo, kutenda na usumbufu”- Chagua kwa busara
Wewe
peke yako unaweza kuchukua umiliki wa MUDA WAKO na uamue ni muda gani
utatumia kwenye KUFIKIRI, MAZUNGUMZO, KUTENDA na hata USUMBUFU WA
MAKUSUDI mbao utakupelekea kufikia mafanikio.
Kama
hujaajiriwa na mtu, maana yake unamiliki masaa yote 24. Lakini kama
wewe uko kwenye ajira maana yake unamiliki masaa 16, yaani.. (masaa 24
KUTOA Masaa 8).
Kwa
mwajiriwa tunatoa masaa 8 kutoka kwenye masaa 24, nikiwa namaanisha
yale masaa 8 yalishauzwa kwa mwajiri na thamani yake ni huo mshahara
unaoupata kila mwisho wa mwezi.
Kwahiyo, ulinde sana muda wako kama uwekezaji wa thamani. Upangia kazi MUDA wako kila wakati.
Kila
shughuli ya siku lazima ikamilishwe kwa muda uliopangwa. Na kikubwa
zaidi kila shughuli lazima iwe ni ile inayochangia kwenye ndoto yako
kwa siku, mwezi au mwaka. Ufinyu wa muda utakusukuma kuzingatia na kuwa
mwenye ufanisi katika kile unachokifanya.
Bila
wewe kujali mambo yaliyo mbele yako, jitahidi kuwa wazi, ili ujue ni
kipi cha kuzingatia na kimsingi ujue ni kipi cha kufanya pale unapopata
muda wa ziada!
Kumiliki
muda wako siyo kuwa na muda wa kukaa bure; BALI ni kujua unataka nini
na kutumia muda wako kufanya vitu vyenye tija na vinavyokusogeza au
kukufikisha kwenye ndoto yako.
Unahitaji
kuanza leo kumiliki MUDA wako na kama suala la kumiliki muda wako ni
jambo la kipaumbele kwako, basi endelea kufuatilia tandao huu wa
MAISHA NA MAFANIKIO BLOG ( LIFE AND YOU )
No comments:
Post a Comment