Rooney nje ya kikosi cha Man United dhidi ya Feyenoord
15 SEPTEMBER 2016
Mshambulizi matata wa soka Wayne
Rooney, ameachwa nje ya kikosi cha Manchester United cha wachezaji 20,
watakaosakata mchuano wa Alhamisi wa ligi kuu barani Ulaya mjini Rotterdam
dhidi ya timu ya Uholanzi -Feyenoord.
Licha ya kufanya mazoezi siku ya
Jumatano, nahodha huyo mwenye umri wa miaka 30 atakosa mechi hiyo ya ufunguzi
barani Ulaya.
Wengine ambao wameachwa nje ni
pamoja na Luke Shaw, Antonio Valencia na Jesse Lingard.
Maneja wa Manchester United Jose
Mourinho, amesema kwamba Rooney amepumzishwa mapema ili kucheza mchuano wa ligi
kuu ya Uingereza siku ya Jumapili uwanjani Watford.
Phil Jones pia hayupo baada ya
kupata jeraha la goti.
Jeraha hilo litamfanya mlinzi huyo
kutocheza kwa muda wa mwezi mmoja hivi.
BBC SWAHILI
BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment