Mpendwa msomaji wa MAISHA NA MAFANIKIO BLOG ( LIFE AND YOU) , napenda nianze kwa kusimulia jinsi nilivyokosa FARAJA kwa kuandika makala hii:
“Leo nimeamka usiku saa tisa na nusu, na tayari nimeanza kuandika makala hii ambayo upo unaisoma. Lakini NIMEKOSA FARAJA kutokana na uwepo wa mbu wengi wanaonisumbua sana, achilia mbali hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa malaria. Niko tayari KUKOSA FARAJA, kwasababu ni kwa njia hii nitaweza KUPATA FARAJA kama ambavyo imekuwa ikitokea pale wasomaji wa mtandao wa MAISHA NA MAFANIKIO BLOG ( LIFE AND YOU ) wanaponitumia ujumbe kuwa makala zangu zina mchango mkubwa kwenye maisha yao”. .
Kisa
hiki cha mbu walionisumbua kinatuonyesha kwamba, FARAJA ni kitu kizuri
sana kwa binadamu na kwa wengine ni kichocheo kikubwa kwao kufanya kile
wanachokifanya.
Niseme tu, FARAJA ni ile hali ya kujisikia vizuri na huru kutoka kwenye maumivu, matatizo au msongo wa mawazo.
Ukweli
ni kwmba watu wengi wanapenda FARAJA. Matokeo yake FARAJA imekuwa ni
kizingiti kikubwa katika kuyafikia maisha ya mafanikio na utajiri.
Watu
wengi wemejikuta wakishindwa kuchangamkia fursa kwasababu fursa nyingi
ambazo ni kubwa zinakutaka huwe tayari kukosa FARAJA kwa muda Fulani
ndio upate tena.
Kutokana
na tabia hiyo ya kupenda sana FARAJA, wengi wamejikuta wakifanya vitu
vidogo vidogo sana na vya kawaida ILIMRADI tu haviwaondoi kwenye FARAJA
yao ya awali.
Ni vizuri kutambua kwamba FARAJA endelevu itapatikana kwa wale ambao wako tayari kukosa FARAJA kwa muda.
Ukweli ni kwamba, vitu vingi vyenye kuleta FARAJA ENDELEVU vinafanyika katika mazingira ya kukosa FARAJA.
Mfano
ukitaka kuwa na afya nzuri, lazima uwe tayari kuacha kula vyakula
Fulani hata kama ni vitamu sana, lazima uwe tayari kupunguza sukari,
lazima kuamka mapema na kufanya mazoezi—hapa lazima uwe tayari kukosa
raha ya usingizi wa asubuhi n.k,
Wengi wetu katika kusaka mafanikio huwa tunapenda njia iliyonyooka. Martin Luther King aliwahi kusema kuwa;
“Kipimo kizuri cha binadamu siyo mahali aliposimamia wakati wa FARAJA, bali pale anaposimamia wakati wa changamoto na ubishani.”Binadamu tuna tabia ya asili ya kuegemea zaidi kwenye HADHI tuliyonayo na tunapinga kile tusichokijua, ili tuweze kuendelea kukaa na FARAJA yetu.
Tabia
ya kupenda FARAJA inafungamana na tabia ya mababu zetu ya kuhofia
kuhatarisha maisha. Tunaogopa kujaribu vitu vipya. Tunataka tukwepe
mabadiliko.
Kwahiyo,
hatujisukumi mbele kwenda katika kiwango kingine cha maisha mazuri.
Katika dunia ya sasa ya usumbufu na inayobadilika kwa kasi, inasaidia
wewe kubadilisha mahusiano yako na mabadiliko na kuwa tayari kufurahia
KUKOSA FARAJA.
Wengi tunafikiri maisha ni kutafuta ulinzi na usalama na FARAJA peke yake.
Hivi
vitu ni muhimu na ni sehemu ya maisha ya kila siku, LAKINI maisha
yamejaa RAHA na MAUMIVU, KURIDHIKA na KUTESEKA, URAHISI na UGUMU.
Kwa
kuangalia tu! upande mmoja wa sura ya FARAJA, tunajitenga na safu
kamili ya uzoefu wa maisha ya binadamu—na maarifa, ujuzi na huruma
itokanayo na upande mwingine wa (KUKOSA FARAJA).
Kama haujisikii vizuri KUKOSA FARAJA, bilashaka huwa unakaimbia mabadiliko. Katika dunia ya sasa, huwezi kukimbia mabadiliko!
Kila
kitu kiko katika hali ya kubadilika mara kwa mara. Ngozi yetu
ubadilika, majani ubadilika, watu ubadilika. Kwahiyo suala la kubadilika
linatokea kila mahali muda wowote.
Kuishi
kikamilifu, lazima uwe tayari kukanyaga kwenye visivyojulikana, sasa
hivi kuliko siku zote. Mfumo wetu wa kufanyakazi kidigitali na
utandawazi unakuhitaji kufanyiakazi hata vile usivyojulikana pale
unapoanza.
Lazima
uwe tayari kujipa changamoto ili kukua na kubadilika. Na mabadiliko
huwa yana harufu ya KUKOSA FARAJA kwa wengi wetu. Woga na wasiwasi na
kukosa FARAJA ni asili ya mapambano ya kimaisha kwa binadamu.
Kujifunza
namna ya kuwa na FARAJA kwa KUKOSA FARAJA, pengine ni mojawapo ya somo
muhimu sana ambalo nimejifunza kama mjasiriamali.
Anza
leo kujiandaa na uzoee wakati Fulani KUKOSA FARAJA ili kupata FARAJA
ENDELEVU hasa wakati huu unapoanza safari yako ya mafanikio.
Kuendelea
kujipatia ujuzi na maarifa juu ya pesa, kazi, biashara, ujasiriamali,
afya, uongozi na suala zima la uchumi wa kaya; jaribu kuendelea kusoma na kujifunza katika MAISHA NA MAFANIKIO BLOG ( LIFE AND YOU )