Bakhresa
aonesha jeuri ya fedha Zimbabwe
Said Salim Bakhresa
Na
Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BILIONEA
Mtanzania, Said Salim Bakhresa, amepanga kutumia dola za Marekani milioni 30
sawa na Sh bilioni 65.5 kuchukua umiliki wa kiwanda cha usagishaji Zimbabwe,
Blue Ribbon Industries (BRI).
Kwa
mujibu wa gazeti la Zimbabwe Mail, Bakhresa Group, moja ya himaya kubwa ya
kampuni nchini Tanzania, imeifahamisha rasmi Tume ya Ushindani na Forodha ya
Zimbabwe kuwa inapanga kununua umiliki wa asilimia 100 wa kampuni hiyo
iliyotaabani.
Mwaka
2014, Bakhresa Group ilishinda zabuni ya kumiliki hisa katika BRI baada ya
wanahisa wake wakuu kukaribisha zabuni kwa wawekezaji wainunue au kuingiza
mtaji katika BRI ili kufufua operesheni za kampuni hiyo.
BRI,
ambao ni watengenezaji wa mkate na vyakula vya mifugo imekumbwa na matatizo ya
kifedha na ilikuwa ikihangaika kulipa mikopo iliyokopa kutoka ubia wa mabenki
ya Zimbabwe na washirika wa kibiashara.
GAZETI LA MTANZANIA, IJUMAA, 01/07/ 2016
No comments:
Post a Comment